JE UNAJUA NI
JINSI GANI MAKANISA YALIVYOJIINGIZA KWA MIUNGU NA KUJITENGA NA MUNGU WA KWELI?
WAGALATIA 1: 15-16
“15 Lakini MUNGU, aliyenitenga tangu tumboni mwa
mama yangu, akaniita kwa neema yake. 16 alipoona vema kumdhihirisha
mwanawe ndani yangu, ili niwahubiri Mataifa habari zake; mara sikufanya shauri
na watu wenye mwili na damu.”
BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI, mataifa mlioumbwa na
MUNGU aliyeumba mbingu na nchi MUNGU anawapenda sana ili msiangamie na hata
mlioangamia tayari endapo utayasikiliza maneno haya nikuelezayo Nabii Hebron na
wewe utapona. Alichonituma MUNGU ni kuharibu ufalme wa shetani katika ulimwengu
wote na kubomoa ufalme wa miungu yote ya kila aina katika dunia hii na hata
iliyopo kuzimu na kazi hiyo imeshaanza. MUNGU anataka aabudiwe yeye peke yake
wala siyo kupitia vitu alivyoviumba yeye mfano hata jua, mwezi, nyota, miti,
wanyama, hata vya kazi ya mikono ya wanadamu kama vile vinyago au sanamu.
Nitaelezea kwa ufupi na naamini utaelewa na utapona na
utakuwa huru. Shetani pamoja na miungu yake wamejiingiza katika makanisa mengi
katika ulimwengu wote na kumfanya MUNGU wa kweli asionekane katika makanisa na
wakabakia miungu tu 98% ya makanisa yote katika dunia ni makanisa ya miungu
ndiyo inayoyaongoza pamoja na waumini wake, na hata waumini hawaelewi ni ki
vipi wanaabudu miungu na bado wanajiita ni wakristo au kanisa ni la kikristo na
wanasoma biblia na kila jumapili wanaenda kanisani. Walifikiri wanaenda
kumuabudu MUNGU wa kweli na kumbe wamepigwa upofu kimwili na kiroho na kumbe
wanaabudu miungu na kufanyika kuwa rafiki wa miungu na kuwa adui wa MUNGU wa
kweli. Nawafunulia haya mimi Nabii Hebron sababu hata mimi katika maisha yangu
nilipotezwa kwa kufundishwa uongo nikajiona ni mkristo safi namfurahisha MUNGU,
ila aliponiita nikamtumikie 2010 hapo ndipo nilijiona nilikuwa ninanuka harufu
mbaya mbele za MUNGU, sababu sikuujua ukweli na akaniambia mimi ndiye niliye
kuumba wewe na hata mifupa ya nyama katika mwili wako ni mimi ndiye niliyeipa
nguvu ikue na ukuwe mpaka ulipofikia hapa. Nimekuumba kwa kusudi langu peke
yake na nilijua ikifika muda wake nitakutumia ila wewe hauna tofauti na Musa
nilivyomuita nikamficha hata alipowekwa katika mto ule ni mimi MUNGU ndiye niliyoifanya hiyo
njia kumhifadhi mpaka wakati ulifika akawatoa wana wa Israeli na wewe ndiye
Musa wa sasa uwapeleke watu Kaanani kwa jinsi nilivyokuelekeza.
Katika makanisa ya sasa pamoja na watumishi wengi wao siyo
watumishi wa MUNGU bali ni watumishi wa miungu na watu wameshindwa
kuwatofautisha watumishi wa MUNGU wa kweli na wa miungu sababu wote wanajiita
ni watumishi wa MUNGU. Kila jambo unaloliona mtumishi analifanya lipime katika
neno la MUNGU, je anafuata kweli au uongo, ki vipi? Nitakueleza na utaelewa.
A.
Watumishi wa miungu.
Hawa ni watumishi wachungaji, wainjilisti, manabii, mitume,
waalimu vile vile ila wewe cha kukusaidia ili umuelewe yupo katika upande gani
chunguza haya kwa watumishi wa miungu na bado wanalitaja jina la YESU na kumbe
tayari ni watoto wa shetani au waajiriwa wa shetani na ndiyo sababu
wanaziendeleza kazi ya baba yao.
