Pages

Friday, December 12, 2014


MAHUBIRI YA NABII HEBRON KUPITIA YOUTUBE: VIONGOZI VIPOFU.


MUNGU anakupenda, 

 Usiogope!

 Nitaanza kuomba: BABA katika jina la YESU nawaombea watoto wako wote, ninafungua fahamu zao, nakomboa mioyo yao,  macho yao ya rohoni ninayafungua, kwa jina la YESU KRISTO wa Nazareti naondoa mapando yote kwa nguvu na malaka uliyonipa, naachilia upanga  na moto nabomoa  kila namna ya uchawi na upinzani, kwenye anga, kwenye ardhi  na kila nyumba ambapo wananiangalia sasa hivi naachilia moto ukaondoe kila aina ya uchawi na kila  mateso kwa jina la YESU  KRISTO wa Nazareti, BABA asante kwa ajili ya neno lako na ujumbe ulilonituma siku ya leo niwapelekee watoto wako, maana umeniambia unarudi na sasa nitengeneze kanisa lako, BABA nakurudishia sifa, heshima na Utukufu, Amen.

Watoto wa MUNGU na wanadamu wote mlioumbwa na MUNGU ninakwenda kufundisha somo kuhusu viongozi vipofu na mengineyo mengi yatakayo fululiza hii yote ni  kukufungua wewe maana viongozi vipofu ndio wanaofanya watu wasiende mbinguni japo wewe mwenyewe unapenda kwenda mbinguni lakini anayekupeleka mbinguni humjui ni wa kweli au wa uongo.

 BWANA YESU ASIFIWE,

 Nimewaona wengi kuzimu, wanateseka, wanalia, wanajuta walikuwa wakiishi makanisani wakijiona wao ni wakristo safi, kumbe si safi na kumbe walikuwa wamewekewa mapando ya shetani, na YESU anaangalia Neno lake alitimize basi, sio robo robo au nusu.

BWANA YESU ASIFIWE

Utafungua kitabu chako cha Neno la MUNGU, Biblia takatifu, Mathayo: (15:8-9 ) mstari wa nane na wa tisa “Watu hawa huniheshimu kwa midomo; ila mioyo yao iko mbali nami, Nao waniabudu bure, wakifundisha mafundisho yaliyo maagizo ya  wanadamu,” nitaruka mstari wa Kumi na tatu mpaka wa kumi na nne (Mathayo15: 13-14)….:”Akajibu, akasema, kila pando asilolipanda BABA yangu wa Mbinguni  litang’olewa, Waacheni: hao ni viongozi vipofu wa vipofu. Na kipofu akimuongoza kipofu mwenzake, watatumbukia shimoni wote wawili.”

Hii ni habari ya makanisa kwa sababu yamebadilika, utafungua kitabu chako tena katika kitabu cha Yohana 15:7 Neno la MUNGU linasema hivi ….”ninyi mkikaa ndani yangu, na maneno yangu yakikaa ndani yenu, ombeni mtakalo lote nanyi mtatendewa”

BWANA YESU asifiwe, watoto wa MUNGU kila mtu anampenda MUNGU, lakini wapo ambao wanampenda shetani na shetani amepiga upofu kanisa, kupitia watumishi wake wanasema uongo wanafundisha uongo, mafundisho ya wanadamu, YESU anasema wanasema hivi wananipenda kwa midomo, wanafundisha mafundisho ya wanadamu, wewe ni mwanadamu, Mwanadamu umeumbwa na MUNGU, wewe umekuja duniani ukiwa tupu haya mafundisho umeyatoa wapi? MUNGU anataka watu wafundishwe mafundisho yake peke yake, Wala sio mafundisho ya mtu wa aina yoyote.

