Pages

Thursday, April 2, 2015

ZIJUE TOFAUTI KATI YA MAMA MARIA WA MBINGUNI NA MAMA MARIA WA KUZIMU.

BWANA YESU ASIFIWE! YESU WA NAZARETI. Wengi watashangaa huyu Nabii Hebron anasema nini, lakini ukweli ndio kuwa yupo Mama Maria aliyemzaa YESU WA NAZARETI wa kweli na yupo pia Mama Maria aliyemzaa yesu wa uongo vile vile. Ila tofauti iliyopo Mama Maria aliyopo mbinguni  yeye ndiye kamzaa YESU wa kweli na yeye yupo mbinguni. 2014 niliongea na yeye, kwa kweli namshukuru MUNGU kwa kunipa kibali akasema na mimi, yeye aliyemzaa YESU. Aliongea na mimi katika habari ya kunitia moyo hadi machozi yalinitoka kwa yale aliyoniambia ambayo nitayataja machache.

Aliniambia iendeleze kazi aliyokuelekeza YESU. Kipindi kile tulipokuwepo Uyahudini walimtenda mabaya sana, walimtemea mate mwanangu na kumtukana matusi ya ajabu lakini yeye hakutikisika, aliangalia kusudi la BABA tu. Na wewe sasa upo hapa ulimwenguni yeye yupo mbinguni, atakuja ule mwisho katika unyakuo. Tazama aliwaita watumishi na baadhi yao wengi wamemsaliti. Umeinuliwa sasa wewe na kupewa maagizo kuhusu kazi ya MUNGU, songa mbele. Akaniambia mengine, mwanangu Hebron, mimi siyo MUNGU ni mwanadamu tu kama wewe au hao walioumbwa na MUNGU, je kwa nini waniabudu mimi? Tazama hata mimi ninamsujudu MUNGU vile vile. Waeleze watu wamepotea na wasipoacha wataangamia na hata wanaoniabudu tayari wameshaangamia ila ipo neema sababu wengi hawajui wanafuata mkumbo wa shetani, akasema kwa sauti ya uchungu ambayo hadi leo sauti hiyo haijaishaga ndani ya moyo wangu, nikarudi duniani na nikawaeleza watu wote wa mataifa yote ili wapone.

Nikabakia nina maswali mengi sana kuhusu mama yake YESU, anatoa machozi, anachukia kuabudiwa, mimi pia sikulijuaga hilo ila akaja tena akanifundisha na uwaeleze watu wote ili wapone. Akaja YESU akanishika mkono akiwa na Malaika Mikaeli tukaenda kuzimu. Ndipo YESU akaniambia, huyu ndiye Mama Maria wa kuzimu ambaye ndiye aliyemzaa yesu wa uongo na yeye nilimwona, ila fuatilia masomo ya Nabii Hebron utakuta nimemwelezea alivyo; akasema YESU ndiyo sababu nilivyokuwepo hapa ulimwenguni nilisema muwe makini sababu atakuja kristo wa uongo na atatumia jina kama langu na atawateka wengi kama ilivyo sasa Hebron wengi wa wakristo hawapo katika upande wangu bali wapo katika upande wa yesu huyo wa uongo ambaye mama yake ndiye huyo hapo na yeye anaitwa Maria. Baada ya kuonyeshwa nilimpiga sana kwa jinsi ilivyokuwa haielezeki na kuchoma madhabahu yake kuzimu na vyombo vyake vya sadaka.

Ni mengi sana niliyoyajua na hata ulimwengu hayajui, ila neema yake MUNGU ilimpendeza mimi Nabii wake Hebron anijulishe hayo. Sasa huyu Mama Maria wa kuzimu ambaye ndiye aliyemzaa kristo wa uongo yeye yupo kinyume na Maria wa mbinguni. Maria wa mbinguni yeye amezishika amri za MUNGU zote, wala yeye haabudiwi, wala hana madhabahu yake, bali yeye yupo mbinguni anamfurahia MUNGU kama BABA yake. Ila Mama Maria wa kuzimu yeye ameruhusiwa aabudiwe na wanadamu, na pia yeye ndiye hutengenezwa kama kinyago huku duniani ila Mama Maria aliyopo mbinguni yeye siyo kinyago ni mtu kamili mwenye sura ya mbinguni kwa sasa na mbinguni hakuna vinyago. Kuzimu ndipo kuna vinyago, hata YESU WA NAZARETI siyo kinyago wala sanamu ila yesu wa uongo yeye kule kuzimu ana sura mbili; moja ya kipepo na ya pili ni ya kinyago. Sasa ili aabudiwe wakabuni sanamu ndizo zikaletwe huku duniani, watu wakaziita kwa majina yao na unapoitolea sadaka au kuibusu basi uelewe umebusu kuzimu na mambo ya yesu wa uongo, na unapoigusa unakuwa unajikabidhi kiroho na kimwili, japo wewe hauwezi ukaona kwa macho ya nyama ila wapo walio na neema wanaona na wanakimbia hawashiriki tena.

Mama Maria wa kuzimu yeye anamsaidia mtoto wake ambaye ndiye yesu wa uongo kuendeleza kazi ya mtoto wake na ya shetani ili waendelee kuimarisha ufalme wao ili katika ule mwisho wakachomwe wakiwa wengi, na pia hilo ndilo agizo la kuzimu kuwa watu wapotee watu wasiende mbinguni na zipo njia nyingi ikiwemo hii ya Mama Maria wa kuzimu au mzimu.
Swali:
a.      Iweje kama ni mama yake YESU halafu aruhusu sanamu ziabudiwe? Jibu unalo.

b.     Iweje ni Mama yake YESU wa kweli halafu akataze watu wasiokoke, wasibatizwe ubatizo wa maji mengi au wasibarikiwe wakiwa watoto kama alivyomsimamia mtoto wake akabarikiwa akiwa mtoto mdogo? Hivyo basi hakuna ubishi kwa njia nyingine kuwa kama angekuwa ni Maria wa mbinguni basi angeonyesha yale yaliyo mapenzi ya MUNGU hata kwetu sisi tokea tumezaliwa kwa kubarikiwa tukiwa watoto na siyo tukiwa watu wazima.

Elewa sasa huyu ni Mama Maria wa kuzimu ayasimamiaye mafundisho ya yesu wa uongo na sasa yamejaa katika ulimwengu wote, yanafanya watu wavunwe na Jehanamu. Ipo neema ya YESU na rehema kwako wewe utakaye tubu sasa.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe sasa nimeujua ukweli, sitamwabudu Maria yeyote yule zaidi yako wewe YESU, ROHO MTAKATIFU na MUNGU tu. Uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima. Namkataa Maria wa kuzimu na mtoto wake yesu wa uongo kwa jina la YESU WA NAZARETI na vitu vyeny vyote, sivitaki tena. YESU naomba uniongoze wewe uliye kweli nifwate kweli yako milele. Amen.

Zaidi ingia katika website www.prophethebron.org, ingia katika link ya blog, usome vitabu na makala na YouTube, utafunguka zaidi na roho yako itaponywa zaidi.


NABII HEBRON.