Pages

Saturday, April 4, 2015

HERI YA PASAKA KWA MATAIFA YOTE 2015

Kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, kupitia Nabii na Mtume Hebron, nawatakia pasaka njema. Neema ya MUNGU iwaokoe na mliookolewa msimame imara na kuendelea kuyatenda matendo mema na kuzifuata amri zake na kumtegemea YESU WA NAZARETI kama yeye ndiye BWANA NA MWOKOZI wa maisha yako kiimani na kimatendo wala siyo nusu nusu, iwe ni full full. Enyi mataifa nawakumbushia katika pasaka hii mkumbuke pia MUNGU alimtoa mwanae wa pekee ili awe sadaka ili mataifa yapone, na sasa YESU huyu muda wake wa kurudi umekaribia kama alivyonieleza ila muda na siku ndiyo sijui. Atakuja kuwachukua wale walio wake tu yaani waliookoka na majina yao yapo mbinguni na walioishi maisha ya utakatifu wala siyo wachawi, waabudu miungu na sanamu.

Sasa ni wakati wako uokoke na uwaambie marafiki na watu mbali mbali ujumbe huu. YESU anawahitaji mataifa yote wamrudie yeye, hiki ni kipindi cha neema yake ya kuwaponya watu wale ambao watakaomtafuta na kumfuata, fanya haraka kabla mlango haujafungwa. YESU akilinyakua kanisa (yaani aliyeokoka) ukabakia katika kipindi cha dhiki kuu, Je! Kipindi hicho utaweza kuokoka? Huu ni wakati wa amani, okoka leo ili akija katika unyakuo akuchukue, usije ukabakia ushuhudie kipindi cha dhiki kuu kwa miaka saba, joka kuu ataonekana hadharani na kila atakaye kuwa anabakia duniani atahojiwa kama anampenda YESU, utateswa mateso yasiyoelezeka. Utakatwa viungo vya mwili, nyama za mwili, utachemshwa kwenye tank la mafuta kama vile chips inavyokaangwa ili tu uteseke mpaka umkatae YESU. Na watakaomkiri shetani hao hawatateswa watasubiri hukumu ya mwisho wa dunia.

Sasa swali, je! Si bora uokoke leo wakati wa amani hii kuliko usubiri hadi kipindi cha dhiki kuu? Na hata katika dhiki kuu siwezi kuelezea mateso hayo kama mtu atayaweza kuyavumilia, na upate picha je iwe ni sasa je upo tayari kuyavumilia hayo mateso na shetani umuone kwa macho yako na mapepo yakikutesa pasipo kupata msaada wowote ule kwa miaka saba? Upo tayari uwekwe kwenye tank la mafuta yanayochemka halafu haufi? Mateso hayo hayaelezeki sijui ni nani atakaye yavumilia kwa miaka saba ndipo YESU akija tena upone. Dhiki kuu neema ya YESU haipo tena ni wewe peke yako, je! Utaeza kuyavumilia? Hata kama utakuwa umekufa utafufuka uyashuhudie hayo.

Nawasihi muokoke leo ili mateso ya dhiki kuu yasikupate na pia Jehanamu. Sema YESU WA NAZARETI naomba unisamehe dhambi zangu zote, nakukiri wewe na uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele, mimi ni mwanao sasa. Uniongoze siku zote nisipotee tena, shetani simtaki kabisa. Amen.

Zaidi ingia katika website ya kanisa www.prophethebron.org ingia katika link ya blog na YouTube utajifunza mengi na utafunguliwa.

WISH YOU ALL THE BEST.
HAPPY EASTER 2015.


NABII HEBRON.