NINI
MAANA YA CHRISTMAS CARD?
JE
UNAJUA KADI ZA KRISMASI NI MPANGO WA SHETANI?
SOMA
HAPA….
Nawasalimu watu wote wa mataifa yote, ambayo yeye YESU wa
mataifa yote ndiye atakayewaokoa wanadamu ili wamrejee MUNGU kwa kupitia yeye
peke yake. Ni miaka mingi shetani aliifanya dunia kama anavyotaka na kuipindua
pindua na kuwakosesha wanadamu wapotee wamfuate yeye hata wale wasiompenda
shetani wakatekwa pasipo kujua na yapo mambo mengi aliyoyabuni shetani na
serikali yake na yakaletwa hapa ulimwenguni na wanadamu wakayaona ni mazuri kwa
macho ila katika roho ni hatari sana. Hata mimi sikuyajua mpaka pale YESU
aliponitokea, akanijulisha hayo, na YESU aliniambia, nawapenda watoto wa MUNGU,
nilikosa wakumueleza na kuufichua uovu wa shetani ambao amewatekea wanadamu na
wengi hawajui watumishi waliomsaliti na kama nilisalitiwa ina maana tayari
wamekuwa katika umoja wa adui hivyo habari zangu haziwezi kwenda mbele. Ila
sasa uwaeleze watu wote ukweli atakayesikia na kuifanyia kazi atapona,
atakayekaza shingo ataangamia.
Mimi mwenyewe kama Hebron mara nyingine kwa jinsi
nilivyooneshwa ulimwengu ulivyopotea natamanigi hata niondoke katika uso wa
nchi, ila siku moja nilipokuwa nikiwaza tu, nikasikia sauti ya MUNGU kwa ukali,
ni maneno gani hayo unayoyawaza? Akaniambia, hautaondoka katika uso wa nchi
mpaka pale atakapokuja mwanangu kulinyakua kanisa lake, akaniambia,
nimekuchagua wewe uikomboe dunia na watu watoke kwa shetani, watoto wangu
wamepotezwa na adui na wanajiona wapo sawa. Nitautumia mwili wako kama chombo
changu, utukufu wa kanisa la mwisho ni mkuu kuliko wa kwanza, na ndio unatimia
na itakuwa kama vile kipindi cha Sodoma na Gomora. Wengi waliambiwa watubu
wakacheka na baadaye waliungua kwa moto. Na itakuwa kama vile kipindi cha Nuhu,
walimcheka Nuhu amechanganyikiwa na kwako ndivyo itakavyokuwa, mimi ndiye ninayesema
na wewe peleka habari zangu. Na mimi Hebron nakuletea wewe na wewe uwatumie na
wenigne na siri hii ulimwengu wote hawaijui zaidi ya vyama vya illuminati na
freemason kuhusu kadi za Krismasi zinazotumika hapa ulimwenguni, asili yake ni
wapi na ni nani aliyezibuni hizi kadi za Krismasi na malengo yao ni nini?
Ukisoma katika kitabu cha Mathayo 2:9-11
“9 Nao waliposikia maneno ya mfalme, walishika
njia; na tazama, ile nyota waliyoiona mashariki ikawatangulia, hata ikaenda
ikasimama juu ya mahali alipokuwapo mtoto. 10 Nao walipoiona ile
nyota, walifurahi furaha kubwa mno. 11 Wakaingia nyumbani, wakamuona
mtoto pamoja na Mariamu mamaye, wakaanguka wakamsujudia; nao walipokwisha
kufungua hazina zao, wakamtolea tunu; dhahabu na uvumba na manemane.”
Utaona YESU alipozaliwa mamajusi walimpelekea zawadi, hazina
walizozifunga, vitu vya thamani dhahabu na vinginevyo. YESU hakupelekewa kadi
alipelekewa kitu halisi, kadi haina kitu chochote. Kadi siyo soda, siyo
dhahabu, siyo zawadi, zawadi siyo maneno, zawadi ni kitu halisi. Nikuulize
swali je kadi hayo maneno unayoyasoma ni kitu halisi? Jibu siyo. Watu wengi
walipigwa upofu, hata mimi Hebron nilikuwa sijui haya na nilipojua nilishtuka
nikayahifadhi mpaka muda wake umefika niwajulishe maana ya kadi ya Krismasi.
Asili ya MUNGU au mpango wa MUNGU katika siku ya Krismasi, ni siku ya kumpa
MUNGU zawadi na ni siku ya watu kupeana zawadi halisi na kufurahi. Lakini
imekuwa ni kinyume, shetani akaipindua akabuni kitu kinaitwa kadi za Krismasi
na zikaletwa hapa ulimwenguni.
