Nashukuru sana MUNGU akubariki.
Napenda kuomba kumshukuru MUNGU kwanza kwa ajili ya muda huu.
“BABA yangu na MUNGU wangu
uketiye mahali pa juu asante kwaajili ya watangazaji wa redio hii ,asante
kwaajili ya kila mmoja anayesikiliza muda huu maana wewe MUNGU umempa kibali
hicho. Baba nitumie upendavyo kwaajili ya ujumbe ule ulionipa kwaajili ya
kanisa la ulimwengu mzima. Baba ninafungua masikio ya kila mmoja akapate
kusikia. Ninatuma Malaika wako
wakawakusanye watu wako wakapate kukusikiliza wewe wala wasisikilize kama
kuniangalia mimi bali MUNGU nitumie upendavyo. Ni kwa utukufu wako sifa
nakurudishia wewe AMEN.”
BWANA YESU asifiwe ndugu
msikilizaji mahali popote nchi yote,
mkoa wote, wilaya yote uliyopo wa kanisa lolote, mpagani mwislamu leo hii niko
mbele yako kukuletea ujumbe ambao YESU ameniagiza kuwaeleza kanisa lake na
kuwaeleza watu wake wote wa ulimwengu mzimaa. Aliniita nilivyokuwa Serengeti
katika kazi yangu ya u’DRIVER GUIDE akanirudisha Arusha akaniambia nakutuma
nahitaji mwili wako uende ukaeleze haya yote ninayokueleza maana moyo wangu
unauma na MUNGU amehuzunika kwasababu ya mambo mabaya yanayofanyika kwenye
makanisa, mambo mabaya yanayofanyika na watumishi wamemsaliti wakaenda kunyume
nay eye alivyowaagiza. Nikamwambia “Baba nitumie lakini mimi siwezi.”
Akaniambia nahitaji mwili wako tu wala usiogope nimekushika mkono hata Paulo
nilimuita hivyohivyo na wewe ndivyo hivyohivyo na zaidi na zaidi nitakutumia.
Sasaivi ni wakati wa wa kuupindua ulimwengu wote ubadilike uniridie mimi YESU
maana sasa nakaribia kuja wakati wowote na kanisa limetekwa na shetani.
Akaniambia 2% ya kanisa ulimwengu mzima ndio iko na yeye,98% hayupo watu
wanapiga kelele tu wakijua wanamwimbia YESU na kumwabudu YESU lakini YESU
haonekani makanisani.
Ndugu msikilizaji kwa siku ya leo
penda embu chukua kitabu chako utafungua Injili ya Marko mtakatifu 11:15-17
nami nasoma;Wakafika Yerusalemu nae akaingia ndani ya hekalu akaanza kuwafukuza
wale waliokua wakiuza na kununua ndani ya hekalu akazipindua meza za wabadili
fedha na viti vyao wauzao njiwa wala hakuacha mtu achukue chombo kati ya kati
ya hekalu akafundisha akisema, je; haikuandikwa nyumba yangu itaitwa nyumba ya
sala kwa mataifa yote? Bali ninyi mmeifanya kuwa pango la wanyang’anyi.
BWANA YESU asifiwe. YESU alinipa
na ujumbe huu wakati akiwa ananifundisha na kunieleza hili jambo alikwisha
kulifanya enzi hizo akiwa katika ulimwengu huu kabla hajapaa kwenda kwa baba
yake. Akaniambia, nyumba yangu ni nyumba ya sala, sasa hivi imekuwa sio nyumba
ya sala, imebadilishwa kama vilevile nilivyokataa na ndio maana sionekani
makanisani. Watu wanalia, wanakata tama, wanazunguka na kutoa machozi
wakifikiri kwamba mimi YESU nimewaacha. Mimi YESU ninawapenda, tatizo wamekuwepo
mafarisayo na masadukayo, tena wameibadilisha injili yangu na kufuata yale
ambayo ni ya adui.
BWANA YESU asifiwe. Ndugu
msikilizaji ninakutia moyo usiogope, maana unakwenda kufunguliwa siku ya leo
hata kama ni mtumishi uliyepo katika madhabahu nyingine yoyote, yawezekana
mwingine umerithi kutoka kwa baba wa kiroho, ambao walikwisha kutekwa na
shetani. Watu wamekuwa wakijiona kwamba wamesimama na YESU, kumbe wamekwisha
kutekwa na shetani. Shetani ameingiza tekniki (technique) ndani ya makanisa,
amewaingizia roho ya kupenda fedha, amewaingizia roho ya kufanya kanisa la
MUNGU kuwa nyumba ya biashara, sasa hivi YESU haonekani makanisani. Tukija katika Injili ya
Neno la MUNGU tulilosoma hapa katika kitabu cha Marko, YESU alivyoingia
hekaluni, aliwakuta wafanyabiashara akawafukuza lakini leo hii wameyarudisha.
Na baada ya kufukuza ukiendelea kusoma mistari ya chini unaona watu walimfuata
wakaenda kupokea uponyaji. Leo hii YESU hayupo kabisa maeneo hayo, na
ameniambia niwaeleze ulimwengu mzima, atakayesikia asikie, atakayekasirika
akasirike, lakini ni BWANA amesema. Imechosha, imechosha jina lake kutukanwa.
Watumishi wamekuwa wakitumia jina lake kunyang’anya magari, kunyang’anya fedha,
watu wa MUNGU wamekuwa wakiteseka, wanafunga na kuomba na kulia; majibu hakuna.