·
Ukikuta mtumishi hajabatizwa kwa ubatizo wa maji
mengi ambao upo katika biblia umetoka kwa MUNGU wa mbinguni, uelewe yeye yupo
upande wa miungu na ndiyo sababu amebatizwa kwa ubatizo wa maji ya kichwa tu au
kisima, au kubatizwa kwa jina la mchungaji, watumishi wa aina hii wote
wawaeleze wapo chini ya miungu.
·
Watumishi wanaonyang’anya watu mali zao kwa
kusema au kutumia jina la YESU hao ni majambazi na ni wanyang’anyi, na kazi ya
unyang’anyi ni ya miungu bali MUNGU yeye hubariki.
·
Anayezini na kondoo au waumini, mlevi, anafanya
mazingaumbwe anachangisha watu pesa kanisani katika kanisa na waumini wanatii
waelewe hapo sipo mahali MUNGU wa kweli yupo, bali ni makao ya miungu, MUNGU
amekataa mahali pake ni mahali pa sala tu na kumuabudu yeye na kumsifu, ila kwa
miungu mambo hayo yanaruhusiwa na miungu, inawatendea watu miujiza ya kipepo
sasa uelewe jinsi miungu ilivyojiingiza kwa njia ya makanisa, na makanisa mengi
yanajengwa kwa pesa za miungu na maagano ya shetani. Nilikwisha wafundisha kuwa
yupo yesu wa uongo na sasa nawajulisha pia yapo mungu wa uongo na yeye ndiye
joka kuu, ila yeye anayo makundi mengi mengi ya miungu kwa jinsi alivyoiumba
ili kuwapotosha wanadamu na kuwafarakanisha na MUNGU wa mbinguni ndio wanadamu
wasiwe watoto wa MUNGU wawe watoto wa miungu na kuwa adui wa MUNGU aliyeumba
mbingu na nchi.
·
Watumishi wote wenye kofia za kuvaa wakiwa
wanahubiri, hiyo ni alama ya miungu sababu imeandikwa mwanaume anapohubiri
kanisani asivae kofia sababu kichwa chake ni mahali ambapo MUNGU anapitishia
utukufu wake, ila miungu wamejiingiza katika kanisa na watumishi wameikubali. Kukubali
ni kule kuyatii mambo ambayo MUNGU ameyakataa halafu wanayatenda na hata
kuyafanya ndiye uniform zao, hizo ni uniform za miungu.
·
Wagalatia 1: 6-8
“6 Nastaajabu kwa kuwa mnamwacha
upesi hivi yeye aliyewaita katika neema ya Kristo, na kugeuka injili ya namna
nyingine. 7 wala si nyingine; lakini wapo watu wawataabishao na
kutaka kuigeuza injili ya Kristo. 8 lakini ijapokuwa sisi au malaika
wa mbinguni atawahubiri ninyi injili yoyote isipokuwa hiyo tuliyowahubiri na
alaaniwe.”
Neno la MUNGU linaonyesha wazi wazi,
unapoigeukia injili ya tofauti na biblia au kuchanganya na uongo tayari
umelaaniwa, hii ni sababu MUNGU tayari yeye ameshalaani miungu yote na mambo
yake na miungu ikafanya ujanja ikawateka watumishi na wengine siyo kutekwa
wamejipeleka kwa miungu ili iwasaidie katika kazi za utumishi wao wa kutafuta
pesa na kuharibu maisha ya wanadamu wa mataifa yote kwa kuwapoteza kwa kuwafundisha
uongo, na uongo unapouamini au kuupokea hivyo ndivyo unakuwa na wewe unaongozwa
na miungu.
·
Kila dini ni pando la miungu, dini zilikuwepo
kabla ya YESU kuja na dini ilimkataa YESU WA NAZARETI kwa kusema ameleta elimu
gani, elimu ambayo siyo ya wanadamu bali ni elimu ya mbinguni, hata wakati wa kuhukumiwa
na baadaye ndiyo walimuua, hata wale mitume wa YESU waliuliwa na viongozi wa
dini. Sasa cha ajabu ujiulize sasa kama dini ina muakilisha MUNGU wa kweli kwa
nini impinge YESU WA NAZARETI? YESU alileta wokovu peke yake kupitia jina lake
na damu yake iliyomuagika msalabani. Mbinguni hakuna dini mimi nimefika wala
hakuna mahali pa dini ila pako mahali pa wokovu peke yake na atakayeokoka na
kuishi maisha matakatifu ndiye atakaye kwenda, huo ndio ukweli, usipoteze muda
usije ukajuta leo uokoke. Baada ya dini na viongozi wake kumuua YESU
wakabadilisha makanisa yao wakayaita ni ya kikristo tu na watu katika makanisa
wakaamini wao ni wakristo na Kristo alianzisha dini, kumbe ni uongo wao siyo
wakristo bali ni upofu wa mbinu za miungu.