Vizazi vingi vikashiriki kuwa na kadi za Krismasi na kutumiana
zoezi hili mpaka sasa nafikiri katika
ulimwengu huu 90% ya watu wote tayari wameshapokeaga kadi za Krismasi au hata
kutumiana wao kwa wao. Ila ufurahi kwa sababu ujinga wa shetani alioutumia sasa
naufichua wazi na kueleza kila kitu na lengo lao. Waliipindua siku ya Krismasi
ndiyo siku ya kupeana zawadi ambayo ndiyo 25.12 kila mwaka, wakaifanya iwe
26.12 wakaiita boxing day. Nikuulize swali, je siku alipopelekewa YESU zawadi
ilikuwa ni siku ya pili ya kuzaliwa kwake? Jibu, ni siku ile ile walioona nyota
usiku na wakaifuata na hawakwenda mikono mitupu. Sasa shetani akaipindua ili
kuivuruga Krismasi, ile siku ya Krismasi wanatakiwa wampelekee YESU zawadi,
akabadilisha wampelekee kadi, na ile siku ya kumpelekea YESU zawadi ambayo ni
siku aliyozaliwa ikabadilishwa jina boxing day. Je ushawahi kujiuliza kwa nini
iitwe boxing day 26.12? majibu utayapata sasa, na je umeshajiuliza siku zote
kwa nini imeitwa boxing day? Na swali lingine hivi ikiitwa boxing day ina maana
pia katika maboksi ni empty, hiyo ni empty day. Hii yote ni ili kuvuruga watu
wasipate Baraka za YESU na wamkosee MUNGU kama ilivyo watu wengi hawaelewi ila
sasa uelewe ukweli ndio huo, hakuna kadi ya Krismasi.
Madhara ya hizi kadi, kila unapoitumia tayari wewe unakuwa
umewatumia kuzimu kadi yao na unasherekea na yesu wa kuzimu sababu na yeye
sherehe yake huanza 23.12-27.12 kila mwaka.
Na pia unazikosa Baraka za kweli za Krismasi za mbinguni
pasipo wewe kujua. Nilipoingia kuzimu niliyaona na niliyajua hayo na kitendo hiki
cha kutengeneza Kadi kilikuwa chini ya Maxwell ambaye alikuwa ni mtu wa tatu
katika ufalme wa shetani na aliyeficha siri zake zote, ila YESU alinituma
nimemtoa na sasa ni mwanadamu wa kawaida anaitwa Isaya. Unapoitumia hiyo Kadi
tu hata ukimuandikia mtu uelewe ulikuwa unamtumia joka kuu, lusifa na Maxwell
na watu wengi wamemtumia ikiwemo hata mimi Hebron pasipokujua. Yaani kile kitendo
cha kuvinunua tu tayari umeungana na kuzimu au kuitamani tu. Na katika hiyo kadi
ya Krismasi zipo rangi saba ambazo nitazielezea katika makala nyingine
zinamaanisha nini ila kwa ufupi zinawekewa nguvu za roho za uongo au mpinga
kristo azidi kusambaa huku duniani hata kwako wewe unayetumiaga kadi hiyo. Ila
sasa uelewe.
Na pia wakabuni njia ya haraka zaidi, wakatumia internet
wakaweka kadi ya Krismasi ili watu washiriki kwa haraka wawapate wengi kabla ya
YESU kurudi, shetani awe amewateka wengi. Ila ashukuriwe MUNGU anayetupenda.
Nataka uelewe haya mambo mawili. MUNGU yeye hutoa zawadi kamili inayoonekana
siyo zawadi ya maneno matupu. Ila mpango wa shetani yeye anatumia kadi na watu
hawaelewi. Tazama hata enzi za kina Ibrahim watu walipeana zawadi na siyo Kadi,
jiulize hizi kadi sasa zimetokea wapi? Je ndio ufunuo wa MUNGU? Jibu,umelipata.
Ila sasa mkitii mtakula mema ya nchi na kuyatapika ya shetani. Ni ajabu sana hata katika makanisa
utakuta mtu au mkristo amenunua kadi kadi ya Krismasi ameiandika special for
JESUS (yaani kadi ya YESU tu). Amemuandikia YESU nakueleza ukiandika hivyo
unakuwa umemuandikia yesu wa uongo wakati wewe haupendi.
Nimekurudisha katika formula ya MUNGU yeye hatumii kadi ni
kitu halisi. Ila shetani ili amuunganishe wanadamu na Krismasi ya kuzimu
akabuni kadi na zimekubalika hapa ulimwenguni na zaidi shetani na serikali yake
wanafurahia sana na kushangilia pale mtu akiwa nayo au kumtumia mtu wanafurahia
kazi yao inakubalika na wanadamu, na mpango wa MUNGU umepuuziwa. Sasa swali je
wewe unataka mzigo wa kadi za shetani au zawadi tu? Na katika zile kadi za
Krismasi kuna vitu vimewekwa na vyote vinavyo maana yake nitawaelezea maana
yake.