YESU anasema leo hii, anakufungua mahali hapo hapo ulipo katika jina la YESU
KRISTO WA NAZARETI maana wamekuwa na mioyo migumu, wamekataa kuacha kupenda
fedha, wamebadililika, japo fedha ni nzuri; sio zenyewe zikumiliki katika jina
la YESU. Wamefanya kazi ya MUNGU kuwa ni mradi na wewe hata kondoo zake BWANA
YESU ameniambia wamekuwa wakinyang’anywa mali, wkainyang’anywa fedha wakijua
wanamtolea MUNGU. Watumishi wamekuwa wakitumia jina lake kusema, BWANA amesema
toa, akaniambia, mimi ndiye director wa kanisa. Je; mimi ni masikini?
Nimekwesha kusema, nimewapa bure, mtoe bure. Kwa nini mnawaambia wanangu watoe
pesa ndio muwaombee? Akaniambia MUNGU hutoa bure, shetani lazima ulipe.
BWANA YESU asifiwe. Najua wako
wengi wamekwisha kuumia sana, lakini umefika wakati sasa ni mwisho. Ameniambia
YESU ulimwengu mzima, mlioko Canada, mlioko China, mlioko Malaysia, wote na
nchi zote lazima mnasikia. Huko ni mnaenda kufunguliwa. Iwe ni mtumishi yeyote
unayetaka kuponywa, siku ya leo unaenda kuponywa na ubadilike. YESU amekataa,
mwisho wake unakuja, mtachomwa kama moto. Mmefanya YESU amebaki asilimia mbili
(2%), asilimia tisini na nane (98%) shetani ndiye amekamata kanisa.
BWANA YESU asifiwe. Ni mambo ya
kutisha, ni mambo ya kutia aibu. MUNGU anasema watumishi wanamdharau, ameanza
nao vizuri, na amewaita wamefika mbele wamekengeuka. Akaniambia sema kila
ninachokuambia. Ole wake atakayekugusa, mimi niko na wewe katika jina la YESU
KRISTO wa Nazareti. BWANA YESU asifiwe. Akanifunulia tena, akaniambia; Paulo
nilivyomuita, nilimtuma na yeye hivi hivi. Alikuta wameenda kubadilisha injili,
injili ambayo niliwaambia wameenda kuipindisha pindisha yale niliyoyaagiza
wamekataa. Ukisoma katika kitabu cha Wagalatia 1:6-8, Injili imebadilishwa
kabisa kabisa na mpango wa YESU aliouacha maana yeye ndiye kiongozi wa kanisa.
Kanisa limevamiwa, na shetani amewaingizia watumishi, watumishi wamekuwa kama
taahira, hawajui wengine wanafanya nini, japo kuna wengine wanakwenda kuzimu.
Ila wanaokwenda kuzimu, BWANA YESU mwezi uliopita aliniambia kwa kuomba nifunge
njia zote za kuzimu kule wanakokwenda kuchukua maana baba yao lusifa
alikwishakufungwa na mtumishi ambaye MUNGU alikwisha kumuandaa wakati wa nyuma
ila na yeye alikataa kumsikiliza, MUNGU akamuweka pembeni. Sasa hivi MUNGU
anakwenda na wanaokwenda, maana YESU anarudi kulichukua kanisa lake, na shetani
amechukua wengi hata hii asilimia mbili (2%) iliyobakia anataka izidi kupungua,
azidi kuichukua ili achukue ulimwengu wote. YESU amesema, hapana, hapana. Mawe
yatazungumza, anga litazungumza, ardhi itazungumza, miti itazungumza, viumbe
vyote vitazungumza kwa ajili ya yeye.
BWANA YESU asifiwe. Ujumbe huu YESU alionipa,
alivyonieleza nililia sana, maana na mimi nilikuwa sijui wala kuelewa. Ni vitu
vya kutisha. Kimwili binadamu ukitembea nje, utafikiri watu kweli wanamwabudu
YESU, lakini mioyoni mwao hamna. Viongozi wametekwa asilimia kubwa ulimwengu
mzima, na wengine hawajijui wala hawajielewi. Mambo aliyoniambia ni mengi sana
zaidi ya elfu moja na hata hapa sasaivi kuna kitabu ambacho amenipa maagizo
nikiandike kwa ujumbe ule alionieleza. Kitabu chenyewe kiko madukani sasaivi
kikotayari. Ujumbe wake juu ya kichwa cha habari ‘JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA
SHETANI.’ Sasa YESU analitaka kanisa lake. Nyie aliowatuma mmemsaliti.
Kumsaliti mnalitaja jina lake lakini hamtendi yale ambayo anayataka yeye YESU. Sasa
kama hamyatendi yale ambayo ameyaagiza
YESU ,hayo mnayoyatenda ni ya nani? Jibu ni ya shetani. Unamtumikia
shetani kwasababu unafanya ya shetani.
Kitu cha kwanza watu na
wanaoamini kanisani, wamekamatwa katika sadaka sasaivi ni habari ya sadaka tu.
Toa toa tu, toa toa tu, sawa kutoa ni kuzuri ; akaniambia mwanangu sadaka ni ibada ya mtu mwenyewe na mimi peke
yangu. Lakini sasaivi sadaka mtu anaambiwa aandike jina lake kwenye sadaka ya
fungu la kumi na aandike mpaka namba ya simu na kiasi. Kwani mimi MUNGU ninahitaji simu ya kuangalia
na kumpigia simu aminitolea kiasi gani? Akaniambia huyu ni shetani. BWANA YESU
asifiwe. Akaniambia katika maandiko imeandikwa kwamba wakati unanitolea sadaka
yako ficha hata kulia na kushoto isijue. Je;nyie watumishi haya yametoka wapi?
