BWANA YESU asifiwe ndugu
mtazamaji na msikilizaji, karibu tena kwenye kipindi cha Mtume na Nabii Hebron.
Siku ya leo nitakwenda kufundisha somo kuhusu”mtumishi ni nani na mnyang’anyi
ni nani “. Kwanini YESU alisema watokeao nje ni wanyang’anyi na alisema ni
wezi? Alikuwa anmaanisha ni nani na ni akina nani.
“Baba ninawaombea na kuwatakasa
mioyo yao maana YESU wewe ulivyoleta ujumbe huu uliuleta ili kwamba na kuacha
iwe kumbukumbu yetu na sisi tukapate kujifunza tusikutane na wanyang’anyi na
wala tukikutana na wanyang’anyi wasitunyang’anye.”
BWANA YESU asifiwe.Tutafungua
neno la MUNGU kutoka kitabu cha Yohana 10:1-2, 7-10.BWANA YESU asifiwe. Neno la
MUNGU lina sema hivi,”YESU akawaambia Amin amin nawaambieniyeye asiyeingia
mlangoni katika zizi la kondoo lakini akwea penginepo ,huyo ni mwivi nae ni
mnyang’anyi. Aingiaye mlangoni ni mchungaji wa kondoo. ” ”Basi YESU aliwaambia
tena amin amin nawaambieni mimi ndimi mlango wa kondoo wote walionitangulia ni
wevi na wanyang’anyi ,lakini kondoo hawakusikia .Mimi ndimi mlango; mtu
akiingia kwa mimi ataokoka ;ataingia na kutoka nae atapata malisho. Mwivi haji
ila aibe na kuchinja na kuharibu na mimi nilikuja ili wawe na uzima ,kisha wawe
nao tele. Amen”
BWANA YESU asifiwe ,nitawaeleza
maana ya mnyang’anyi na kwanini YESU alielezea wanyang’anyi.YESU alikwisha
kujua kuwa atakapoondoka watakuja wanyang’anyi na watafanya kutumia jina lake
kujiita, kufundisha na kujiita wachungaji lakini kumbe ni wanyang’anyi.BWANA
YESU asifiwe.
YESU alikwisha kuona mbali BWANA YESU asifiwe, kwamba kupitia jina lake
shetani amekwisha kuandaa watu waje kutumia jina lake ili kuja kuwanyang’anya
na sio kuchunga kondoo. Mnyang’anyi siku zote kazi yake ni kufilisi na
kunyang’anya bali mchungaji sio kunyang’anya wala mchungaji hata siku moja halipwi
mshahara yeye amejitolea. BWANA YESU asifiwe.
Nitakuja sasa tuongee katika
kifungu tulichosoma, BWANA YESU asifiwe kuhusu unyang’anyi na utumishi. Kwanza
kabisa naeleza katika kanisa maana uko unyang’anyi wa aina nyingi lakini mimi
naeleza katika kanisa kazi aliyonituma YESU. BWANA YESU asifiwe uko unyang’anyi
katika kanisa sasa hivi lakini watu wanaona ni utumishi, jambo la kwanza
wamemnyang’anya MUNGU neno lake halafu nitakuja ya pili wananyang’anya kondoo
kivipi. BWANA YESU asifiwe. Wamemnyang’anya MUNGU neno lake kwanza wameondoa
ubatizo wa maji mengi wameweka ubatizo wa maji ya kikombe. Hao wanaitwa
wanyang’anyi wa neno la MUNGU . wanyang’anyi wamemnyang’anya YESU haki yake
hawataki ile haki ya YESU ikapate kusimama ndio maana wameweka ubatizo wa maji
ya kikombe. Nikuulize swali ndugu mtazamaji na msikilizaji yamkini unajua na
wewe unajiita mchungaji kumbe umeshakuwa mnyang’anyi na hupendi maana hukujua.
Achana na hiyo kazi maana na wewe umeshakuwa ni mnyang’anyi.
