KWA NINI
YESU ALISEMA WENGINE NI WANYANG’ANYI NA SIYO WATUMISHI WAKE?
INA MAANA
GANI? WANYANG’ANYI NI NANI HAO?
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE. Karibu katika shule ya YESU
akufundishe neno lake na akufungue ufahamu na macho na masikio ili umsikie yeye
na umuelewe ili uzifuate njia zake. Nitaelezea katika kipengele kimoja kwa nini
YESU alisema wengine ni wanyang’anyi na siyo watumishi wake? Soma katika kitabu
cha Yohana 10: 1-2, 7-10
“1YESU aliwaambia, Amin, amin, nawaambieni, yeye
asiyeingia mlangoni katika zizi la kondoo, lakini akwea penginepo, huyo ni
mwivi naye ni mnyang’anyi. 2 Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa
kondoo. 7 Basi YESU aliwaambia tena, Amin, amin, naawambieni, mimi
ndimi mlango wa kondoo. 8 Wote
walionitangulia ni wevi na wanyang’anyi lakini kondoo hawakuwasikia. 9 Mimi
ndimi mlango; mtu akiingia kwa mimi, ataokoka, ataingia na kutoka naye atapata
malisho. 10 Mwivi haji ila aibe na kuchinja na kuharibu; mimi
nalikuja ili wawe na uzima, kisha wawe nao tele.”
Hapa watoto wa MUNGU wengi wamepigwa upofu hata kushindwa
kulielewa neno la MUNGU na bado wakashindwa kutofautisha kati ya mnyang’anyi na
mtumishi, YESU alimaanisha nini? Alimaanisha akijua kabisa mtumishi ni yeye
mwenyewe anamuita na anaishi ndani yake na mnyang’anyi yeye haishi ndani yake,
yeye ni mwizi. Lakini mfano huu umekuwa ni fumbo sababu hakuna mtumishi
anayejiita mnyang’anyi sababu alijiita hivyo, hakuna mtu atakayemfuata sababu
neno linasema kazi ya mnyang’anyi ni mwizi, kuiba, na sasa 98% ya wanaojiita
watumishi katika ulimwengu wote ni wanyang’anyi na watu hawawaelewi na
wanapigwa upofu na mtu kujiita mtumishi tu. Watu wakamuamini na kumbe ni
kinyume. Katika kanisa ili umuelewe mtumishi ni nani chunguza matendo yake na
ili umjue mnyang’anyi chunguza matendo yake, yale yote ayatendayo huyo anayejiita
mtumishi ambayo ni mabaya; mfano kazi ya michango, harambee makanisani,
kukusanya madeni, kutoa huduma kwa kuchaji pesa au hata ukitaka umuone lazima
ulipe malipo ya kiingilio upate appointment, hao ndio wanaitwa wanyang’anyi,
ila wanajificha kwa jina la mtumishi. Mpaka hapo natumanini sasa umepata picha
kiasi fulani, kutofautisha mtumishi ni nani na mnyang’anyi ni nani?
Mtumishi siku zote yeye husema neno la MUNGU katika kweli na
halibadiliki, hana kuficha ficha yeye injili yake ni kweli tupu ili mpone,
sababu hiyo ndiyo sauti ya YESU, na injili ikiwa ni ya kuficha ficha ukweli,
uelewe injili hiyo ni ya kutoka katika kitengo cha unyang’anyi; mfano halisi
ili uelewe wanyang’anyi anaowataja YESU katika neno lake, ni nani hao na
wakoje? Hawa wanyag’anyi ni watumishi wanaojiita wao ni watumishi wa YESU na
kumbe siyo sababu ya kwanza wamemnyang’anya YESU neno lake lisitumike katika
makanisa yao, jambo la kwanza wamemnyang’anya YESU ubatizo wa maji mengi ambao
ndio uliotoka mbinguni wakautoa wakaweka wa maji ya kikombe, huu ni mfano wa kwanza
hivyo hao ni wanyang’anyi na wala hawatampeleka mtu mbinguni ni sababu ya
kwanza wao wenyewe hawaendi mbinguni sababu ni wezi na pia ni adui wa MUNGU.