Akaniambia waeleze,waeleze. Mimi ndio mtumishi mkuu(ndio YESU) na mimi ninakaa
ndani ya mtumishi ambaye namuongoza mimi. Nikiwa ndani yake yale
niliyoyakataa na aliyoyakataa baba yangu
MUNGU hayawezi kufanywa kanisani.
BWANA YESU asifiwe. Ni mambo ya kutia aibu. akaniambia
waambie huu ujumbe ni kwaajili ya watu wote mimi YESU sitafuti pesa ya mtu wala
mimi sio masikini ninyang’anye watu mali zao. Maana jina langu linatukanwa na
mimi sasaivi kanisani nimeitwa mnyang’anyi. Jina langu linatukanwa. Lakini YESU
ananiambia yeye hahusiki huko ni hao na mambo yao wameyapata hukohuko.
Nimewaonya, nimewakataza wamekataa. Akaniambia na ujumbe huu ninaokupa wapo
ambao niliwapa wapeleke, nimesema nao lakini wamekataa; wamekuwa kichwa ngumu,
wamekataa kabisa kusema, wamekataa kusema wameukalia. Watu wanazidi kuteseka shetani anazidi kulipiga
kanisakama anavyolipiga sasahivi;amelipiga mpaka kanisa limechoka, direction
hakuna, watu wameanza mpaka kutafuta majini muhubiri,jinni maono ndio wamekuwa
nayo, mwisho wao umefika. YESU amesema watubu kinyume cha hapo wataangamia.
MUNGU amekasirika kabisa amechukia;ni ulimwengu mzima mabara yote. Na
akaniambia Tanzania ndio EDEN,anaanzia Tanzania. Mwanangu usifikirie pesa
utatoa wapi,mimi baba yako nitaleta pesa na kila kitu cha kukuongoza,nahitaji
mwili wako tu. Hata sasaivi usione ni Hebron anazungumza ni MUNGU mwenyewe
anapita kwenye kinywa kukueleza ujumbe wake. Wewe uliyeumia na majeraha leo
MUNGU anakwenda kuyatengeneza, majibu ambayo ulikua huyapati leo unakwenda
kuyapata live, live na ni bure.
BWANA YESU asifiwe. Oh! Inatia
huruma sana. Leo nilivyokua nyumbani kwangu akaniambia katika watumishi mia
moja(100), wawili tu ndio wasafi. Sasa
tunakwenda wapi? Kanisa lirudi sasa lijipange upya. Upendo umeondoka makanisani
wenye pesa ndio wanapendwa wasio na pesa hawaangaliwi. Akasema yeye ni MUNGU
anawapenda wote. Mahali penye madhabahu kama hiyo amesema hiyo madhabahu
imekufa na ambayo inachangisha watu ela kanisani hayupo;amesema watumishi
wamuulize yeye pesa. Amesema wapige magoti yeye atazileta, si kuwakamat akondoo
zake. Kondoo wamekamatwa na kukamatwa matokea yake hawabarikiwi wala
hawainuliwi. Umaskini unazidi shida zinazidi na mimi katika neno langu katika Malaki 4 “ukininyooshea na kunitolea
nitakuinua” Kwanini hunyanyuliwi? Mimi MUNGU ni muongo? Tatizo liko kwenye
kanisa; wana wa MUNGU tuombe kanisa liko kwenye tatizo. Kweli imeondoka kabisa,
watu wanapakana mafuta BWANA atafanya. Unaambiwa nenda na neema ya MUNGU
ikuongoze matokeo yake ni nuksi balaa na
mikosi. Sasa YESU analikamata kanisa , analibadilisha ukubali usikubali. Wewe
un ayeenda chini nakwambia sasaiva malaika wanakuteketeza. Kazi zote zimefungwa
katika jina la YESU. Hakuna amani kwa
wabaya ,wabaya ni washirikina wote , wabaya wanaongozwa na shetani. MUNGU
amekuumba wewe kwa sura ili umtumikie, ili umwabudu yeye lakini leo unamwabudu shetani . je;
hujapotea? Ziko namna nyingi sana ndugu msikilizaji ninitaendelea kukuelezea na
vitabu nitaendelea kuvitoa anavyonielekeza MUNGU ili nikufikishie ujumbe wewe.
Hata ukusema kuandika siwezi inabida sasa niseme vile vinavyoshuka maana ni vingi na ni mazito na ni makubwa. Shetani ameukamata ulimwengu,
YESU anawahitaji, YESU anakuhitaji. Wewe
uliyekuwa umekata tama, na kuona kwamba YESU hayupo, YESU yupo nakuambia.
Ameniambia watumishi wamemsaliti. Mtu yeyote anayefanya kazi ya MUNGU kwenda
kinyume na YESU, huyo anamsaliti. YESU alisema kwanza, nyumba yake ni nyumba ya
sala lakini angalia leo nii nyumba yake ni sehemu ya kukusanyia hela tu. Nyumba
yake leo hii ni mahali pa michango, nyumba yake leo hii ili uambiwe neno
ubarikiwe unaambiwa utoe hela. Je, YESU anahitaji hela yako ili akubariki? YESU
hubariki bure bure. Ukipenda kumtolea MUNGU mtolee bure, usiogope mtu.