A. CARD
YENYE PICHA YA NYOTA
Ile nyota inatumika sasa kuiba nyota yako na shetani
anaichukua na ndio sababu watu wengi unakuta hata hawajalogwa na wachawi ila
maisha ni magum na ni mabaya ni sababu nyota yako imeibiwa na shetani. Kwa njia
ya ile card iliyopo Krismasi kadi na shetani anakucheka hauna ujanja. Hivyo ni
lazima anyanganywe nyota za watoto wa MUNGU arejeshe mara moja.
B. ALAMA
YA MWEZI
Alama hizi zinatumika katika kadi za Krismasi, ina maana
kupitia ule mwezi uliopo katika hiyo kadi kila mara maisha yako yanachomwa na
huo mwezi kwa ncha yanatobolewa katika ulimwengu wa roho.
C. CHRISTMAS
LIGHT
Maana ya zile taa zinazowaka na kuzimika pale inapowaka
inasababisha maisha yako kuwaka na kuzimika, hata wale wanaoenda disko zile taa
za disko light kazi yake ni kuuzimisha maisha yako, iwe ni mahali popote unaona
taa hiyo uelewe maana yake ndiyo hiyo ila watu wanaona ni urembo tu. Shetani
yupo kazini.
D. MIPIRA
YA KUNING’INIZA KATIKA MTI WA CHRISTMAS TREE.
Ile mipira unakuwa ndio wewe uliyezihifadhi au kurembea na
ile kamba ni mikuki wa kukuchoma maisha yako. Nataka muelewe jinsi shetani ni
mbaya na hawapendi wanadamu, na sasa wewe uamuzi ni wako.
E. VIBOKSI
Zile picha za viboksi unapokuwa navyo katika kadi ya
Krismasi katika ulimwengu wa roho Baraka zako zinaibiwa zote na maisha yako
yamebakia boksi yaani tupu na shetani anawanyanyulia bango ninao uhalali sababu
wana vitu vyangu, kwanza hawa wanadamu hawakupendi, wakati kawateka fahamu,
sasa shukuru sababu maisha yako na vitu vyako ulivyoibiwa nitakuombea uje
kanisani nimnyang’anye shetani vyote uwe sawa sawa na usizitumie tena wala
kuwatumia watu, ili usipatikane kwa njia hiyo na kama unazo zichome.
Hivi vitu vinavyoitwa Christmas tree, father Christmas, kadi
za Krismasi na boxing day vyote vimetoka kuzimu vikaletwa ili wanadamu wamuuzi
MUNGU na wapate kuwaibia watu maisha yao na baraka zao. Ninajua inauma sana
lakini ukweli ndio huo. Ili Krismasi yako iwe nzuri usiweke hivyo vitu katika
nyumba yako, hata ofisini, hata
hotelini, unakuwa kuzimu yote iko kwako sababu wanaona vitu vyao na hiyo ni
njia.
Zaidi katika huo mtandao wa kadi kuzimu, bado hawakuishia
hapo tu katika kadi za Krismasi, walitengeneza kadi za mapenzi, uchumba,
marafiki, baba, dada, uncle, son na nyinginezo kwa majina yao. Mfano ukikuta
kadi imeandikwa U&ME ina maana ni wewe na majini ya kuzimu japo wewe
unamaanisha kimwili na huyo unayemtumia hiyo kadi, inakuwa ni kinyume sababu
kadi zote ni zao, ili wampate binadamu wametumia njia hiyo.
Ukiwa na kadi imeandikwa darling- wewe unakuwa kwanza ni
darling wa kuzimu na kisha wanazini na wewe katika nafsi yako muda huo huo
pasipo wewe kujua.
Kadi iliyoandikwa fiancé- unakuwa tayari unakuwa mchumba wa
jini lililohusika kubuni hiyo kadi na madhara yake uchumba unakuwa ni vuruguu,
balaa na hata kuachana sababu yupo mwingine, mchumba ambaye yupo naye japo wewe
haujui.
