UBATIZO WA KWELI NA UNABII KUHUSU TANZANIA MPYA.
Karibu sana ndugu msomaji
katika kipindi cha Mtume na Nabii Hebron wa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.
Kwanza nitaanza kwa kukuombea,
“ Baba katika jina la YESU, asante kwa ajili ya watazamaji na watoto hawa zaidi
tu ya kutokuwa watazamaji ni watoto wako tu MUNGU uliowaumba wewe. Baba
ninawakomboa nakuwasafisha na kuwatakasa, ninavunja nguvu zote, za uharibifu
maeneo yote , ninakomboa akili zao
fahamu zao, nawatenga na roho zote za uovu kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti, ninabakiza nguvu
zako tu, ndani yao zile ambazo tu ni mapenzi yako. Ninafungua, masikio
fahamu na akili zao kwa damu ya YESU
KRISTO wa Nazarethi. Asante Baba nina kukabithi
ninakurudishia wewe mwenyewe
watoto wako, sifa na utukufu. Asante Baba kwa muda na wakati huu
unapokwenda kusema na watoto wako. Amen!
Ndugu msomaji MUNGU akubariki
sana. Siku ya leo nitakwenda kuzungumzia
somo la Ubatizo. Sawa sawa na YESU alivyoniita toka mwaka 2010, na mambo aliyo
kwisha kuniagiza, kuyaeleza na
kuwafungua watoto wake na shetani
asiwapate. Kwa sababu hii yote anawapenda. Lakini leo nitaelezea jambo moja
kuhusu Ubatizo na pia nitaelezea kuhusu
mambo yanayokwenda kutokea katika nchi ya Tanzania ambayo MUNGU ameichagua ni nchi yake teule Takatifu ambayo
ameiita EDENI.
Wengine watajiuliza ni kwa nini
Ameiita EDENI? Ni yeye ndiye ameiumba.
Mtayaona hayo na yeye ndiye amepanga. BWANA YESU ASIFIWE..!
Aa.. nitaelezea kuhusu ubatizo, MUNGU ule aliouanzisha lakini
umekwenda kuachwa na kama umeachwa
ukaenda tofauti ina maana watu hawajabatizwa. Ndugu msikilizaji na mwana wa
MUNGU kila mmoja, anaijua katiba ya MUNGU ni hii BIBLIA. Hii ndiyo mwongozo
wako, yeye mwenyewe ndiye ameipitisha kwa ajili yako wewe, na wengine wote
ambao hawaangalii, BWANA YESU asifiwe,!
Nitaeleza kuhusu ubatizo. Ubatizo ni kiapo kilichopo kati ya Mtu na MUNGU. Na jambo la
ubatizo lilianzishwa na MUNGU baada ya anguko la Adam na Hawa katika bustani ya
EDENI. MUNGU alichokifanya aliitroduce
Ubatizo na akamtuma Yohana kuwasafisha,
Bwana YESU asifiwe! Akamtumia Yohana wakabatizwa kwa maji mengi yanayotembea
mtoni kijito cha utakaso.
Na kupitia hivyo hivyo akamtuma
mwanawe YESU wa Nazarethi ambaye ndiye mwana wake wa pekee aje aonyeshe njia
namna gani sisi tutakavyo batizwa ili
kwamba tuwe tumeokolewa na kusafishwa
kama yeye. Na alipo kwisha maliza kazi yake, alirudi juu mbinguni lakini suala
hili MUNGU alilolianzisha kuhusu
ubatizo, limewekwa pembeni 98%. Na leo ninakuwmbia wote ambao wamekwenda
kinyume na mpango wa MUNGU na hata
katika Biblia ,wote hamjabatizwa na MUNGU hawajui, na amesema hamtaenda mbinguni. Iwe ni watumishi,
na hata kama ni watumishi nyie siyo watumishi wake maana kama ni watumishi wake
mngefundisha yale yale aliyoyafundisha YESU ambaye ndie njia ya uzima na kweli,
kwa hiyo watu wanafuata uongo wenu, wanaacha kufuata kweli namtahukumiwa bila
kuokoka upya na kubatizwa. Bwana YESU asifiwe!
Nitasoma katika kitabu cha
Mathayo 3:13-17, Neno la MUNGU linasema hivi wakati huo YESU, akaja toka
Galilaya kwenda Yordani kwa Yohana ili abatizwe, Lakini Yohana alitaka kumzuia
akisema, mimi ninahitaji kubatizwa na wewe
nawe waja kwangu, YESU akajibu
akamwambia , kubali hivi sasa kwa kuwa
ndivyo itupasavyo kuitimiza haki yote. Basi akamkubali, naye YESU
alipokwisha kubatizwa mara akapanda
kutoka majini, natazama mbingu zikamfunikia akamwona Roho wa MUNGU
akishuka kama huwa akija juu yake,
natazama sauti kutoka mbinguni ikasema , huyu ndiye mwana wangu mpendwa
ninayependezwa naye. Bwana YESU asifiwe. Ndugu msikilizaji wa Neno la MUNGU,
njia sahihi aliyo onyesha ni YESU, na MUNGU alimtumia Yohana kuanzisha hiyo
njia. Lakini Yohana alijua huyu ni mkubwa kuliko hata akatii Mungu aliyopanga.