Nimekuambia muangalie MUNGU wewe ni wa wa thamani sana, wala pesa yako
usimruhusu aizoee zoee mmefanywa ATM machines. MUNGU amekasirika, umasikini
umezidi, umasikini unaingia mpaka kwenye vitanda. Leo ni mwisho wewe
unaesikiliza ufunguke ufahamu maana hata wengine mnasikiliza mpo mia saba
ishirini (720) sasa hivi nyie watumishi mnanisikiliza na mnaniona, mnaumwa
matumbo, omba toba maana unaijua kweli MUNGU hakutuma kazi hiyo. MUNGU anabaki
kuwa wa rehema pale pale.
Mtumishi wa MUNGU; ndugu
msikilizaji anaposimama kuhubiri uwe makini sana. Manabii wa uwongo wamejaa.
Mtu yeyote anayesema kinyume cha neno la MUNGU kanisani ni nabii wa uwongo. Sio
mpaka aende kuzimu, ile kufundisha tu kinyume na mapenzi ya MUNGU . Oooh MUNGU
tusaidie, saidia ulimwengu wote, ufungue BWANA YESU, fungua kila mmoja, fungua
wanaosikiliza, ondoa majeraha kwa kila mmoja, ondoa BABA yangu. Hata wale
waliopotea wamekata tamaa sasa hivi ni watumishi wako wanaonyanyaswa,
wamenyang’anywa na huduma zao kwa kutumia nguvu za kipepo. Malaika wafanye kazi
akiwepo malaika Mikaeli wafyekefyeke na kuwarejeshea vitu vyao. Wasio na nyota
warudishiwe maana wengine ni misukule, hawana nyota, wanazurura tu na kanisani
asubuhi, mchana na jioni ni kuomba, kuomba, suruali zimetoboka, mapigo kila
mahali. MUNGU aonekane, MUNGU yupo kuanzia siku ya leo. Wewe uliyemsikiliza
ninakuambia mwana wa MUNGU utaona mabadiliko. Usiangalie jina kubwa la mtu
anayehubiri wa siku nyingi. Kama ana MUNGU sikiliza. Kama hana MUNGU achana
naye. Macho ya rohoni watu mmevunjwa vunjwa, YESU anawarejeshea macho yenu.
YESU akaniambia, mtumishi wangu
ninakupenda, sio kwamba ninawachukia hao, ninawapenda. Upendo wangu uko pale
pale, ila mpaka atakayetubu kwa sababu wamefanyika kuwa geti la kuziba wengine
wasinione mimi, lakini ninakutumia kama chombo, napeleka ujumbe wangu mwenyewe.
Lazima wafunguliwe na akaniambia sasa hivi watu idadi kubwa ndio nahitaji
iingie Kaanani. Na anakwenda kutumia watumishi wale waliodharauliwa na
kukataliwa. Ndio anakwenda kuwatumia kwa kiwango kikubwa sana na atawatumia kwa
namna isiyo ya kawaida. Ambao hawajawahi kuonekana hapa ulimwenguni akaniambia,
sasa hivi najua mnasubiri ujio wangu, na neno langu linasema utukufu wa kanisa
la mwisho utakuwa mkubwa kuliko wa kanisa la kwanza; lakini je; angalia utukufu
wangu ni mkubwa au kanisa ndio limeangamia? Akaniambia kanisa limeangamia,
nashindwa kushuka; nitashukia wapi? Watu wanafikiri niko kwenye mavinanda tu.
Wako watumishi waliojificha mpaka kwenye migombani. Nasema nao hawasikilizi, wanapigwa
lakini sasa yatosha wanakwenda kuaibika. Na MUNGU anakwenda kuwanyang’anya.
Ananyanyua watumishi wengine ili kazi yake iende. Mmekuwa sugu, ni wizi tu
kanisani, akaniambia; mimi YESU enzi zangu nikiwa ninahubiri hapa ulimwenguni,
nilishaanza kuwaambia watu nipe gari lako, nipe nyumba yako, mimi ni masikini?
Akasema, wanangu wananipenda sana, wakisikia jina langu wanatetemeka wakijua wananitetea mimi kumbe hawanitetei
mimi. Akaniambia, wengine wameongeza ‘toa mpaka ikuume’watu wanatoa mpaka
wanauza vitu vya nyumba, mpaka wanalala chini. Matokeo yake hawapati kitu.
Siletewi mimi, wala mimi siagizi vitu vya namna hiyo. Kaini na Abeli
waliponitolea, Abeli alinitolea kwa roho ya upendo na furaha sana na amani,
bila kuuma. Lakini Kaini moyo wake ulikuwa unauma. Mimi sipokei sadaka za moyo
kuuma. Akaniambia, mafungu ya kumi watu wanaambiwa andika namba ya simu halafu
anawekwa kwenye attendance, mwisho wa mwezi usipotoa shetani anaingia ndani ya
mtumishi anakupigia simu anakuambia, “we mbona huonekani wewe, unajua umerudi
nyuma sana kiroho?”. Mimi YESU siangalii pesa. Sadaka yako wewe mwana wa MUNGU
ni siri yako kati yako wewe na MUNGU na ndio maana haineni unapoandika jina au
upapowapa hao inanena kwao, thawabu yako imebaki hapohapo. Usiandike jina tena,
ni mapinduzi YESU ameanza ulimwengu mzima ili wewe unyanyuliwe na uwe makini pia
unapotoa. Kama hiyo madhabahu ni ya kuzimu, asilimia Fulani inaenda kuzimu
ungine inabaki kwa huyo mtumishi, matokeo yake Baraka unazozipata ni za
shetani; nuksi, balaa, mikosi na kufilisika. Lakini ukitoa mahali ambapo yeye
yupo utainuliwa, utabarikiwa na
utaurithi uzima wa milele. Kataa kabisa hata nyie mnaokataa tena mshindwe
kabisa katika jina la YESU. Ninawaona na kuwasikia. Mlizoea, kuzime imesikia,
bab yenu amesikia na anakula bakora sasa hivi kuzimu na mtandao mzima wa
watumishi wanaokwenda kuzimu ulimwengu mzima, malaika Mikael kamata teketeza.
