Pages

Wednesday, January 7, 2015

UNABII KATIKA NCHI YA TANZANIA 2015.

Nawasalimu kwa jina la YESU WA NAZARETI aliye hai na kwa jina lingine anaitwa Nabii Issa, yeye ambaye atakuja kulinyakua kanisa lake na pia atakuja katika wakati wa kiama. Yeye ndiye aliyenituma nikafanye kazi yake na akaniambia katika nchi uliyotokea MUNGU alikuisha iandaa ndiyo Edeni yake ya sasa ila nitaiinua mimi mwenyewe YESU (Nabii Issa) kwa utukufu wa MUNGU mbinguni. Tokea mwaka 2012 April kama nilivyoelezea katika vipindi vya redio, television, na hata katika makala ya Nabii Hebron mengi mmeyaona na yametokea, nilisema uchawi haufanyi kazi tena katika nchi ya Tanzania, na katika meneo yote na mmeona. Walioiibia nchi wakatumia na uchawi ili wasijulikane wamejulikana, nilisema mawaziri wazembe, waizi na wasio waaminifu watafukuzwa na wengine wataacha wenyewe na mmeyaona, zaidi usome makala ya Nabii Hebron 2012, 2013 kuhusu nchi ya Tanzania utayaona yametimia, nilieleza mengi ila yasome tena na na uangalie tarehe yaliyotokea, unabii wa Nabii Hebron kuhusu nchi umetimia kuanzia kiuchumi, amani na mengineyo imetimia kuhusu viongozi wa nchi kunyanyuliwa yaani Rais Jakaya Kikwete katika Umoja wa Mataifa, viwanja vya ndege, mbuga za wanyama na mengineyo mengi kama nilivyoelezea huko nyuma.

Haya yote ni MUNGU kayafanya ili kuiinua nchi yake kama Edeni ya pili ambaye hata sasa yeye yupo Tanzania na ndio sababu Tanzania haitakaa ivamiwe na nchi yeyote ile na tokea niwaeleze haijatokea nchi ya Tanzania kuvamiwa kivita na haita tokea, huo ndio ukweli japo wapo maadui wa nchi hii waliopo nje ya nchi na hata ndani ya nchi hawatafanikiwa lolote wakafanye kazi nyingine watafanikiwa ila siyo kuigusa nchi hii, hata kama ni nchi matajiri kiasi gani hawataweza na wameshashindwa tokea 2012. Hayo mengine ni yangu mimi mwenyewe kama nilivyoelezwa na MUNGU. Katika mwaka 2015 yapo mambo mengi ambayo MUNGU atayafanya yeye peke yake na lazima yatatimia kabla ya 2015 kuisha na hata sasa tayari ameanza mengine:-

A.    UCHUMI
Uchumi utapanda na kuvunja historia tokea nchi ipate uhuru. Uchumi utakuwa zaidi katika viwanda, mbuga za wanyama, madini, viwanja vya ndege na Watanzania wataongezeka kununua ndege zao binafsi za usafirishaji.

Katika kilimo 2015 mvua zitanyeesha nyingi na kwa wakati na ardhi itazaa zaidi sababu ardhi imerejeshwa uthamani wake ulioibiwa na joka kuu pamoja na baadhi ya wakoloni na wawekezaji ambao waliwekezaga katika nchi hii wakiwa wana nia ya kuifilisi tu na siyo mema. Mashamba ya serikali yatafufuka na viwanda vilivyokufaga na yale niliyotabiri 2012, 2013 yataendelea kuwa juu na kukua zaidi. Haya yote ni MUNGU ndiye aliyeamua wala hakuna wa kuzuia tayari imeshakuwa na MUNGU ameniambia Hebron nitayafanya haya yote na mengineyo.

B.    BUNGE
Kama nilivyokuisha sema bunge la Tanzania linabadilishwa na MUNGU kalishika yeye peke yake. Mliona bunge lilivyobadilika wakijali maswala ya nchi hii, na kufichua uovu na mengineyo. 2015 watafanya zaidi na yapo mambo mengi ambayo MUNGU atawafungulia wabunge wayajue tena kwa wepesi na yatafichuka peupe peupe, ikiwemo rushwa, mikataba mibovu, uwizi wa pesa za nchi katika manispaa na wizara mbali mbali. Wabunge watakuwa wakali sana katika kusimamia maswala ya sheria za nchi hii tofauti na 2014, MUNGU ameshayaandaa hayo na mengineyo ambayo sijaruhusiwa niyaseme.

C.     UNABII KUHUSU RAIS WA TANZANIA 2015.
Kama nilivyoelezea 2012, 2013, 2014 kuhusu Rais wa Tanzania 2015, tayari MUNGU amekuisha muandaa mwaka huu na uchaguzi nawaeleza rais hatatoka kwa waganga wa kienyeji au  kwa kuiba kura au kwa kuwanunua watu kwa pesa. Wengi wanaotamani cheo hicho watatoa pesa na kuwahonga watu ili wawachague wakianzia katika vyama vya siasa na katika makundi makundi, haya yote MUNGU kasha yaona. Nawaeleza, muache, mtajuta kwa jinsi mambo yatakavyogeuka. Watu walizoea wanajipangia wenyewe, mwaka 2015 MUNGU atamweka rais peke yake kupitia Watanzania ambao ni watoto wa MUNGU aliyewaumba yeye, hawatalogeka, siku ya uchaguzi atawabadilisha wapige kura kwa yule ambaye MUNGU anamtaka na nataka muelewe Watanzania siku zote kusudi la MUNGU halizuiliki kabisa na ndivyo itakavyokuwa maajabu 2015. Itakuwa hivyo hivyo pamoja na Zanzibar pia.

D.    UCHAGUZI WA UBUNGE.
Wabunge wapya wataingia katika bunge na wapo ambao ikikaribia kipindi cha uchaguzi watakosa kupewa nafasi na vyama vyao. Wengi watahamia katika vyama tofauti tofauti na baadhi yao 70% watashinda ubunge, wapo mawaziri watakaopoteza ubunge kabisa na hii itafanyika pia kwa madiwani, madiwani wengi watakuwa ni wapya. Na pia mpaka sasa wapo wabunge ambao tayari nawaona wameshapita katika uchaguzi wa ubunge na ushindi ila wakati wake wa kuyasema haya sijaambiwa, haya alinijulisha MUNGU wakati nikiombea nchi kwa jinsi nilivyomuomba yeye anionyeshe ila akanionya usiyaseme hayo na mimi ninayatii maneno ya BABA yangu wa mbinguni.

NOTE:

Watakaotumia uchawi hawatashinda kiti chochote, MUNGU hapendi uchawi kabisa. Yeye atasimamia uchaguzi mwenyewe na mtaona waliotumia uchawi watakavyoaibika baadhi yao. Na pia wengine watashindwa kutokana na hali ya wananchi kutokumpigia kura pasipo yeye kushiriki uchawi katika hali ya kawaida tu.

MUNGU IBARIKI TANZANIA, UZIDI KUIINUA KATIKA JINA LA YESU WA NAZARETI. AMEN.


NABII HEBRON.