BWANA YESU asifiwe, YESU na
yeye akabatizwa akaingia kwenye maji akabatizwa baada ya kubatizwa ROHO MTAKATIFU akashuka juu yake akashuhudia
“Huyu ndiye mwanangu mpendwa “ BWANA YESU asifiwe. Sasa jambo ambalo MUNGU
alikwisha kulianzisha sasa hivi ni tofauti na imeandikwa katika kitabu cha Ufunuo ya kuwa atakaye ongeza
maneno ya kitabu cha unabii huu sehemu yake haipo kabisa, BWANA YESUasifiwe.
Kwanza kabisa nitaeleza maana ya kubatiza. Kubatiza
ina maana ya kuzamisha. Lakini sasa
siku hizi imekuwa ni tofauti haijalishi unabatiza kwa jina la BABA , la
MWANA na la ROHO MTAKATIFU, hiyo yote ni fake lazima kuingia katika maji
yanayotembea ya Mtoni kama Yordani, ubatizwe kwa jina la BABA na la MWANA na la ROHO MTAKATIFU. Bwana YESU asifiwe.
Sasa hii imekuwa ni tofauti , katika mithali 13: 1
Mwana mwenye hekima husikiliza
mahusia ya baba yake, lakini Yule anayemdharau hukataa kusikiliza mahusia ya Baba yake,
na wanadamu wamekataa kusikiliza mahusia
ya MUNGU wamemdharau, kwa nini hambatizwi? Kama Neno la MUNGU linavyosema?
Mmejitengenezea njia zenu na hizo njia sio za kwenu ni mmepotea acheni mambo ya
wamissionary wamepotea wamekuja kupoteza watu, injili Ulaya hakuna imekufa.
Wote ambao hamjabatizwa ubatizo wa maji mengi, hamjabatizwa na YESU ameniambia
wote, wote ni kazi bure! BWANA YESU ASIFIWE!
Ukisoma katika kitabu cha
Yohana 3: 5-7, Asiyebatizwa hatakwenda mbinguni, sasa nakuuliza wewe hujazamishwa katika maji, halafu unasema ni
mkristo, halafu unasema unaenda mbinguni, Yohana 3: 5-7 inasema hivi? Asiye zaliwa
kwa maji haendi. Na wewe wewe hujaenda, YESU ndiye njia ya uzima nay a kweli,
lakini njia hiyo wewe pia hujaifuata, umefuata uongo. BWANA YESU asifiwe, watu wengine wanasema ubatizo ni imani yako, wanabatiza watoto wakiwa wadogo, nikuulize
swali, wewe mtoto mdogo ulikuwa na imani? Tazama YESU alipo batizwa wakati anaenda kubatizwa hakuwa na msimamizi hata mmoja, sasa nyie wanadamu hata na nyie watumishi wa huyu
msimamizi mwanamke na mwanaume wametoka wapi? Tafuta katika Biblia kama
MUNGU alianzisha hivyo? hakuna! Mmepotea mrudi mkabatizwe kwenye maji, ni AMRI na kiapo kinyume cha hapo huendi mbinguni. Katiba
ya MUNGU umeshaivunja wala wewe
sio mkristo, Bwana YESU asifiwe. YESU amechukia kabisa, mambo yameharibika, huku ndiko
kutekwa na shetani. Kila aliyebatizwa ubatizo wa
kumwagiwa maji kichwani ametekwa na shetani na ile siyo ubatizo ni ndiyo
namba ya 666, watu wanafikiri kwamba
itakuja jina limeandikwa kwenye paji la
uso 666, inakuja katika roho, ndiyo hii 666 lazima ukabatizwe, kinyume na hapo
YESU akija mbinguni hauendi.
Hajalishi kwamba mnamtaja YESU,
BWANA YESU asifiwe! Hayo ameniambia na mimi sipunguzi ninawaeleza.
BWANA YESU
asifiwe!Hivi nikuulize, YESU alionyesha
njia akiwa mtoto mdogo anaenda
kubarikiwa Mariamu na Yusuphu walimsindikiza mtoto wao kubarikiwa. Sasa siku
hizi mapepo na mashetani yakaliteka kanisa, mwanaume na mwanamke wakati mtoto anapelekwa kubarikiwa , ikageuzwa kibao
ndio anabatizwa. Sasa anabatizwa wapi?
BWANA YESU asifiwe! Wengi
hamjabatizwa na ninawaeleza ukweli, na siyo wakristo na wala hamuendi mbinguni
iwe ni askofu, uwe sijui wa dini gani NO!! Tena
mtachomwa kwa sababu mmeharibu,
Neno la MUNGU ukisoma katika kitabu cha
Wagalatia 1: 6 injili aliyoianzisha MUNGU imebadilishwa, imepindishwa , imewekwa
uongo, huu ndio uongo ninaowaambia ndugu watazamaji na kama ukislkiliza injili
ya uongo na wewe umekuwa muongo, umepotea. Mnatembea mnaona mnaenda
mbinguni, hakuna mbingu, muulize huyo anayekubatiza wapi kuna
ubatizo wa maji ya kikombe?
