Pages

Tuesday, January 20, 2015

DALILI ZA KUJUA KANISA NA MTUMISHI ANAYEONGOZWA NA ROHO MTAKATIFU 100%.

Katika neno la MUNGU katika kitabu cha Yohana 14:  16-17
16 Nami nitamwomba BABA, naye atawapa msaidizi mwingine, ili akae nanyi hata milele; 17 ndiye ROHO wa kweli; ambaye ulimwengu hauwezi kumpokea, kwa kuwa haumwoni wala haumtambui; bali ninyi mnamtambua, maana anakaa kwenu, naye atakuwa ndani yenu.”

YESU aliahidi kutuletea ROHO MTAKATIFU ili awe ndiye msaidizi wa kusimamia kazi za MUNGU katika dunia hii na kuwaongoza watoto wa MUNGU katika ile njia ya MUNGU na kulithibitisha neno la MUNGU kama ilivyoandikwa katika biblia ikiwemo pamoja na kutuombea. ROHO MTAKATIFU yeye ana umoja na MUNGU BABA, NA MWANA hana unafiki hivyo lililopangwa na hao watatu nao ni lazima lifuatwe lilivyo sababu mpaka sasa wote watatu ni marafiki na hawajagombana na hawatagombana milele, na pia wote watatu ni marafiki zangu wakubwa. Wamenituma nikaeneze habari njema kwa watu wote na nikisaidiwa na ROHO MTAKATIFU. Nitaelezea kwa ufupi ili upate kuelewa japo kidogo sababu watu wengi hawaelewi.

·        Kanisa linaloongozwa na ROHO MTAKATIFU kwanza ni lazima huyo kuhani awe ameteuliwa na MUNGU peke yake na siyo mwanadamu.

·        Kanisa hilo ni lazima watu wabatizwe katika maji marefu yanayotembea kama vile YESU alivyobatizwa.

·        Huduma za kiroho hutolewa bure, hakuna kuchajiwa malipo ya aina yoyote ile.

·        Hakuna michango wala harambee, wala hakuna kuandika sadaka majina wala email, wala namba zako za simu, wala hakuna kushawishiwa utoe sadaka bali ni hiari yako wewe na MUNGU ili akubariki pamoja na asante yako kwa MUNGU.

·        Halina watu wanaoitwa partners kabisa.

·        Halikopi pesa benki wala halifanyi biashara linaongozwa na bwana mmoja tu na siyo mabwana wawili.

·        Linasema kweli na halibadilishi neno la MUNGU au kuchanganya mahali pengine ukweli na uongo.

·        Halina huduma sita lina huduma tano tu alizozianzisha YESU. Nabii, Mtume, Mchungaji, Mwinjilisti, Mwalimu basi, hii ya sita YESU hajaileta ni pando la shetani kupitia roho mchafu (uaskofu).

·        Watumishi wake hawavai kofia wanapohubiri au kubeba silaha wakiwa kanisani mfano fimbo, mkuki (hairuhusiwi na MUNGU).

·        Hawavai majoho (Majoho yalitumika tokea zamani na mafarisayo kama ndiyo uniform na YESU yeye hakulijenga kanisa la mafarisayo, tena ndiyo lilimpinga hata kumuua. Hayo majoho yanawakilisha roho ya ufarisayo.

·        Kuhani ni lazima awe na mke mmoja, siyo mzinzi, mlevi, mchawi, mnyang’anyi. Anatakiwa awe mtakatifu kweli kweli.

·        Halina ibada za wafu, ibada za misalaba, hawaabudu sanamu, hawabariki pombe na kila muumini wake ni lazima aokoke.

·        Halifanyi miujiza ya kipepo mfano kufufua misukule au kutoa watu vitu katika miili yao mfano mawe, chuma, nywele (huo ni uchawi).

·        Kanisa haliwi omba omba.


NOTE:
Yapo mambo mengi sana ila endelea kusoma makala ya Nabii Hebron wa Arusha yapo mengi yatakutoa katika giza na hautabakia tena kuongozwa na kanisa ambalo haliongozwi na ROHO MTAKATIFU.


NABII HEBRON.