NINI MAANA
YA MJUMBE WA MUNGU?
NINI MAANA
YA MJUMBE WA SHETANI?
Marko 1: 2-3
“2 Kama ilivyoandikwa katika Nabii Isaya, Tazama,
namtuma mjumbe wangu mbele ya uso wako, atakayeitengeneza njia yako, 3 sauti ya mtu aliaye
nyikani, itengenezeni njia ya BWANA, yanyosheni mapito yake.”
Mjumbe ni mtu aliyetumwa kupeleka habari fulani kwa kusudi
fulani. Ila hapa nitaelezea kuhusu
ujumbe wa MUNGU hapa ulimwenguni pamoja na wa shetani hapa ulimwenguni sababu
shetani anatumia sana wajumbe wake waje kuwapoteza watoto wa MUNGU na pasipo
watoto wa MUNGU kuelewa sababu hawamjui MUNGU. Ili shetani amteke mtu ni lazima
amletee mjumbe wake kwa njia ya binadamu apitishie hapo ujumbe wake kama chombo
chake na asambaze uongo na unapopokelewa na yule aliyeupokea hapo tayari
anakuwa ameshafungwa pingu na shetani katika ulimwengu wa roho na kuwa mali ya
shetani kabisa.
A.
MJUMBE WA MUNGU KATIKA KANISA
·
Lazima awe ameitwa na MUNGU na anajuana na MUNGU
na akitumwa haendi kinyume na neno lake wala habadilishi, ataitengeneza njia
salama na siyo njia ya upotevu.
·
Hajifananishi na MUNGU sababu MUNGU hafananishwi
na chochote kile wala kushiriki sehemu ya utukufu wa MUNGU.
·
Anahakikisha anayaendeleza yale aliyoyafanya
YESU au Yohana na siyo kuyapindua, mfano Yohana alivyotumwa abatize ubatizo wa
maji mengi wala yeye hakubadilisha.
·
Maneno au unabii anaoutoa unatimia.
·
Kanisa lake halichangishi watu pesa, wala halina
partners, wala michango katika hekalu lake, ni sehemu ya sala peke yake na
sadaka ni lazima ziwekwe katika bahasha bila kuandikwa jina wala haupewi risiti,
sababu hapo siyo sokoni.
B.
MJUMBE WA SHETANI KATIKA KANISA
Wapo watumishi (wanyang’anyi) wachawi, waganga wa kienyeji,
majini, mapepo, lusifa hawa wote baba yao ambaye ndiye joka kuu.
·
Wanaitwa na shetani na wengine ni wale watumishi
waliomsaliti YESU wakajiunga na freemason, kazi yao ni kuleta ujumbe wa
kuwapoteza watoto wa MUNGU ili waifuate na wanapoifuata inakuwa tayari
wameshaishika njia ya Jehanamu katika ulimwengu wa roho.
·
Nataka ujiulize na utaelewa kwa wepesi zaidi
kuhusu wajumbe wanaojiita ni wajumbe wa MUNGU kumbe ni wajumbe wa shetani
wanawapiga watu upofu. Tuje katika tendo la ubatizo, tazama ubatizo wa Yohana
ndio ulitoka mbinguni ili wanadamu wote waufuate huo ujumbe. Sasa iweje
wanaibuka wengine. Picha halisi katika kanisa tazama katika ubatizo utapata
picha japo wanaobatiza katika ubatizo wa maji 98% ni wanyang’anyi au wachawi au
freemason. Katika ubatizo wa maji ya kikombe je huu ujumbe umetoka mbinguni? Jibu,
hapana, umetoka kwa shetani na kama wewe unawabatiza watu kwa jinsi hiyo uelewe
wewe ni mjumbe wa shetani na kama ulikuwa hauelewi basi wacha kazi hiyo utubu
sasa ili upone na uelewe hata hiyo kazi unayoifanya ni pando la shetani 100%
ndio sababumnaratibu jumbe zake mkitumia jina la YESU kuwapiga watu upofu
(Ezekiel 23) itawahusu watu ambao wanaeneza ujumbe wa shetani na kuwaangamiza
watoto wa MUNGU katika njia ya jehanamu.
