JE UNAJUA
KUWA UNAPOANDIKA SADAKA JINA LAKO NI KUMTUKUZA SHETANI?
Ukisoma katika injili ya Mathayo 6: 2-4
“2Basi wewe utoapo sadaka, usipige panda mbele
yako, kama wanafiki wafanyavyo katika masinagogi na njiani, ili watukuzwe na
watu. 3 Amin, nawaambieni, wamekwisha kupata thawabu yao. Bali wewe
utoapo sadaka, hata mkono wako wa kushoto usijue ufanyalo mkono wako wa kuume; 4
sadaka yako iwe kwa siri; na BABA yako aonaye sirini atakujazi.”
Maana ya neno hili alilolitoa YESU ni amri kutoka mbinguni
akifundisha jinsi ya kumtolea MUNGU iwe ni siri yako, inapojulikana tayari
umetupa chini au ukapita kanisani unazionyesha katika mikono yako ili uonekane
umetoa nyingi, huo ni uchafu na ni dhambi na watu wafanyayo hivyo sadaka hizo
hazipokelewi na MUNGU bali zinaenda kwa shetani na katika mtandao wa freemason
katika ulimwengu wa roho. Ila makanisa yamemuasi mwenyezi MUNGU na kulivunja
neno lake. Tazama sadaka zinavyotolewa katika makanisa halafu njoo katika
kipengele hiki, je MUNGU hatukanwi? Jibu, ametukanwa na kudharauliwa na kazi
hii inafanywa na viongozi wa makanisa.
Sasa waulize kama wanamheshimu MUNGU mbona wanavunja neno
lake? Huko ndiko kulipindua neno la MUNGU. Sasa mtoto au watoto wa MUNGU
madahara yake unapoandika sadaka jina lako au ukasema unatoa kiasi gani au
ukapewa risiti au akaandika email yako na simu au mtaa au address yako, tayari
hiyo siyo sadaka inayokwenda kwa MUNGU bali inakuwa umetoa kwa mashetani pasipo
wewe kujua na wengine wanajua. Pia unakuwa umemtukuza shetani kwa kutii
kuandika sadaka jina na ikawa siyo siri tena. Je ni wangapi mmefanya hivyo
pasipo kujua? Jibu, inawezekana hata wewe ulitoa kwa mashetani au kwa wanyang’anyi
ambao YESU aliwataja, muwe makini na wanaojiita ni watumishi.
Mfano kuomba pesa za vipindi vya TV au Redio au chochote,
huko ni kumtukana YESU yeye ni masikini, hata ukitoa uelewe umeitoa kwa
mashetani au wanyang’anyi. Hivyo mataifa yote msidanganyike tena watumishi
wanatumia njia hii zaidi kuwafilisi, nyang’anya watu mali zao wakitumia jina la
YESU na mwenyezi MUNGU na kuwafarakanisha wanadamu kwa njia hii. Unapoona hayo
wewe endelea songa mbele YESU atakupigania, na wengine wanawaeleza watu wasaini
katika nguo zao viwango vya pesa yaani huyo ni pepo sadaka, mnyang’anyi mkubwa
aliyekomaa na yupo makini katika kunyang’anya watu pesa zao.
Nikuulize swali, tokea lini sadaka inaandikwa katika nguo ya
mtumishi na ukapiga saini mgongoni au miguu katika suruali yake na akajipangia
unaye saini juu unatoa zaidi na unayesaini miguuni kiwango kidogo? Huyo ni
JAMBAZI wa kiroho. Amemtukuza shetani na mkitoa hapo pesa zote zimeenda kwa
freemason na shetani na nyota zenu na Baraka zenu. Halafu yeye anastawi nyie
mnabaki na mateso. Na pia kuhusu kapu la mama mchungaji au baba mchungaji
unapotoa umemtukuza shetani. Nikuulize swali, je imeandikwa umtolee MUNGU sadaka
au mke wa mchungaji au mchungaji? Jibu, umtolee MUNGU peke yake. Sasa hauoni
tayari umefanyika kumtukana MUNGU na umuinue shetani? Wengi mmepotezwa na
kudanganya na watumishi (wanyang’anyi) imefikia kipesa sasa hata wake wamenyang’anywa
hata watoto, je utabisha? Kanisa halijatekwa na shetani? Na kumtukuza shetani
na MUNGU akapuuziwa? Funguka ufahamu, tubu ili hiyo laana itoke kwako.
Sema YESU naomba unisamehe, niandike jina langu katika
kitabu chako, najikabidhi kwako, nisamehe. Sitamtukuza shetani tena na sirudi
huko wanapomtukuza shetani tena. Nakutukuza MUNGU WA IBRAHIM WA ISAKA NA
YAKOBO.
NABII HEBRON.