Pages

Thursday, January 8, 2015

A. JE UNAJUA MINARA YA BABELI BADO INAJENGWA KATIKA MAKANISA YA LEO?

B. JE UNAJUA KUWA MINARA INAYOJENGWA KATIKA MAKANISA NI SATELLITE ZA SHETANI?

C.  NINI MAANA YA MNARA WA BABELI?

MWANZO 11:4-9
4  Wakasema, haya, na tujijengee mji, na mnara, na kilele chake kifike mbinguni, tujifanyie jina; ili tusipate kutawanyika usoni pa nchi yote. 5 BWANA akashuka ili auone mji na mnara waliokuwa wakiujenga wanadamu. 6 BWANA akasema, Tazama, watu hawa ni taifa moja, na lugha yao ni moja; na haya ndiyo wanayoanza kuyafanya, wala sasa hawatazuiliwa neno wanalokusudia kulifanya. 7 Haya, na tushuke huko, tuwachafulie usemi wao ili wasisikilizane maneno wao kwa wao. 8 Basi, BWANA akawatawanya kutoka huko waende usoni pa nchi yote; wakaacha kuujenga ule mji. 9 Kwa sababu hiyo jina lake likaitwa Babeli; maana hapo ndipo BWANA alipoichafua lugha ya dunia yote; na kutoka huko BWANA akawatawanya waende usoni pa nchi yote.”

BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE enyi watu wote wa mataifa yote, YESU anawapenda sana pia na mwenyezi MUNGU anawapenda na hataki mpotee na kama mlipotea sasa mumrejee yeye sababu injili katika ulimwengu huu imebadilishwa inachanganywa na uongo kupitia watumishi waliomsaliti YESU WA NAZARETI wakajiunga na illuminati na freemason pamoja na mitandao ya joka kuu ambaye ndiye baba yake lusifa. Hapo mwanzo baada ya gharika kuu shetani aliwaingilia wanadamu katika fahamu zao walipokuwa katika nchi ya Shinari, katika mji wa babeli wanadamu wakajenga mnara mrefu ili wamfikie MUNGU alipo na muone, na jambo hili halikuwa ni mpango wa MUNGU bali ni mpango wa shetani ili wanadamu na wao waangushwe chini kama yeye. Joka kuu alipojiinua mbinguni (Isaya 14: 12-13) na yeye akatupwa chini na MUNGU. MUNGU hapendezwi kabisa na wanadamu kufanya kinyume cha mapenzi yake.

Sasa nitaelezea kuhusu minara ya kawaida na minara ya kipepo ili watu muelewe na mpone katika ulimwengu wote. Nitaelezea mfano wa minara ya simu kama mahali hakuna minara ya simu fulani hata ukiwa na simu yako haupati network na hauwezi kupata mawasiliano, katika mnara ambao ulijengwa babeli lengo la shetani alitaka ufike mbinguni ili apate mawasiliano ya mbinguni na pia wanadamu watupwe chini kama yeye sababu watakuwa wanakosea MUNGU. MUNGU akasema hapana akawachafulia lugha sababu zamani watu walikuwa wanaongea lugha moja wote, sasa ili wasielewane MUNGU akawachafulia lugha hivyo kila mtu hakuelewana na mwenzake hivyo kazi ikagoma hapo. Na zaidi kupitia kujenga mnara wa babeli hapo ndipo lugha tofauti zilianza na ndio sababu hata leo hii lugha ni nyingi sana na makabila yote yana lugha tofauti tofauti asili yake ni pale kizazi cha Nuhu baada ya gharika walipotawanyika wakaingiwa na shetani baadhi yao wakajenga mnara wa babeli na MUNGU hakupendezwa na ujenzi huo.

