Watoto wa MUNGU jambo lingine
ambalo nitakuja kuongea katika kitu kinachoitwa Christmas tree ni nini na asili
yake ni nini. Napenda kukuuliza kwanza ndugu msikilizaji, Biblia imeandika
Christmas tree? Christmas ni nini? Christmas ni birthday ya BWANA
YESU wa Nazareti peke yake. Sasa inapokuwa imewekwa Christmas tree, ina maana
kuwa YESU amenyang’anywa birthday yake. Na zaidi, hakuna mti wa
Christmas. Christmas ni birthday ya BWANA YESU peke yake, Mfalme wa
wafalme, mwana wa MUNGU ambaye jina lake tunalitukuza tunamwita YESU.
BWANA YESU asifiwe, sasa shetani
akaja, akaingilia ili awateke wana wa MUNGU. BWANA YESU asifiwe. Christmas tree
maana yake ni mungu mmea ambaye yuko huko kuzimu ambapo hapo zamani watu wa
huko Uingereza, BWANA YESU asifiwe; walikuwa wanaufanya huo mti kama ni MUNGU.
Kila wakiona wakila vitu vya kijani walikuwa wanaamini maisha yao yanasonga
mbele wanakuwa na uhai. Kwa hiyo wakaona mti wauite mungu unaitwa tammuz. BWANA
YESU asifiwe, Haleluya… Sasa tammuz hilihili, ndilo likaingizwa kwenye siku ya birthday ya BWANA YESU
wakasema huu mti uitwe Christmas tree ili kuchukua nafasi ya BWANA YESU kama
ilivyoibiwa; ikachafuliwa.
BWANA YESU asifiwe. Sasa ile siku
ya Christmas watu wanakuwa wameweka ule mti ndani kumbe wanakuwa wamemweka
mzimu wa tammuz na nilipokwenda kuzimu mimi tammuz nilimuona. Ni limzimu
likubwa lina mandevu, na likubwa kama li-mbuyu, BWANA YESU asifiwe; ili kwamba
kuhakikisha kwamba, wana wa MUNGU siku ya Christmas YESU asipite kuzibariki
nyumba zao, kutembea na kushiriki nao. Zaidi, unapoweka ule mti, unakuwa
umemsujudu mzimu anaitwa tammuz na kule kuzimu pia wanasherehekea pia siku ya
Christmas; lakini wanavyosherehekea wao, wanaweka ule mti vile vile ndani ya
nyumba, imeitwa Christmas tree. Sasa unavyoweka Christmas tree, na wewe
mwanadamu unaunganishwa huko, tayari umeunganishwa na mizimu.
BWANA YESU asifiwe. Ni ajabu sana
hata makanisani hiyo miti imejaa, YESU angemtuma nani? Wangemweleza nani? Kwa
sababu wamekimbilia pesa, hawataki kumsikiliza BWANA YESU. Mimi nawaeleza
ukweli kwa sababu watu wamefanyika kuasi pasipo kupenda, na wengine hawajui;
hata mimi nilikuwa najua Christmas tree ni kitu kizuri. Ninakuambia, tupa,
kachome. Hakina uhusiano na BWANA YESU. Haleluya… BWANA YESU peke yake ndiye
unatakiwa umwamini na usherehekee siku ya Christmas umpambe katika roho yako na
moyo wako. Lakini cha ajabu siku hizi miungu ndiyo inayokuwa katika makanisa.
Tazama miezi ya 12, tazama watu wameficha na manailoni yametengenezwa na
mataifa mbalimbali. Imeweka mzimu unaitwa tammuz huko kuzimu. Madhara yake,
unakuwa umemwasi MUNGU, umemwasi BWANA YESU, umemwasi ROHO MTAKATIFU na wote
watatu na YESU hayuko kwako. Sasa imefichwa katika ulimwengu wa roho, matokeo
yake wewe umemwabudu tammuz mungu mmea pasipo kujua na wengine wanajua. Ni
ajabu sana. Tazama kwenye makanisa miezi ya 12 yamejaa kwenye mahoteli sehemu
mbalimbali wanasema Christmas tree. Wewe birthday ya YESU haipambwi kwa mti, inapambwa kwa utakatifu na
kumshukuru na kumsifu ndani ya moyo wako wewe, sio katika mti. Sasa shetani
akaiba uthamani wa Christmas akaweka mti. Aliiba katika mambo mawili ambayo
nitakwenda kuelezea. Jambo lingine ni father Christmas, lakini nina-base
(ninasisitiza) katika jambo la Christmas tree. Unapokuwa umenunua ule mti tu,
ina maana wewe una aina ya mungu anaitwa tammuz; tayari wewe umeshamwasi MUNGU.
