JE UNAJUA NI YOHANA MBATIZAJI WA KUZIMU NDIYE ALIYEZILETA AINA NYINGINE TOFAUTI ZA UBATIZO; TOFAUTI NA UBATIZO ALIOBATIZWA YESU WA NAZARETI?
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE! Kabla mada hii nitaelezea
ulimwengu kuhusu Ubatizo wa Yohana mbatizaji wa kuzimu. Wengi mtashangaa sana
kuwa yupo mbatizaji wa kuzimu anayeitwa Yohana vile vile. Aliponiita YESU
nikamtumikie mimi Nabii Hebron nilikuwa sijui lolote na nilimwambia YESU sasa
unanituma kwa ulimwengu wote nikaukomboe mimi sijui lolote; hata neno lako
silijui. Akanitia moyo Hebron nayajua hayo, mimi nilishakuandaa kabla ya wewe
kuzaliwa na nikajua ikifika wakati wake nitakutumia tu na wakati ndiyo sasa. Nitakufundisha,
nitakuongoza na nitatembea na wewe kila mahali niifanye kazi yangu kupitia
mwili wako. Ni mambo mengi sana ila naelezea kwa ufupi tu hapa, ila zaidi ingia
katika website yangu www.prophethebron.org
ingia katika link ya YouTube na blog, utasoma mengi baadhi niliyoelezea kutoka
kwa YESU WA NAZARETI.
YESU aliniambia nenda kwa mataifa yote uwaeleze habari zangu
na uwaeleze watu wote wabatizwe ubatizo niliobatizwa mimi ndiyo uliotoka kwa
MUNGU na kama mtu asipobatizwa kama mimi yeye hatafika mbinguni sababu MUNGU
alishaandaa njia yake, akamtuma Yohana mbatizaji kutoka mbinguni na hata katika
kitabu kitakatifu inaonyesha wazi wazi na katika kitabu cha Ufunuo wa Yohana
22: 18-19; imeandikwa atakaye yaongeza au kuyapunguza maneno ya unabii wa
kitabu hiki atahukumiwa. Ina maana MUNGU aliuhakikisha ubatizo wa maji mengi
akaupiga mhuri ndio utumike, sasa kwa sasa idadi kubwa ya wakristo
hawajabatizwa kwa ubatizo alioupigia mhuri MUNGU kuwa ndio utumike bali watu
wamebatizwa kwa ubatizo ambao haupo, MUNGU hajapitisha na watu hupigwa upofu
wakifikiria wanabatizwa kwa ubatizo ambao MUNGU kauleta kumbe wanabatizwa kwa
ubatizo uliotoka kuzimu na wanapobatizwa ubatizo huo unakuwa umewafungia watu
wasiwe wakristo wa kweli na wasije wakaenda mbinguni.
Kama nilivyoelezea katika mafundisho ya Nabii Hebron
nilivyofundishwa na YESU aliponifundisha habari hii niliogopa sana kwa sababu
niliangalia katika ulimwengu huu kwa haraka nikapiga mahesabu nikaona kama
angekuja sasa hivi YESU katika unyakuo kwa kweli mabilioni ya wakristo
wasingeenda mbinguni kwa sababu kubwa hawajabatizwa kwa ubatizo alioupiga MUNGU
mhuri ufwatwe. Akaniambia, uwaeleze haya kwa sababu wengi hawaujui ukweli
wanapotoshwa na watakaoyasikiliza maneno haya na kubatizwa upya watapona. Hivyo
nawsihi sasa mkabatizwe, neema ya YESU ipo bado na inawasubiri, ila msichelewe
neema ikaondoka tena.
Akaniambia Hebron, MUNGU alileta ubatizo wa maji mengi
akamtuma Yohana kutoka mbinguni na yeye akazaliwa akaonyesha njia na mimi mwana
wa MUNGU nikaifwata nikabatizwa pale katika mto Yordani. Baada ya shetani kuona
MUNGU anatengeneza agano lake kati yake na wanadamu kwa njia ya ubatizo wa maji
mengi, joka kuu na yeye akamtengeneza Yohana wake wa ubatizaji na yeye akamtuma
aje ulimwenguni kwa njia ya roho mchafu na mpinga kristo; wakaingia katika
makanisa ambayo siyo yangu mimi YESU hata
kama wanalitaka jina langu. Elewa pia yupo yesu wa uwongo huko kwenye
elimu ya uwongo, sipo mahali pangu ni mahali
pa yesu wa uwongo. Wakaanzisha na wao ubatizo tofauti na mimi YESU
nilivyobatizwa, ule ubatizo uliotoka mbinguni, na watu wakaipokea pasipokujua
na wengine kwa kujua kabisa kuwa ni uovu kabisa. Na sasa hata mataifa
wanampenda YESU lakini wameongozwa katika ubatizo ambao haujatoka kwa BABA
yangu, haya ni maneno ya YESU aliyesema na mimi ninayaelezea hivyo hivyo na
alieleza kwa sauti ya ukali sana.
