Pages

Thursday, April 30, 2015















TOFAUTI KATI YA ROHO MTAKATIFU NA ROHO MCHAFU.

a) NINI MAANA YA ROHO MTAKATIFU?

b)NINI MAANA YA ROHO MCHAFU?

ROHO MTAKATIFU ni nafsi moja wapo ya MUNGU ambazo ni tatu na wana umoja MUNGU BABA, MWANA NA ROHO MTAKATIFU na roho mchafu na yeye ni roho wa shetani ambaye anaye umoja wake akiwemo Joka Kuu, Lusifa na Maxwell. ROHO MTAKATIFU ndiye kiongozi wa kusimamia neno la MUNGU na kuwaongoza watu njia ya mbinguni sababu yeye ndiye anayeijua. Ukisoma katika kitabu cha Matendo ya Mitume 1: 7-9 inaelezea ahadi aliyowaeleza wanafunzi wake kuwa atawatumia ROHO MTAKATIFU, yeye atawaongoza na ahadi hiyo ilitimia. Ukisoma katika kitabu cha Matendo 2:1-4 inaelezea vizuri.

Sasa nachotaka kuelezea kwa undani zaidi ni kuhusu roho mchafu au anaitwa roho wa bandia sababu kanisa halikupewa roho mchafu awaongoze watu ila kwa sehemu kubwa katika nchi mbali mbali roho huyu mchafu amejificha makanisani akitumia jina la ROHO MTAKATIFU pasipo watu kuelewa, ila katika ulimwengu wa roho anaonekana ni roho mchafu ndiye anayesimamia matendo ya shetani yaimarishwe katika ulimwengu huu na ROHO MTAKATIFU yeye akiwa anafukuzwa na wanadamu.

Ninapo sema kumfukuza ROHO MTAKATIFU ni pale unapokuta au kuona wakristo wanamwabudu YESU lakini wanaabudu sanamu, au wanabatizwa kwa ubatizo ambao haujatoka mbinguni (yaani ubatizo bandia). Inapokuwa kinyume tu uelewe ROHO MTAKATIFU hayupo hapo sababu angekuwepo yeye angeyasimamia yale MUNGU anayoyataka na siyo kubadilisha biblia na kuchanganya na uwongo. Watu wengi hawaelewi siri hii yawezekana hata ni watumishi wanampenda MUNGU kutoka katika mioyo yao ila wamepigwa upofu, hawaongozwi na ROHO MTAKATIFU bali ni roho mchafu ila wanamwita ni ROHO MTAKATIFU.

Sasa cha kujua wewe chunguza matendo ya kazi hiyo ya huyo mtu hapo ndipo utaweza tofautisha ROHO MTAKATIFU ni yupi na roho mchafu ni yupi na anatendaje kazi kwa sababu roho hauwezi ukamwona kwa macho yako japo wapo wengine wamepotea wakampa njiwa ndiwe anaitwa ROHO MTAKATIFU, nawaeleza mtubu ili mpone. ROHO MTAKATIFU siyo mnyama au njiwa haya yamefichwa katika siri za mbinguni na dunia haijui. Jambo la kujiuliza je ROHO MTAKATIFU alitumwa afanye nini? Alitumwa asimamie kazi ya MUNGU na awaongoze watumishi pamoja na kanisa la MUNGU kwa kufwata njia alizozianzisha YESU na kuhakikisha neno linafuatwa kama lilivyo ili watu wasipotee na kuangamia.

Sasa shetani na yeye akatuma roho wake kwa makanisa kupitia viongozi, akajaa ndani yao wakaacha kuifuata biblia isemavyo na kuifuata kweli katika mambo mbali mbali. Na unapoona katika ukristo upo tifauti na ahadi za biblia uelewe kiongozi ambaye ndiye ROHO MTAKATIFU hayupo ila yupo kiongozi mchafu anatenda kazi yake. Anaitwa mchafu kwa sababu yale aliyoyaingiza katika kanisa ni machafu na watu wakiyafuata nao wanakuwa wameongozwa na roho mchafu na roho huyo mchafu atawapeleka katika ule umoja wa shetani pale utakapomaliza safari ya maisha yako hapa ulimwenguni. Roho mchafu kazi yake ni kuwateka watu nafsi zao na kuwalisha chakula cha mauti ambacho ndicho neno la bandia. Mfano wa mambo ya kazi za roho mchafu japo huko makanisani yakifanyika kimwili anatajwa ROHO MTAKATIFU inakuwa ni upofu watu wamepigwa kwa sababu katika ulimwengu wa roho ni roho mchafu au bandia ndio anayesimamia tendo hilo.

Mfano wewe unajua ubatizo aliouleta MUNGU ni ule wa Yohana na YESU alibatizwa hivyo hivyo na baada ya YESU kubatizwa ROHO MTAKATIFU ikasikika sauti yake. Hii ina maana roho yule mtakatifu alikuwa anasimamia ubatizo wa MUNGU katika ulimwengu wa roho kwa sababu yeye yupo kusimamia kusudi la MUNGU tu.

