Pages

Wednesday, January 21, 2015

DALILI ZA KULIJUA KANISA  NA MTUMISHI ANAYEONGOZWA NA ROHO MCHAFU 100%.

Kama nilivyokuisha kusema katika makala ya dalili ya kulijua kanisa linaloongozwa na ROHO MTAKATIFU, hivyo hivyo na shetani na yeye alituma msaidizi wake ili kuja kuwasaidia wale watakao kataa kufuata kweli na kuwasaidia kuwapeleka jehanamu. Kazi ya roho mchafu ni kazi ya mpinga kristo ambayo kazi yake ni kulibadili neno la MUNGU kama vile ilivyo sasa katika mataifa mbali mbali, watu wanajiita ni wakristo lakini kumbe ndiyo maadui wakubwa wa MUNGU sababu ya kuongozwa na roho mchafu kwa njia ya kuwapiga watu upofu wanatumia biblia lakini wanachanganya ya kweli na ya uongo. Na tukijua kuwa nuru na giza hawachangamani au YESU na shetani hawana ushirika ila biblia inatumiwa makanisani halafu na mengine yanaongezwa, inapokuwa hivyo tu uelewe hapo yupo pepo au roho mchafu ndiye anayesimamia kuwaongoza na kuwasimamia hilo kundi ili alipoteze kwa kwenda jehanamu. Nitaelezea mambo machache ya kuelewa kanisa au mtumishi anayeongozwa na roho mchafu na mtapona sababu watu wanafikiri wanaongozwa na ROHO MTAKATIFU kumbe ni roho mchafu anajaa sehemu nyingi katika ulimwengu wote.

·        Inawezekana mtumishi aliitwa na MUNGU kabisa ila alipomsaliti YESU tu basi anakuwa anaongozwa na roho mchafu.

·        Watumishi wake huteuliwa na wanadamu na pia hawajaitwa na MUNGU wala hajawahi hata kusikia akiitwa na MUNGU, hawa wanajiita, wanatafuta pesa au mishahara tu.

·        Kanisa hilo ni lazima libatizwe ubatizo ambae siyo YESU alibatizwa nao na siyo ubatizo wa Yohana wa maji mengi yanayotembea na yamejaa tele wala siyo ya kisima, hapa tayari roho mchafu amepindua neno la MUNGU.

·        Utakuta mtumishi anabatiza kwa jina lake iwe ni ubatizo wa maji mengi au ya kikombe.

·        Wanabatiza watoto wadogo na kubariki watu wazima (hii ni tofauti na biblia).

·        Watumishi wake wanavaa kofia, wanaingia na fimbo na mikuki kanisani wakati biblia inakataa.

·        Wanaabudu wachungaji kama ndiye mungu wao na wengine huwaita wao ni mungu wa majeshi, mungu mweusi, mungu mweupe, na wenigne hujiita wao ni YESU.

·        Huta huduma za kiroho kwa malipo mfano wanadai sadaka ya ukombozi au vitu vyako ndio wakusaidie kama ilivyo kwa mganga wa kienyeji anavyoongozwa na mapepo anateka vitu vyako.

·        Wanaabudu sanamu, misalaba, kufungisha ndoa za mashoga, bariki pombe, wanaandika sadaka majina, na email na namba zao za simu na kiasi.

·        Wanatoa vyeti vya hongera kwa wale wanaotoa pesa nyingi na kuwasoma madhabahuni wapigiwe makofi.

·        Makanisa yenye watu wanaoitwa partners (special).

·        Yanakopa pesa na kulipa riba na mengine yanachaji watu riba.

·        Wanafanya miujiza ya kipepo.

·        Makanisa yao yana nembo za freemason na illuminati.

·        Wengine viongozi wao ni wanachama wa illuminati na freemason.

·        Makanisa yana huduma sita badala ya zile tano alizozianzisha YESU ikaongezewa ya sita ya uaskofu na zipo nyinginezo kwa majina yake zinafika kumi na zaidi.

·        Walevi, wazinzi, wachawi, wanyang’anyi na kutenda ufisadi.

·        Watumishi wake ili umuone lazima utoe pesa na wengine ili umguse ni lazima utoe kiwango fulani cha pesa ndio akuombee au unayetoa kiasi kikubwa cha pesa utasaini katika suti yake katika mabega yake na wale wa viwango vya chini wanasaini katika suruali eti ndiyo watakayobarikiwa. Hawa ni mapepo ndiyo yapo ndani yao yanaiba pesa za watu na roho inayofanya kazi hapo haina tofauti na roho za wachawi au waganga wa kienyeji. Kiongozi ni roho mchafu.

·        Kufanya ibada za wafu.

·        Wakati wa kuapishwa kuifanya hiyo kazi wengine wana lala chini ndiyo kiapo chao.

·        Ni mambo ya dini na sheria kama enzi za Mafarisayo ndiyo zinaendelezwa.

·        Wanabatizia ndani ya kanisa lipo kisima.

·        Fungisha ndoa za kishoga na kufungisha kwa agano la shida.

·        Watumishi baadhi wapo katika mtandao wa internet ni illuminati na freemason.

·        Hakuna kuokoka na wengine wanasema ukiokoka umepotea.


NOTE:

Hii yote nimekufunulia uelewe jinsi kanisa la sasa katika dunia yote kiwango kikubwa sana linaongozwa na roho mchafu kama ndiye msaidizi wa kuyaendeleza hayo ambayo hayapo katika biblia na kama hayapo basi jiulize yametokea wapi? Wakati biblia imeeleza neno la MUNGU lisiongezwe au kupunguzwa chochote, MUNGU amekihakikisha na akaupiga muhuri. Sasa niwaulize je kama MUNGU amepiga muhuri biblia ndiyo katiba yake ifuatwe na ukienda kinyume ujue umeivunja katiba ya MUNGU na hata katika nchi yeyote unapoivunja katiba unashtakiwa na kuhukumiwa. Hivyo ndivyo ilivyo na wakristo wengi na makanisa tayari yamejiingiza katika hukumu kwa kuongozwa na roho mchafu na adhabu yake imeandikwa katika kitabu cha Ufunuo 22: 18-19, je na wewe upo upande upi? Sasa utubu sema

BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu sikujua kama naongozwa ma roho mchafu na nikaishi chini ya ufalme wa roho mchafu naomba unisamehe. Uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Namkataa shetani na roho mchafu kwa jina la YESU WA NAZARETI nakuunguza uteketee, achilia nafsi yangu sasa hivi. BWANA YESU nishike mkono na ROHO MTAKATIFU aniongoze na siyo tena roho mchafu. Niongoze YESU katika kanisa linaloongozwa na roho wako mtakatifu wa kweli. Amen.



NABII HEBRON.