Lakini hii sio kwamba watumishi wa sasa hivi walipenda; walitekwa na wale
watumishi wa zamani ambao waliacha njia ya YESU, wakawaua kina Paulo, BWANA
YESU ASIFIWE, na wanafunzi wa YESU; wakaingiza mambo yao na niliwakuta huko
kuzimu toka wale watumishi wa enzi ya Ufilipi walioharibu Injili. Wakati huo
kuna makanisa machache ambayo yalikuwa yanasema ukweli, sasa hivi yamejaa mengi
ambayo ni uwongo. Ni pesa, uwongo na kutafuta pesa za wana wa MUNGU.
BWANA YESU asifiwe, nikuulize
mwana wa MUNGU, muulize mchungaji wako ni kwa nini wanaweka huo mti? Hana jibu.
Muulize maswali, na kama hajui, basi. Which GOD anamwabudu? Hajui. Kama wewe
vile ulivyo unaabudu mungu usiyemjua badala ya kumwabudu MUNGU unayemjua,
aliyekuumba, aliyeumba mwezi, nyota na jua pamoja na kila kitu.
BWANA YESU asifiwe. Hii miti
haipaswi kushiriki utukufu wa MUNGU au wa YESU, wala kiumbe chochote.
Hafananishwi, anaitwa mwana wa pekee. Kama ni mwana wa pekee, leo hii iweje mti
uwekwe hapa uchanganywe na mwana wa pekee? Lazima uelewe. BWANA YESU asifiwe.
Ni wakati wa kumjua YESU na wakati wa kumjua MUNGU wa kweli, na ni wakati wa
kweli tupu mpaka atakapokuja. Unayesikia utapona, unayekaza shingo shauri yako;
lakini sitadaiwa damu yako katika mikono yangu, na MUNGU damu yako haitamlilia
katika mikono yake. Wakati ni huu sasa kuna wengine hawatendi dhambi lakini
hawajui ni mahali gani wameanguka.
BWANA YESU asifiwe. Unapokuwa na
Christmas tree, miungu, majini, mapepo yapo nyumbani kwako; iwe umeokoka,
haujaokoka ukweli ndio huu. Uamue leo. BWANA YESU asifiwe. Katika kabila ya
Uchagga niliyotoka, miti imejaa ya Christmas; yaani tammuz ndio limekamata.
Ninawaambia watupe katika jina la YESU. Nimekufundisha, chagua leo unataka
miungu au unamtaka BWANA YESU? Na YESU anakukodolea macho yake kutoka mbinguni,
anakuona wewe mwanadamu unasikia, na siku yake ile ya Christmas unakwenda
kuwapa miungu badala ya yeye. Inatakiwa umrudie yeye mwenyewe; mambo
yameharibika watoto wa MUNGU; kanisa limetekwa na shetani limepoteza direction
(mwelekeo) halisemi kweli. Mambo ni mengi sana ninayowafundisha, lakini bado
sijaanza kufundisha, hii ni mwanzo. BWANA YESU asifiwe, Haleluya,… acheni mambo
ya miungu, nimekueleza habari ya Christmas tree, sasa umeelewa.
BWANA YESU asifiwe. Jambo lingine
tena naeleza ni kuhusu kitu kinaitwa father Christmas. Kama nilivyokwisha
kuwaeleza kwamba Christmas tree ni makosa, na tukisema father Christmas; hivi
nikuulize; father Christmas ni nani? YESU au ni mdoli, YESU au ni hiyo sanamu?