ZIFUATAZO NI KAZI ZA ROHO MCHAFU:

1.     Ubatizo wa kikombe, wa kisima, wa kubatizwa kwa majina ya wachungaji. Kubatizwa kwenye drum na nyinginezo zote tofauti na ubatizo wa maji mengi yanayotembea.

2.     Ibada za sanamu, kanisa kufanya biashara.

3.     Michango makanisani, kutoa huduma za kiroho kwa kuchaji pesa.

4.     Watumishi wa mishahara, ibada za wafu.

5.     Wakristo kuzuiliwa kuokoka, kubariki pombe.

6.     Sadaka kujazwa fomu umetoa kiasi gani na kusomewa wale waliotoa sadaka.

7.     Sadaka kutolewa na kutupwa katika miguu ya mtumishi na akaanza kuzikanyaga na kuziombea ( anawakanyagia uchumi wenu uende kwake ili mfilisike, analo pepo mchafu.


NOTE:

Ndugu msomaji wa makala ya Nabii na Mtume Hebron zaidi endelea kuyasoma makala haya na vitabu nilivyoviandika utafunguliwa mengi na uwajulishe na wengine, hata mimi sikuyajua haya ni pale alipotaka YESU mwenyewe akanifundisha nikaifanye kazi yake na kusema ukweli. Sababu kanisa la sasa asilimia kubwa zaidi limepotea haliongozwi tena na ROHO MTAKATIFU bali ni roho mchafu. Nimekujulisha machache wewe yachunguze utapata jibu. Na umshukuru YESU kwa sababu sasa hivi ROHO MTAKATIFU atakutia nguvu umjue yeye na umkatae roho mchafu aliyekushirikisha mambo yake ya bandia kama nilivyoyaelezea japo yapo mengi.

Nikuulize swali YESU alianzisha huduma ngapi? Jibu tano. Je, kama huduma ya uaskofu haikuanzishwa na YESU, je ROHO MTAKATIFU ataisimamia? Hataisimamia bali roho mchafu ataongoza. MUNGU amekataa watu waisabudu sanamu, sasa wakristo wanaoabudu sanamu na wanamtaja ROHO MTAKATIFU, je ni ROHO MTAKATIFU ndiye anayesimamia hayo mambo ya bandia? Jibu siyo, ila kibinadamu mmedanganyika anapotajwa ROHO MTAKATIFU ila katika ulimwenguni wa roho ni roho mchafu. Nitatoa mfano ili mtu aitwe mlevi ni lazima awe anakuywa pombe, au ili mtu mwongo ili aitwe mwongo ni lazima aseme uwongo na ndipo ataitwa yeye  ni mwongo. Hivyo hivyo na kanisa linapofuata mambo ya bandia halafu wakamtaja ROHO MTAKATIFU haiwezekani ikawa sawa  sawa sababu lile tendo ni cheo cha roho mchafu.

Haya sasa ni wakati wako enyi mataifa yote umjue ROHO MTAKATIFU na pia uelewe  sababu ya wewe kuteseka ni sababu hayupo msaidizi akuombeaye katika ulimwengu wa roho, nafasi hiyo inachukuliwa na roho mchafu kazi yake yeye ni kuangamiza na kuziongoza nafsi za watu zielekee jehanamu pasipo wanadamu baadhi yao kuelewa. Amenituma YESU niwaeleze mataifa yote mrejeeni YESU. ROHO MTAKATIFU hana nafasi kubwa ila roho mchafu yeye anayo nafasi kubwa zaidi anawaongoza watu. Na uelewe pia roho mchafu huyu na yeye anayo siku yake ya pentekoste vile vile na mahali anapopatikana ni katika makanisa au kwa watumishi waliomuasi MUNGU, freemason, wenye kufwata mapokeo bandia. Mfano usitegemee kabisa ROHO MTAKATIFU atashuka kwa kanisa au mtumishi ambaye anayebatiza watu kwa ubatizo ambao siyo wa Yohana bali unatumika ubatizo bandia.

Kanisa linalochangisha pesa katika nyumba ya sala

Kanisa lenye benki.

Kanisa linalofanya mazingambwe, kumwabudu mchungaji yeye ndiye MUNGU na wengine hujiita wao ni YESU.

Kubatiza watoto wadogo na kuwabariki wakiwa watu wazima tofauti na YESU alivyofanywa.

Yapo mengi sana, hata mimi Hebron sikuyajuaga na niliabudu kwa miaka mingi katika makanisa yaliyoongozwa na roho mchafu ila sasa namshukuru YESU aliyeniokoa na wewe anakupenda uokoke na uongozwe na ROHO MTAKATIFU na utoke katika sehemu hizo, madhara yake unapoendelea kuabudu katika eneo hilo uelewe bado roho mchafu atakushikilia kwa sababu ni roho yake ipo katika madhabahu hiyo au ndani ya mtumishi na madhara yake utazidi kujazwa roho mchafu japo wewe haujui. Hii ni siri iliyofichika sana na wengi wameshikiliwa hapo.

Sema BWANA YESU naomba uniokoe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima uniondolee roho mchafu na mambo yake aingie ROHO MTAKATIFU wako sasa aniongoze siku zote za maisha yangu. Amen.

NABII HEBRON.