BWANA YESU ASIFIWE,

Mnaelewa watoto wa MUNGU, sasa viongozi vipofu ni watumishi ambao wanafundisha kinyume na Biblia, nitakueleza kivipi? Kwa kifupi tu, YESU amenituma niyang’oe mapando ya shetani, ili Neno lake liingie ndani yako ili wewe upate kupona unapokaza shingo na kukataa hilo pando litakupeleka na wewe kule kule shimoni.

Kuna vipofu wa aina mbili wako vipofu kiroho na kimwili – Nitaelezea upofu wa kimwili, wa kimwili utaona mtu anapapasapapasa hivi na sasa wa kiroho ni mtumishi ambaye anafundisha vitu ambavyo havijui wala havioni wala havijatoka kwa YESU.

Wanafundisha mafundisho ya kumtaja BWANA YESU, BWANA YESU, BWANA YESU! BWANA YESU asifiwe lakini ndani yao mmmhhhhhhh!. Nami nimekutana naye, nimekaa naye nimeongea naye amenituma niwaeleze mrejee katika neno lake yeye anakuja, atachukua wale ambao hawana mapando ya shetani, mwenye mapando yake, Hayo mapando watu wasifikiri yanapandwa kama mgomba au mahindi hapana, yanapandwa katika moyo wako kwa namna ya  maneno ya shetani.

Maneno ya shetani hautaambiwa ni maneno ya shetani, yanachanganywa  makanisani mfano mwepesi kabisa ubatizo wa kikombe, ubatizo wa kikombe ni maneno ya shetani, YESU alisema fuateni njia zangu ambaye yeye ndiye kweli alionyesha mfano sasa huu ubatizo wa kikombe umetoka wapi? Kubatiza mtoto mdogo na kumbariki mtu mzima ! Hii kupindishwapindishwa yote ni maneno ya shetani na kila ambaye yuko hivyo haendi mbinguni labda abadilishwe,aokoke, abatizwe  na aishi maisha matakatifu na atoke huko, na atoke huko ndio atakwenda, ninawaambia niliyoyaona na sitaacha kuwaeleza na kila nikikaa  nakasikia mzigo, kwanini husemi ujumbe wangu, kwanini husemi ujumbe wangu,
Mimi ninavyokuwaambia hapa maneno haya sio mpaka maombi, haya umeshafunguka, nawaeleza watu wote mkabatizwe,ubatizo wa maji mengi muishi maisha matakatifu na neno lake MUNGU  siku zote,  milele siorobo, robo au nusu nusu.

BWANA YESU ASIFIWE!

Jambo lingine imeandikwa utoapo sadaka yako mtu yeyote asijue sasa unaandika jina, unapewa risiti na hayo yote yakishajulikana ni mapando ya shetani, na MUNGU hachukui na sadaka zote hizo mmetupa.

BWANA YESU ASIFIWE!
Nitakuja kuelezea mfano mwingine, nataka muelewe habari ya viongozi vipofu, kama vile dereva alivyo, asiyejua anaenda wapi,anaenda kuwatumbukiza watu shimoni huko na ndivyo ilivyo watumishi sasa hivi vipofu wanawapeleka watu shimoni huko. Nimewaona.

BWANA YESU ASIFIWE!

Nimewaona ni roho,  zamani ilikuwa  kimwili sasa hivi ni katika roho. Kulitokea mfano mmoja hapa Tanzania habari ya vikombe wakasema mtumishi ameoteshwa na MUNGU, ameambiwa kwamba atachukua shilingi mia tano tu, wengine mia mbili, na hizi zilifanyika na watumshi katika nchi nzima, sasa ninawaeleza kuwa ule ulikuwa ni mtandao wa shetani, lakini kwa sababu viongozi walikuwa ni vipofu, walitangulia na kusapoti, ukirudi kwenye Neno la MUNGU, limesema hivi nimekupa bure toa bure iweje, huyo ni MUNGU aliandika Neno lake ambalo tunasoma katika Biblia, sasa iweje huyu MUNGU abadilike aseme, toa shilingi mia tano tu? Je MUNGU anaangalia shekeli yako? Je MUNGU ni hospitali?

