JE? UNAJUA
NI KWA NINI BAADHI YA WATUMISHI WA MAKANISA WANAUZA MADAWA YA KULEVYA?
JE , UNAJUA
ASILI YA MADAWA YA KULEVYA NI NANI?
BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA
NAZARETI aliye hai, watu wengi wanakuwa wakikosa majibu sababu ni kwa nini
baadhi ya wachungaji, manabii, mitume na wengineo wanakuwa wakifanya biashara
hizo na hata kulifanya jina la YESU lichafuliwe kwa ajili ya mtu anayejiita
mtumishi wa MUNGU anapokutwa au kujishughulisha na kazi hiyo, nimeamua kuwapa
jibu na wala msimsulubishe YESU katika lawama hizo kabisa, hao ni watumishi wa
YESU wa uwongo na wapo hapa ulimwenguni kuuchafua ukristo ili shetani azidi
kutawala na kuwavuna wanadamu zaidi.
Aliponituma kuifanya kazi yake
alinifundisha mengi na hata sasa bado ananifundisha yeye ni mwalimu mzuri sana
sijawahi kuona katika dunia hii na wala hatakuwepo. Madawa ya kulevya asili
yake ni shetani na shetani ndiye aliyeumba huo mti wa madawa ya kulevya asili
yake ni shetani na shetani ndiye aliyeuumba huo mti wa madawa ya kulevya ambapo
alitumia kinyesi chake kutengenezea huo mmea na lengo lake ni kuwateka wanadamu
ili wachanganyikiwe wasije wakawa wana wa MUNGU au na MUNGU asije akawapata
wakaenda mbinguni, huo mti upo kuzimu unaitwa JWCBL, mti huu ndio unao toa
nguvu hiyo na kusambaza huku duniani katika ulimwengu wa roho na cha ajabu
nilishangaa kule kuzimu wao hawavuti madawa ya kulevya ya huo mti ni sababu
wanajua ni kinyesi cha shetani, hivyo unapotumia madawa ya kulevya, unakuwa
umekula kinyesi cha shetani na kazi yake ni kukuvuruga akili yako na ufahamu
wako uwe kichaa na hata katika akili yako na ufahamu wako usije ukawahi kumfikia MUNGU au kumfuata MUNGU na kwa njia
hiyo kila aliyetumia madawa hayo aelewe anatumia kinyesi cha shetani na
kumtenga yeye na MUNGU, ila huku duniani
hawajui kama kuzimu madawa hayo yanaitwa kinyesi cha shetani.
Nawaeleza mkatae kabisa hayo
madawa ya kulevya sababu zake mmeshazijua jina na pia ni kinyesi cha shetani, na
katika huo mti alipewa jinni mkuu katika kitengo hicho anayeulinda anaitwa
GEORGE yeye ni jini, na ni pepo na anaroho ya shetani. Jini huyu yeye ndiye husimama na kuwasaidia
watu waifanye hiyo kazi huku duniani katika ulimwengu wa roho na kuwalinda wafanyabiashara
hizo wasionekane ila tokea 2012, kama nilivyokwisha elezea katika blog yangu
Nabii Hebron nilisema katika nchi ya TANZANIA na katika viwanja vya ndege
madawa ya kulevya hayatapita yatakamatwa tuu mimi nilijua alichokifanya YESU
kaharibu nguvu za huyo jini, hata kama madawa yakipimwa yalikuwa yanapita tuu,
eiza anazubaishwa yule anayekagua mizigo
katika machine au hilo jini lilikuwa linauwezo wa kuchezea machine na mkaguzi
anaona tofauti. Sasa madawa ya kulevya biashara hiyo katika nchi ya TANZANIA
itaendelea kufifia na itafika wakati TANZANIA haitakuwa tena na hayo ya kulevya
yanayoletwa na hao, njia zimefungwa na YESU.
Na zaidi nitaelezea kwa ufupi
ni kwa nini wachungaji baadhi au makanisa baadhi katika ulimwengu huu
yanashiriki biashara hiyo, lengo kabisa ikiwa ni pastor uelewe yeye ni pastor
wa shetani kabisa siyo wa YESU wa mbinguni, ni masharti aliyopewa kutumia jina
la kanisa ili asijulikane na anapewa nguvu za kumlinda na ni wengi hawajulikani
watu wanabakia kusubiri ila ushahidi hawaoni, ila sasa watakamatwa wote katika
nchi zote na ushahidi utapatikana tayari yule jini GEORGE ameangamizwa na
mtandao wake wote hawana msaada tena, na wakishirikiana na chama cha freemason
na Illuminati, sasa ufalme wa shetani umeporomoka na cha ajabu nilishangaa sana
wapo watumishi maarufu ni manabii na huku duniani watu wanawaona ni watumishi
wa MUNGU kumbe ni watumishi wa shetani wanawapiga upofu watu na hawajulikani
ndiyo na muda siyo mrefu watakamatwa na madawa hayo, hivyo myaonapo msishangae,
hao ni maajenti wa shetani na wewe unaposali kwake na wewe muumini unafanyika
agent wa shetani bila kupenda na kujua.
Nawasihi watu wa ulimwengu
usitumie hayo madawa sababu unapotumia kikubwa zaidi unaharibika na kutengwa na
MUNGU na ni shetani ndiye anayefanyaga kwa kutumia njia hiyo, sasa uelewe na
muwakatae kabisa wachungaji wanaouza hayo madawa sababu lengo lao ni moja,
kuwapeleka watu kwa shetani tuu.
Sema BWANA YESU, naomba
unisamehe dhambi zangu nisafishe mwili wangu na nafsi yangu pale nilipotumia
madawa ya kulevya au kula kinyesi cha shetani, nakitapika kwa jina la YESU, uniandike
jina langu katika kitabu chako cha uzima, sitaki tena kinyesi cha shetani
kuanzia sasa. Amen.
NABII HEBRON.