JINSI YESU
ALIVYOJARIBIWA NA SHETANI JANGWANI, IMETOKEA NA KUTIMIA KWA NABII HEBRON
KUJARIBIWA NA JOKA KUU.
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE. Katika tendo la kukubali
kumtumikia YESU na kuifanya kazi yake kwa ajili ya kuukomboa ulimwengu na kumuandalia
watoto wake ili atakapokuja anawachukua wale tu ambao watakubali na kuyatii
yale aliyonieleza na wayafuate kama serikali ya mbinguni ilivyopanga. Sikutegemea
katika maisha yangu, nije nikawa mtumishi na sikujua hata kama MUNGU ameniwazia
jambo hili ile baadaye aliniambia nilikuumba kwa ajili ya kazi rasmi ya
kuukomboa ulimwengu na kuikamilisha kazi yangu ila nilikuficha adui asikujue
kuwa wewe ni nani kama vile nilivyomficha Musa mpaka wakati wa kumtumia
ulipofika nikamtumia na wewe Hebron ilikuwa ni hivyo hivyo mpaka wakati
ulipofika nimeanza kukutumia mimi mwenyewe nakuongoza na kukupa maelekezo ya
safari ya nchi ya Ahadi katika roho ili kuwaongoza sababu mimi MUNGU ninayeijua
njia ya kuja kwangu na hakuna aijuaye.
Mwanadamu yeyote asiyekusikiliza atapotea na kuangamia. Hata
kipindi cha Musa wale wana wa Israeli ambao hawakumsikiliza Musa waliangamia
jangwani na ndivyo ilivyo kwako. Niliogopa na kushtuka sababu sikuzoeaga
kusikia maneno mazito kama haya. Akanifundisha mengi na kumuangamiza joka kuu
na mengine ni yangu kama mimi. Akanikabidhi kwa malaika mkuu Mikaeli na Malaika
Gabriel na hata Musa ambaye aliwaongoza wana wa Israeli na Eliya, Baba wa
mataifa Ibrahimu, wazee 24 wote nimewaona na kuongea nao, sababu MUNGU anapenda.
Jamani hapa ulimwenguni ni pabaya, mbinguni ni pazuri sana hapaelezeki ila
jitahidi uokoke na uishi maisha matakatifu siku zote, siku moja ya mwisho
utafika.
Nawashangaa wanadamu wanaipenda dunia ni sababu hawajui
waendako, mimi napajua nawaeleza. Sasa naelezea yaliyonikuta 9.12.2014 kwa mara
ya kwanza nilikutana na joka kuu kama vile YESU alivyokutana naye jangwani
akamjaribu YESU.
Mathayo 4:7-9
“7 YESU akamwambia, tena imeandikwa, usimjaribu
BWANA MUNGU wako. 8 kisha ibilisi akamchukua mpaka mlima mrefu mno,
akamwonyesha milki zote za ulimwengu, na fahari yake, 9 akamwambia,
haya yote nitakupa, ukianguka kunisujudia.”
Na mimi Joka Kuu akaniambia umenitesa sana na kila siku
unaharibu ufalme wangu na kunipiga basi sasa Hebron ninaomba uwe rafiki yangu
tushirikiane na mimi na nitaamuru kaskazini na kusini ilete vyote na nitaamuru
vyote nilivyonavyo nikupe wewe sasa hivi. Nilimuangalia joka kuu, nikamuambia
rudia unachosema, akasema hivyo hivyo. Nilimjibu mali zako sitaki, kwanza hauna
chochote, mimi ninavyo vya BABA yangu wa mbinguni, akanisihi tena nikamchapa
kofi, akaniambia hata miguu yako iwe rafiki yangu, nikamkemea, sina uhusiano na
shetani, akalia kwa uchungu joka kuu baada ya mimi kumjibu na kumkatalia ahadi
zake, baada ghafla akatoweka. Nikabakia nimeshikwa na mshangao hii ni nini? Kwa
nini aje aniambie maneno hayo, nikakumbuka na YESU alivyokuwa jangwani baada ya
shetani kushindwa kwa njia zote sasa akamfuatia jangwani na bado YESU
alimshinda, na kusudi la MUNGU lilitimia tu, nikapata tafsiri, nikapata tafsiri
alivyoniletea YESU muda huo akaniambia na wewe ameshakufuatilia kwa njia zote
alikushindwa, sababu upo na mimi na akakujaribu kama alivyonijaribu mimi na
wewe ulisimama imara, umeshinda vile vile na hii ni dalili umeshinda na ndio
sababu Amelia. Na wengine niliowaita walikataa kunisikiliza wakampa joka kuu
masikio yao badala ya kunipa mimi YESU hivyo akawateka. Mimi YESU nilimsikiliza
BABA yangu siku zote na ndio sababu hakuniweza na wewe unanisikiliza mimi tu na
ndiyo sababu hatakuweza.
Watoto wa MUNGU shikeni sana ninayowafundisha sababu
unapoyasikia hata jaribu liweje likija utakuwa unalo neno la kusema au njia ya
kushinda. Katika maisha yangu nimejaribiwa mengi ila hili la kuambiwa uwe
rafiki yangu nitakupa vitu vyote vya dunia hii. Nikuulize swali je ungepona au
ungeangamia na muda huo huo ilikuwa itimie vyote upewe na joka kuu, je
ungeshinda? Namshukuru MUNGU sana kwa kuniwezesha na kuniimarisha nikamjua yeye
ni nani na kutokuangalia vitu kama YESU alivyoangalia vya MUNGU tu na mimi
imewezekana.
Tamaa ni mbaya watumishi wametekwa hapo, idadi kubwa sana ya
wale aliowaita YESU, tazama hata Yuda aliangalia vitu akatekwa na shetani na
wasihi msitamani vya shetani, mbinguni vipo vingi kwa ajili yako, hivi ni vya muda
mchache tu na ni shida na utaingia jehanamu na yeye. Makanisa yanapenda misaada
hayajui misaada inatoka wapi. Wengi walipopokea misaada na mashirika mbali
mbali yakajiingiza katika kanisa wao wakafikiri ni upendo wa KIMUNGU kumbe ni
joka kuu anawaletea pesa na miradi na
walipoipokea tu tayari anawakamata sababu si wamepokea vyake, wengi mmepokea
pasipo kujua na wengine wanajua. Zaidi soma makala yangu na website www.prophethebron.org.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, uniandike
jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele. Unishike mkono nisipotee
tena. Amen.
NABII HEBRON.