BWANA YESU asifiwe . Unyang’anyi
kupitia neno la MUNGU, imeandikwa kwamba watu wasiabudu sanamu lakini leo hii mchungaji
anawaambia watu waabudu sanamu makanisani,hao ni wanyang’anyi, kwanza
wamemnyang’anya MUNGU, MWENYEZI MUNGU wanamdhulumu.BWANA YESU asifiwe. Ninakuja
kwa upande wa MUNGU halafu nitakuja tena kwa upande wa wanadamu wapate kuelewa
namna gani wanyang’anyi walivyo maana mnyang’anyi akijiita mnyang’anyi watu
hawatakwenda, akijiita mchungaji, mwalimu, mtume, na nabii watakwenda.Sasa YESU
alikwisha kujua iko siri inayofanyika hapo watajificha kwa ndani kwa mlango wa
nje.Mlango wa nje ina maana ya kwamba maneno ya nje ya Biblia ndiyo yameingizwa
na ndio yamejaa makanisani. BWANA YESU asifiwe, ukisoma neno la MUNGU linasema
‘nimekupa bure toa bure’ huo ni mlango wa kondoo. Lakini mlango wa nje ‘leta
pesa yako ndio ufunguliwe’.Hao ni wanyang’anyi; sio watumishi hao si
wachungaji, hao ndio wanyang’anyi. BWANA YESU asifiwe. Wanyang’anyi kama vile
watu wanavyokwenda sokoni wanataifishwa mali zao,sasa watu ambao wanaenda
kusali kwa wanyang’anyi wanakwenda kusali katika masoko. Alisema hivi YESU,
wanapita na manguo yao marefu wakisalimia watu masokoni wakijifanya wako na
mimi kumbe ni wanyang’anyi au ni mbwa mwitu. Huu mfano wa sokoni ilikua ni
jingo ambalo linaitwa kanisa sasa. Mahali kuna michangomichango popote hapo ni
sokoni. Sasa nikuulize wewe unavyokwenda sokoni si unakwenda kunyang’anywa?
Utapata kitu? Utapata matango bila kutoa hela? Jibu hupati. Sasa kanisani
unapata baraka zako bure mahali alipo
Mchungaji YESU wa Nazareti. Haleluya lakini usiogope MUNGU anakwenda
kuwafungua amenituma habari njema yeye ambaye si mnyang’anyi BWANA YESU mpate
kuuelewa ukweli wake maana wengi wametekwa na shetani kwa kutokujua.
BWANA YESU asifiwe. Wengine sasa wameanza
kumnyang’anya mpaka MUNGU wanawabatiza
watu kwa majina yao, hoa wanaitwa wanyang’anyi.BWANA YESU asifiwe, sasa suala
la wanyang’anyi watu wanatakiwa walielewe, sio kwamba atakuja kuwanyang’anya
nguo mikononi hapana. Unyang’anyi wa kutumia jina la YESU makanisani,
unatengenezewa mistari unatoa mwenyewe kwa nia yako. Unajua watu wamezoea kuita
majangili ni wanyang’anyi , hao ni wa kimwili sasa kuna wanyang’anyi wa kiroho.
Wa kiroho anakumaliza kila kitu ni bora hata jangili anaweza kukuonea huruma, lakini
wa kiroho anakunyang’anya kila kitu. Maana jangili au mwizi vile ana hofu ya
MUNGU anavokutana na MUNGU anaacha, lakini hawa wanaitwa wanyang’anyi kwasababu
wameshamkufuru MUNGU. Wanamnyang’anya MUNGU haki yake yeye na kunyang’anya watu
wasipokee neno la MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Mfano imeandikwa niabudu mimi peke
yangu lakini leo utaambiwa abudu nyota, abudu mwezi, abudu jua BWANA YESU
asifiwe abudu Yohana,Mathayo watoto wa MUNGU wale waliokufa, tayari hapo
mmeshamnyang’anya MUNGU kwahiyo nyie mnaofanyo hivyo ni wanyang’anyi. BWANA YESU asifiwe. Sasa
kama unaongozwa na mtumishi wa namna hiyomnyang’anyi na wewe maisha yako kwamba
huyo anakupeleka katika shimo uangamie. Uelewe kwamba haupo katika kuongozwa na
mchungaji mwema bali unaongozwa na mchungaji mnyang’anyi aliyevaa ngozi ya
kondoo kwa nje kumbe na mwizi ni jangili na wamejaa kila mahali.