BWANA YESU ASIFIWE!

Sasa uzidi kuelewa hao ni vipofu, na wote waliokwenda kule, walikwenda kupingwa namba 666 na mpaka sasa hivi wanazo, waulize ni wapi  MUNGU amesema kwamba tukipewa cha kwake tutoe hela! Ndio upewe? imekuwa hospitali? Lakini watumishi ndio wamekuwa wa kwanza kwenda huko, sasa nyie si watumishi wa MUNGU nyie ni vipofu na hizo roho mlizokwenda kuzipoteza MUNGU atawadai zote mikononi mwenu maana ni mafundisho ya wanadamu hayo.

Mafundisho ya wanadamu kivipi? Mafundisho ya MUNGU unatoa bure, Ya mwanadamu leta pesa, mafundisho ya wanadamu asili yake yanatoka kwa shetani.

Watu wote wanaokwenda kwa waganga si mnaambiwa mlete pesa au kwa kitu fulani? eti MUNGU kasema! haaa hayo ni mafundisho ya wanadamu, ambapo mungu Shetani, mungu aina ya shetani, shetani ndio hutapeli na huchukua vitu vyenu.

BWANA YESU ASIFIWE,

Sasa kanisa likajenga barabara na vyoo, wakisema MUNGU ametenda katika nchi ya Tanzania! ninawaambia hivi yule ni “mchawi”  watu wote waliokwenda walipigwa namba ya 666, hataiona katika macho, inakuja katika roho, kingekuwa cha MUNGU mpaka leo kingestawi kiko wapi? nikuulize !  Wangapi mmekunywa na mpomnashida palepale na mnakufa?

BWANA YESU ASIFIWE!

Haiwezekani watu wanakwenda kumfuata YESU, ambapo eti kwenye kikombe ndio YESU huyo, alafu wanafia njiani, wanakunywa na wanakufa, hapana mfunguke huo ni upofu.

BWANA YESU ASIFIWE!

Biblia inasema msiabudu sanamu, kanisani watu wanaabudu sanamu, ni maneno ya wanadamu ni upofu, MUNGU sio mbao! Wala MUNGU sio sanamu! wala YESU sio sanamu, amekwisha kusema katika kitabu chake, lakini watu wanachukua  maneno ya shetani ndio wanayoyatumia, kuabudu sanamu ni maneno ya shetani, ninawaambia ukweli ukubali au ukatae, mimi nakuambia YESU anarudi.

 BWANA YESU ASIFIWE!

Mmezoea kuambiwa YESU anarudi! YESU anarudi! Hamuoni , sasa ahaaa! sasa ninayowaambia yanatimia yote nikiwa hai hivi hivi na maisha yangu, na hata atakapokuja nitamwona.

BWANA YESU ASIFIWE!

Na atashukia nchi ya Tanzania, ninawaeleza mjirekebishe msije mkawa, kama YESU kule Galilaya alipozaliwa watu wakamdharau, lakini huko sehemu nyingine wakamkimbilia, na ndivyo ilivyo isije ikawa kwa Tanzania. Mataifa mengine wasije wakakimbilia wakapona nyie msije mkazubaa. Ninawapenda Watanzania, ninawapenda Wakenya nina wapenda watu wote wa Dunia nzima, wa Afrika Mashariki ni wakati wa kuokoka, bila kuokoka, kuishi maisha matakatifu na kubatizwa ubatizo wa maji mengi, ni bure.

 BWANA YESU ASIFIWE!

Siku ya Pasaka amekuja akaniambia, “BWANA YESU”, “Hebron”! Nimekutuma kwa mataifa yote, waeleze wabatizwe ubatizo niliobatizwa mimi, waishi maisha matakatifu,yanayonipendeza mimi,.

BWANA YESU ASIFIWE!