·
Ubatizo wa maji ya kikombe siyo ujumbe wa MUNGU
na pale mtu anaposhiriki tu basi anakuwa anashiriki ubatizo wa shetani sababu
shetani ili awapate watu ametuma na yeye wajumbe wake wamtengenezee njia ili
ule mwisho shetani apate watu kama ilivyo sasa anavyoendeleza ubatizo wa
shetani (zaidi soma kitabu cha Mtume na Nabii Hebron UBATIZO WA KWELI KWA
ULIMWENGU WOTE) utafunguka na utajiona kama wewe kweli ni wa MUNGU au
unapelekwa kwa shetani. Chunguza pia ukibatizwa kwa jina la mchungaji
haijalishi ni maji mengi uelewe huyo ni mjumbe wa shetani, anaitengeneza njia
ya shetani kwa mtu aliyembatiza na wengi wamewekewa njia hizo. Amenituma YESU
niwaeleze ukweli kuhusu wajumbe wake muwaelewe na wa shetani vile vile sasa
kazi ni kwako wewe uamue ni yupi utakayemfuata ni MUNGU au ni shetani?!
·
Majina yao yapo katika mtandao wa freemason,
google utayaona.
·
Wanajiita wao ni MUNGU, maana asili ya
kujifananisha na MUNGU ilianza kwa shetani mbinguni na akatupwa, wakati tunajua
kuwa MUNGU hafananishwi na kiumbe chochote kile hata jua, nyota, mwezi, ng’ombe,
mmti, bahari, ila wajumbe wa shetani hujiita MUNGU kwa majina yao wapendavyo
wakijua kuwa wanamtukana MUNGU na kumdharau kuwa MUNGU ni taka taka tu na ndiyo
wakaona wajiite wao ni MUNGU, moto umeandaliwa kwa watu wa jinsi hii, siyo siri
nawaeleza ile siku ya kiama mtawaona wakitupwa katika ziwa la moto sababu ya
kuwa wajumbe wa shetani.
·
Wajumbe wa shetani huwatengenezea watu mazingira
ya kuabudiwa wao kama vile MUNGU aabudiwavyo au atukuzavyo (biblia inasema
usishiriki utukufu wa MUNGU, hata YESU aliomba akasema utukufu wako sishiriki,
ukurudie wewe peke yako. Leo hii wamejaa dunia nzima wanaouchukua utukufu wa
MUNGU sababu ni wajumbe wa shetani.
·
Wanaabudu sanamu badala ya MUNGU aliye hai,
wanaabudu misalaba, wanawaabudu wanadamu eti wawaombee wale waliokufa mfano
Petro, Maria, Musa, Eliya, Yakobo wakati mjumbe tulioletewa kupitia kitabu
kitakatifu tumepewa ROHO MTAKATIFU ndiye atakyetuombea. Sasa iweje unamuita
mwanadamu kama wewe amekufa akuombee na zaidi MUNGU hajaruhusu njia hiyo. Elewa
hao ni wajumbe wa shetani.
·
Kubadilisha neno la MUNGU na kwenda kinyume au
kuchanganya pengine kweli pengine uongo, haifai, (hapo tayari ni kuwa mjumbe wa
shetani). Na uelewe ni mhuni wa mahali pa jinsi hii uelewe upo katika hema la
kupokea jumbe za shetani na unaandaliwa na kulindwa na mapepo au malaika wa
shetani ukae hapo usitoke, ili ule mwisho ukija uzolewe na wewe katika moto. Na
zaidi hakuna Baraka za mbinguni bali Baraka za kuzimu ndizo zitakazo tawala
maisha yako na mateso hapa ulimwenguni na baadaye kifo, kuzimu.
Sema YESU naomba unisamehe ninaujua ukweli, uniandike katika
kitabu chako cha uzima, uliondoe jina langu katika kitabu cha wajumbe wa
shetani niwe katika upande wako na uniongoze na nisirudi tena katika sehemu
zenye wajumbe wa shetani ili na mimi nisije nikawa tena mtoto wa wajumbe wa
shetani. Amen.
NABII HEBRON.