Tafuta hakuna. ! Muulize wapi
imeandikwa mtoto mdogo ana imani ya ubatizo? Kwa nini YESU alionyesha njia?
Akiwa mtoto mdogo yeye ndivyo inatakiwa
. Yohana 14: 6 , Yeye ndiye njia ya uzima na kweli. Sasa uzima upi na kweli ipi
unaifuata? Hamjabatizwa mnapoteza muda mtachomwa, mtaangamia. Badilika hii ni
Dunia nzima.
Ninawaambia ukweli, na wengine
wameanzisha mtindo mwingine, hii kuchafua wanatumia nguvu za kichawi,
watumishi, anakubatiza kwa hivyo hivyo
kwa maji mengi anakubatiza kwa jina la BABA na la MWANA na la ROHO MTAKATIFU halafu anakuwekea na la
Hebron hapo au la kwake. Haipo hiyo
kitu? Sasa wewe unaweka agano na mwanadamu ndio maana mmeshikwa, pesa zote
mnapeleka kwa mtumishi hata mpaka unashangaa unachanganyikiwa, wanajua siri
wanayofanya. Waulize! Kama ni mahakama
ya ya kibinadamu wanatakiwa washitakiwe
kabisa , kwa nini wanabatiza watu kinyume na MUNGU? BWANA YESU asifiwe, ninawaeleza siri
hii, Roho zenu zina kufa mkabatizwe upya!!.
Yeyote hujabatizwa kama YESU wewe siyo mkristo. Fuata njia za YESU
alibatizwaje, BWANA YESU asifiwe,
Ninacho kitabu hapa ambacho nimekielezea UBATIZO WA KWELI usome katika internate utaujua ukweli hapa. Na
hiki kitabu hakuna wa kukupinga dunia nzima, hata wewe unayebatiza kwa maji ya
kikombe ukisoma hiki kitabu utajiona ni sifurihujui kitu,. BWANA YESU ASIFIWE,
.
Na jambo lingine ni UBARIKIO
WA KWELI KWA WATU WOTE soma hiki kitabu hakuna mtu mzima
kubarikiwa, ni mapepo hayo mnafanya, Bwana YESU asifiwe, lakini msijali mambo
yameharibika shetani amelikamata kanisa,analivuruga vuruga kiapo YESU
alichofanya kwamba ni yeye na wanadamu sasa kimeingiliwa. YESU hana watu, ana
watu majina tu, wewe unaambiwa msimamizi wako ni Roho Mtakatifu, anakaa
mwanamke anakaa mwanaume, mwanaume huku amelewa pombe yake, mwanamke huku ni
mchawi wanakusimamia nini wewe? Roho Mtakatifu atashuka wapi? Nafasi ya MUNGU
imechukuliwa halafu kumwagiwa maji sio ubatizo!! Ila ni alama ya chapa 666 na
wanaofanya kazi hiyo ni wachapa 666.
Na ninawaeleza kazi zote za
shetani zimeshavurunjwa vunjwa, YESU anarudi anahitaji watu wake sasa.
Aliponitoa kwenye kazi ya
utalii amenitoa, “ najua hujui chochote, mimi nitasema ndani yako maana
nimewatuma wamenikataa, wamenisaliti.”
Watumishi wamependa pesa, wizi, ufreemason. Ni pesa kunyang’anya mali za
watu tuu. Hawataki kusema kweli yangu, na nyie ndio maana mnapotea, sio kwamba nawachukia nawapenda mataifa yote lakini yupo
wapi wakuwaambia kweli? Mimi ni kweli mngeangalia Neno langu ambalo ni kweli,
nyie mnaambiwa uongo ambaye siye mimi, uongo ni shetani lakini hatajwi shetani.
BWANA YESU asifiwe.
Niwaulize ndugu watazamaji
tafuta kwenye kitabu cha Biblia, Hakuna ubatizo wa kikombe!, sasa umetoka wapi?
Wanakuambia ukifa utaenda mbinguni. Kwani yeye hajui watoto wadogo wapoje?
Watoto wadogo hawana dhambi wametoka mbinguni wakikaa mpaka wakifika wakati wao
wakiwa wakubwa ndipo waamue na imani yao kwamba nimeamua kubatizwa, watu wanakubatiza kwa jina la MUSA, JOHN, sijui
YOHANA, kwa jina la HEBRON mnaokubali mmeangamizwa, lazima maji mengi tena yanayotembea hivi, churuuuuu…na ya kisima pia fake! BWANA YESUasifiwe. Ndivyo jinsi mambo
yalivyoharibika. BWANA YESU asifiwe, Katika ubatizo YESU wakati anaenda kubatizwa,
hakutoa ada ya kubatizwa, hivi ada zimetoka wapi? Katika kanisa hutakiwi kulipa
ada yeyote, kanisa siyo secondary wa chuo. Nikuulize ndugu mtazamaji hiyo
sadaka unavyotoa unapewaga receipt, kuna mtu anakudai? Sasa haya yametoka wapi?