BWANA YESU asifiwe. Sasa wengine
nitakufundisha ndugu msikilizaji na mtazamaji, nikufundishe; hivi sadaka siku
zote kanisani inatolewa wapi? Si inatolewa kwenye kikapu cha sadaka? Sasa iweje
leo mchungaji (ndio mnyang’anyi hao nawaita) wanasema usaini hapa juu ya nguo
milioni, elfu hamsini, na mguu elfu tano tano, mia tano; sasa niwaulize swali
ndugu watazamaji na wasikilizaji, je, ule mwili wake ndio kapu la sadaka? Jibu
sio. Je, MUNGU aliamuru sadaka watu wasaini kwenye nguo ya huyo mnyang’anyi?
Hajaruhusu hivyo. YESU mwenyewe katika nguo yake haijawahi kusainiwa hivyo.
Sadaka ni kitu cha shukurani kati yako wewe na mwenyezi MUNGU. Lakini iweja
sasa leo hii wanaibuka wanyang’anyi na wanawanyang’anya wana wa MUNGU na
wanaona kweli nikisaini kwenye mabega maisha yangu yatazidi kunyanyuliwa.
Nikisaini hapa kwenye miguu, katikati, maisha yangu na mimi yatazidi
kunyanyuliwa. Watu wanajikakamua kumbe wananyang’anywa mali zao na pesa zao.
Hao ninasema ni wanyang’anyi, ndio YESU anasema wako hapa. Wanyang’anyi ni
watumishi wanaosoma majina ya watu kanisani wametoa shilingi ngapi, wakupa
risiti, wanataka email, box namba na tarehe uliyotolea. Kwa YESU hakuna mambo
kama hayo, hizo ni saikolojia za wanyang’anyi. Wamesema hivi, wanapita mlango
wa nje. Huo ndio mlango wa nje mwana wa MUNGU uliyopita kwako na maisha yako
vile ili na wewe upate kuelewa kwamba yameshaangamia, umeibiwa kila kitu kwa
hiyo hufanikiwi. Mikosi, balaa, unafikiri unaenda mbinguni kumbe
umeshanyang’anywa pia haki yako ya kwenda mbinguni. Hata unabaki na haki ya
kupelekwa kwa shetani, leo upate kufunguka.
BWANA YESU asifiwe. Ndugu
mtazamaji na msikilizaji, nimefundisha kwa ufupi unyang’anyi, watumishi wanavyomnyang’anya
MUNGU haki yake kwa ufupi. Na sasa nitaingia kwa jinsi mnyang’anyi
anavyokunyang’anya wewe kanisani. BWANA YESU asifiwe. Wewe ukiona ni mtumishi
wa MUNGU anakuambia kasomeshe watoto wangu MUNGU anakuambia, huyo ni
mnyang’anyi. Muulize swali; wakati unazaa watoto wako wewe, hukujua kuwa
unatakiwa kuwasomesha? Muulize swali; wakati unazaa watoto wako hukujua
wanatakiwa kula? Wewe mtazamaji nikuulize; wewe unavyowazaa watoto wako hujapanga
maisha yao uweze kufikiria watasomaje, utawasaidia, yeye anakuja kukupangia?
Hao ni wanyang’anyi. Wanakuibia mpaka haki ya watoto wako na Baraka zako wewe
unaona unapeleka kwa mwenyezi MUNGU, kumbe unailaani familia yako wewe
mwenyewe, inabaki na mateso. Na siku ile ya mwisho mwenyezi MUNGU atakuuliza.
BWANA YESU asifiwe. Wanyang’anyi
wanaonyang’anya wana wa MUNGU wanajiita watumishi. Hao sio watumishi bali kila
anayekula kondoo, anazini na kondoo, huyo ni mnyang’anyi. Ni ajabu sana
ukiangalia simu za watumishi utakuba wanaita kondoo zao bebi (baby) na hani (honey)
na ana mke. BWANA YESU asifiwe. Na ukisoma meseji wakizituma ni maajabu watoto
wa shule yaani wanavyowaharibia maisha yao. Hawa ni wanyang’anyi. Wanawalaani
wanawajaza mimba, wanawapa ukimwi. BWANA YESU asifiwe. Ni wanyang’anyi,
wanatumia jina la YESU. Ninawaambia leo hao sio watumishi wa MUNGU. Ukikuta
mtumishi anachangisha pesa kwenye redio, mwambie huyo ni mnyang’anyi. Biblia
inasema, asisumbuke atafanya nini; MUNGU atafungua milango. Kwa sababu yeye ni
mnyang’anyi anaendeleza kazi ya unyang’anyi kupitia jasho lako wewe na
ukitegemea kwamba MUNGU atakubariki lakini hakubariki. BWANA YESU asifiwe.