MINARA YA KIPEPO IKOJE?
Minara ya kipepo ni minara yote ambayo inajengwa katika makanisa au kanisa lolote lile, uelewe madhabahi hiyo inayo satellite ya kuzimu na ipo kinyume na MUNGU haijalishi wanalitaja jina la YESU au MUNGU. Nilipokuwa nikiomba na kuongozwa na Malaika Mikaeli katika kubomoa mawasiliano ya shetani alivyoyaweka kati yake yeye na wanadamu kiukweli mimi kama Hebron nilishtuka sana sababu sikuelewaga maana yake hadi pale Malaika mkuu wa vita Mikaeli aliponijulisha kazi ya hiyo minara kwa kiundani zaidi ila nitaelezea kwa ufupi sababu ni somo refu ila ufuatilie zaidi katika website yangu www.prophethebron.org na uingie katika blog nitaendelea kuelezea kwa wakati nyingine. Akaniambia Hebron, hii minara yote unayoiona katika makanisa yote katika ulimwengu wote hizo ni satellite za shetani kufanya mawasiliano na hizo madhabahu kupitia majini na mapepo. Akaniambia kama ulivyokwisha fundisha ni jinsi gani kanisa la YESU WA NAZARETI liwe au jinsi ulivyoliona kanisa la mbinguni lilivyo na ukaonyeshwa kanisa la kuzimu lilivyo, je Hebron hauoni tofauti? Nilishtuka fahamu zangu sababu kila kitu kumbe MUNGU anachokuonyesha lazima anayomaana ili kukusaidia katika picha ya kanisa la mbinguni analosali YESU WA NAZARETI, halina msalaba, halina mnara, halina kisima cha kubatizia watu.

Ila kanisa la yesu wa kuzimu niliona lina misalaba, lina minara, lina kisima cha kubatizia  watu ndani ya kanisa na dini mbali mbali na aina za ubatizo pamoja na masanamu pamoja na mengineyo. Akanieleza Mikaeli hii minara yote unayoiona inaungana na minara yote iliyopo katika kanisa la kuzimu na kwa kupitia hiyo minara majini yanajua hapo ni mahali pao na huja kuziteka roho za wanadamu pasipo wao kujua au kwa lugha nyepesi ili uelewe hiyo minara inasimama badala ya mnara wa babeli katika ulimwengu wa roho ili kuwafanya wale wanaoabudu katika kanisa hilo wawe chukizo kwa MUNGU na pia watupwe katika shimo la moto wasiende mbinguni.

Jambo lingine ni alama ya kanisa la mpinga kristo haijalishi linaitwa kanisa la MUNGU hii ni kuwapiga watu upofu na siri hii wanaijua waanzilishi wa hizo dini na hata wao wote wapo kuzimu wanateseka na wanasubiri moto wa jehanamu. Hivyo watu wote wa mataifa yote mpate kufunguka akili na kuelewa, shetani alicheza na fahamu za watu na kuwapiga upofu, sasa amenituma YESU WA NAZARETI niwaeleze ukweli watu wote, wewe utakayetii utapona na wewe utakayepuuzia haya ile siku ya hukumu damu yako hautamlilia MUNGU katika mikono yake sababu umeujua ukweli na umeupinga, heri ya hao watakaotii na kujitenga na sehemu za ibada yoyote yenye minara.

Na zaidi wapo watumishi waliotokea katika kanisa la kuzimu kabisa na wengine waliitwa wamtumikie YESU aliwaita ila baadaye wakamsaliti YESU wakaenda kumtii yesu wa kuzimu akawa ndiyo baba yao kabisa. Moja ya masharti wanavyo pewa pesa ni lazima wajenge minara katika makanisa yao hata katika nyumba zao au mahali popote ambapo anajua huwa anakaaga au kulala usiku au mchana. Ukiona hivyo unaelewa hao ni wachawi kabisa na ni watumishi wa kanisa la shetani na ndiyo ni wawakilishi wake hapa ulimwenguni na hata watu wanaosali katika kanisa hilo haijaishi wanajiita ni wakristo, waelewe wapo katika kanisa la shetani 100%. Ila wanapigwa upofu, sasa amenituma YESU niwafunulie siri hizi ili mfunguke ndivyo shetani alivyoliteka kanisa. Na pia ujiulize kwa nini watumishi wanajenga minara katika nyumba zao? Je wanahitaji mawasiliano gani? Jibu unalo. Mtumishi wa YESU WA NAZARETI wa kweli yeye haitaji mnara wowote, anaye ROHO MTAKATIFU ndiyo direction yake. Ila watumishi wa kipepo ni lazima awe na minara, sasa wale waliofaulu vizuri katika kazi ya shetani sababu wanaenda kwa grade tofauti, na wengine minara hii inakuwa ni midogo kama vile mita moja tu unaona kitu linajengwa kidogo kama becon au nguzo uelewe huyo ni mchawi, na hiyo ni satellite yake ya mawasiliano na shetani na majini yanakuja kusema na yeye na kumsaidia kufanya kazi za muendelezo wa lengo la kanisa la shetani ili kuwateka watu wengi zaidi.

