Kama nilivyokuisha kufundisha katika blog yangu kuhusu
msalaba ni nini na nikaelezea kuwa hakuna msalaba mtakatifu katika ulimwengu
wote wala haipaswi kuitwa msalaba mtakatifu sababu ni MUNGU peke yake ndiye
anayestahili kuitwa mtakatifu, yeye hatendi dhambi. Msalaba ulitumika kuwaulia
watu walio laaniwa katika kipindi hicho cha zamani. Nataka uelewe pia hata
msalaba aliosulubiwa nao YESU kipindi hicho, msalaba huo huo ulishasulubia
wengine kabla yake, ilipokuwa inatumika ilikuwa ilikuwa inahifadhiwa tena hadi
itokee mtu ahukumiwe kifo tena. Ukisoma katika kitabu cha Yohana 14: 6 inasema
hivi, YESU akawaambia mimi ndimi njia na kweli na uzima. Mtu haji kwa BABA ila
kwa njia ya mimi. Nataka muelewe enyi watu wote wa mataifa yote mnaompenda
MUNGU na hamtaki mumkosee MUNGU kwa kutokujua japo wapo wanaojua kabisa
wanafanya makusudi ili kuwapoteza watu na kuwapeleka jehanamu.
Ili uende mbinguni njia ya kukupeleka ni YESU peke yake na
njia hii ni katika roho na tena ni mpaka uokoke na uishi katika maisha
matakatifu na kulifuata neno la MUNGU kama lilivyoandikwa katika biblia wala
kulibadilisha au kulichanganya na uongo. Katika ulimwengu huu inashangaza sana
shetani analitawala kanisa katika sehemu mbali mbali kwa kuanzisha ibada za
njia ya msalaba. Sasa nikuulize wewe msomaji tafuta katika biblia hautaona
tumeambiwa tufuate njia ya msalaba ili kutupeleka mbinguni, hakuna. Na kama
hakuna basi hayo ni mafundisho ya jehanamu ambayo uliyafuata unakuwa na wewe
unaifuata njia ya Jehanamu. Na pia nataka uelewe kila unaposhiriki ibada ya
njia ya msalaba ina maana na wewe katika ulimwengu wa roho una beba msalaba
ukahukumiwe kwenda jehanamu, na hata unapovaa msalaba shingoni ina maana wewe
upo tayari kuhukumiwa na shetani na YESU alibeba ili tusisulubishwe tena.
Sasa nawauliza mataifa je yale mateso aliyosulubiwa YESU ni
ya bure? Sasa kama siyo ya bure je hamuoni kuwa huku ni kumkufuru MUNGU? Na kama
ni kumkufuru MUNGU basi malipo yake ni jehanamu. Na zaidi watu wakapotezwa
kabisa haikutosha njia ya msalaba tu, bali wakaamua kutengeneza mwili wa bwana
na wakauwekea alama ya msalaba hata mimi Hebron nilisha ila sana pasipokujua,
ila nilipojua ukweli nilitubu na nikaponywa na YESU. Sasa unapokula huo mwili
wenye msalaba ujijue nafsi yako imekula hukumu na katika ulimwengu wa roho
mapepo ya kiyahudi yanakuhukumu bila kipingamizi na utakapokufa unaenda
jehanamu.
Sasa mfunguke, amenituma YESU WA NAZARETI niwaeleze ukweli
na wewe utakayeupokea utakuwa huru. Na pia hata unasali pale unapoweka alama ya
msalaba kwa kulitaja jina la baba na mwana na roho mtakatifu uelewe ni njia ya
kumdharau MUNGU na kumfanya yeye ni msalaba wakati MUNGU hafananishwi na
chochote. Sasa fikiria ni mara ngapi umemuuzi MUNGU kwa kumfananisha na msalaba
au ni mara ngapi umeifuata njia ya jehanamu? Na hata ukaletwa katika nyumba
yako. Ikatae kuanzia sasa na ujitenge ili usije ukachomwa moto siku ile ya
mwisho na wote wanaoendelea na njia hizo bila kutubu na kutoka katika madhabahu
za jinsi hiyo hawatapona na tena waokoke.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote. Uniandike
katika kitabu cha uzima wa milele na unitoe miguu yangu katika njia ya Jehanamu
na niifuate njia yako ya mbinguni ambayo ndiye wewe YESU na siyo kingine. Amen.
NABII HEBRON.