JE UNAJUA NI
KWA NINI WATUMISHI BAADHI WANAZIKA BIBLIA , JE UNAJUA NI KWA NINI MUUMINI
ANAELEZWA NA MCHUNGAJI AIKANYAGIE BIBLIA CHINI KWA MIGUU YAKE?
BWANA YESU ASIFIWE aliye hai na
aliye peke yake ndiye mwana wa pekee wa
MUNGU, kama alivyonituma YESU kulitetea jina lake na kuwakomboa mataifa yote
wamrudie YESU wa kweli, sababu idadi kubwa imepotea na hawajijui wanaona wapo sawa kabisa na mpango wa MUNGU
na wengine wameokoka ila wokovu wao ukauwawa kiroho, mfano kuishiwa nguvu za
kuomba, kusoma neno, kushinda dhambi na mengineyo ila YESU atakufufua utakapotubu katika sala ya
toba, kila mtu anajua Neno la MUNGU lipo
katika biblia na ni kitabu kitakatifu
alicho kihakikisha MUNGU ili kitumike katika kumjua yeye au muongozo wa
kwenda mbinguni. Kitabu hiki unapoona
mchungaji anakifukia madhabahuni kwake hiyo inamaana analiuwa
neno la MUNGU katika kanisa hilo
ili watu wasielewe neno hata wakisoma na
hata wakielewa wasimshutukie mchungaji yupo kinyume na neno la MUNGU, na wote wanaozika biblia asili ya mtumishi wao
ni maagano ya nguvu za giza.
Jambo lingine muumini ukiambiwa
na mchungaji ukanyage biblia usikubali, unapoikanyaga kwa kutii yale aliyokuelekeza huyo mtumishi, tayari
unakuwa unaingia katika kiapo cha kumkana MUNGU pasipo kujua na karama uliyonayo shetani anaiiba anampa huyo mtumishi aliye
kushirikisha hicho kiapo, na wengi
wanafanya hivyo kwa kutegwa na watumishi walioamua kumtumikia shetani
ila wanatumia jina la YESU kumbe ni mbwa mwitu. Hao ni maadui wa MUNGU na hata
kazi za mahubiri anayoyafanya yote anasambaza mazao ya shetani kwa wanadamu na
kuwafungia watu wasiende mbinguni pasipo kujua, huu ni wakati wa mataifa yote kuujua ukweli,
watu wamedanganywa sana neno
likapinduliwa na watu wakayafuata yaliyopinduliwa na unapoyafuata yaliyogeuzwa basi na wewe unakuwa umegeuzwa
katika ulimwengu wa roho upo upande wa shetani.
Waeleze na wengine wote wasidanganyike tena, mahali pa jinsi hiyo ni
lango la kuzimu au anayefanya hayo yeye ni Agent wa shetani 100% mtawajuaje, chunguza
matendo yao, hivi umeshajiuliza je
injili imeandikwa iende mbele au ifukiwe ardhini, au ikanyagiwe kwa miguu?
Mwenye kuelewa aelewe sasa. Na kama ni neno la MUNGU basi uelewe kuwa unapoagizwa
uikanyage biblia yako kwa miguu basi unamkanyaga MUNGU kwa miguu yako ili
asionekane tena katika maisha yako bali shetani ndio atawale katika maisha
yako, na wengine hupewa kiapo cha kuichana biblia anapoichana tuu tayari
anakuwa anaingia kiapo na shetani hamtaki MUNGU wa kweli bali anamtaka shetani
na ndivyo inavyokuwa katika ulimwengu wa roho.
Sema BWANA YESU, naomba
unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua naomba
uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele uniongoze YESU
wewe wa kweli sikutaki tena yesu wa uwongo. Amen.
Visit www.prophethebron.org kwa zaidi utajifunza mengi na karibu katika
kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE, Arusha, Tanzania.
NABII HEBRON.