Akanionyesha kitengo cha kubatiza cha kuzimu na nikamuona
Yohana mbatizaji wa kuzimu na kazi zake, akaniambia YESU huyo ndiye anayeleta
ubatizo tofauti na ule ubatizo niliobatizwa mimi na wanadamu wakaupokea na
kuingia agano na shetani pasipo kupenda au kujua . Niliwatuma watumishi niliowaita kabla yako wakaseme
habari hizi ili watu wapone nao wengi wao wamenisaliti sasa hivi na mimi
nimewaacha na sasa wameamua kuwa ni wachawi na wakawa wanapewa nguvu na shetani
ambaye ndiye baba yao. Sasa wamekuwa wanyanganyi na hata kuwaua kiroho
watumishi wa kweli wasikue kiroho. Ila sasa nipo na wewe Hebron uipeleke injili
yangu kama nitakavyo mimi YESU; karibu narudi kwa unyakuo na sina watu wengi,
ni 2% ya watu wote katika ulimwengu huu nyingine yote ni ya shetani amewateka.
AINA
ZA UBATIZO AMBAZO NI ZA YOHANA MBATIZAJI WA KUZIMU
1.
Ubatizo wa maji ya kikombe.
2.
Ubatizo wa maji ya kisima.
3.
Ubatizo wa kubatizwa ukiwa mtoto mdogo.
4.
Ubatizo wa kubatizwa kwa maji mengi ila
unabatizwa kwa jina la mchungaji, iwe ni ubatizo wa kisima au maji yanayotembea,
ubatizo huo ni wa Yohana mbatizaji wa kuzimu.
5.
Kubatizwa kwa mavumbi.
NOTE:
Zipo na nyinginezo ambazo sijaziandika ila nitaendelea
kuelezea vizuri zaidi ili watu mpone roho zenu msije mkalia na kusaga meno mkijuta
laiti ningeliaga wakati ni sasa umeujua ukweli. Hizi batizo zote tofauti na ule
wa YESU ambao ndio uliopigwa mhuri na MUNGU mwenyewe tubatizwe watu wote. Sasa shetani
akaleta wa kwake ambao haupo katika biblia kupitia Yohana wake wa kuzimu ili
aingie agano na wanadamu wawe ni wafuasi wa yesu wa uongo na wasije wakaenda
mbinguni ila waende kuzimu ambapo ndipo lilipo agano la batizo hizo.
Kama hujabatizwa kama
YESU uelewe haujaingia agano la kupigwa mhuri na MUNGU ili uende kwake. Hata kibinadamu
soma biblia katika kitabu chote hautaona hizo ubatizo zimeletwa na Yohana
mbatizaji wa mbinguni. Na kama hazijaletwa basi wacha ubishi ukabatizwe upya
ili uende mbinguni kinyume na hapo ukweli ni siku ya mwisho hata kama
ulishakufa watakuwepo malaika wa MUNGU na malaika wa shetani wakiangalia mihuri
yao ya ubatizo. Je wewe utakuwa na mhuri wa ubatizo wa mbinguni au wa ubatizo
wa kuzimu? Jibu unalo.
Wakati ndio sasa ufanye uamuzi ukabatizwe na utoke
katika batizo za jinsi hiyo inakuonyesha wazi wazi kabisa hapo hayupo YESU wa
kweli yupo yesu wa uwongo ndio sababu wamewekewa mhuri wa ubatizo wa kuzimu
kutoka kwa Yohana wa kuzimu. Na unapoupokea unakuwa unafanyika ni mfuasi wa
yesu wa uwongo bila kujua na hiyo ni dalili kuwa basi hata katika maisha yako
wewe ulikuwa unamwabudu yesu wa uwongo pamoja na sadaka zako zote ulimpa yesu
wa uwongo. Ipo neema ya MUNGU.
Sema BWANA YESU WA NAZARETI wewe uliye ndiye njia ya kweli
na uzima naomba rehema, unisamehe dhambi zangu. Sikujua au nilijua nikakubali
kubatizwa ubatizo wa Yohana mbatizaji wa kuzimu pasipokujua. Siutaki tena,
uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima. Uniongoze nikabatizwe kama
wewe unavyotaka na siyo vinginevyo. Amen.
Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE ukabatizwe, uwekwe huru na utafunguliwa vifungo vyote na kutolewa
laana ya ukristo wa uwongo na mihuri ya Yohana wa kuzimu.
NABII HEBRON.