JE
UNAJUA MAANA YA SADAKA KUTUPIWA KATIKA MIGUU YA WATUMISHI, NABII,WACHUNGAJI INA
MAANA GANI? HIYO NDIYO NJIA YA KUFUNGA
UCHUMI WA WATU.
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE,
miaka mitatu iliyopita siku moja nilikuwa naongea na YESU na siku hiyo aliongea
na mimi kwa sauti ya hasira na uchungu sababu alikuwa anaangalia ulimwenguni na
akawa anaona watoto wanavyoteseka na kudanganywa na kuibiwa baraka zao na
maisha yao kufungwa na watu hao, waumini wakafikiria wanamfanyia YESU ili awabariki kumbe baadhi ya watumishi
wameungana na shetani. Wakitumia jina la YESU kuwapoteza na kuwaibia vitu vyao
pasipo wao kujua.
Akaniambia HEBRON baadhi ya
watumishi niliowaita wanitumikie na
kusema ukweli na kuyakemea badala yake wao wakaamua kuyakataa yangu na
kuyafuata ya shetani na mimi sasa siwataki wamefanyika kuwa vyombo vya shetani
wanatumia jina langu kuwafungia maisha yao na kuwalaani waumini na waumini
wakifikiria wamebarikiwa. Nenda waeleze na ulitetee jina langu watu waujue
ukweli mimi YESU muda wangu wa kurudi umeshafika ila ni saa na muda na siku
ndiyo haijulikani ila nakueleza HEBRON uelewe na ndivyo BABA yangu mbinguni
alivyoniambia ila siku na muda hayo yapo katika siri yake peke yake MUNGU.
Napenda kuwajulisha watu wote wa
mataifa yote kuwa sadaka yeyote ni ibada kati yako na MUNGU na siyo mwanadamu
hata mtumishi. Sadaka ni kitu maalum cha kuheshimiwa na ikiwa inawekwa katika
chombo chake maalum. Sasa sadaka inapotolewa na watu ikawekwa katika miguu ya
mtumishi yeyote yule sadaka yake inakuwa siyo ibada tena, bali baraka zako
kupitia ile sadaka uliyoitoa zinakanyagiwa chini na huyo mtumishi asiye
muheshimu YESU, na sadaka inapokanyagiwa chini madhara yake uchumi wako wote
unaenda kwake yeye na hivyo kwa njia hiyo unajifungia maisha yako wewe peke
yako na siri hii anaijua huyo mtumishi ambaye yeye anakanyagia sadaka kwa miguu
yake na watu wanapanga mstari kumuwekea katika miguu. Hiyo ni njia ya shetani
ambayo anawatumia watumishi ambao ndani yao analo agano nao la kufanya kazi na
mapepo. Watu wengi maisha yao yameharibika hata wanajishangaa imekuaje ,
nakukumbusha kumbuka ni wapi ulipo toa sadaka ukaitupa katika miguu ya mtumishi
yeyote yule.
Nikuulize swali ndugu msomaji
wa makala ya Mtume na Nabii Hebron Kisamo, hivi baraka zinatolewa kwa kutumia
miguu au mkono? Je umeshawahi kuona mtumishi anaenda kanisani halafu anawaeleza watu Neema ya
MUNGU iwe juu yenu akitumia miguu kama ishara badala ya kuwanyooshea
mikono?
Jibu unalo, siyo miguu
inayotumika ni mikono, sasa wewe kwa
nini unaweka sadaka katika miguu ya mtumishi? Je itakubariki? Jibu hapana. Kila
aliyeshiriki na anayeshiriki bado uelewe hapo amemalizwa kiroho na kiuchumi na
watumishi wa jinsi hiyo wanawaibia watu vitu vyao katika ulimwengu wa roho
wanaviiba na wao ndiyo wanaendelea halafu wewe uliyetoa pesa miguuni maisha yako yanayumba.
Niajabu sana nilipokuwa naongea
na YESU kuhusu jambo hili la kukanyagia sadaka aliniambia hivi, Hebron hata
mimi sijawahi kukanyagia sadaka za watu kipindi kile wala kutupiwa katika miguu
yangu. Wala watumishi wangu hawajafanya
hayo na wewe Hebron mtume wangu ufuate
njia yangu kama kina Petro uwaokoe watu katika elimu ya shetani na kuwaleta
kwangu wale watakao kubali na kutii.
Ila wale watakao kataa wewe
utakuwa umeimaliza kazi, hawataweza na kujitetea ile siku ya mwisho. Watu wa
jinsi hiyo walikuwepogo hata katika kipindi changu hata sasa watakuwepo tu, ila
wale walio wangu watakusikiliza na watapona roho zao. Jambo lingine sadaka
inatolewa halafu labda ni Nabii au mtumishi yeyote anazikanyagia madhabahuni
eti anaziombea, nawaeleza maombi hayo katika ulimwengu wa roho ni kinyume na
akili zenu zinakanyagiwa mnakuwa watumwa wa mtumishi wa jinsi hiyo na shetani anafurahia sababu
amewaweza watu nao wakatii upumbavu.
Soma katika biblia hakuna
mahali sadaka zimetupwa mguuni wala kukanyagwa, ila zinawekwa katika chombo
kisha zinakabidhiwa MUNGU, ila unapoona zinatiwa katika miguu na kukunyagiwa
pale lile tendo lina maana shetani anakabidhiwa na kuwafunga watu, leo furahia
sababu umepona na zaidi uje ufunguliwe na YESU WA NAZARETI na imetosha kujua
kabisa huyo ni mtumishi aliyemsaliti YESU 100%.
Na wengine wanawaeleza
waumini walete pesa zao halafu eti unazitandika chini wewe
muumini unazikanyaga halafu yeye anakuombea, yaani tendo hilo lina maana wewe
peke yako kwa hiari yako umeamua kumpa baraka zako shetani ziende kwa huyo
mtumishi. Tazama maisha yako enyi mlioshiriki kutoa pesa miguuni na
kukanyagiwa. Je sasa si ufahamu umefunguka, mwambie asante YESU, walikufunga na
wewe pasipo kujua ukatii, YESU anakupenda siyo yeye aliyeyaagiza hayo. YESU
yeye alifutwa miguu na yule mwanamke kwa nywele zake lakini yeye hakutupa
sadaka miguuni. Zaidi ingia katika
website ya w.w.w.prophethebron.org ingia katika link ya blog yapo masomo mengi
yatakusaidia. Watumie na wengine ujumbe huu utakuwa umefanya kazi ya YESU na
utapokea taji siku ile ya mwisho.
Mkristo usikubali kuwa
mpumbavu, sasa wakatae kabisa watu wa jinsi hiyo hao tayari ni adui na mwenyezi
MUNGU na ni adui wa Nabii Issa( YESU )
ila hao ni marafiki wa shetani kupitia mpinga kristo .( utawajuaje , kwa
matendo yao).
Sema BWANA YESU naomba
unisamehe dhambi zangu zote ikiwamo ya kupeleka sadaka zangu katika miguu ya
watumishi walio kinyume na wewe, uniokoe unirejeshee uchumi wangu, vitu vyangu,
uwanyang’anye sasa, uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele.
Usiniache YESU uniongoze wewe unishike mikono yangu mimi ni wako. Amen
NABII HEBRON.