MAELEZO YA YOUTUBE: UJUMBE KWA AFRIKA MASHARIKI KUTOKA KWA YESU.
Ndugu watazamaji nawasalimu katika jina la YESU KRISTO ambaye ndiye BWANA na mwokozi wa mataifa yote, leo hii nina ujumbe ameniagiza niwaeleze. Katika nchi hizi nitakazoenda kuzitaja, Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi, ameniambia niwaeleze, anajua wapo watu wanaomba , wakina mama wanaomba kwa ajili ya kanisa na mambo yameharibika kabisa, kabisa hasa upande wa Uganda. BWANA amesema, ameshawajibu. Muda sio mrefu mtamuona akifanya kazi yake, anajua kwamba mnateseka sio kwamba MUNGU hawasikilizi, ameyaona yote. Uganda shetani amelishika kanisa kabisa, Uganda, Kenya, Burundi, Rwanda vile vile, lakini msiogope, MUNGU amesikiliza maombi yenu, wakati wowote mtauona mkono wake ukifanya kazi. Nawajulisha ya kuwa watumishi wote wenye majina makubwa katika hizi nchi, ni wachawi. Ameniambia niwaeleze hawatumii nguvu zake, wanatumia nguvu za mapepo na kuwaibia pesa na kuwanyang’anya hata watoto wadogo, kazi yao ni sadaka tu, mafungu ya kumi, magari, mashukrani, wa kila aina ya unyang’anyi na wizi ameniambia ameyaona lakini imetosha imefika mwisho, atakuja kuwakomboa yeye anavyojua. Hayo anavyotumia mimi sitawaeleza njia zake mimi sitazijua. Kwenye ulimwengu wa roho tayari, hivyo msiogope, msimamieni mwangalieni yeye enyi wamama waombaji, MUNGU amesikia kilio chenu, anayajua katika nchi zenu yanayotendeka, huduma yake imekuwa ni biashara, imekuwa ni pesa kama vile unaenda hospitali, lakini usiogope, muda umefika sasa endeleeni kumuomba MUNGU, na kumsihi wakati wowote mtamuona BWANA. BWANA YESU asifiwe, kikubwa zaidi, nachopenda kuwaambia wakati alikuwa ananieleza mimi Hebron ili na mimi niwaeleze ni kwamba, watumishi wamemwacha, huo utajiri walio nao sio wa kwake, sio mpango wa MUNGU japo MUNGU anabariki ni uchawi wanaotumia, waimbaji hivyo hivyo. BWANA YESU asifiwe! MUNGU amechukia sana jina lake linatumika kutafutia pesa, BWANA YESU asifiwe! Sio mpango wake alioutuma zaidi mtasoma katika website www.prophethebron.org mtaona mambo mengi na mtajifunza huko. MUNGU atawafuata msiogope endeleeni kumuomba MUNGU kwa ajili ya kukombolewa na nchi zenu, sasa hivi nchi zenu hizo zote zimeshikiliwa na shetani. Tanzania hivi sasa imekwisha tolewa humo, sasa ni zamu ya ninyi, kwa wakati wake na muda wake, hakita salia hata kimoja.
