MAELEZO YA
YOUTUBE: UJUMBE WA KILA MTU KWA
ULIMWENGU WOTE.
Ndugu msomaji nakusalimu katika
jina la YESU KRISTO WA NAZARETI, mwokozi wa mataifa yote ninakuletea ujumbe
ambao YESU ameniambia niupeleke katika ulimwengu mzima. Japo nitasema kidogo
tu. Aliponitoa katika kazi yangu nilikuwa nikiifanya ya utalii aliniambia
kwamba waambie wanadamu wote wamrudie yeye YESU mambo yameshaharibika. Sasa hivi
watumishi wamekuwa wachawi, kazi aliyowatuma wameikataa na watu wengi
wanaangamia na yeye YESU anawapenda na sio kwamba hawapendi, tatizo ni
watumishi wamemkataa, wengi wamekuwa wachawi wameingia freemason 98% ya watumishi
wote katika ulimwengu mzima sio wa kwake wala hawapo na yeye wameshakuachana
naye kwa sababu aliwaonya wamekataa.
BWANA YESU ASIFIWE!!
Akaniambia mambo mengi sana
lakini nitakuambia kiasi mengine utaingia katika website www.prophethebron.org. Utaingia kwenye
blog utasoma vitabu vyote vile, ni YESU ameniagiza niueleze ulimwengu mzima.
Amenituma niukomboe ulimwengu mzima na watu wote wamjue yeye na kazi hii
ataifanya yeye na hakuna atayezuia maana kanisa sasa hivi limetekwa na shetani,
kweli haipo.
Kazi yake yaani kwa jina lake
kazi yake kanisa limekuwa ni mahali pa kukusanyia pesa tu, watumishi ni waongo,
wamekuwa ni wazinzi, wamekuwa niwauza madawa ya kulevya. Akaniambia, “Hebron”
mtumishi akiuza madawa ya kulevya, ina maana ni mimi ninatukanwa na kila
mtumishi ambaye MUNGU anamtumia ina
maana YESU yupo ndani yake. Sasa kama anauza madawa ya kulevya huyo sio
mtumishi wake .
Ameniambia niwaambie watu wote,
mbatizwe ubatizo wa maji mengi aliobatizwa yeye. Huo ubatizo mwingine sio wa kwake kabisa, na kila ambaye
amebatizwa ubatizo mwingine tofauti na huo hataenda mbinguni na hata hao
wanaobatiza sio watumishi wake. Maana yeye hakuwafundisha wanafunzi wake hayo,
hata kitabu cha Biblia haupo. Kwa hiyo mnapoteza muda na
ninawaeleza wazi, iwe ni askofu, iwe ni mchungaji, iwe una cheo gani
chochote, kama umebatizwa na maji hayo
wewe sio mkristo kwa sababu Kristo hakubatizwa hivyo na tafuta katika biblia
imeandikwa , “Ole wake aongezaye maneno ya kitabu cha unabii huu”. Sasa
haya yanatokea wapi? Mnamuabudu MUNGU msiye mjua. MUNGU mnatakiwa mumfuate kwenye
biblia. BWANA YESU ASIFIWE!!
Nataka nieleze pia kuhusu
ubarikio, wote wanaobarikiwa wakiwa watu wazima sio mpango wake, tafuta kwenye
biblia ambayo ndiyo katiba yake, sasa mnafanya kazi gani, hii ni kazi ya
matakataka isiyo na mbele kabisa wala
MUNGU hapendezwi nao. Na watu mnatakiwa muelewe msikilize, haya ni mapokeo
yaliyoletwa kutoka Ulaya baada ya wale watumishi waliomkataa MUNGU, wakabadilisha
wakiingiliwa na shetani kwa hiyo sasa hiyo ni kazi ya mpinga kristo. Imeandikwa
msiabudu sanamu. Lakini kanisani mnamtaja YESU halafu bado mnashika masanamu. Je!
Ndugu wasomaji YESU anashirikiana na sanamu? Jibu ni hapana! Sasa njia ielewe ,
hawa wamekwisha kupotea na mimi nakuambia ukweli na nitaendelea kusema kweli na
kufichua kila uovu, maana yeye ndiye yupo ndani yangu wala sio ukaniona ni Hebron, mimi nilikuwa sijui
kusoma biblia, amenitoa kwenye kazi ya kuendesha watalii niliyokuwa nafanya Serengeti kama
nilivyo akanibadilisha na ndiyo
nakueleza ujumbe, maana wamemkataa amewaonya wamekuwa freemason, wachawi
kupindukia.
