SADAKA ZA
MAZISHI HAZIPASWI KUTUMIKA NA KANISA AU WATUMISHI NI ZA WAFIWA, HIYO NI POLE
KUTOKA KWA MUNGU.
KANISA
LINAPOCHUKUA SADAKA YA IBADA YA MAZISHI LINAKUWA LIPO KINYUME NA NENO LA MUNGU
LIA NA WANAOLIA.
SADAKA HIZO
NI HAKI YA WALIOFIWA KUTOKA KWA MUNGU.
Yohana 11:33-35
BWANA YESU ASIFIWE, natumaini baadhi ya watu watafikiri
Nabii Hebron amechanganyikiwa sababu mtaliona ni jambo jipya na kumbe siyo
jipya ila shetani aliwafunga watu ufahamu wasielewe bali wapo wanaoelewa siyo
sahihi kanisa au mtumishi achukue pesa za sadaka za mazishi. YESU aliposema lia
na wanaolia, wafarijini, watieni moyo, alikuwa anaongelea katika mazishi hata
YESU mwenyewe alipoelezwa Lazaro amefariki na akawaona Martha na ndugu zake
wakilia na YESU alilia katika ule msiba japo alimfufua Lazaro. MUNGU ameibiwa
haki yake ya kuwatia moyo wafiwa na ikabakia wanadamu tu ndio wanawatia moyo
wafiwa, nitaelezea uelewe.
MUNGU ndiye mfariji wa wafiwa kwanza kwa kupitia neno lake
kama alivyosema YESU lia na wanaolia. Hii ina maana kuwa; kwanza MUNGU anawatia
nguvu wale wafiwa na pili pole nyingine ni zile sadaka zinazotolewa katika
ibada ya mazishi, zile zinatakiwa kuachwa kwa wafiwa na siyo zipelekwe kanisani
hata siku moja. Ila watu hawaelewi, amenituma YESU nikaeleze yale yote
anayoyataka yeye yafuatwe sababu shetani aliyapindua pindua na kumwibia MUNGU
nafasi moja wapo ya kuwafariji wafiwa. Na mimi na kanisa langu ndivyo
tunavyofanyaga katika mazishi, pesa hizo wanapewa wafiwa na wanahesabu wenyewe
hizo ni zao kutoka kwa MUNGU.
Japo limekuwa na upinzani kwa baadhi ya
wachungaji katika maeneo tuliyoenda kuzika katika vijiji vyao walichukia sana
sababu pesa tulikataa zipelekwe makanisani bali wapewe wafiwa, cha ajabu maelfu
ya watu walifurahia jambo hili cha ajabu wachungaji wa mahali fulani walikuja
kuzidai hizo sadaka bila aibu mbele za watu na tuliwanyima sababu siyo mpango
wa MUNGU sadaka za wafiwa zichukuliwe kanisani hiyo ni pole ya kutoka mbinguni.
Dini zimeacha kulia na wafiwa badala yake zinachukua ile
pole ambayo MUNGU anataka ibakie kwa wafiwa, hiyo ndiyo maana ya lia na
wanaolia, siyo kuchukua pesa za msiba, na cha ajabu watumishi baadhi yao
hufurahia sana panapokuwa na msiba wa watu maarufu au tajiri kwa sababu wanajua
watakuja watu wengi na wenye uwezo hivyo sadaka itakuwa ni nyingi na ndio
sababu hata ukiangalia kibinadamu je umeshawahi kuona maskini akienda kuzikwa
na viongozi wakubwa wa dini? Jibu unalo. Hii ni kwa sababu katika mazishi hayo
itapatikana sadaka nyingi na wataichukua.
Sasa MUNGU anachukia sana kuhusu
kitendo hiki ni cha kumwibia MUNGU sehemu yake ya kuwafariji wafiwa. Sasa wacha,
utakayeendelea shauri lako, sasa umeshaujua ukweli hiyo ni dhambi kubwa sana na
kwa tendo hilo wanaofanya hivyo wanafanya MUNGU siyo MUNGU wa wajane na madhara
yake hao wafiwa wasipopewa hiyo sadaka shetani anapata nafasi ya kuitesa hiyo
familia na kufanya MUNGU asiwe ni MUNGU kwao kwa wajane hao au wafiwa hao na
ndiyo sababu familia nyingi zilizofiwa zimebakia yatima mpaka leo ni kwa sababu
tuu ya pesa iliyotolewa katika ibada ya kuuhifadhi mwili ikachukuliwa na kanisa
au watumishi.