Hao watumishi wachawi wameshajua, watakwenda kuwa vichaa, wataenda kuaibika watashushwa chini wengine wataenda uchi barabarani, kiboko cha MUNGU, kwa sababu wanatumia jina kuwatesa watoto wa MUNGU, wanawaibia watoto, hadi watoto wadogo, hizi sadaka mnaambiwa mtoe, mtoe,mtoe ndio wizi yaani imekuwa ni bora jambazi wa kimwili ana huruma kuliko mtumishi. Mtumishi atakunyang’anya mali zote, unazitoa mwenyewe, jambazi anaweza ona hata huruma asimdai mtoto mdogo , lakini wewe unadaiwa tu je, ? Injili ni pesa? Injili ni biashara? Wengi mnafikiri mnaenda mbinguni, kama watumishi hao wakubwa wote afrika mashariki ni wachawi, nasema hivi watumishi wote wakubwa katika Afrika mashariki ni wachawi. Na katika Afrika wote ni wachawi na Ulaya ni wachawi. Hawapo na MUNGU tena, MUNGU amesha waacha, kwa hiyo fungukeni muwe macho msiwakimbilie tu, mambo yameshakuharibika lakini MUNGU ameanza kazi yake, utukufu wa kanisa la mwisho ni mkubwa kuliko ule wa kwanza. Tunajua kwamba tunamsubiri YESU lakini mbona huo utukufu hatuuoni? Mateso ndio yanazidi, aliowatuma wamekataa na wengine ndio wamekuwa wana mazingaumbwe, ndio maana hakuna tena mazingaumbwe katika mashule ya misingi kama zamani, ambayo ni mambo ya kipepo, kiini macho, wanayoyatumia. Ni wauzaji wa madawa ya kulevya ni wavuta bangi na wengine ni walevi lakini wamejificha kwa kutumia jina la BWANA.
Enyi serekali na viongozi wa nchi zote mfunguke macho, hao ndio wanafanya nchi zinalaaniwa wanamfanya MUNGU asionekane. Msidanganywe hata ninyi marais, viongozi na hao watu wanaomba omba wachunguzeni. Nawafungua na watu wa usalama wa nchi zote muwaone hawa ndio wanaofanya nchi zenu zisinyanyuke. Nyie mnaenda mnalia MUNGU tusaidie mnawafuata hao wakati ni wachawi !! wale wanaosema kweli wadogo wadogo wanawaua, wanawaloga, hawana nguvu, hata mimi nilifanywa hivyo hivyo lakini MUNGU amenitoa hawaniwezi na ninakuja mpaka kwenye nchi zenu kwa wakati wake na muda wake, maana YESU anawapendeni wote, hataki mteseke si ndie aliye waumba? Sasa kama ameumba yeye, njia zake sio njia za wanadamu. Lakini anakuja mtayaona, anakuja mtakuwa huru. Na ninyi watumishi mliouliwa hamuwezi hata kuongea mkanyang’anywa na huduma zenu, MUNGU atakuja kuwarejeshea endeleeni kumuomba MUNGU na kumsihi na kumkumbusha sio kwamba hawasikii aaa.. anawaona sana, amtume nani? Akinyanyuka kidogo freemason, akinyanyuka kidogo mchawi, amtume nani? Wamekamatwa na pesa na wanajijua kabisa msidanganywe na hizi. Haya majoho wanayovaa haya na suti na nini.., mali zenu ndizo wamezikalia utajiri ninyi mnakaa uchi mnalala njaa.. sio mpango wa MUNGU.
Hata YESU wakati anahubiri hakuchukua vitu vya watu, wala waliokuwa wanamfuata walale njaa au wawe masikini sana sana alimuomba MUNGU na hata ile mikate na samaki iongezeke, sasa siku hizi ni kunyang’anya, nyang’anya, kunyang’anya…. Mfunguke macho wala msiogope haya yanakuja kutokea. Na MUNGU azidi kuwainua kuwatengeneza na afungue njia na kila uchawi kwenye nchi zenu na ubomoa,! madhabahu zote nazibomoa! Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi zote nabomoa kwa jina la YESU!! Na bomoa mpaka Kongo, mpaka Malawi na Bara lote la Afrika na dunia nzima kwa jina la YESU. Kila anayesikiliza afunguliwe fahamu zake, kwa jina la YESU, iwe ni viongozi wa nchi, mawaziri, wabunge mpaka magavana wote, tumsimamie YESU wa kweli sio mambo ya sanamu, sanamu hii ahaa.. uongo lazima muelezwe ukweli ili mbadilike. BWANA YESU ASIFIWE!! AMEN.
NABII HEBRON.