ILLUMINATI
NI NINI?
Illuminati ni chama cha joka kuu ambacho lilianzishwa katika
mwaka wa 1000 ila lilijulikana mwaka 1700 hapa ulimwenguni. Aliponiita YESU
nikaifanye kazi yake ya kuupindua ulimwengu umrudie MUNGU akaniambia Hebron
ninayokueleza kuupindua ulimwengu ina maana tayari upo ufalme uliojengwa na
lengo lake ni kuwazuia watu wasiende mbinguni. Sasa Hebron nimekupa mamlaka kwa
jinsi ya tofauti kwa ajili ya kuharibu ufalme wa shetani alioijenga hapa
ulimwenguni na akashirikiana na watumishi hata niliowaita mimi wakanisaliti,
badala ya kuendeleza kazi yangu na kujenga ufalme wangu baadhi yao niliyowainua
hata kwa kiwango cha kimataifa na wengine hata siwajui wamechipuka na kuungana
na shetani wakaupindua ulimwengu.
Sasa Hebron nakutuma na mimi YESU akanipa maelekezo na
nilifanya na bado naendelea jinsi aniongozavyo yeye. Akaniambia, adui mkubwa wa
MUNGU pamoja na mimi ni hicho chama cha illuminati sababu ndicho chama cha joka
kuu alichokianzisha mwaka wa 1000. Lengo ni kuupindua ulimwengu hicho chama
hicho ndicho lengo lake, maneno hayo alinieleza YESU, ila nitaelezea kwa ufupi
ila endelea kusoma makala ya Nabii Hebron Kisamo nitaendelea kuelezea kila mara
sababu ni somo refu sana. Chama hiko ndicho chama chenye pesa kuliko chama cha
freemason. Illuminati ni chama cha joka kuu na freemason hiki ni chama cha
lusifa amekianzisha yeye chama hiki lilianzishwa na mtu anaitwa Adan. Hichi
ndicho chama ambacho kilitaka kuanzisha mtandao wa mashoga hapa ulimwenguni
kupitisha katika ncho mbali mbali na baadhi ya nchi wamekataa huu mpango wa
shetani na mimi nawaeleza endeleeni kuwapinga na mumkatae, mnapoyakubali mjue
mmemkubali joka kuu na mnapokataa muelewe mmemkataa joka kuu.
Ni ajabu sana hapa ulimwenguni yapo makanisa yanayoruhusu
ushoga tena wanafungisha ndoa, hayo makanisa yanayofanya hivyo kazi yake ni
kuupindua mpango wa MUNGU na kujenga wa shetani, uyakimbie ili upone.
Aliponituma YESU kwenda kuzimu kumtoa aliyemsaidizi namba tatu katika ufalme wa
shetani ambaye alikuwa ni mwanadamu na ni mtanzania nilishangaa sana kukuta
yeye ndiye aliyekuwa mwenyekiti wa chama hicho cha illuminati na ndiye
aliyemiliki hata account zote za pesa zao alikuwa anaitwa Maxwell sasa anaitwa
Isaya ameokoka. Yeye alihusika kusimamia kitengo hicho pia ila hapa duniani
kimwili anaonekana ni mtoto ila nilipoenda kuzimu alikuwa ni mtu mkubwa sana
ambaye ukubwa wake ni kama mlima mrefu, alikuwa ana mikono nane ana macho
matatu na anayo radio call katika kichwa chake, hawa ndio walioanzisha ushoga
na chama cha mashoga ambacho ni mtandao (MWUNWM)- Mashoga Wa Ulimwengu Na Wake
za Majini, hicho ndicho kirefu chake na mtu huyo kule kuzimu anaitwa P.BW 16
ndiye kiongozi wa mashoga, hivyo mtu yeyote aliye shoga yeye ni mke wa majini.
Sasa ni ajabu nchi zimekubali wananchi wake wawe wake za majini na baadhi
makanisa yana thubutu hata kufungisha watu ndoa za jinsia moja ili kuwageuza
wanadamu wawe wake za majini. Hivi ndivyo hiki chama lilivyoshughulika katika
kuupindua ulimwengu, sasa ni mwisho kila mtu aelewe na alikatae kama anampenda
MUNGU ila kama anampenda joka kuu atabakia nacho na baba yake atakuwa ni
shetani milele na hata sasa wale waliopo katika chama hicho hao baba yao ni
shetani na mungu wao ni joka kuu.