Jambo lingine ujue ni mnyang’anyi, Biblia inasemama hivi, sadaka yako utoapo,
kushoto wala kulia isijue, mtu yeyote asijue. Wao wanakuambia andika jina. Ile
kuandika jina, tayari wamemnyang’anya MUNGU Neno lake. Unaona
wanavyomnyang’anya MUNGU? Na wewe sasa ukitoa vile waziwazi, umenyang’anywa na
zaidi nawatangazia leo kila sadaka yako inapojulikana na kiasi, ina maana
umemtukana mwenyezi MUNGU, umemwambia shetani wewe uko juu MUNGU si kitu.
Ninakueleza kama ulikuwa hujui, ndio maana ninapiga kelele kutetea Injili, watu
mfunguke MUNGU asitukanwe tena, Neno lake lifuatwe. Vile vile hata katika
mahakama, sheria na katiba mtu anapovunja tayari ameenda kinyume na mpango wa
MUNGU. Sasa sadaka leo hii majina, risiti, ni tayari katiba ya mwnyezi MUNGU
imevunjwa. Sasa malipo ni ule mwisho utayapata na wengine wataanza kupigwa sasa
hivi, na tayari wamekwisha kuanza.
BWANA YESU asifiwe. Watoto wa
MUNGU, mtumishi sio mnyang’anyi sasa jina la mtumishi linaharibika kwa sababu
ya nini? Sababu ya utapeli. Nyie wenyewe ni mashahidi mmechoka, sasa hivi kila
kitu ni habari ya pesa, kama ni habari ya pesa ndio njia ya unyang’anyi.
Anasema mlango wa nje; wewe ulifikiri mlango wa nje utafunguliwa uone wapi?
YESU akasema ni wanyang’aniyi hao. Sasa na wewe uwe makini, siku ya leo ukapate
kufunguka, usiitwe mnyang’anyi. Kama unampenda MUNGU, achana na hayo. BWANA
YESU asifiwe. Wanyang’anyi wanakuwa na mabenki ya kanisa, kanisa halitakiwi
kuchaji riba. Mwenyezi MUNGU hachaji riba; amekwisha kukataa riba. Sasa kama wamemwibia
jina la MUNGU wakaingiza kuchaji riba, wamemsaliti MUNGU, wamemchukia MUNGU,
lakini wanasema BWANA akae na wewe; wapi? Chunguza matendo yao ni namna gani
wanavyokwenda. Hapo ndipo utaelewa tofauti ya mtumishi na mnyang’anyi. Nimekuja
nikufundishe; wanyang’anyi siku zote wanavunja katiba ya Neno la MUNGU lakini
kwa kivuli cha utumishi; wanabatiza ubatizo wa maji ya kikombe, wanabariki watu
wazima, wanabatiza watoto wadogo, wameongeza huduma ya sita ya Uaskofu. MUNGU
alianzisha huduma tano, zimekuwa sita. Unaona unyang’anyi huo? Hao ndio
wanyang’anyi. Jambo lingine wanavaa kofia wakati biblia inasema mwanaume asivae
kofia wakati anapohubiri. BWANA YESU asifiwe. Sasa hao ndio wanyang’anyi lakini
wanajiona mtumishi wa MUNGU.
BWANA YESU asifiwe. Jambo lingine
mnyang’anyi hamjui MUNGU, wala MUNGU hajamuita, ila yeye amejiita, anatafuta
maslahi yake. Mnyang’anyi anatoka kwa shetani, lakini hamtamjua akijisema hivyo
utamjuaje? Chunguza matendo yake kuanzia sasa na ukishajua uondoke hapo.
Haiwezekani mtumishi akubatize wewe kwa jina lake, amemnyang’anya BWANA YESU.