MUNGU amekasirika. Imefika mahali mnamchezea MUNGU ni wakati sasa wa BWANA YESU
kudhihirika ulimwengu mzima.
Nakurudisha katika habari aliyoniambia.
Akaniambia wako watumishi wanavaa nguo, zile nguo wanapozivaa anakupangia wewe
utakayesaini kwenye mikono au kichwa utatoa milioni. Nyie ambao wa elfu kumi
kumi mtasaini miguuni. Mwana wa MUNGU, akaniambia BWANA YESU, mimi YESU
niliwahi kufanya kitu kama hicho? Hicho kimetoka wapi? Wengine wanamtupia hela
hata mpaka miguuni wanamwambia hizo ndio za kwake za kula. Mimi niliwaambia;
wasisumbukie watakula nini, watavaa nini. Je, mimi ni masikini? Maua
ninayanyeshea maji, ndege wa angani wanakula. Je, niliyemuumba kwa sura yangu
si zaidi? Funguka mwana wa MUNGU, funguka watumishi hao wametekwa, n wengine
sio kwamba wametekwa, wanajijua kabisa. Sadaka ya kweli ni funfu la kumi nay a
shukrani na kumtolea MUNGU mtu asikupangie, mambo ya sadaka sijui za majengo
amekataa. Sijui za Injili amekataa. Amesema pesa zote zipangiwe kazi yake. Haya
matabaka-tabaka hizo nyingine zinakwenda wapi?
BWANA YESU asifiwe. Sikiliza
mwana wa MUNGU, YESU amekataa ili akunyanyue, ili akuinue. Endelea kukaa kwenye redio yako. Chochote
kilichopungua ndani yako, leo utarudishiwa, balaa zote na mikosi zinaenda
kufutwa juu yako na utakuwa huru sasa. Akaniambia, leo hii mimi nimesema kwamba
mimi ndio kiongozi wa kanisa, director. Nawaambia msikope, si kanisa lisikope?
Akaniambia ni machukizo matupu. Leo hii kanisa linakwenda benki. Likipelekwa
jina langu kanisa si inajulikana ni mimi YESU? Wanapeleka proposal wanakopa
hela kwa ajili ya kunijengea eti mimi jengo. Mimi MUNGU masikini? Wakati
nimekwisha kusema msikope, wala msilipe riba kanisani. Mnaambiwa mchange hela
kwa ajili ya kulipa deni la kanisa, eti mimi nikalipe riba? Ina maana nyie
mnapoenda kutoa mimi YESU ninakwenda kulipa riba. Mimi sipo hapo, sipo
uliyekuwa unafanya hivyo umeliwa. Ulimwengu mzima hata mliopo Japan,
badilikeni. MUNGU amekasirika. Mambo yote hayo mikopo kazi aliyoituma YESU kwa
watumishi wake ni kuponya roho watu sasa hivi kanisa lina-deal na mahoteli,
lina-deal na ma-saccos, ndio kazi YESU ametuma hiyo? YESU amewapa watu
muwaombee wakafanye kazi hizo na wataleta kanisani.
BWANA YESU asifiwe. Kingine alichoniambia,
sasa hivi kuna watumishi wanaenda kwenye hizo nchi wanazozijua wao. Wanajua ubatizo
ni kiapo changu mimi na mtu, lakini wao nanabatiza kwa majina yao. Mfano labda
mtumishi anaitwa Ndoo, anakuita, anakubatiza kuanzia leo ninakuita ninakubatiza kwa jina la Ndoo. Wewe ni wa
kwangu. Watu wamenyang’anywa, YESU hakupati wewe uliyebatizwa kwa jina la mtu
mtafute mtumishi anayeongozwa na ROHO wa MUNGU akubatize tena na kufuta hilo
agano. Ikishindikana, njoo Moshono, nitakufungua. BWANA YESU asifiwe. Akaniambia,
waeleze wanangu, watumishi wengine wamebadilika, wanachukua picha na pesa za
waumini wanachimba pale madhabahuni wanafukia. Akaniambia, waambie wanazikwa
hapo. Hawatakaa wanione wala kufanikiwa kiroho, ni kurudi nyuma, wanakuwa
watumwa wa yule yule mtumishi. Sasa YESU anasema, mtu wake ndio yuko namna hiyo?
YESU aliyafanya hayo? Alichukua picha zenu akafukia chini? YESU aliwafungia
mashida na balaa na mikosi? Watu wengine wamekata tamaa, wameingia mpaka kwenye
wokovu wanataka kuacha wokovu maana tangu wameingia ndio mambo yamebadilika
kuwa mabaya zaidi. Watumishi 45% ni washirikina ulimwngu mzima lakini
wanalitaja jina la YESU. YEU akasema, siku ile ya mwisho nitakuambia sikujui,
sikujui. Oooh! Tulitoa pepo kwa jina lako,… sikujui. Iko siri kubwa sana hapo
mwana wa MUNGU. Akaniambia, hapa Tanzania nina watumishi wangu nilianza nao,
tena alikuwa anawatumia mpaka akina malaika Mikael anakaa nao, wengine alianza
nao hata katika biashara zao za kuuza maandazi na wengine katika hali Fulani mpaka
amewanyanyua. Ilikuwa ni jambo la kutisha maana ukisikia YESU, YESU kweli yupo.