Ni biashara umedanganywa umeliwa wala mbinguni hamna 98% dunia nzima mambo
yameharibika. Ninasema hivi!! Ni bora hata wamissionary wasingekujaga, maana
ukisoma Biblia inasema kweli, wakatudanganya, wakatueleza ujinga , wengine
wakasikiliza wengine wanaujua ukweli kabisa lakini hawataki kuusema.. ni wakati
wa kila mtu kumjua MUNGU na kubadilika, mbinguni bila wokovu hakuna. YESU
hana tabaka, ni wokovu peke yake. BWANA YESU asifiwe, na ndio maana ile siku ya mwisho ndie yeye amechaguliwa
kuja kuwakomboa wana wa MUNGU.
Dini nyingine
wanamuita Nabii Issa. Sasa wewe kama hujakuwa kwenye chama chake
unategemea nini? Hivi mnamuona MUNGU ni mpuuzi ana waangalia, laity ungepata kuisikia sauti yake
usingefanya upuuzi. Mimi mwenyewe hata biblia nilikuwa siijui. Utiisho wake naogopa,
sitaki kabisa lazima niwaambie ukweli. Ananiambia tarehe hii nenda kawaambie
hivi, hata sasa usifikiri ni Hebron ni
MUNGU anakuambia; ile mwisho zitapita
computer na video zako utasema kwamba hujasikia na umeona. Mnabaki kudanganywa
ukifa hauendi mbinguni. Utaenda mbingu gani wewe hujabatizwa? Soma Yohana 3:5-7
hakuna kitu waulize wamesoma digrii na
madigrii , digrii gani matakataka mnafundishwa? Hii ni kazi ya wamissionary
bora wangebaki huko huko .
BWANA YESU asifiwe! Na huko
ndiko wameharibika sasa watakuja Tanzania kuponea hapa. Hili ndilo Taifa MUNGU
amelichagua kama ni EDENI amekwisha kulikomboa ni nchi yake. Tanzania bwana
hakuna nchi itayoivamia Tanzania tena. Nimewaambia mimi MUNGU ndiye kaniambia
hakuna nchi itakayo ivamia yeyote. Ila huko ndani wale ambao hawana MUNGU
wataendelea kutandikwa tuu kwa namna yake.
BWANA YESU ASIFIWE. Kwa sababu MUNGU hawezi kuangalia kama hamumtaki lakini mnanitaja wa nini? Yeye atawapa
njia gani? BWANA YESU asifiwe, ni wakati wa mabadiliko lazima ubatizwe na
wakati wa kubatizwa usikubali kubatizwa
na Nabii wa uongo, usikubali kubatizwa na mchungaji ambaye hajabatizwa na maji
mengi na yeye hajabatizwa! Wala sio
mwanafunzi wa YESU.
Tazama wale mitume wa YESU ndio walofundishwa kazi hii? Jibu siyo. Walimuua Petro halafu ndio wakaanzisha mambo yao sasa
nakuambia Petro wa leo Nabii hebron, nakuambia mimi hakuna kitakacho
nisimamisha , Bwana YESU asifiwe, kama hili jiwe hili, mimi sisikii kitu. Bwana
YESU asifiwe, YESU amelijenga kanisa , nakuambia ukweli ubadilike, mnaua wananchi , mnaua mataifa, watumishi
mnawapa sumu, kitu gani? Hata nyie viongozi na wasomi kaangalieni Biblia hii
tafuta kama kweli wanampenda MUNGU, kama kweli hawamchukii huyu MUNGU tafuta kwa nini hawafuati Neno
lake, wanatafuta ya huko? Je! Wewe mwanadamu umeumbwa ili uwekewe ya huko au ya hapa!
BWANA YESU asifiwe, soma katika
kitabu cha Ufunuo 22: 18-19 “ na mtu yeyote akiondoa lolote katika maneno ya
unabii wa kitabu hiki MUNGU atamuondolea sehemu yake katika ule mti
wa uzima na katika ule mji mtakatifu ambao habari zake zimeandikwa katika
kitabu hiki. Sasa kuna nafasi ya kubadilika hii ndiyo nafasi ya kumrudia MUNGU,
kinyume na hapo No! haijalishi ulibatizwa Yordani wapi? Wengine wanabatizwa
kwenye maji mengi mnadanganywa tuu, kwanza muangalie anayekubatiza kama ana
MUNGU kweli, utamjuaje? Chunguza matendo yake ukikuta habari ya pesa tu hamna
kitu, michango kanisani hukuna kitu, ndio kazi kanis la sasa hivi iliyobakia na
MUNGU hahusiki nalo. Na ameniambia YESU
waambie Hebron, wamepotea. Mimi siangalii pesa zao, mimi sijatuma
wakachangishe harambee, mimi sijatuma wakawe na mapartiner na kutafuta watu
wenye pesa kuwaambia ndio wasapoti huduma zangu, mimi najisapoti peke yangu.
