Pages

Tuesday, May 5, 2015
















JE UNAJUA MAANA YA KUPELEKA UDONGO KWA WATUMISHI WAKAUOMBEE?

BWANA YESU WA NAZARETI  ASIFIWE. Nitaelezea katika somo hili kuhusu ibada ya kuombea udongo ambao unapelekwaga kanisani, katika sehemu baadhi watumishi wanaagiza waumini waulete wa sehemu anayoishi au wa nyumbani kwake halafu auombee kisha uurudishe nyumbani uuweke akishauombea.

Watoto wa MUNGU wa nchi zote, sasa hivi mambo yameharibika kwa kiasi kikubwa katika kanisa hasa kwa kupitia wale watumishi ambao wameamua kumtumikia shetani  ila wamejificha kwa jina la kivuli cha kanisa na kutumia jina la YESU na hata kuwanajisi watumishi wengine ambao wanampenda MUNGU wakafuata mapokeo yao na kufanya na wao wapotee pasipo kujua au kupenda. Ila wa kupona atapona tuu na wajehanamu atabakiwa hivyo.

Hii hata mimi Hebron sikujuaga sababu hata mimi nilishapelekaga ila aliponifungua YESU katika eneo hilo niliogopa sana sababu ya mambo niliyofanyiwa kupitia udongo nilioupeleka kwenye kanisa fulani nilikuta maisha yangu yamebakia kwa mchungaji huyo na zaidi katika nyumba hiyo aliimiliki kama yake katika ulimwengu wa kiroho na zaidi kupitia udongo aliouombea kwa njia zake za kipepo pasipo kujua mimi alikuwa anatuma mapepo yake yajue vitu vyangu ninafanya nini na alipotaka pesa nikimnyima aliweza kuharibu sababu mapepo yalikuwa yananjia ya kuja katika vitu vyangu kwa sababu ni kupitia ule udongo, na mengi.

Hivyo ikiwa ulipeleka udongo uelewe hayo yanakuhusu kama MUNGU anatulinda yeye hutulinda kupitia damu ya YESU na siyo kupitia udongo ila kwa udongo  anakuunganisha na kuzimu na zaidi zile baraka zako ya kuwa MUNGU atakubariki ardhi yako zitakuwa hazipo tena umezipeleka pasipo kujua, ila hao wanaofanyia watoto wa MUNGU wanajua wanachokifanya.

Amenituma YESU WA NAZARETI usidanganyike tena, baraka zako hubarikiwa kupitia sadaka zako, katika madhabahu yenye MUNGU wa kweli isiyo ya michango, harambee na ufisadi. Ukipeleka tu udongo mahali pa jinsi hiyo wewe mwenyewe umekwisha ujue ukweli hapo ni hatari kwako kiroho na kimwili, ndio sababu nyumba hazina baraka, mambo hayaendi, vifungo hata katika mazao, mifugo,nyumbani hapakaliki ni nuksi, balaa, mikosi kwa sababu mapepo yanaishi kwa ajili ya uhalali wa udongo ulioupeleka.

Sema asante YESU WA NAZARETI naomba uniokoe uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima, unirejeshee vitu vyangu vilivyoibiwa na hao unaowajua YESU kupitia udongo nilioupeleka , usiwaache YESU. Nakupenda. Amen.

Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, utaombewa , utafunguliwa na kuwa huru. YESU anakupenda wewe ni wa thamani kwake usimkatae YESU ila mkatae shetani.
Amen.

NABII  HEBRON.