YESU anaongea na watu na YESU anashuka. Akaniambia, hasira yangu nikishuka mimi
kama mimi, nchi yote, milima itasambaa, hakuna kitakachobaki lakini ninatumia
mwili wako mimi nitashuka kwa mwili wangu ule mwisho. Nenda niandalie kanisa. Usijidharau
ulivyo, niangalie mimi.
Japo utasemwa sana, usijali hata
mimi nilisemwa, utazushiwa maneno, tena furahi sana kama mimi nilivyofurahi
maana ndio unanyanyuliwa. Kama huna kitu cha MUNGU hufuatwi na na wanaokufuata
ni shetani yupo ndani yao. Hata mimi mafarisayo si walinifuata japo walikuwa
wanamuomba MUNGU? Ni MUNGU yupi anipinge mimi. Ndugu msikilizaji, ninakuomba na
ninakusihi rejea kwa BWANA YESU, uliyekata tama, wengine mmepigwa na watumishi,
wengine BWANA YESU akaniambia mnaenda makanisani wanawake, wachungaji au wale
viongozi wanawaangusha kiuzinzi wanawaambia bwana amesema. Akaniambia, mimi
ninakaa ndani ya mtumishi. Je, mimi nafanya uzinzi? Mengine akaniambia mwenye
pesa sasa hata akifanya uzinzi hagombezwi, lakini asiye na pesa hafanyi kitu,
atatangazwa kila mahali. Je, mimi ni MUNGU wa namna hiyo? Mimi ni MUNGU wa
haki. Rudi kanitumikie. Nikamuuliza, nitapata wapi pesa, akaniambia, habari ya
pesa achana nayo. Usifikiri, niulize mimi ndiyo director wa pesa. Nitakuletea watu,
na watu nawaleta mwenyewe. Kusi na kasi italeta, niangalie mimi. Anza Tanzania,
utaingia Rwanda, utaingia Uganda. Akaniambia, na wanafunzi nitakaokuwa nao
atawatumia kwa kiwango kikubwa sana; usiende shule ya aina yoyote. Nilizuia hata
elimu yako ulivyokuwa mdogo kupelekwa Marekani, nilizuia mimi. Nilikuwa
nikimkasirikia baba yangu kwa nini hanipeleki chuo, au shule; nilirudi na
kuomba rehema, kumbe ni YESU aliniambia mwenyewe alizuia maana wangesema
nimesoma mahali fulani. Utukufu wangu sishirikiani na mtu.
Ndugu msikilizaji, ni mengi sana
na katika vipindi vingine kutakuwa na na vipindi kwa ajili ya kuwaombea laivu
(live) kwa simu na unafunguliwa hapohapo. Haijalishi umekaa wapi, hata kwenye
msitu, utatolewa, YESU anashuka sasa kuwatoa watoto wake. Umekuwa ukizurura,
huna makao, YESU atakulisha kama kunguru anavyodondosha mkate. Ni wakati wa
kweli.
Ndugu msikilizaji, mrudie YESU
umwangalie BWANA YESU. Na wewe unayempenda YESU, endelea kumpenda BWANA YESU. Nina kitabu ambacho
tayari nimeshaki-register, kiko sawasawa, utakipata madukani. Kichwa cha habari
cha kitabu hicho “JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI”. Utayakuta mengi, mengi
japo kuna mengine mengi mengi. Ni wewe meletewa ujumbe na YESU upate kuelewa. Injili
yangu sio ya kibinadamu, mimi sikuitwa na mwanadamu. Paulo aliitwa na MUNGU
alileta ya ki-MUNGU vile vile. Haya ninayokueleza unaweza ukashangaa,
aliniambia, wewe ndio mtu wa pili kwenda kupeleka habari hizi laivu (live) sasa
baada ya mimi kuzisema wakati huo. Niliowatuma wamekataa, wameogopa lakini mimi
niko na wewe milele na milele. Wasaidie watu wote, wapende, wafungue, wasaidie,
japo wapo ambao watakuja kwa ajili ya kunisanifu, ameniambia atanionyesha. Kwa hiyo
ukija kwa ajili ya kunisanifu sikuhudumii.
BWANA YESU asifiwe. BWANA YESU
atusaidie. Akaniambia, watumishi wengi wameenda kuharibikia kwenye mabara ya ulaya. Wameanza vizuri, hapo wakienda ulaya
wanavalishwa majoho ya vyama fulani vya freemason wanapewa pesa nyingi sana
kwenye account zao zinatisha na mpaka nchi ya Tanzania imeingia kwenye mateso;
kanisa halijakaa mahali pake. Nchi itaponywaje sasa? lakini sasa hivi YESU
ameikamata Tanzania, mtaona mabadiliko yasiyo ya kawaida sasa kuanzia serikali
kila mahali. Elimu ya Watanzania iliibiwa, wanyama wa Tanzania waliibiwa
uthamani wao hata watu, wageni wanakuja wanaiba vitu. Uchawi mtupu…. Airport zote hakuna tena madawa ya kulevya
yatakayopita. Uchawi sasa hivi haufanyi haufanyi kazi. Hayo ni baadhi ya mambo
tu YESU aliniambia.
Sasa YESU aliingia hekaluni
akaykuta, leo wameyarudisha na kama
wameyarudisha ndugu msikilizaji, ninakuuliza, je, ni ya YESU au ni ya shetani?