Mimi sijawatuma watumishi wakatume namba za account kwenye TV na kwenye M-Pesa kuomba pesa za kuwezesha, mimi
sijawatuma hao ni wezi, Biblia inasema, usijisumbukie utakula nini, utavaa nini, maua
ninayanyeshea, je wewe mtumishi wangu kweli si bora zaidi? Mbona mimi siombi?
Nikukuambia nimekutuma,nimekutuma inatosha. Hicho ni kibali mambo yatanyooka.
Sasa hivi ni uchawi, mnatishwa na majengo, sasa hivi siyo majengo ni mapango, BWANA YESU asifiwe, mimi nimekaa
hapa kwenye mawe nipo na YESU, bwana.
Haya majengo bwana yamekuwa ni masoko,
wizi mtupu!
Hamna kitu. BWANA YESU asifiwe, kawachunguze ndani yao ndiyo wauza madawa ya
kulevya, ndio wanao walala wanawake zenu, na wanaume zenu, na watoto wenu, hawa
hawa!! YESU anakaa ndani ya mtumishi na ina maana kama yupo ndani ya Mtumishi
ina maana Mtumishi ni YESU anakaa ndani yake. YESU hazinigi jamani, hawa wana
mambo yao, BWANA YESU asifiwe!
Inaudhi sana, inaumiza
sana lakini ole wao. Mimi ni Nabii bwana
ninakuambia, ukubali ukatae usinione mtoto nipo hivi ninachokuambia hayo
ndiyo ya YESU NINAYOKUELEZA. Wote
ninarudia mliomwagiwa maji hapa! Uwe mchungaji askofu sijui cheo gani
hujabatizwa wala wewe sio mkristo, wewe sio mwanafunzi wake, wala huifuati
kweli yake unafuata uongo wake, kitabu kinachoelezea kweli ni Katiba, ninacho
kitabu cha UBATIZO WA KWELI kisome. Hakuna kitu, sasa badilika. Badilika utubu
utubu! Wako wengine wana kiburi. YESU akaniambia wanajifanya awana shingo
ngumu, mimi ninawaangalia, ninawaangalia, ninawaangalia lakini!? Ole wenu.
Mtakavyobaniwa, hamtaamini. Uchawi sasa hivi hakuna tena, hakuna tena ni ajabu
katika nchi ya Tanzania mwaka 2010 nilipelekwa mbinguni. Jina la Mtumishi
lilikuwa la MOSES KULOLA tu!! Hao wakubwa, sasa ameondoka kuna nani? Uchawi
mtupu! Wote hao watumishi wenye mali
kubwa, nyingi, matajiri wengine wanasema mimi nawaonea wivu, hakuna! Hizo mali
ni za kunyang’anya watu na uchawi na mazingaumbwa. BWANA YESU asifiwe, wote
wenye mabenki hayo hata wanasoma Biblia na mifungo yote ni fake nawaambia
watoto wa MUNGU. BWANA YESU asifiwe.
Nitaelezea mambo yanayokwenda
kutokea Tanzania. Nitaelezea katika uchumi kwanza MUNGU ameirejesha Tanzania.
Ndege zitajaa nchini Tanzania, watalii watajaa Tanzania, ni nchi ijipange na
miundo yake. MUNGU anawarejeshea na uthamani wa Tanzania uliibiwa, na hawa hawa
wageni. BWANA YESU asifiwe. Viwanja vya ndege vimeinuliwa mtaona mabadiliko
makubwa sana. Na jambo lingine katika bandari ya Dar es Salaam, ndiyo bandary
sasa hivi kwenye ulimwengu war oho namba moja katika Afrika Mashariki. Mtasona
mabadiliko pale, meli nyingi zitakuja ipo siri iliyofanyika pale na hawa
watawala wa zamani lakini MUNGU amekwisha kuibomoa.
Jambo lingine ni kuhusu
Zanzibar, Zanzibar! Ooh Namshukuru MUNGU sana, kwa kuifungua Zanzibar. Zanzibar
itakuwa, haaa..!! sijui nikuelezeje,
nitaelezea kwa kidogo. Ni kiini cha soko watu wengi wanakimbia Dubai,
wanakimbia China, sasa wataanza kwenda Zanzibar. Wengine watasema itakuaje,
ndugu mtazamaji, embu nikuulize, hapo zamani Zanzibar ilikuwa nini? Si ndio
ilikuwa sako la watumwa. Sasa unafikiri ile connection kwa nini nchi zote
zinzenda pale, ule uthamani wake uliibiwa ukapelekwa nchi ambayo siitaji. Sasa
imerejeshwa, Zanzibar sio ya kawaida imenyanyuliwa.