BWANA YESU asifiwe! Katika Afrika watumishi wameoza. Msitishwe na
habari sijui nabii nani hakuna! Wameamua jina hilo wanafanya uchawi, nchi zimeharibika, wananchi
wameharibika kwa sababu manabii ni
watapeli, manabii ni waongo, manabii wapo kwa pesa tuu, hao ni manabii wa
MUNGU? Hao sio manabii wa MUNGU. Lakini YESU ameniambia mwisho
wake umefika. Kuzimu nimeshabomoa na
wanaenda kuporomoka na watakamatwa, wala hakuna chochote ambacho
kitakachosalia. YESU peke yake ndiye anawaadhibu na kazi hiyo imekwisha anza na ameanzia
Tanzania, walizoea. Imeanza Tanzania na hakuna atakayeweza kunistopisha, MUNGU hastopishwi, ajaribu! “Ataondoka”.
Mambo mengine aliyoniambia YESU
ni wizi wa sadaka. Sadaka ya kweli ni fungu la kumi na shukurani, hizo za
ujenzi nyingine zote ni za uongo, na pia ameniambia niwaambie ya kuwa yeye siyo
omba omba, MUNGU yeye ni tajiri hao
wanao omba omba, hao wote hajawita. Maana kama mtumishi ameitwa , anamwandalia
njia usidanganyike na habari ya jina la YESU, jina langu watu wanalitumia
vibaya kwa sababu wanajua jina langu lina thamani ndiyo wanatafutia pesa, na
nyie mnahangaika , mkiteseka mkilia lakini hamna chochote, lakini mwisho
umefika.
BWANA YESU asifiwe !!!
Jambo lingine aliloniambia kuna
watu wengine wanajiita MUNGU wa majeshi, na wengine YESU, Embu nikuulize ndugu
msomaji, wao walizaliwa na Maria? Wao walikufa na kufufuka? Akili kichwani.
Nchii imeharibika sababu, ya hawa
watumishi ambao wamemuasi MUNGU, kwa hiyo MUNGU anazidi kupiga nchi. Wamebaki
kulaumu viongozi hawafanyi kazi, viongozi wanatenda vibaya, wao ndiyo source,
waache kuwalaumu viongozi.
Lakini MUNGU ameshawanyanyua
viongozi na Tanzania ndio EDEN. BWANA
YESU ASIFIWE !!
Jambo lingine aliloniambia, nitazungumza kwa kifupi ili nijaribu kuyapanga, maana mengine yote
utayapata katika kitabu changu cha JINSI KANISA LILIVYOTEKWA NA SHETANI.
BWANA YESU ASIFIWE!! Jambo
lingine aliloniambia, habari ya kuandika majina sadaka, yeye amesema utoapo
kushoto wala kulia isijue sasa hawa watumishi wanaandika majina ya ujenzi ya
matofali wanatoa hadi vyeti vya congratulation, na wengine wanawaambia watu
waandike majina yao kwenye bahasha, email address, poastal address, street,
hawa wote siyo watumishi hawa ndio wale wanyang’anyi YESU alisema watapitia
mlango wa nyuma. Mlango wa nyuma ina maana, ni maneno inayotoka nje ya biblia
ambayo ni hayo sasa, kwa hiyo hao ni wanyang’anyi. Je ! Biblia inasema
hivyo? Jibu sivyo amenituma niwaambie,
watumishi sasa hivi wananyang’anya mpaka waumini wake zao. Sio watumishi wake
hao, amenituma niwaeleze watumishi wa sasa hivi wanauza madawa ya kulevya,
amenituma niwaeleze watumishi ukiingia katika mtandao wa freemason, majina yote
unayoyakuta ni kweli, maana lazima atoe damu, lazima uvue nguo uchi
uingie kwenye hicho chama cha freemason ili jina lake liweze kuingia huko.
Kwa hiyo sasa? YESU anafanya
kazi na freemason? ! Lazima ufunguke. Lakini njia zake sio njia zetu, yeye
mwenyewe anajua anachokifanya. Na kazi hii ameshaianza na serikali ya Mbinguni.