Wewe ni wake. Sasa nikuulize; wewe ni wa mchungaji au ni wa mnyang’anyi? Na
kama wewe ni wa mchungaji YESU, kwa nini umekubali kubatizwa kwa jina la
mchungaji? Amenituma habari njema, kanisa sasa hivi limechakazwa. Hii ni dunia
nzima, uwongo mtupu. Pamenuka, ni wizi. BWANA YESU asifiwe. Wanabaki kucheka
serikali zina ufisadi, ufisadi uko kanisani ndio umeanza mizizi na ndio
umestawi; na yale matunda yakaingia kwa
waumini, uovu unaendelea. Ninawaombea hata nchi mbalimbali muache ufisadi. Haya
matawi ninayakata kwenye ulimwengu wa roho, kwa sababu ufisadi umeanza katika kanisa.
Kanisa lingesema ukweli, watu wasingekuwa na ufisadi lakini ukiiba ndio
unapendwa kanisani, ukiiba kwanza ndio unakumbatiwa kanisani kuleta pesa, na
zaidi unakuta hata mchungaji na yeye anaingia huko. Sasa ni mchungaji wapi?
Huyo ni mnyang’anyi.
BWANA YESU asifiwe. Watoto wa
MUNGU mpaka sasa mmepata picha na kuelewa mtumishi ni yupi na mnyang’ani ni
yupi. Haleluya.. Anapokuwa anaeleza habari za watu huyo ni mnyang’anyi, hiyo ni
dalili ya kwanza kwamba ni mnyang’anyi. BWANA YESU asifiwe. Ukikuta kanisa kuna
kikapu cha mama mchungaji, baba mchungaji cha sadaka yake, hao ni wanyang’anyi.
Wamemnyang’anya MUNGU. Kwanza biblia haijaruhusu kuwe na kikapu cha baba
mchungaji au mama mchungaji. Kikapu ni kimoja tu peke yake cha sadaka. Na zaidi
ukiona kanisani mtumishi (anajiita mtumishi huyo ni mnyang’anyi) anakasirika
kabisa watu hawatoi mpaka anataka kulia, huyo ni mnyang’anyi amekikosa
alichokuwa anakitafuta, sio mtumishi au ukikuta mtumishi anaangalia anachagua
sadaka, anachukua noti, hizo za coin (sarafu) anazipiga kikapu huko, au
anawaambia ndizo hizo mnamtolea MUNGU? Ninawaambia hivi, MUNGU kwake hakuna
sadaka kubwa wala ndogo, ni ajabu sana hata ukisikia mtu anaombea sadaka,
anasema MUNGU awabariki wale waliotoa kidogo na wale waliotoa nyingi; nawaeleza
hao ni wanyang’anyi. Sadaka wewe unapotoa ndugu mtazamaji, unampa huyo
mchungaji au unampa MUNGU? Nikuulize swali, MUNGU amesema ni ndogo au ni
nyingi? MUNGU ndiye anayejua. Kwa MUNGU kila kitu; sadaka ni ya kwake lakini
wanaanza kutengeneza mazingira aliyetoa ndogo na kubwa; ni wanyang’anyi.
BWANA YESU asifiwe, Haleluya; ni
wakati wa kuelewa maana jina la utumishi limeoza. Sasa si utumishi, nimeamua
kupasua katikati, kutenganisha utumishi na unyang’anyi. Na zaidi utaingia
katika website www.prophethebro.org
halafu ingia katika blog pale, BWANA YESU asifiwe. Utakuta somo lililoelezea
zaidi la unyang’anyi kwa hiyo utamjua mtumishi na mnyang’anyi. Na kwa kupitia
somo hili ukirudisha picha yako katika maisha yako, utajiona mara nyingi
umehudumiwa na wanyang’anyi. Na mnyang’anyi haji ili kubariki, anakuja ili
kuiba anakufanya uwe kitegauchumi kampuni yake, kukutumikisha kama vile punda
wako unavyompa kubeba mizigo ya maji akupelekee. BWANA YESU asifiwe, ndivyo
unavyofanywa mwana wa MUNGU. Amenituma BWANA YESU niwaeleze habari yake kwamba
msikubali kuongozwa na wanyang’anyi, wanapita mlango mwingine. Mlango mwingine
ni maneno yanayotoka kwenye biblia mengine, BWANA YESU asifiwe, halafu
wanatumia jina la YESU. Mtawajuaje? Kwa matendo.