MAANA YA
YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE!
Kila mwanadamu na watoto wa MUNGU nawasalimu kwa jina la
YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE. Neno hili siyo ligeni katika masikio
ya watu katika ulimwengu wote. Aliponiita YESU aliniambia nimekuita
ukaniandalie kanisa langu ambalo nikija nitakuja katika kanisa hilo katika ule
mwisho yaani unyakuo. Hebron kanisa uliite hivi YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE, na mimi nilifanya hivyo hivyo na imetokea sasa ninalo kanisa
linaloitwa kwa jina hilo hilo. Kwa nini limeitwa hivyo na YESU peke yake? Ni sababu
ni kanisa ambalo litaponya mataifa yote kupitia madhabahu hii ya YESU NI BWANA
NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE na kuwapeleka mbinguni, hivyo siyo kwa ajili ya hapa
Tanzania tu hapana, ni katika kila nchi MUNGU atawaokoa watu wake, atafanya
yeye ajuavyo wala hakuna litakacho weza kuzuia kusudi la MUNGU.
Nilivyoanza huduma watu walinichukia, walinitukana,
waliniona nimechanganyikiwa, nimepoteza mwelekeo, lakini mimi nilijua kusudi la
MUNGU lazima litimie na matunda yanaonekana na itakuwa katika ulimwengu wote. Imeandikwa
YESU atakuja kulichukua kanisa lake, ina maana litakuwa ni moja siyo mengi kama
ilivyo, sababu 98% ni makanisa ya uongo, yalishatekwa na shetani, watumishi
wamemsaliti YESU, wanatumia jina lake kutafuta pesa, kunyang’anya watu mali na
kufanyia mambo mengine maovu na kufanya shetani atawale kwa kiwango kikubwa na
kumfanya YESU awe na watu wachache, ikiwemo hata mtu yeyote anayejiita yeye ni
mkristo lakini hajaokoka, ajijue yeye ni mkristo wa uongo. Sababu YESU alikuwa
ameokoka na haina maana ukajidanganye wewe ni mkristo halafu haujaokoka. Ili uwe
mkristo ni lazima uokoke kama yeye. Makanisa mengi yanajiita ni ya kikristo
sehemu mbali mbali katika ulimwengu huu, hawajaokoka na wala hawana kitu
kinaitwa wokovu.
Sasa kama hamna wokovu basi uelewe ni feki (ukristo wa
uongo) ndio unaitwa hivyo sababu haujakamilika. Ila sasa uokoke ili uwe mkristo
na uachane na ukristo wa uongo ili YESU awe BWANA NA MWOKOZI wako na nyie wote
katika mataifa yote. Na zaidi YESU atawakusanya wale wote watakaomkubali katika
madhabahu yake na atawapeleka mbinguni, sababu ndivyo ilivyo pangwa na MUNGU,
hata biblia haijasema makanisa ya mwisho yatakuwa na nguvu za kushinda kuzimu,
bali neno linasema ni kanisa la mwisho milango ya kuzimu haitaliweza. Sasa hapa
uelewe, YESU atawakusanya mataifa yote hata sasa ameanza awakomboe yeye
mwenyewe na awatoe kwa shetani. Alinituma kuibomoa kuzimu, nimemfunga joka kuu
na msaidizi wake wa tatu katika ufalme wake alikuwa ni mwanadamu aliyeitwa
Maxwell nimemtoa, sasa hivi yupo katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE anamfurahia YESU.
Zaidi visit YouTube ya Prophet Hebron na blog utapata na
maelezo ya jinsi nilivyoitikisa kuzimu pia soma na vitabu. YESU NI BWANA NA MWOKOZI
WA MATAIFA YOTE, ninamshukuru alivyonieleza Hebron muda wangu wa kurudi
umeshafika wakati wowote, jiandae na uandae mataifa, na nyie mliopo mbali
mnaposoma na kutubu huko huko unaongozwa katika kanisa la YESU NI BWANA NA
MWOKOZI WA MATAIFA YOTE unawekwa na malaika katika listi ya waliomrudia MUNGU.
Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu, uniandike
katika kitabu chako cha uzima wa milele. Uniongoze nisipotee nipo kwako sasa
mimi ni mali yako YESU. Amen.
Zaidi karibu Tanzania katika kanisa lake YESU NI BWANA NA
MWOKOZI WA MATAIFA YOTE ili uwe moja
wapo wa kondoo wa kanisa la mwisho. Ubarikiwe!
NABII HEBRON.