BWANA YESU ASIFIWE! Hakuna cha dunia
nzima, kila mahali pameharibika.
BWANA YESU asifiwe! Kumeoza msitishwe na miujiza, imekuwa ni
mazingaumbwe MUNGU hajawaita, wanatafuta pesa tu. Hata wanao omba omba kwenye
TV, siyo yeye amewaita maana kama amewaita ameniambia yeye, angetengeneza njia
lakini hiyo siyo njia wanawaibia pesa
ni wizi, wanawaibia viongozi wa serikali ni wizi, mawaziri, watoto kila kitu.
Ameniambia ndiyo wanaoongoza kutoa makafara
kuua watoto wa MUNGU. BWANA YESU ASIFIWE!
Ameniambia niwaeleze
msidanganyike na kuimba kwa muda mrefu makanisani na kutembea na hata kubeba
misalaba, yeye hakai kwenye mbao, yeye yupo Mbinguni. Imeandikwa mwabudu MUNGU
katika roho nyie mnakwenda wapi. Ameniambia niwaeleze, mtu akifa, kama hajatengeneza maisha yake baasi. Mnadanganyika
na hizi ibada za wafu ni uongo.
Amenituma niwaeleze ukweli,
amenituma niwaeleze ya kuwa yeye anawapenda, mnaodanganyika msidanganyike tena
hata unavyoisikia sauti hii unafunguliwa. Na uendelee zaidi kusoma vitabu
katika website www.prophethebron.org utazidi
kufunguka, na shida yeyote inayonayokusumbua imeshindikana dunia nzima , wewe
njo! Maombi ni bure, unafunguliwa bure, mmepewa bure toa bure, hayo mengine yote ni ya wizi. Akaniambia kwa sauti
ya uchungu sana. Hebron, kwa nini wanatumia jina langu na hawanitaki?
Akaniambia , midomoni mwao wana nitaja BWANA , BWANA, lakini ndani yao ni mbwa
mwitu, ni walevi, akaniambia , mimi YESU sifanyi biashara, mimi YESU nimekwisha
waeleza msichukue riba, sasa makanisa leo hii ndiyo yana mabenki. Mabenki ni
kwa ajili ya waumini na serikali, ya Kaisari mpe ya Kaisari hayo hayanihusu
mimi!! BWANA YESU ASIFIWE. Na mengineyo mengi utaendelea kufuatilia katika vipindi
vyangu vya redio, makala na vitabu
utafunguka.
Mwezi uliopita siku moja katika nchi ya Tanzania katika watu wote walio kufa, watu kumi na
nane tu ndio walikuwa wameenda paradiso na kuanzia mwaka 1949-12th
December 2013 hakuna kiongozi yeyote iwe mfalme iwe rais ambaye ameenda paradiso,
ndugu wasikilizaji kama ni viongozi wanaombewa ni marais lakini bado hawaendi. MUNGU yupo
kwenye haki, hukaa kwenye haki, tengeneza
maisha yako. Mnadang’anywa na hao ni wapinga Kristo ninakueleza ukweli kama hutaki
shauri yako. Hujui leo upo au kesho
kutwa mwisho umefika. BWANA YESU ASIFIWE!!
Ila
nakutia moyo, mtafute BWANA YESU wa kweli, maana makristo wa uongo wamezidi ndio wamejaa kila mahali 98% dunia nzima. Ni makristo wa
uongo. Na kama wewe umeshiriki hayo mafunzo na wewe pia ni mkristo wa uongo,
hata mimi nilibatizwa ubatizo wa maji ya kikombe ile ni chapa 666 lakini wewe
huwezi kuijua kama ile ni chapa 666 inakuja katika roho maana kila mtu angejua angekimbia,
makanisa sasa hivi yamekuwa ni Makaini, yana
roho ya laana tuu, hayatendi vyema, yamekwenda kinyume. BWANA YESU ASIFIWE!
Uokoke umkamate YESU katika roho na kweli. Hata makanisa ya wokovu yameoza!! Ya
dini yameoza! YESU hakuleta dini, YESU hana dini, dini yake ni Wokovu.
