NINI MAANA
YA BOXING DAY 26.12 KILA MWAKA!
Boxing day tafsiri yake kwa Kiswahili ni siku ya wapiganaji
yaani watu wanaopigana, na pia ina maana kwa Kiswahili ni siku ya wabeba
maboksi. Ila hapa watoto wa MUNGU ninaelezea katika ile siku ya 26.12 kila
mwaka ambayo inaitwa boxing day eti wanaiita ndiyo siku ya kupewa zawadi za Krismasi. Mimi nawaeleza jamani ulimwengu ulishatekwa na shetani na wanadamu
hawaelewi hata maana ya boxing day kuwa ni siku ya wagombanaji au wapiganaji,
au wanabeba maboksi, lakini wao wameiita ni siku ya kupeana zawadi za maboksi
ya Krismasi. Watoto wa MUNGU nataka muelewe YESU hachezewi na hastaili
kuchezewa hata kidogo.
YESU alipozaliwa wale mamajusi walivyokwenda kumuona siku
hiyo hiyo waliongozwa na nyota na walifika siku hiyo hiyo na siyo siku ya pili,
walimpelekea zawadi wakaondoka. Sasa shetani akaja akaipindua ile siku ya
Krismasi ndiyo siku ya kupeana zawadi, akawakamata fahamu miaka mingi
akashirikiana na watumishi waliomuasi YESU miaka mingi wakaipindua ile siku ya
Krismasi ya kupeana zawadi maana ndivyo ilivyo stahili, shetani akaiita 26.12
ni boxing day. Sasa nimeshakuelezea maana ya boxing day kama unayo akili timamu
utaelewa vizuri kabisa haya ninayokuelezea. Na wanadamu walipoikubali na
ikapitishwa hata katika kalenda ikajulikana rasmi na watu wakaitii. Sasa shetani
anachokifanya ile siku ya boxing day anakuja kupanda magomvi katika mioyo ya
kila mtu ambaye atampa mtu zawadi na kumuambia happy boxing day.
Jambo lingine inaitwa boxing day sababu siku hiyo ni siku
ambayo kuzimu inakuja kuiba kila kitu cha mtu ambaye atatoa zawadi kwa mtu na
kuziita boxing day, kinachofanyika hapo wewe mwanadamu utanyang’anywa kila kitu
katika ulimwengu wa roho ambavyo ulibarikiwa navyo katika siku ya Krismasi
katika ulimwengu wa roho na utabakia boksi tupu ndiyo maana inaitwa boxing day
siku hiyo. Hivyo YESU alivyonijulisha hayo anataka baraka zenu zisiibiwe tena
na kufilisiwa na shetani katika siku hiyo. Usishiriki ili usinyang’anywe vitu
vyako ubakie boksi. Boxing day ni siku ya shetani na serikali yake kuja kuiba
vitu vya watu katika ulimwengu wa roho, na ili usiibiwe ukitoa zawadi hata siku
moja zawadi yako usiitoe boxind day, hata leo hii ukisema hivyo unaibiwa baraka
zako katika ulimwengu wa roho. Haya tungeyajua miaka mingi sana ila YESU WA
NAZARETI alikosa wa kumfunulia haya na kuwaeleza watu wote wa mataifa ili
wapone. Na wewe uwatumie na wengine katika nchi zao na YESU atakubariki, na
shetani hiyo siku anayowaibiaga watu vitu ateketee na ashindwe katika jina la
YESU WA NAZARETI. Na mimi Nabii Hebron nawatakia mpeane zawadi na msiite tena
ni siku ya boxing day mkafilisiwa na shetani. Ukweli uwaweke huru na mkae katika
utakatifu siku zote ili akija YESU akupate.
NABII HEBRON.