Jibu ni ya shetani. Haya wanayoyafanya ni ya YESU? Jibu sio ya YESU. BWANA YESU
amekataa katu katu, na ili aonekane makanisani mambo hayo yaachwe majibu
mtayaona na majibu ya YESU sio mpaka utoe hela ndio ujibiwe. Hao wanokuambia
alikuja mtumishi mmoja akaniambia, sio mmoja, hata zaidi ya wane. Unataka umuoe
yule? Haya ngoja nitaomba, halafu unipe kiwanja basi. Jamani, YESU yuko hivyo? Mwingine
una madeni yako, anakuambia, ninaomba halafu ukisamehewa utanipa shilingi
ngapi? YESU yuko hivyo? Ndio kanisa sasa limekuwa hivyo. Sasa sio kanisa, YESU
amekaa pembeni na wako wengine watumishi ambao amewaandaa MUNGU anaenda
kuwafungua ambao wanataka kusema kweli yake. Wamekuwa wakifungwa na kubaniwa na
kukataliwa tena wanaitwa wana mapepo ya kuzimu na utambuzi. Nawaambia, wewe ni
bora zaidi. MUNGU akuinue huko uliko, MUNGU akubariki. Mwangalie YESU. Mwangalie
BWANA YESU. Mtegemee yeye peke yake. Mambo ya kuambiwa toa toa tu, YESU
hakufanya hivyo, amekataa; kanisa limepoteza ramani, direction, ni dunia nzima
manaosema Tanazania kwanini unasema hivi, ni dunia nzima mpaka wameona kanisa
halina nguvu, wameona ni shetani tu ana nguvu. Kila kitu ni Nigeria tu, ni
Nigeria tu. Mmeenda kuzimu. Manaona YESU hana hata pesa. YESU utukufu wake
umerejea sasa. Na kanisa la mwisho ndio hili limerejea. Jina la huduma hii
aliniambia kanisa langu liitwe YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, na
ndivyo nimelifanya. Sibadilishi, sipunguzi, ninamheshimu YESU. Wewe unayemdharau,
shauri yako. Moto unakusubiri. Tafuta ushirika
na YESU. Usiwe mnafiki, hata kama unakaa kanisani unanena, unanena unanena nini?
Watu wana majini yananena. Kipindi kijacho nitaendelea kuelezea. Naomba niombe.
Wewe ambaye hujaokoka nitakuongoza sala hii. Utengeneze maisha yako na YESU.
Hata na wewe mtumishi.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe
makosa yangu yote, niliyoyatenda kwa kujua au kwa kutokujua, nishike mkono
BWANA YESU. Nitengeneze, nifungue fahamu zangu nikujue wewe YESU wa kweli. Nikujue
wewe YESU wa kweli. Nimekutafuta sana, na sijakuona. Nishike mkono sasa.
BABA, asante kwa majina ya watoto
wako, upige mhuri duniani na mbinguni, roho hizi zote zilizokusikiliza,
watengeneze, wakumbatie. Usimwache hata mmoja aliyekusikiliza, nakuomba aurithi
ufalme wa mbinguni. Napiga muhuri duniani na mbinguni, BABA yangu na MUNGU
wangu, nakuomba, nakurudishia sifa na utukufu. Kwa nyie wagonjwa, ninatuma
malaika, mahali popote unapoumwa ninatuma malaika waende wakarejeshe wengi
wamekuwa makaburini, nyota zenu, fahamu zenu. Mliofichwa kwenye makanisa ya
kipepo nawachomoa, akili zenu, fahamu zenu, baraka zenu, uthamani wenu, ndoa
zilizofungiwa kwa waganga, kwa wachawi mpaka kwa lusifa mliowekwa malaika
Mikael nenda na kikosi chako kila mahali kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI.
Mabara yote waliowekwa makaburini, baharini watolewe wote. Nyota zao kwenye
maduka, kwenye maviwanda, dunia nzima kwenye milima kule upareni Same mtolewe
wote kwa jina la YESU. Mliochukua nyota za watu, vyeo vya watu dunia nzima,
serikali ya aina yoyote mnaotumia uchawi ninauharibu kwa jina la YESU KRISTO wa
NAZARETI. Ninaharibu mipango yenu yote. Ninawateketeza na YESU
amekwishawashikilia wote mnaoteswa; mwisho wa kuteswa. Yeyote anayekupeleka kwa
mganga malaika kamata, teketeza na hakuna uganga utakaofanyika na uchawi juu ya
mtu yeyote. Maisha yaliyokwama, kukata tama na wewe unayetaka kujiua hakuna
kujiua katika jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Roho za mauti, pepo la ukimwi,
cancer, asthma toka katika jina la YESU. Nyie mliowapata waume na wanawake kwa
kwenda kwa waganga ninafuta hizo ndoa katika jina la YESU. Na makanisa
yaliyopitisha hizo ndoa, YESU hahusiki kupitisha ndoa za kipepo katika jina la
YESU. Kanisa limepigwa upofu, lishindwe katika jina la YESU. Ndio maana ndoa ni
shida, balaa na mikosi na watumishi wanasema BWANA amefanya. BWANA hajafanya.