Wanadamu ni namna gani mmetekwa fahamu badala ya kumtukuza YESU baba yetu
tukatengenezewa midoli halafu tukaiita father Christmas. Sasa ninakupa siri
kidogo ya asili ya father Christmas. father Christmas ni mzimu wa mtu anaitwa
Saint Nicholas. Alikuwa ni mtu maarufu sana zamani katika nchi za Ugiriki na
Uturuki, alikufaga. BWANA YESU asifiwe. Baada ya kufa kwa sababu alikuwa na
matendo mazuri, BWANA YESU asifiwe. Ndio wakampa jina wamuite father Christmas.
Sasa leo hii amekufa, hivyo kila unapokuwa na huyu mdoli unaoitwa father
Christmas, unapeleka watoto, hata yule mtu amevaa lile linguo anacheza cheza
ajue kama huyo mtu tayari ameshavaliwa na huyo mzimu linaitwa Saint Nicholas. BWANA
YESU asifiwe, sasa ni kuelewa kwamba mambo yameharibika. YESU siku yake ya
kuzaliwa imechafuliwa, badala ya kutukuzwa yeye amepewa mdoli ambaye anaitwa
Nicholas ambaye sasa hivi ni mzimu. Sasa watu wanaacha kumtukuza YESU na
kumsherehekea yeye katika roho na kweli. Shetani akatengeneza kitu akasema,
ngoja wanadamu nimewashika fahamu zao niwaambie huyo ndio father Christmas.
Nikuulize swali, huyo mdoli ndiyo BABA YESU? Jibu siyo. Na nikuulize swali, je
inastahili huo mdoli uitwe father Christmas? Tazama ni pepo lina mandevu, lina
manywele, hata watoto wakiona wanaanza kucheka na mavidole makubwa kama jini.
Ni namna gani Wakristo, ni wakati wa kumrudia MUNGU. Mambo yameharibika,
yalianzia ulaya, Injili imebadilika, na makanisa yamepigwa upofu, hayajui ukweli.
Kanisani yenyewe kwenda, utakuta ni lipepo limekaa. Hivi mnajua midoli ndio
mapepo yanakaa? Na leo ndio anaitwa father Christmas badala ya YESU kurudishiwa
utukukufu peke yake na MUNGU kushukuriwa kwa sababu ametuletea YESU. BWANA YESU
ASIFIWE. Ninawatangazia katika ulimwengu mzima, hakuna mtu anatakiwa kuitwa
father Christmas, hakuna kitu kinatakiwa kuitwa Christmas tree; ni YESU peke
yake birthday yake na kutukuzwa MUNGU kwa kazi aliyoifanya kutuletea
Mfalame wa wafalme, Bwana wa wafalme. Kupitia jina lake leo sisi sote
tumekombelewa na tunaenda mbinguni. Iweje leo shetani anakamata fahamu za
wanadamu akachomeka Christmas tree iitwe Christmas, akaleta mdoli uitwe
Christmas. Ni sawasawa na hawa amabao wanajiita YESU, ni wakati wa kukataa. Ni
sawasawa na hawa ambao wanajiita mungu wa majeshi, ni wakati wa kukataa. BWANA
YESU asifiwe. Ninawaambia mambo yameharibika; kama leo hii mtu wanasema wao ni
Adam wa pili, kesho kutwa utasikia mtu anasema yeye ni Adam wa kwanza wakati
Adam wa pili ni YESU peke yake. Watu wanachukua nafasi za BWANA YESU. Ni wakati
wa kusimama imara kama unampenda MUNGU.
BWANA YESU asifiwe. Amenituma
habari njema kwa mataifa yote kuwaeleza ukweli, kufungua fahamu zenu na akili
zenu kwa sababu kila unapokuwa na yule ndoli, shetani hata siku unakufa
anakunyanyulia bango wewe uliabudu sanamu siku ile ukamuita father Christmas.
Nikufundishe wewe Mkristo na wewe mpagani; Je YESU ndilo hilo limdoli? Je siku
ya kuzaliwa ndio inaitwa mti wa YESU? Hakuna mti wa YESU hapa duniani. BWANA
YESU asifiwe. YESU peke yake hafananishwi na chochote ndio anaitwa mwana wa
pekee hata miti na viumbe vya MUNGU.
BWANA YESU asifiwe, lakini
shetani akaamua kuwateka wanadamu wamkosee MUNGU, hata mti waite ni mungu wao.