YESU alipokuwa anaenda katika misiba yeye hakuchukua pesa,
aliwatia moyo na aliwafufua. Alipofufua ile ni ibada aliifanya kaburini,
akafufua tu lakini yeye hakuchukua chochote kutoka kwa wafiwa. Sasa kama yeye ndiye
kiongozi wa kanisa yeye hajachukua, je hao
wanaochukua wapo chini ya YESU yupi? Hata mimi Hebron sikuyajua hayo ni
mpaka aliponifundisha kabla ya kuanza kazi yake na sijachukua pesa hizo tokea
nianzishe huduma yake kama alivyonituma. Ila cha ajabu nashangaa hata baadhi za
familia tulipomaliza ibada ya mazishi nikatangaza pesa hizo zibakie kwa wafiwa kwa sababu YESU
ndiye anayelia nao na kwa njia hiyo MUNGU na yeye anawapa pole pia baadhi ya
hata wazazi waliwanyang’anya hizo pesa nikaletewa mashtaka, nikaingilia na
nikawaeleza mtapigwa na MUNGU hiyo siyo haki yako wala siyo ya kanisa,
walielewa na walirudisha na wakapokea amani na kusamehewa hiyo dhambi.
Mtumishi usiyeyajua haya sasa uyaelewe na uwatumie na wengine
mataifa yote kwa sababu mgeujua ukweli msingeyafanya haya , ila wapo baadhi
wanafurahia kuchukua pesa hizo na hawataki kuacha. Mimi ninafikisha ujumbe
utakayekaza shingo mimi hayanihusu, utapambana na MUNGU wa wajane na hiyo ni
laana na ni uwizi. Jambo hili ni katika ulimwengu wote myajue haya. Sadaka ya
mazishi ile haitakiwi itumike mahali popote zaidi, ni ya wafiwa peke yake. YESU
analia na wanaolia na kuwapa pole. Hivi nikuulize sadaka ni za nani? Ni za
MUNGU na yeye ndiye azipangiaye kazi, na
kazi ya sadaka ya misiba hizi zote ni pole ya wafiwa.
Jiulize ni sadaka ngapi
za wafiwa zimeliwa miaka yote, katika nchi zote? Je hizo familia ni ngapi
ambazo MUNGU amezuiliwa kuwa MUNGU wa wajane hao? Shetani aliwapiga watu upofu
miaka mingi na makanisa yakafuata ili kumzuia MUNGU asiwe MUNGU wa wajane na
inapochukuliwa sadaka hiyo tu shetani humwekea MUNGU mashtaka sadaka zako
wamezichukua hivyo hauna uhalali wa kuwa MUNGU wa wajane kuwatunza na
kuwafariji. Ni mahali pangu shetani pa kuwatesa hizo familia na MUNGU ni wa
haki, analiangalia neno lake. Je mnapenda MUNGU awe ni MUNGU wa wajane kwa
wafiwa? Jibu ndiyo, basi msikubali sadaka zichukuliwe tena bali zibakie kwa
wafiwa.
NOTE:
Cha ajabu kitatokea endapo sadaka za mazishi hazitachukuliwa
na kanisa tena baadhi ya watumishi hawatafurahia tena kuzika watu kwa sababu
pesa hamna tena. Hapo ndipo mwenye akili na ajue na atafakari. Ulimwengu ulitekwa
na shetani pamoja na kanisa, kama kanisa linachukua pesa za mazishi je hauoni
siyo elimu ya MUNGU na hata biblia inasema usifanyie mabaya, usimnyanganye
yatima wa MUNGU utapigwa na MUNGU! Watumishi wengi wanayo hiyo dhambi tubu sasa
kwa sababu ulikuwa haujui, uliyapokea mapokeo ya wanadamu. Tafuta katika biblia
hakuna mazishi yoyote ambayo pesa ya sadaka ilipokelewa kanisani au kuchukuliwa
na watumishi. Sasa hii elimu inatokea wapi? Kwa mpinga kristo.
Sema BWANA YESU WA NAZARETI wewe uliye ndiye njia ya kweli
na uzima naomba rehema, unisamehe dhambi zangu. Asante kwa kunifungua ufahamu kuhusu
sadaka za mazishi. Sitashiriki tena kuchukua au kudai sadaka za wafiwa,
uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima. Uniongoze wewe unavyotaka
na siyo vinginevyo. Amen.
Zaidi ingia katika website yangu www,prophethebron.org ingia
katika link ya blog na YouTube utajifunza mengi, utakuwa huru. Ubarikiwe. Ni kujilaani
unapochukua sadaka za ibada ya mazishi iwe ni kanisa au mtu yeyote yule, hizo
ni pesa za wafiwa, baada ya ibada zikusanywe wapewe wafiwa na wahesabu wenyewe
na wazipangie matumizi yao wenyewe bila hata kuangaliwa na yeyote. Huo ndio
mpango wa YESU. YESU ainuliwe juu shetani akanyagiwe chini milele.
NABII HEBRON.