YESU hashirikiani na kanisa la kipepo. YESU hashirikiani na mtu anayenda kwa
waganga, ninafuta katika jina la YESU. Na nyie wanawake mnaowaloga waume zenu,
kuwakamata waume wa watu waachilieni mara moja dunia nzima. Hakuna lolote
litafanyika katika jina la YESU. Mnaopanga kuua watu na kufukia ndani ndani mpate madini watu wote
wale natuma malaika wakatolewe waogeshwe kwa damu ya YESU waongozwe sala ya
toba na malaika wa Injili, pelekwa Paradiso. Misukule mnaowekwa kwenye magari
mtolewe wote kwa jina la YESU KRISTO wa NAZARETI. Akili zenu zilizofukiwa
ardhini umekuwa taahira hujielewi nakufungua kwa jina la YESU KRISTO wa
NAZARETI. Na wewe uliyepewa cheti cha ‘congratulation’ unatoa fungu la kumi,
hilo kanisa limekuga katika jina la YESU na ndio maana matokeo yake
haufanikiwi. Ati hongera unatoa fungu la kumi vizuri. YESU ametoka wapi kusema
mambo hayo. YESU hakusifu. Hiyo ni saikolojia kutoka kwa shetani baba yao
lusifa. Eti hongera; na wewe mtumishi unayechukua majina majina ya watu unasema
unasoma, hawa wametoa fungu la kumi unawataja pale mbele wewe MUNGU amesema
kulia wala kushoto isijue. Hayo unayoyazungumza yametoka wapi? Wacha, wacha
katika jina la YESU. Utapeli mtupu kila mahali, wacha. Na usitishwe mtu yeyote unayesikiliza,
usiogope tai, usiogope joho. Mwangalie YESU, kama hana YESU ndani yake ni
mshanii chapa mwendo katika jina la YESU. Usiwe mtumwa, wewe ni mtumwa wa BWANA
YESU.
BWANA YESU asifiwe. Kuna mtu
mmoja, wewe ambaye umekaa mguu wako umepinda na mbele yako unaona sura ya mbwa
hiyo sura ya mbwa ni pepo la uzinzi, ninaliondoa sasa hivi kwa jina la YESU
KRISTO wa NAZARETI na mguu wako ninaufungua unyooke moja kwa moja katika jina
la YESU KRISTO wa NAZARETI. Wewe mwenye cancer ninaiondoa kwa jina la YESU
KRISTO wa NAZARETI. Ninakutamkia uzima, wewe mwenye uvimbe na utumbo ambao
umeshonwa nyuzi zinaachia zinatoboa damu inatoka, ninakufunga kwa jina la YESU
KRISTO wa NAZARETI. Mliopangiwa kufa, wote mnaosikiliza ulimwengu mzima
ninafuta hamna kufa kifo cha kipepo, utakufa kifo cha MUNGU tu peke yake, kifo
anachotaka kwa wakati wake na kwa makusudi yake. Watu wengi wanateseka, kanisa
limekosa mwelekeo. Mnaenda kwenye maombi, mnaomba Januari mpaka Desemba hakuna
majibu; matokeo yake nguo zinatoboka, suruali zinatoboka BWANA hafanyi; hakuna,
ni usanii tu. MUNGU ameniambia; MUNGU amekuambia nini? Wewe unayesema MUNGU
amekuambia, wewe umejiona matawi ya juu eti una experience kwenye kazi ya
MUNGU, Kazi ya MUNGU haina experience, anaifanya mwenyewe. Na nyie mnaotumia
maandiko, maana akaniambia shetani anatumia Biblia. Nikamuuliza, sasa kwa nini
anatumia Biblia? Akaniambia, shetani anaifahamu Biblia lakini anaitumia katika
maandiko. Shetani hana NENO (udhihirisho). Neno linaponya, maandiko ni historia
tu. Hata wengine wanaenda kwa waganga wanaambiwa ngoja nimuulize MUNGU nisome
Biblia. Sasa jiulize, MUNGU anashirikiana na shetani? Hapana. Lakini shetani ni
aina ya mungu na ndiye aliyeukamata ulimwengu lakini sasa mwisho wake. Unabaki kusema,
Neno la MUNGU linasema mstari Fulani itakuwa hivi, nitabarikiwa, atatuponya. Hakuponyi,
kwani kwanza hauna nafsi, hauna ufahamu au umezikwa. Ni umasikini tu. Nyumba zenu zote malaika
sasa hivi waingie fyeka fyeka mapepo katika jina la YESU. Na nyie mlioanguka
hapo msiogope hapo wenzenu msiogope malaika wanawafungua wanawatoa kila kitu. Wenye
upofu ambaye amesogeza jicho lake kwenye redio, ninalikomboa lile jicho,
ninaondoa katika jina la YESU. Na umrudishie YESU sifa na utukufu. Usiniinue mimi,
mimi ni mwanadamu, ni chombo tu.
Ndugu msikilizaji, mwangalie
YESU, mwangalie YESU anarudi.
Maombi ni bure na lazima umuone
MUNGU. Hakuna cha baadaye, hapo hapo kama alivyofanya YESU. Hakuna hela ya
sadaka ya ukombozi. Wewe umewekwa gerezani huna hata shilingi kumi, unaambiwa
ulete hela ndio uombewe; huyo sio MUNGU, cha shetani lazima ulipe. Wewe unakuta
upo ICU, huwezi hata kupumua, unaambiwa MUNGU amesema ulete sadaka mara tatu. Uwongo.
YESU ameniambia, wapende, waombee, wasaidie; nimekupa bure toa bure. Hao wanaosema
pesa, ni nguvu ya shetani. Kwa maelekezo zaidi, ingia kwenye website yetu www.prophethebron.org, kuna blog kuna
masomo mengi. Utafunuliwa sana. MUNGU akubariki, MUNGU akuinue sanana. Umetoka gerezani,
wewe ni mshindi sasa. Pokea afya, pokea uzima, pokea amani, uishi salama, mwaka
mzima uwe ni mwema kwako, umfurahie YESU. Amen.