Ili uwe mkristo ni lazima upokee kila
alichokileta yaani wokovu. Sasa hizi dini zinasema ni za kikristo embu waulize
mbona hawaokoki? Wala kumkiri YESU na kuacha uovu na kutenda matakatifu? Jibu hawana.
Nawaeleza mataifa yote YESU atakuja kumchukua aliyeokoka kikweli na hata kuja kuchukua
dini za kikristo sababu yeye hakuanzisha dini yeye alileta wokovu, hizi dini ni
za miungu na ndiyo sababu zinaendeleza injili zake kama elimu ya shule za
duniani na siyo elimu ya shule ya mbinguni na kuwafanya wanadamu wamekuwa chini
ya miungu ya dunia hii badala ya kuwa chini ya MUNGU aliyewaumba. MUNGU
anapendezwa na wokovu mtakatifu peke yake wala siyo dini. Asili ya dini ni miungu
kama vile mila zote hizi ni dini, matambiko na hili ni pando la miungu na
katika sehemu nyingi, nchi nyingi kupitia hawa viongozi nchi zao zimekosa amani
sababu ni miungu inawatawala na nchi imetawaliwa na miungu kupitia watumishi wa
jinsi hiyo.
·
Makanisa yenye misalaba, hiyo ni sanamu na kama
ni sanamu basi hapo ni mahali pa miungu, hata vazi la mtumishi likichorwa
msalaba ile wakiwa ni wa miungu (soma Wagalatia 3:1-3), watu wamepotea sababu
ya viongozi vipofu na upofu umeshika mizizi katika dunia yote hata watu
wanakata tamaa kama vile hakuna MUNGU tena bali wamebakia waganga, wachawi na
shetani. Nawaeleza MUNGU yupo na anakaa na hao wanaomtii ila wasipomtii ni
miungu inakaa na waumini wakafanyika kuwa kanisa la miungu. Sasa ufunguke macho
ya rohoni na mwilini. Zaidi endelea kusoma makala ya Nabii Hebron na uingie
katika website yangu www.prophethebron.org
utajifunza mengi na utapona, hautakuwa kama mtu asiye na akili ya kumjua MUNGU
wake.
·
Kila Nabii anayejiita mfano yeye ndiye MUNGU ,
au yeye ndiye mungu mweupe, au mungu mweusi, au yeye ni YESU, au yeye ni
Malaika Gabriel au Mikaeli, au yeye ni Maria na wengineo. Hao wote ni mashetani
ndiyo yapo ndani yao yanafanya kazi, na miungu inawavurugia na wanakubali
iwatumikishe na hata makanisa yao na waumini wao wanakuwa wote tayari ni mali
ya miungu ya dunia hii, wafunguke ufahamu watoke wakajitenge nao, dunia
imeharibika kiasi ambacho mtu anajiita yeye ni MUNGU au anajifananisha na YESU
na watu wakamuamini, wakati MUNGU hafananishwi na chochote kile, na MUNGU siyo mwanadamu,
wala MUNGU haoi, wala MUNGU hazai. Sasa jiulize huyu anajiita yeye ni MUNGU aonyeshe
nchi yake aliyoiumba au watu aliowaumba, jibu hana, hawa ni vipofu walioteuliwa
na shetani ili kuwapofusha watu wabakie kwa miungu. Sasa ikatae na usishiriki,
hata sadaka unazozitoa uelewe unazitoa kwa miungu siku zote za maisha yako. Na hata
miujiza wanapoitenda ni miujiza ya miungu au mapepo au mazingaumbwe.