Na zaidi ukiona wanajiita ni watumishi halafu wanaenda kufanya ibada katika minara uelewe siyo ibada wanapoenda katika minara hiyo na wengine hutoa sadaka na hata kuyawekea mataji, anapoenda pae anaenda kupewa nguvu za shetani na kupewa cheo kingine na kuwapeleka au kuwatoa waumini wake kafara au sadaka kwa shetani.

Na njia rahisi ya kujua hii minara ya babeli au satellite za shetani ukikuta myingine inawekewa kengele ya kupigwa kanisani, na nyingine ni katika juu ya paa utaona ncha kali kama msumari imetoboza juu peke yake. Na nyingine inakuwa juu ya misalaba ncha tofauti na nyingine wanaweka ncha katika kitu mfano wa mwezi, na nyingine ni bendera kabisa zinakuwa makanisani na ipo milingoti kabisa. Hayo yote ni satellite za shetani, mambo haya watumishi wanajua siri hizo na lengo lao ni kuuangamiza ulimwengu wote.
Minara nyingine ya shetani ni mikuki, fimbo zinazobebwa makanisani na watumishi viongozi, hizo ni satellite za shetani ili kuwaongoza watu waende kuzimu na kuwachunga wasitoke katika zizi hilo la shetani, japo kimwili linaitwa ni kanisa kwa kuwapiga watu upofu, sasa mataifa yote fungukeni ufahamu katika jina la YESU WA NAZARETI aliye hai.

Kama mtumishi unampenda MUNGU kweli na umehsajua ukweli ili upone utubu na uondoke hapo hata wewe muumini. Mshukuru YESU aliyenifunulia haya natumaini mamilioni ya watu mmepona sasa na hautadanganyika.

NOTE:
Kila kitu ambacho unaliona lipo tofauti na biblia linajengwa au kuwekwa katika kanisa uelewe hapo pana satellite za kupeleka watu kuzimu na siyo mbinguni, haijalishi wanatenda miujiza, wanapiga vinanda na miziki mizuri na mengineyo. Zaidi chunguza katika nchi yako utaiona ni nyingi na katika nchi nyingine ipo wazi wazi kabisa, hiyo ndiyo minara ya babeli ambayo ni satellite za shetani ambazo anawawekea wanadamu ili waangushwa chini katika shimo la moto, na kila mtu ambaye yupo katika kanisa lenye minara ajielewe tayari na yeye yupo kuzimu roho yake na nafsi yake. Sasa utubu, sasa utolewe kuzimu na nafsi yako irejee na utoke hapo usishiriki tena.

Sema BWANA YESU WA NAZARETI, naomba unisamehe nimetenda dhambi nimejenga mnara wa babeli kwa kujua au kutokujua naomba unisamehe na mengine yote, uandike jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Uniongoze wewe peke yako nisipotee tena. Amen.

Nakufunika kwa damu ya YESU WA NAZARETI na nateketeza minara yote ya shetani na kuharibu mawasiliano yao yote duniani, angani na kuzimu. Naibomoa kwa moto wa mbinguni iwe majivu na YESU nakuomba uwafungue mataifa yote wakurejee sababu unarudi sasa. Nakuomba uwaponye wengi zaidi na wakurejee wewe. Amen.

Zaidi endelea kusoma masomo katika makala ya Nabii Hebron Kisamo utaelewa mengi na utafunguka hautapotezwa tena katika jina la YESU WA NAZARETI.

NABII HEBRON.