Chama hiki lengo lake ni kuwafanya wanadamu watoke kwa MUNGU
wa kweli na kuwapeleka kwa shetani na zaidi waliotumika wahubiri waliojenga na
chama hicho wakawa ni makuhani wa shetani, halafu hapa duniani wanajifanya
wanahubiri injili. YESU amenituma niwaeleze mataifa yote ili mpone sababu
anawapenda.
Katika hii benki ya Illuminati ipo kuzimu ambapo katika
ardhi ukitoka kuzimu unatokea katika nchi ya Bangladesh, ila sasa
nimeshailipua.
PICHA
YA LANGO LA CHAMA CHA ILLUMINATI KUZIMU

Katika picha ya lango la illuminati kuzimu, sasa utaona upo
msalaba na unayo alama yake ya mnara juu ya ncha. Hii misalaba ililetwa na hawa
illuminati ili kuwapoteza watu wakijua kuwa msalaba ndiyo YESU wakati YESU siyo
msalaba, na ndiyo sababu ukiona wanachama wake utaona wanavaa misalaba
shingoni. Embu wachunguze wanamiziki wale walio wanachama wake utaona wanayo
misalaba na wengine kwenye pete, kama nilivyoeleza katika makala zangu embu
endelea kusoma nimeelezea kuhusu misalaba na kuwa msalaba haupo katika kanisa
la mbinguni ila upo katika kanisa la kuzimu, na ndio sababu wale watu
waliookoka wakristo wa kweli hawaweki misalaba. Waliijua siri hii kupitia ROHO
MTAKATIFU, mimi nimeyaona kuzimu na macho yangu na nimeyabomoa na amenieleza
YESU niwaeleze, wewe unayetaka kupona utapona na wewe unaye kaza shingo damu
yako haitamlilia MUNGU kwenye mikono yake wakati wa hukumu. Na makanisa ni
mengi sana ya illuminati ambayo ni ya joka kuu.
HII NI
PICHA YA KIKOMBE CHA KUWAPAKA MAFUTA WATUMISHI WANAOTUMIA NGUVU ZA GIZA NA
MANABII WA UONGO ILI WAPANDISHWE VYEO
(NIMEKICHOMA
HAKIPO TENA).

MAANA
YA ALUMINATI
A= THE ADAN
L= LEARN TEAM
U= UNITED
M= MIRROW
I= IBRAHIM AND ADAN
N= NEW
A= AREA
T= TO
I= KILL THE HUMAN.
Hii ndiyo maana kwa kila herufi.
Sasa ukiangalia katika ulimwengu hata labda katika eneo lako
wewe jichunguze utaona kuwa hiki chama kinaongozwa makanisa mengi na hata
kuwafanya watoto wa MUNGU wanaompenda MUNGU na wasijue kuwa wameingizwa katika
hichi chama kupitia makanisa na kutengwa na MUNGU pasipo wao kujua, enyi watu
wa mataifa yote YESU WA NAZARETI anarudi kila unabii umetimia na amenieleza
kila mara ninapoongea na yeye waeleze watu wamrejee waeleze ukweli ili wapone
roho zao wengi wamepigwa upofu hawaelewi sasa uwajulishe Hebron na mimi YESU WA
NAZARETI nawaangalia na Malaika wanachukua rekodi yao hao watakaochukua hatua
sasa kutoka katika makanisa yaliyojiingiza huko na yaliyo wanachama wa
illuminati, watajua waeleze kwa mifano wataelewa sababu hayaandikwi majina. Ila
chunguza wewe mwanadamu utapona.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, unitoe
katika pango la illuminati uniokoe na uniandike jina langu katika kitabu chako
cha uzima, ulitoe katika kitabu cha shetani. Uniongoze milele wewe peke yako,
na siku ile ya mwisho naomba uninyakue nisishiriki mateso ya dhiki kuu. Amen.
Ubarikiwe, nawafunika kwa damu ya YESU KRISTO WA NAZARETI
aliye hai na yupo mbinguni anayejiandaa sasa kuja kulinyakua kanisa lake.
NABII HEBRON.