Na katika Serikali ya Zanzibar
kule kuna mawaziri wataanza kufukuzwa, muda sio mrefu na mafisadi. Nilikwisha
kueleza kuhusu Tanzania na mmeona wanavyofukuzwa nab ado wataendelea kufukuzwa.
Ni YESU mwenyewe anafanya na anatumia
watu hivyo hivyo. Usalama wa Taifa na Jeshi la Tanzania limeinuliwa juu sana.
Sio lakuchezea tena, siyo la kudharau maana MUNGU ndiye amewashika na
anawapenda. BWANA YESU asifiwe. Bunge la Tanzania mtaendelea kuona mabadiliko
sana, katika vyama vya siasa, yeyote anayekwenda kinyume na mapenzi ya nchi hii
au anania mbaya kuhusu nchi hii atakuwa anatolewa tu , anatolewa tu, anakataliwa
hata afanyaje hata alogeje, Jambo lingine katika uchaguzi mwaka 2015 katika
nchi ya Tanzania, watu wengi watalia wagombea, wabunge wengi watalia na mawaziri, hawatakubaliwa,
kwanza na vyama na wananchi. Wote wanaoenda vibaya na atakaye tumia uchawi hatapata
urais. Hayo mengine nitayasema kwa wakati wake. Watu walizoea kuwa na kikundi
hiki nitapanga watu wangu,
oohoo..!! pangeni tu, hao watu ni wa
MUNGU, atawageuza mwenyewe watakula hela zenu, wanaishia wewe mrudie MUNGU,
muombe MUNGU lakini MUNGU mpaka sasa hivi anamjua rais wa Tanzania ni nani. Kwa muda wake na wakati wake,
lakini hayo hajaniruhusu kuyataja mpaka muda wake na wakati wake. Akili za
wanadamu mara Yule mara Yule nawaambia itakuwa ni kilio kwa Rais atakayetolewa.
Siyo huyo mnaemtazamia au hao, nimekwisha kuwaeleza, BWANA YESU asifiwe,
mmeshamuonaga MUNGU, wewe!! Ni wa kuchezea kujipangia tu, hii ni bustani yake
ameamua yeye. Wala mimi hakuna atakaye niua, nakueleza ukweli, amenitoa mimi
ni mtanzania halisi, BWANA YESU asifiwe. Na amenipenda hivi hivi, kwenye nchi yake hivi
hivi na mimi ninaipenda nchi yangu.
Walioiba pesa za Tanzania, huko Ulaya zitarejeshwa, haina muda! Hata
mfanyaje zitarejeshwa kwenye akaunti za Serikali. Hiyo ndiye YESU atakaeifanya
wala sio mwanadamu, wala hakuna wa kuzuia. BWANA YESU asifiwe.
Jambo lingine ndugu watazamaji,
hii habari ya masadaka kanisani. Hizo sio sadaka, sadaka ya kweli ni fungu la
kumi na shukurani. Hizo nyingine zote ni uongo. Soma kwenye biblia hakuna
sadaka ya matofali, ya ujenzi, ya uinjilisti, ya uchungaji ya mtume, hakuna.!
Ni hao wanaiba hizo pesa nawambia hao ni waizi maana MUNGU ameniambia mimi
sikuwatuma hivyo na ole wake, anaye watesa wana wa MUNGU. Watu wengi wamekuwa
wanalalamika na kulia ya kwamba MUNGU mbona hatubarikiwi, MUNGU tunafilisika,
tumetoa mpaka mafungu ya kumi tumechanganyikiwa mambo hayaendi.
Nikuambie?? Hazijaenda kwake, ni kwa jamaa.. na wajamaa
wanaenda kuuzia madawa ya kulevya umewapa wajamaa wamepeleka nyumba ndigo,
unawapa wajamaa wanaenda kunywea pombe, unategemea MUNGU atakubariki? BWANA
YESU asifwe.
Jambo lingine habari ya kuabudu
masanamu, ndugu watazamaji hivi niwaulize, MUNGU ni sanamu? MUNGU ni msalaba?
Kwa nini mnaabudu misalaba? YESU yupo zake mbinguni amestarehe, ameonyesha njia
mumwabudu yeye katika moyo, hata kama umeweka nyumbani kwako hiyo ni laana.
Msalaba ulitumika kuulia watu
toka zamani wenye laana, hakuna msalaba Mtakatifu, BWANA YESU asifiwe, ni kwa
sababu kipindi kile ni kwamba mtu akifa lazima apitie kwenye jambo kama hilo
kwenye msalaba. Ina maana ingekuwa ni kamba, watu wangechukua kamba takatifu?
