UNABII WA
NABII HEBRON UMETIMIA KUHUSU TANZANIA.
Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai au kwa
jina lingine anaitwa Nabii Issa. Aliponiita aliniambia atabadilisha Tanzania na
nchi hii ndiyo Eden ya sasa nilikuisha elezea katika makala ya Nabii Hebron,
usome niliyoyatabiri kuhusu nchi ya Tanzania 2012, 2013, utaona yametimia kwa
macho ya damu na nyama.
1.
Nilielezea elimu ya Tanzania itakuwa bure bila
malipo kuanzia primary school, secondary school na vya serikali, sasa
imeshaanza Zanzibar. Rais katangaza katika sherehe ya miaka 51 ya Mapinduzi
elimu ya primary na secondary ni bure upande wa Zanzibar na huku bara itakuwa
hivyo hivyo, muda siyo mrefu itatangazwa.
2.
Nilielezea kuhusu mgodi wa Tanzanite 2012
utarudishwa kwa nchi na kwa Watanzania na sasa imetokea, migodi ya Tanzanite
upo katika mikono ya serikali na wananchi.
3.
Nilielezea mawaziri watatolewa na bado
watatolewa tena wale wote watakaoenda kinyume, ni MUNGU ndiye anafanya kazi
hiyo ili kuinua nchi yake.
4.
Nilielezea uchumi utainuliwa, mafuta yatatokea,
ndege zitaongezeka na viwanja kuinuliwa na mengine mengi na mnayaona sasa, na
bado yatatokea. MUNGU ameachilia kibali nchi hii ainyanyue, aitengeneze kama
Edeni.
5.
Na kuanzia 2015, wapo wawekezaji ambao
waliwekeza katika nchi hii ila lengo lao ni kuifilisi nchi na wengine wameiibia
nchi na wana nchi wake. Hao wataondoka wenyewe mambo yao hayataenda tena. Watakuja
wawekezaji wema na Watanzania wenyewe sasa watakuwa ni wawekezaji katika vitu
mbali mbali ndani ya nchi yao. Na huu mwaka 2015 mikataba yote isiyo na faida
itafutwa ikiwemo ya makampuni ya mafuta upande wa Zanzibar na pia Bara. Haya yote
ni mwenyezi MUNGU ndiye ayafanyae na amekwisha nieleza na maneno yake ni kweli
na ndivyo ilivyo.
NABII HEBRON.