Lakini uliza, miungu haina kuitu, hata mmea kuupa pumzi, kuinyeshea. Miungu
hata mvua haidondoshi. BWANA YESU asifiwe; haijatoa ila ni MUNGU lakini kanisa
limeenda kinyume na kupoteza ramani; wamejiita, ni wazinzi, wananyang’anya watu
pesa, mali na kudanganya danganya watu kwa injili za upotofu. Ni theolojia gani
hizi? Soma katika kitabu cha Biblia takatifu ambayo ndio katiba; hakuna mtu
anayeruhusiwa kuwa father Christmas. Mwana wa MUNGU hafananishwi na chochote.
Sasa iweje leo mwana wa MUNGU afananishwe na huyo mdoli? Iweje leo mwana wa
MUNGU anafananishwa na mti? Siku yake ni siku tofauti. Unapoweka tammuz,
unapoweka hilo li father Christmas; linaitwa father Christmas la kuzimu, maana
kuzimu na wenyewe wanalo; unapoliweka siku hiyo, YESU ndiyo hahusiki na nyumba
yako, wala baraka zake hazishuki kwako. BWANA YESU asifiwe. Zaidi ile mizimu
kule kuzimu inachekelea inasema “majinga haya”. Mimi YESU alinipeleka nikaona
yote na ninawafundisha, ninawaeleza, anayesikia asikilize. Mimi nina uadui na
shetani, na shetani kila siku tunagombana, na tutagombana milele, na
ninaendelea kumtandika na uendelee. Najua mpaka sasa wengi mmefunguka na fahamu
zenu zinazidi kuelewa. Uelewe macho yako yafunguliwe, na fahamu zako
zifunguliwe uwe na akili timamu. Yamkini umesoma, na una digrii (shahada) tatu,
nne, lakini kwa nini huelewi father Christmas huyu sio YESU? Hii Christmas tree
sio YESU ni dhambi. Haleluya,…
Zaidi karibu katika kanisa la
YESU NI BWANA NA MWOKOZI, shida yoyote inayojusumbua, matatizo yote, njoo
utafunguliwa bure bila hata senti kumi. Amenituma YESU niwaeleze ukweli dunia
nzima. Tazama siku ya Christmas miezi ya 12 ni wakati wa kumwasi MUNGU. Kuweka
mamidoli haya ni kumwasi, kuweka ma-christma tree ni kumwasi. Yamkini na wewe
mwana wa MUNGU hupendi kumwasi MUNGU lakini unafanyishwa kumwasi kwa namna hii.
Jichunguze unaye huko ndani ujue umemwasi MUNGU; wewe ni kuyatoa nje, kuyatupa
na kuyakataa. Na madukani wafanyabiashara mnapoyauza, mjue. Kama mlikuwa
hamuelewi sasa muelewe. Msifanye kazi ya kumuudhi MUNGU mnapoleta hivyo vitu.
Mnampenda MUNGU, lakini inapitishwa kwenye mikono yako; mmepigwa upofu. Watu
wamepigwa upofu wanaleta vitu vya shetani kwenye mikono yenu. Mnasubiri baraka,
huwezi kupata baraka za MUNGU. BWANA YESU asifiwe; Haleluya… Ni wakati wa
kufunguka na kujua ukweli. Atukuzwe MUNGU wa Ibrahimu, MUNGU wa Isaka.
Sema BWANA YESU, naomba unisamehe
dhambi zangu zote nilizozifanya kwa kujua au kutokujua, ninamkataa shetani na
kazi zake zote. YESU unishike, na jina langu liandike, nibadilishe maisha
yangu, ROHO wako MTAKATIFU aniongoze nisitekwe na shetani. Unapokuja usiniache,
uniongoze mahali ulipo wewe, nikutane na wewe, nisinajisike, nakushukuru.
Sitaweka Christmas tree, sitaweka hilo li father Christmas - lipepo katika jina
la YESU KRISTO wa Nazareti. Nakushukuru kwa kuniponya. Tutaonana muda mwingine
tena wakati kama huu, MUNGU akubariki. Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI
BWANA NA MWOKOZI, fuatilia masomo katika blog (prophethebron.blogspot.com),
utakuta masomo haya zaidi kwa undani na vitabu na DVD. Soma, usikilize. Amani ya
MUNGU ikae na wewe. Ubarikiwe. Bye.
NABII HEBRON.