Kila neno la jina la kadi uelewe unapoinunua au kutamani tu
au kutumiwa au kutumia mtu uelewe ni wewe unakuwa wa huyo aliyopo kuzimu na
anakuwa na uhalali kabisa, shetani alibuni siri hii akajua atawateka wengi na
ndivyo ilivyo. Hebu jiulize zamani wazazi au mababu, mabibi hawakuwa na mambo
ya kadi. Walikuwa wakimpenda mtu anachukua kalamu na karatasi halafu anaandika
ujumbe wake na mambo yanakuwa mazuri wanaelewana. Sasa siku hizi watu wanapigwa
upofu wanaenda kununua ujumbe labda kwa ajili ya mchumba halafu unamtumia
mchumba. Nikuulize je wewe mchumba hayo maneno yametoka katika ufahamu wako na
moyo wako? Jibu siyo, na je unamjua ni nani aliyeandika ujumbe huo, jibu
haumjui. Sasa watoto wa MUNGU hamuoni mnadang’anywa tu mnapeana maneno ambayo
unaandikiwa na madahara yake upendo haudumu, unaibiwa na mapepo sababu ulikosa
akili yako ukatumia akili ya walioandika maneno ambayo haujui yana roho gani. Kama
nilivyoelezea sasa mfunguke YESU anawapenda, mfunguke fahamu zenu mumcheni
MUNGU na msiangamie tena enyi mataifa yote. YESU alitaka myajue miaka mingi
lakini alisalitiwa na watumishi akakosa wakumfunulia haya. Na nyie mliofunguka
msimsaliti YESU mkatumia vitu hivi.
Tazama hata makanisani siku ya Krismasi utakuta midoli ya
father Christmas, miti, kadi za Krismasi na taa za kuzimu, maisha ya wanadamu. Zaidi
endelea kusoma makala nilivyoelezea
kuhusu Krismasi ya Nabii Hebron utapata majibu yako hata kama haujaelewa
utaelewa kabisa na utafunguka macho yako na usome masomo mengine na vitabu
nilivyoviandika hakika utapona. Katika makanisa wanapoziweka vitu hivyo kuzimu
yote inajumuika na waumini wote sababu ya hizo kadi na miti, midoli na watu
wanaposherekea boxing day 26.12 badala ya 25.12 aliyozaliwa YESU siku hiyo
kuzimu wanakuja kumuibia kila mtu ambaye atasema anatoa zawadi ni siku ya boksi
day. Unaibiwa kila kitu unabakia mtupu. Ila kama ukimoa mtu zawadi usimuambie
hii ni zawadi ya boxing day hapo utapona, ila ukiandika tena boxing day siku
yeyote ile na wewe unakuwa unajiunganisha na siku ya kuibiwa vitu na shetani
katika ulimwengu wa roho ndiyo inaitwa boxing day.
Mamilioni wanaibiwa baraka zao miaka nenda rudi sababu
hawakuujua ukweli na makosa siyo yao wala siyo ya YESU, ni makosa ya watumishi
aliowaita YESU wakamsaliti na YESU akakosa mjumbe wa kupeleka habari nyingi
ambazo shetani aliwatengenezea wanadamu ili awateke. Krismasi hii usiweke mti,
midoli ya father Christmas, wala kadi za Krismasi wala zile taa za Krismasi,
utaona Krismasi njema na utabarikiwa na YESU na utamfurahisha MUNGU mbinguni na
atakubariki. Ila ukiweka uelewe YESU unamfukuza kwako, na unamuuzi MUNGU na
hautaona baraka zake, sasa funguka.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu ikiwemo na hii
ya kutokujua au kujua nikashiriki katika kadi za krismasi, uchumba na
nyinginezo. Nashukuru YESU kwa kunifunulia haya kupitia Nabii wako Hebron. Nisaidie,
niongoze nisipotee tena, shetani sikutaki tena, father Christmas sikutaki, Christmas
tree sikutaki, Kadi za Krismasi na taa zake na vitu vyote vya shetani
mlivyovianzisha siwataki katika jina la YESU WA NAZARETI ALIYE HAI. Amen.
NOTE:
Kadi za Krismasi zilibuniwa kuzimu ili kuwateka wanadamu na
sasa zinajaa kila mahali ili na wewe unapoitumia unashiriki Krismasi na kuzimu.
Formula ya MUNGU ni kupeana zawadi halisi kutoka katika moyo. Sasa kadi hayo
maneno tu siyo zawadi unayoiona kwa macho, pia hayo maneno siyo wewe unayeandika,
haujui yalipotokea, ni bora umuandikie mtu kwa barua heri ya Krismasi au email
kuliko kadi hizo, na hautakiwi hata ubuni kadi yako, jambo ni lile lile tu,
unakuwa unarejea katika msingi wa kadi ule ule tu.
Nawatakia Krismasi njema isiyo na giza. Karibu katika kanisa
la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, uombewe na ufunguliwe mambo
yaliyoshindikana na mengine na usogezwe kwa YESU.
NABII HEBRON.