Na ole wao, mambo yameharibika. Tazama hata YESU alipo kuwa na wanafunzi wake,
ujue mambo yameharibika ndugu watazamaji mnapewa sumu, YESU alitengeneza ile
chapatti ambayo ndio ilikuwa mwili wake, twaeni mle hivi, sasa nikuulize ule
mwili ulikuwa na alama ya msalaba? Wote mliokula msalaba mmemeza laana. Na wote
wanaotembea na ile misalaba hivi ndani yao wanatembea na laana kwenye ulimwengu
wa roho wamepelekwa golgota. Ndio maana mnakaa na misalaba mnapigwa na mapepo,
mnabondwa! Nimewafunulia siri nanakuambia ndugu mtazamaji hata msalaba
unavyowekwa pale kaburini si unadondoka unaliwa na mchwa, unaenda nao? Unaoza.
Hata YESU alivyozikwa kwa nini hakuzikwa na msalaba? Eti msalaba ndio alama ya
Mkristo? Msalaba ndiyo alama ya YESU? Hakuna. Rudini kwenye neno la MUNGU,
tazama sasa watu walivyopotea, tazama watu walivyopotezwa, hivi mmeshajiuliza
kwa nini makanisa watu waliookoka wajanja hawawekagi alama ya msalaba?
Walikwisha jua sasa mpaka unawekwa kwenye hii inaitwa chakula ya nini wala sio
chakula ya bwana, chakula ya hao, hivi unakula, unakula laana. Inaingia kwenye
damu, kwenye mwili, una dunda nayo na wengine mnatembea na msalaba hapa, YESU
alisema hivi, nimekwisha kubebea msalaba, Yule aliyekuja kubebamsalaba wa YESU
si Simoni? Si alikuja akaubeba?
Ni kwa ajili yenu msibebe tena.
Nani aliye waloga nyie wana wa MUNGU, mnabebeshwa misalaba vitu kama hivyo.
BWANA YESU asifiwe. Zaidi upate kitabu cha MAFUNDISHO YA NABII HEBRON.
Utafunguka ufahamu wako, upate kitabu cha MPINGA KRISTO,hii yote ni YESU
amenieleza nikueleze wewe. Bwana YESU asifiwe.
Jambo lingine usome kitabu MKRISTO USIKUBALI KUWA MPUMBAVU. Vipo kwenye
Internate na kanisani kwangu. BWANA YESU asifiwe, MJUE YESU KRISTO WA UONGO,
yupo wa uongo, sasa wengi wana wa uongo, wa msalaba wa uongo, michango wa uongo
na wewe umekuwa muongo pasipo kupenda, basi pata tena kitabu kingine JINSI
KANISA LINAVYOMUABUDU SHETANI. Lakini hawamtaji shetani Yapo mambo soma huku ndani.
BWANA YESU asifiwe. JINSI KANISA LINAVYOMKUFURU ROHO MTAKATIFU, vyote hivi
visome na vingine vingi na uendelee kufuatilia vipindi vya mtume na Nabii
Hebron. BWANA YESU asifiwe, Haleluya!!
Lakini usiogope leo ni wakati wa wewe kumjua MUNGU na kuujua ukweli. BWANA YESU asifiwe, BWANA YESU asifiwe,
nakwenda kuombea wale ambao hawajaokoka.
Sema BWANA YESU, naomba
unisamehe, dhambi zangu zote, nilizozifanya kwa kujua au kutokujua, uniandike
jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, BWANA YESU nimeteseka sana
nimebebeshwa msalaba, nimedanganyika hata nimebatizwa ubatizo usio wa kwako na
wewe ndie njia ya uzima, lakini angalia mambo yalivyoharibika, YESU niokoe.
“BABA ninaomba uwaokoe,” majina yao ukayaandike kwenye kitabu chako cha uzima,
uwalinde hukohuko. Baba ninakwenda kuombea wagonjwa ninawafungua walioibiwa
nyota, ninazirejesha. Vyeo ninarejesha waliofukiwa maisha yao ninafukua maisha
yenu, faraka kwenye ndoa naziondoa, kila aina ya kifungo nina kivunja, kwa jina
la YESU KRISTO WA NAZARETI. Kaskazini, Kusini napiga mapepo, freemason nalipua,
pepo la umasikini, nabomoa kwa jina la YESU. Ndoa za kipepo navunja kwa damu ya
YESU KRISTO wa Nazareti. Ubaki wewe BWANA YESU peke yako, Bendera yako isimame
na bendera za shetani nazivunja, nang’oa zote kwa jina la YESU KRISTO wa
Nazareti, Baba, nina muinua rais wa Tanzania, mpe nguvu mpe hekima mlinde na
wote wenye nia mbaya kwa jina la YESU mpe hekima akaongoze nchi vizur na
mawaziri na serikali wakuu wa mikoa wote, mpaka idara ya chini wakafanye kazi vizuri
uchumi ukaendelee kunyanyuka juu, wasitishwe na hao wanaiba madini nafunga roho ya kuiba
madiniya watanzania yabaki kwa watanzania na mikataba mibovu naifuta kwa damu
ya YESU KRISTO wa nazareti. Mali hii MUNGU ulileta kwa ajili ya watanzania, na
watanzania ndio wafaidike. Baba, tumekuwa na akili sasa, na hao wana akili
MUNGU, sasa wamiliki, wape uwezo waongoze kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti.
