JINSI PASAKA
YA MBINGUNI INAVYOSHEREKEWA.
Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU WA
NAZARETI aliye hai na sasa yupo mbinguni. Katika kipengele hiki nitaelezea
kuhusu pasaka inayosherekewa mbinguni pamoja na wakristo wa kweli ilivyo kwa
sababu wakristo na watu mbali mbali husherekea siku hii pasipo kujua
inawapasaje washerekee ili wawe wanasherekea pasaka ya mbinguni. Ninasema hivyo
kwa sababu nataka uelewe pia yupo yesu wa uongo, na kama yupo hivyo na yeye
alivikopi vitu vya YESU wa kweli katika njia yake ili kuhakikisha anawapiga
upofu watu kama alivyowapiga baadhi yao badala ya kusherekea pasaka ya mbinguni
wakajikuta wanasherekea pasaka ya kuzimu.
Pasaka ni ukombozi ambao kwanza kabisa asili yake ilianza
pale MUNGU alipowatoa wana wa Israeli kwa Farao na alipomaliza kuwatoa
aliwaagiza wawe wanafanya siku kuu ya pasaka kila mwaka katika vizazi vyote na
ndivyo ilivyo; hata na YESU na yeye akaikuta pasaka na akaisherekea (Mahayo
12:1-3) inaelezea hii ndiyo pasaka ya kwanza na pasaka ya pili ni ile ya kifo
cha BWANA YESU WA NAZARETI ambaye yeye alikufa kwa ajili ya watu wote, siyo kwa
ajili ya wakristo tu ili wapate kukombolewa kama alivyoahidi MUNGU, hiyo ndiyo
sababu wakristo husherekea siku kuu ya pasaka kila mwaka kwa kumtukuza MUNGU
kwa ajili ya ukombozi wake.
Ili ushiriki pasaka ya YESU WA NAZARETI aliye mbinguni
yakupasa ufwate matakwa yake kama yalivyo mapenzi ya MUNGU na endapo utakuwa
kinyume tu na YESU basi uelewe pasaka
hiyo itakuwa ni ya yesu wa kuzimu sababu hata na wao kuzimu huwa wanasherekea
hivyo hivyo na wale wanadamu wanaofuata ya yesu wa uongo. Ili ushiriki pasaka
ya mbinguni ni lazima uwe umeokoka na umebatizwa kwa ubatizo wa maji mengi
katika mto; maji yanayotembea, wala siyo maji ya kisima kazi ya mikono ya
wanadamu na uishi maisha matakatifu.
Mimi pia Nabii Hebron kabla ya kufunuliwa na YESU kuhusu
pasaka ya kuwa ipo ya mbinguni na ya kuzimu niliogopa sana na jinsi alivyonifundisha,
nilijiona miaka mingi nilikuwa ni mkristo wa uongo na nilishiriki kusherekea
hizo pasaka pasipo kujua; nilizaliwa katika dini ya wazazi wangu, nikabatizwa
ubatizo usiotokea mbinguni wa maji ya kikombe. Ubatizo huo ulininyima haki ya
kuwa mkristo wa kweli kwa miaka mingi mpaka pale nilipobatizwa kwa maji mengi
ndipo nikawa mkristo wa kweli na ndipo nilianza kusherekea pasaka na mbinguni.
Nataka uelewe shetani ni mpumbavu, akawaona watu wanaokoka
ila akawateka tena katika huo ubatizo wa kikombe kwa baadhi ya watumishi
waliomsaliti YESU wakageuza tena katika ubatizo wa maji mengi wakawabatiza watu
kwa majina yao. Nawaeleza uliyebatizwa hivyo wewe haujakamilika, huo ni ubatizo
wa Yohana wa kuzimu, na wengine wamebatizwa ubatizo wa kisima, hata hapo
ukristo wako unayomashtaka mbele za MUNGU na shetani anacho kitu cha kukushtaki
kwa sababu hayo maji hayatembei ni kama josho la kuogeshea mifugo.
Faida ya kushiriki pasaka ya mbinguni; kwanza unamfurahisha
MUNGU, unazidi kuinuliwa. Madhara ya pasaka ya kuzimu, unazidi kuangamia kiroho
na kimwili na kujiunganisha utakapokufa uende huko huko alipo yesu wa uongo kwa
sababu umeyafuata mafundisho ya uongo, hayajatoka mbinguni.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote. Uniandike
jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Sitaki tena kushiriki
pasaka ya kuzimu, nimeujua ukweli nakushukuru YESU. Amen.
Zaidi ingia katika website ya www.prophethebron.org, ingia katika
link ya blog na YouTube utafunuliwa zaidi.
NABII HEBRON.