JE
UNAJUA KUWA KITABU CHA SHETANI CHA KUANDIKA MAJINA YA WATU KINAITWA RADO?!
BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote na YESU
anawaoenda, amenituma niwaletee habari zake za mbinguni na kuwatetea na kuwatoa
katika mateso ya shetani wale aliowafunga wote. Ilikuwa ni siku ya kumpinga
joka kuu na utatu wake kuzimu, niliingia na YESU WA NAZARETI pamoja na Malaika
mkuu Mikaeli, tukafika katika ofisi hiyo headquarters ya joka kuu na
nikaonyeshwa jinsi alivyowatesa na kuupindua ulimwengu na watu wakawa wameandikwa
katika kitabu chake, ni kitabu kikubwa sana Malaika Mikaeli akalichukua na
ndani yake niliyaona majina ya watu mabilioni walio hai na hata waliokufa ambao
tayari ni watu wake.
Niliposoma niliogopa sana, niliona ulimwengu karibia wote
wapo, hata sikuweza kusoma nikamaliza. Akaniambia BWANA YESU WA NAZARETI Hebron
hii ndiyo kazi ya shetani aliyoifanya akishirikiana na watumishi waliomsaliti kukijaza
majina ya watoto wa MUNGU kuwapeleka jehanamu. Nikakifunga kitabu nikamaliza
kukisoma, YESU akaongea na mimi kwa sauti ya ukali, akaniambia uwaeleze watu
ukweli wasije wakaenda jehanamu ila ukimueleza mtu akadharau damu yake
haitamlilia MUNGU katika mikono yake, wewe ndiye Nabii wa mwisho, uimalizie kazi
yangu na jinsi tutakavyokuelekeza, sababu kazi hii siyo wewe Hebron uifanyaye ni
MUNGU ndani yako, wewe ni chombo na ni mjumbe wa MUNGU katika hicho kitabu cha
majina ya watu walioandikwa kwenda jehanamu.
Kwa ufupi niliona majina ya wachungaji wanaobatiza watu kwa
ubatizo wa maji ya kikombe, majina ya watumishi wachawi na illuminati pastors,
freemason pastors na wanamziki illuminati, freemason, watu maarufu sana
wakiwemo marais waliopo hai na waliokufa, viongozi wa dini na madhehebu pamoja
na waumini wao. Wachawi, walevi, waongo, watumishi wanaofanya mazingaumbwe,
watumishi wanaojiita wao ni mungu wa majeshi, wanaojiita wao ni YESU, wote
wanaoabudu misalaba, makanisa yanayofanya biashara yenye mabenki, SACCOS, watu
wanaoendaga casino, wanaochezaga miziki ya dunia (disco), wanaoabudu watoto wa
MUNGU na kuwafanya wao ndio MUNGU, na watu ambao hawajaokoka majina yao
yalikuwepo katika hicho kitabu kinachoitwa RADO.
Nitaelezea kwa ufupi, baadaye baada ya kuzinduka ufahamu
nikafundishwa na YESU tena akaniambia zaidi, hata wanadamu hawaelewi maana yake
sasa uwaeleze sababu wengi hawajui ila na wengine wanaijua RADO hicho kitabu
wao walishafika katika hiyo ofisi ya shetani hivyo hao manabii ni lazima wavae
vitu vya jina hilo, akaniambia Hebron wewe ndiye mtumishi wa kwanza kukupeleka
huko na kukuonyesha haya na wala sitapeleka mwingine sababu utaimalizia kazi ya
kuharibu ufalme wa shetani kama nilivyotaka mimi na BABA yangu mbinguni. Sasa
unapovaa kitu chenye jina RADO ujielewe katika ulimwengu wa roho wewe umejiweka
katika kitabu cha shetani na mwili wako na maisha yako anaye yeye. Niliogopa
sana kukuta kitabu cha shetani anachoandikia majina watu kimeandikwa RADO.
Nawasihi mataifa yote muokoke ili majina yenu yatoke katika
kitabu hicho; sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, uniandike
jina langu katika kitabu chako kilichoandikwa uzima na milele, ulitoe katika
kitabu chake kilichoandikwa rado, uniongoze BWANA YESU. Amen.
Nakufunika kwa damu ya YESU WA NAZARETI aliye hai.
NABII HEBRON.