·
Miungu ni masikini, ili huduma zake ziendelee ni
lazima aombe ombe na kuchangisha sababu wanadamu ni matajiri kuliko miungu na
makanisa mengi ni omba omba sababu hawana MUNGU wa kweli bali yana miungu. Au msingi
wa kanisa ambalo ni mtumishi yeye anajua siri yake ametoa wapi hiyo huduma ya
kipepo na ili huduma hiyo iendelee ni lazima michango, kunyang’anya watu vitu
na kuwafilisi watoto wa MUNGU wakiona wamemtolea MUNGU wa kweli kumbe wametoa
kwa miungu. Nawaeleza mnaitolea miungu.
·
MUNGU aliyeumba mbingu na nchi yeye ni tajiri,
ila MUNGU amechafuliwa sana kwa kuonekana yeye ni omba omba, wakati ni makanisa
ya miungu ndio wanaomba omba. Mwaka 2012 MUNGU alikuwa anaongea na mimi kwa
uchungu sana na hasira, akanieleza Hebron, kwa nini hawa watumishi wananifanya
mimi ni omba omba, na kuliabisha jina langu wakati mimi siyo MUNGU wao, wao
wanao miungu ambao ndiyo baba zao. Akasema Ole wao moto upo tayari, na mimi leo
nawaeleza mataifa yote manompenda MUNGU msishiriki tena hayo mambo ya miungu, tena
na watumishi wa jinsi hiyo ni watumishi wa miungu pamoja na makanisa hayo mpate
kuelewa, watumishi wanauza madawa ya kulevya, wenye benki hao ni watoza ushuru,
MUNGU hatozi ushuru, kazi ya ushuru ni kazi ya Kaisari, ila kwa MUNGU hakuna
mambo hayo kabisa, na kanisa linalojishughulisha na mambo ya Kaisari basi lijielewe
tayari limeikaribisha miungu na hiyo ndio njia ya miungu ilivyokaribishwa
katika makanisa 98% ya makanisa ya miungu katika ulimwengu, dunia hii wengi ni
wachawi, wamejiita, na wengine waliitwa kweli na YESU lakini wamemsaliti,
wametekwa na shetani, wamebakia kulitaja jina la YESU kwa mdomo ila ndani ya
mioyo yao ni unafiki mtupu. Wanatafuta pesa na ndio sababu makanisa siku hizi
mengi ni biashara tu, na kama ni biashara ni mahali a kuwaibia watu pesa zao na
kuwafilisi sadaka zao na haifiki kwa MUNGU bali zinapelekwa kuzimu, pesa zao
ndio hizo zinatumika kununulia pombe, kununulia mipira ya kondom, mitaji ya
kufanyia biashara ya madawa ya kulevya na ufisadi.
NOTE:
Kwa uongozi wa kila nchi zote duniani, nchi na wananchi
wanapotezwa na makanisa ya uongo ambayo wanawaangamiza wananchi wenu kwa
kuwaingiza kwa miungu na kuzifanya nchi zilaaniwe kwa kupitia watumishi wasio
waaminifu au wanaotumia jina la MUNGU kujifichia uovu wao na kumfanya shetani
aharibu na apate njia ya kuangamiza nchi zenu. Mimi nawajua kwa macho ya nyama
na damu, nawapa njia ya kuwaelewa matapeli na watumishi wa shetani kila
serikali ikague simu ya kila mtumishi na msome meseji zao au email zao au
mrekodi simu zao. Nawaeleza hata wadadisi watakapozisoma au kusikiliza hizo
simu wanaweza wakachanganyikiwa sababu itaonekana mtu ambaye siyo mtumishi yeye
kumbe ndiye karibu na MUNGU kuliko mtu anayeitwa mtumishi. Katika ulimwengu huu
imebakia 2% tu hao ndio watumishi wa kweli wapo na MUNGU, hao 98% ni watumishi
wa miungu. Je hawaoni sasa miungu imetawala makanisa na miungu imejenga
makanisa yake na watu hawajui.
Sema BWANA YESU WA NAZARETI naomba unisamehe dhambi zangu,
unitoe kwa miungu uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele.
Nakushukuru YESU WA NAZARETI kwa kunifundisha na nimepona. Amen.
Na wewe uwatumie na wengine ujumbe huu ili wapone na utakuwa
umemfurahisha MUNGU na umeichukia miungu kabisa.
NABII HEBRON.