Jambo lingine, wamelipindua neno la MUNGU ambaye ndiye BABA
yake YESU, wanaruhusu kuabudu sanamu, kubatiza watoto wadogo, kubariki watu
wazima, wanaongeza huduma 6 badala yya kuwa tano, huduma ya sita ni (Uaskofu).
Badala ya kumuabudu MUNGU, ROHO MTAKATIFU, na YESU peke yao
wao wameongeza watoto ambao aliwaumba MUNGU na viumbe vyake ikiwemo hata jua,
nyota, miti, makaburi na mengineyo.
Wanaitwa wanyang’anyi na YESU sababu wapo kwa ajili ya
kutafuta pesa tu na kuifanya jina la YESU ni jina la kutafutia pesa tofauti na
ilivyo katika biblia, mtumishi hapaswi kuhangaikia mambo hayo ya kuwachaji pesa
waumini na kuwachangisha.
Ni wanyang’anyi sababu wengine wanabatiza watu kwa majina
yao badala ya jina la YESU, hapa wanamnyang’anya YESU wewe ambae umebatizwa,
badala ya kuwa ni wa YESU yeye hakupati tena sababu a huyo (hawa ndio wanyang’anyi
ni wezi wanakuibia wewe mwenyewe, pia wanamuibia YESU, wanamuibia pia na MUNGU,
ili akukose yeye aliyekuumba na kukupeleka katika ufalme wa shetani pasipo wewe
kujua na wengine wanajijua kabisa tayari wao ni kizazi cha nyoka.
Makanisa yenye benki, SACCOS huu ni msingi wa wanyang’anyi
sababu MUNGU hachaji riba. Sasa benki na SACCOS si zina chaji riba? Riba kwa
kanisa likidai tayari ni kanisa la unyang’anyi au wanyang’anyi, kitu huitwa kwa
jina la matendo yake.
Kuzimu, mtumishi au mnyang’anyi wale wanaozini wote ni
wanyang’anyi na muwe makini, hawa ni wachawi, wanasimamia amri za shetani
ziimarike katika dunia hii ndio sababu wanazini, wachawi, freemason, walevi,
wanavaa kofia kanisani, wanadai mshahara na mengineyo mengi. Hao wote ndio
wanyang’anyi YESU anaowaelezea, wameingilia kwa mlango wa nje yaani wa shetani
na kuwapiga watu upofu hata sasa mamilioni ya watu katika ulimwengu wote
wajijue hawaongozwi na watumishi wa MUNGU wa kweli bali wanaongozwa na wanyang’anyi
au wezi kama ndio viongozi wao wa kiroho. Sasa ujipime na ujiulize kama
unaongozwa na kiongozi anayemuibia YESU je anakupeleka wapi? Jibu, anakupeleka
kwa baba wa waizi shetani na wewe katika ulimwengu wa roho unakuwa baba yako wa
kiroho ni mwizi na unaitwa mwana wa mnyang’anyi. Funguka sasa, uamue, utubu na
uokoke YESU akuongoze yeye peke yake awe ndiye mchungaji wako na uisikilize
sauti yake uachane na sauti za wanyang’anyi
ili upone sasa.
Sema BWANA YESU WA NAZARETI, naomba unisamehe, uniandike
jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele niwe kondoo wako unichunge
wewe. Niliibiwa sana pasipo kujua na hawa wanyang’anyi, nashukuru kwa
kunifunulia sasa mimi nimekuwa huru amen. YESU awe mchungaji wako kuanzia sasa
na uwakatae wanyang’anyi ili usije ukaangamia.
Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE, endelea kusoma blog hii yapo masomo mengi sana yatakuweka huru
sababu mchungaji YESU amenituma niwaeleze habari zake na mumjue yeye awe BABA yenu
na siyo tena baba yenu awe mnyang’anyi, chunguza matendo ya mnyang’anyi
utaelewa zaidi. Ubarikiwe. Ingia katika website www.prophethebron.org, ingia katika
YouTube ya prophet Hebron utasikiliza mengi utakuwa huru, na wewe uwatumie
wengine kila mahali injili isonge mbele na wanyang’anyi wakome sasa.
NABII HEBRON.