Na MUNGU akaniambia Hebron,
mimi nimeumba watu wote, mimi sijaanzisha dini, watu wote mimi ndiye nimewaumba
ni wangu wanirudie mimi kupitia mwanangu
YESU KRISTO wa Nazareti ambaye ndiye njia ya uzima na kweli na hata ule mwisho
utakapofika yeye ndiye atakayekuja. Dini nyingine wanamwita Nabii Issa, sasa
kama wewe hujakuwa mwanachama wake unategemea nani akuchukue?
BWANA YESU ASIFIWE!, unataka
kwenda mbinguni ingia kwenye chama cha YESU, okoka mshike yeye, siku akija
atachukua wale walio wa kwake. Nimekueleza, yakae ndani yako. Lengo kubwa alilonipa BWANA YESU katika kazi yake ni
kuupindua ulimwengu utoke kwa shetani umrudie yeye. Na masomo aliyonifundisha na
yale ninayokufundisha utayakuta katika vitabu vyangu na CD na katika KANISA LA
YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Na yeye peke yake ndiye
anayenifundisha . Mimi sihitaji kufundishwa na wanadamu ameniambia wameoza. Kwa
sababu yale aliyowatuma wayafanye hawafanyi, mafundisho makubwa ni pesa , kuwaibia watu mali zao. Kwa
hiyo, unataka kwenda Mbinguni soma vitabu vya Nabii Hebron, utafunguka yapo
matoleo mengi sana. BWANA YESU ASIFIWE!
Ila wewe usiogope maana anakupenda,
lakini ukubali kwenda na yeye, ukiwa
kinyume bye bye. Lakini watu wengi wamekuwa siyo kinyume, kwa sababu hawaelewi,
wamefundishwa uongo kama wewe
umefundishwa ubatizo wa kikombe ni ubatizo wa MUNGU wakati ni wa uongo tayari
wewe umeshamwabudu mungu wa uongo!, kama wewe umebarikiwa ukiwa mtu mzima
badala ya kubarikiwa kama YESU. YESU alikwisha onyesha njia, sasa una cha
kujitetea? Na cha kujiuliza hawa watumishi wametoka wapi? Ni wa kweli au wa
uongo? Kama wanafundisha masomo ya uongo basi ni wa uongo. Usitishwe na sauti
eti mtu ananena, hata mapepo yananena. Hayo nakueleza kwa ujasiri kabisa, wala
sihitaji nguvu za mwanadamu wa aina
yeyote. BABA YANGU WA MBINGUNI NDIYE ANAYENIFUNDISHA peke yake. Na mimi namuadhimisha. Nasema kweli na nitaenda dunia nzima kwa
wakati wake na muda wake. Na Tanzania ndio EDENI na majibu yameanza. Na Mataifa
yatakuja Tanzania kufuata injili ya kweli.
BWANA YESU ASIFIWE, ni uovu,
uovu, uovu, imebakia sasa hivi ni kuwalaumu wadamu ambao siyo watumishi,
wanamakosa, wanamakosa, chanzo ni watumishi wameoza. Mwalimu akishaoza
atafundisha uozo na uozo utapokelewa, wengi wamejichanja miili yao haifai,
wengi wamejiita, wamejifanya kuifanya kazi ya MUNGU wanatumia jina lake
wakaweka na uchawi huko, watu waone mapepo wanalia ng’angaa. Wanaiba nyota,
mikutano imefanyika mingi sana lakini wanaokwenda kule ni kuibiwa nyota tu..
ndiyo malengo yao. BWANA YESU asifiwe! Mwisho umefika, na kazi hiyo
nimeshaianza. Dunia nzima nimebomoa japo nipo Tanzania. Na nitapenya kila
mahali, kila mtu anayetaka kumuona MUNGU ni wakati wa haki yake. Haijalishi una
cheo gani au nini NO!! kwa MUNGU hakuna, wote ni sawa. Na ndiyo ninamrepresent
MUNGU wa kweli, mambo ya uongo uongo bye bye.. shetani hana chake tena!
Asante sana, karibu
uendelee katika kusoma makala na vitabu vya kanisani kwangu Arusha
Moshono.
Utahudumiwa bure, uponyaji ni
hapo hapo. MUNGU AWAINUE, MUNGU AWAOKOE, Muijue nuru na nuru iwaweke wazi,uongo
muujue na uwakimbie.
NABII HEBRON.