Asante MUNGU wa Ibrahimu, asante MUNGU wa Isaka katika jina la YESU KRISTO wa
Nazareti.
Ndugu wasomaji MUNGU azidi
kuwainua, MUNGU azidi kuwabariki, msidanganyike tena. Kanisa sasa hivi
limetekwa na shetani ukisikia habari ya michango michango, hata harambee
mnaokwenda kushiriki kusema harambee laki,elfu kumi, laki wabaki mmelaaniwa, nyumba ya MUNGU ni nyumba
ya sala peke yake. Kama ni yak wake
atafungua milango, itafanyika, sasa hao wanafanya hivyo wanatumia uchawi,
Afrika imeoza, Ulaya imeoza, hawajui wanachokifanya asilimia mbili tu ndio
imebaki na YESU, yamkini hata na wewe nakuambia hapo haupo na YESU, unafunga
sana mpaka na vidonda matumbo yametoboka, utabaki unakemea unakemea nini wakati
wewe mwenyewe umewekwa kwenye ngome ya shetani, hivi nikuulize wewe umepigwa
chapa 666 hapa, ubatizo wa kumwagiwa hapa. Kwa jina la Baba na la Mwana na la Roho Mtakatifu, yupo
Baba wa kuzimu, yupo mwana wa kuzimu, yupo Roho mchafu wa kuzimu, lakini
hatajwi maana mngekimbia waulize imetoka wapi?
Kataa..!! kabatizwe upya
uwekewe kibali na YESU uwe shirika moja kati yake na wewe, ukatae kabisa katika
jina la YESU. Pia na katika vipindi vya redio mbali mbali, katika nchi nzima ambapo
waneneza habari za YESU. Mliopo nchi zote mfunguke.
Soma katika makala ya Nabii
Hebron, siyo ya kwangu ni YESU ameniambia nikuletee wewe, mimi bwana sijaitwa kwenye kazi ya MUNGU, na baba
yangu, na mama yangu na dhehebu ni peke yangu tulikuwa wawili na hakuna wa
kusimama mbele yangu, kama yupo ajaribu, ni wakati wa watu wote kumjua MUNGU ni wakati wa
kukaa vizuri. Usitishwe hizi biblia unasomewa mistari luka 10, hazifanyi kazi,
zaidi ni watu wanamapepo ya utambuzi, majini, wachawi watupu, ndio wanaopaa
usiku kama mwewe, ndio wanawanga sawa sawa.., nimekuwa nikiletewa simu nyingi
watu wanalalamika mchungaji anamwambia mtu nipe laki tano, milioni, usipompa
anakulaani, usitoe, MUNGU hawezi kumtuma kwako, halafu wewe mwenyewe huna hela,
halafu nakuambia unipe hela, hivi nani amewaloga? Mmewekewa roho ya punda, sasa
hivi ni bye, bye, mbatizwe ubatizo wa maji mengi ambao upo katika katiba ya
MUNGU, mtu asije akakuambia ni imani yako, ukijisikia, soma kwenye Biblia.
Ndiyo kubatizwa ni imani yako, wewe mtoto mchanga anaimani? Wametoa wapi hiyo
akili ya kumuweka mwanaume na mwanamke
mchawi mlevi,biblia imepindishwa pindishwa ndio elimu ya uongo nanyi
mnapokea uongo pasipo nyie kujua. Makanisa yamenuka yamekuwa ni mapango! Hakuna
kitu , wizi mtupu! Na serikali ziwamulike ziwachunguze , hata mimi nichunguzwe
wafuate biblia huu ubatizo huu ni wanaua wana wa MUNGU, hata nyie viongozi
mmeuliwa, hao wamissionary wamepotea, waliwaua wanafunzi wa YESU ndio uongo
sasa. YESU yale aliyofundisha kwa wanafunzi wake ndio amerejesha kwangu
niwaeleze na unaposikiliza mimi ninakufungua,unafunguka. Shida yoyote
inayokusumbua njoo katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI, bure unapona,
hakuna habari ya pesa No!! nimekupa bure toa bure, hao wanakuambia habari ya hela
waizi, waongo, kataa achana nao. BWANA YESU
asifiwe, wanasema wanaombea nchi, wapi?? Ndio nimekuta wameloga nchi ya
Tanzania, viongozi hao wanajifanya kwenda kuwasalimia viongozi wa nchi, labda
waziri fulani, tunakukaribisha, wanavyompa mkono tu hivi,wanamloga, nyan’ganya
kila kitu, anakuwa taahira, kazi mimi nikuombea kufungua viongozi,unafungua,
unafungua, hawa hawa na wewe unaweza ukawa kiongozi, hii kazi ya kanisa
imeharibika. Mwangalie MUNGU mtegemee MUNGU, BWANA YESU asifiwe.
MUNGU akubariki, MUNGU akuinue,
tutaonana tena muda mwingine wakati mwingine, siku kama hii ya leo. Wakati kama
huu.. Haleluyaa.. ubarikiwe.
NABII HEBRON.