JINSI PASAKA
YA KUZIMU INAVYOSHEREKEWA.
PASAKA YA
KUZIMU IPO HIVI…
Kama nilivyokwisha kuelezea kuhusu pasaka ya mbinguni ilivyo
na inavyosherekewa mbinguni pamoja na wanadamu waliomfuata YESU wa ukweli. Hivyo
hivyo na kuzimu pia wanaye yesu wao wa uongo na kila wakati wa pasaka
wanasherekea hivyo hivyo na wanaungana na wakristo wa uongo waliopo hapa
ulimwenguni katika ulimwengu wa roho ili waweze kuwaangamiza na kuwafungia watu
wasije wakaenda mbinguni bali wakifa waende huko huko katika makao ya yesu wa
uongo.
Hapa duniani hakuna mtu anapenda awe ni mkristo wa shetani
na watu wanajua bila kuokoka hauendi mbinguni. Sasa shetani na yeye aliliona
hili akamleta na yeye yesu wa uongo katika dunia hii akaanzisha njia zake
ambazo ni za uongo hazipo katika biblia ili aweze kuwapata wakristo hata wale
wateule wasiende mbinguni wakae, wazubae, wakifikiri wataenda mbinguni kwa
akili zao kumbe laah, shetani anajua nini alichokifanya. Nawaeleza jamani,
shetani ni mbaya, tena hata usitake uione sura yake. Mimi Hebron nimemwona
simpendi kwa kweli, wala usitamani kumwona hata siku moja, unaweza ukawa kichaa
kama neema ya MUNGU haipo na wewe. Ni lijitu linatisha na lina roho mbaya.
Mimi nilipelekwa na YESU mwenyewe hadi alipo na akaniambia
huyu ndiye adui wa wandamu wote, sasa nimekupa mamlaka upindue kazi zake na
ufalme wake katika ulimwengu wote. Uwaeleze watu kweli yangu, uniandalie kanisa
la mwisho, muda wangu wa kurudi umekaribia na huyu amewashikilia 98% ya watu
wote katika ulimwengu wote ikiwemo na watumishi walionisaliti, sasa huyu ndiye
baba yao anayewapa nguvu ya kuujenga ufalme wake shetani na mpinga kristo. Habari
hizi zaidi soma katika kitabu cha JINSI NABII HEBRON ALIVYOITIKISA KUZIMU.
Sasa katika pasaka ya kuzimu wakristo baadhi yao hawaelewi na natumaini wangependa kujua ikiwa
ni pamoja hata na watu wasiomjua YESU ili wamjue wapone roho zao.
ILI
KUJUA MKRISTO UNASHEREKEAGA PASAKA YA KUZIMU SOMA YAFUATAYO:
·
Ukiwa umebatizwa kwa ubatizo ambao haujatoka
mbinguni yaani wa Yohana uelewe wewe ni mkristo wa uongo japo haupendi au
haujui. Uwe umebatizwa kwa maji ya kisima, kubatizwa kwa jina la mchungaji hata
kama ni maji mengi.
·
Ukiwa ni mkristo halafu unasali katika madhabahu
inayoabudu sanamu.
·
Haujaokoka na unapinga wokovu, japo unajiita ni mkristo
wewe ni mpinga kristo. Ukristo huo siyo wa mbinguni bali ni wa yule wa uongo.
·
Kubatiza watoto wadogo.
·
Kuabudu wanadamu na kuwaomba wakuombee badala ya
ROHO MTAKATIFU, ndiye msaidizi tuliyopewa atuombee yeye tu.
·
Kuombea wafu (ibada za wafu), kuchaji riba
kanisa kama ni benki.
·
Kuabudu katika kanisa lolote linalochangisha
watu pesa, partners.
·
Kuabudu msalaba na mengineyo yaliyo kinyume na
mpango wa MUNGU.
·
Kuongozwa na watumishi wachawi, freemason,
illuminati, walioasi, waliojiita, wanyang’anyi, watoza ushuru, kudai malipo
ndio upate huduma ya kiroho.
Yapo mengi ila kupitia haya yatakufunulia na mengi zaidi na
utapona sababu wengi wanaonaga wapo sawa
lakini kumbe wanapotezwa kwa sababu ya mapokeo ambayo hayapo hata katika
biblia, yaliletwa ili kuwavuruga wakristo wawe wakristo wa kuzimu wasiende
mbinguni na wanaposhiriki pasaka wakiwa katika hali hii ambayo nimetolea mfano
mchache ina maana unayo mambo ambayo siyo ya YESU WA NAZARETI, na kupitia hayo
matendo basi hiyo inakujulisha katika ulimwengu wa roho wewe hayo uliyonayo
hayajatoka mbinguni basi shetani anakumiliki bila upinzani wowote.
Sasa nawasihi mataifa yote mrejeeni YESU najua hata wapo
watumishi wanaompenda YESU ila hawakuyajua haya ya ukweli waliotekwa na
shetani. Neema ya YESU ipo sasa wewe rejea na ukatengwe nao, toka huko mahali
pa jinsi hiyo, wewe unaona kabisa pako kinyume na YESU wa kweli sasa unafanya
nini tena? Usiangalie utukufu wa wanadamu, watakutenga, wao hawana mbingu ya
kukupeleka zaidi usipotoka huko sasa na MUNGU na yeye atakukataa na ardhi
itakusubiri kwa hamu kukula nyama yako utakapokufa na pia moto wa jehanamu.
Madhara ya kusherekea sherehe ya pasaka ya kuzimu unakuwa
unazidi kujiunganisha na kuzimu kwa yesu wa uongo na kukufungia usiende
mbinguni na kuzubaishwa ujione utaenda mbinguni ukiwa hapa duniani kumbe katika
ulimwengu wa roho wewe unakuwa ni mfuasi wa yesu wa uongo, na hata alama zake unazo
katika mwili na katika roho. Mfano katika mwili; angalia ubatizo ulionao na
kiroho angalia unapoabudu; je YESU wa kweli anafuatwa au ni masanamu, michango
tu na ufisadi. Zaidi soma kitabu cha Nabii Hebron cha UBATIZO WA KWELI KWA
ULIMWENGU WOTE.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe, nimeujua ukweli, nakukiri
sasa wewe ndiwe BWANA NA MWOKOZI wa maisha yangu. Uniandike jina langu katika
kitabu cha uzima wako mbinguni. Najitoa kwenye pasaka za kuzimu nilizoshiriki
kwa kujua au kutokujua sizitaki tena. Nilijiona ni mkristo safi kumbe nimetekwaga. Nakushukuru YESU kwa ufunuo
uliompa Nabii Hebron kutufunulia siri hizi na sasa nipo huru. Amen.
NABII HEBRON.