 Kinyume na hapo! Mhhhhh! Kwa hiyo kama wewe mpaka sasa hivi haujaokoka, ujue wewe una pando la shetani, ni mkristo lakini eti upo kanisani, hujaokoka, wewe ni pando la shetani YESU hakuja kupanda mapando ya shetani, mapando ya shetani yameletwa na dini na ndiyo yapo kanisani.Makanisa yamekuwa kama makampuni,

BWANA YESU asifiwe,

Sasa hivi , ni habari ya pesa tu, habari ya Michango, kunyang’anya watu pesa zao na mali zao, nami  nawaeleza maana mnafikiri kwamba mtabarikiwa, mnaibiwa hao ni “wezi,”

 BWANA YESU asifiwe,

Ninakuambia hivi hao ni wezi,  kama MUNGU amemwita mtumishi, hatumi kwenda kunyang’anya watu pesa, nyumba yake sasa hivi imekuwa ni pango la kunyang’anyia wana wa MUNGU pesa, nyumba yake sasa hivi sio nyumba ya sala tena, imekuwa ni nyumba ya biashara, walaki, elfu kumi, harambee, matangazo ya kwaya, m’baki, hiiiii! wewe  ukishasikia kanisani matumizi, taarifa, ina maana mnaosomewa nyiie ni kampuni, kama mna hisa hapo.

BWANA YESU asifiwe,

Ni wakati wakubadilika BWANA YESU asifiwe na kishtuka, na kumrejea MUNGU ninawasihi, bila toba, hakuna kwenda mbinguni, toba takatifu.
Wengine wameongozwa sala za toba ni bure, wengine wamesema nimekata shauri, ameomkoka lakini yupo huko huko, kwenye ubatizo wa kikombe na sanamu eti amekata shauri, hakuna kukata shauri ni kuokoka. Hilo neno kukata shauri ni mchomeko wa shetani.

BWANA YESU asifiwe,

Ili wewe uwe mfuasi wa YESU uongozwe na mtumishi ambaye si kipofu, anayemjua MUNGU, ameitwa nayeye, na anaeleza kweli, Ukileta Biblia na sasa hivi uwaulize watumishi wote wanachofundisha hawana majibu. Sasa wewe umeumbwa kuja kuwekewa mambo ambayo siyo katiba ya MUNGU? Katika nchi katiba mtu ukivunja unashtakiwa na katiba katika ulimwengu wa roho ni biblia amesema usiongeze maneno yeyote katika kitabu changu wala kupunguza kuongeza ubatizo wa kikombe? Tayari umeondolewa mahali pema pa uzima ule, nami nawaambia rejea maana wale watangulizi waliwadanganya na walikuwa mapando ya shetani, waasisi wa hizi dini nao wako chini kuzimu wanateseka.

BWANA YESU asifiwe,

Kibinadamu ukimuuliza hawa waasisi wameanzisha haya madhehebu, yamekuwa makubwa dunia nzima, hivi hili neno la “ubatizo wa kikombe” ndio YESU amewatuma? Mbona yeye hakubatizwa kama sisi? kwanini sisi tumebatizwa hivi? Ina maana wamewapiga upofu, mpotezwe na nyie.
Utasema mimi siendi kuzimu, wapi wewe! Kama haujabatizwa, nakuambia maji mengi mpaka sasa hivi jina lako liko kuzimu, ukubali! ukatae, habari ndio hiyo unapobisha, ile siku utajuta nakuambia, utanikumbuka.Na wapo wengine wana batiza watu feki feki tu, wamejiita na wanatumia uchawi, wamejaa Tanzania, wamejaa Kenya, wamejaa Uganda wamejaa Rwanda, naongea habari ya Afrika Mashariki Ole wao, Wataumwa magonjwa yasiyotibika, wako watakaopata magonjwa ya aibu  kwa ajili ya kuwatesa wana wa MUNGU, umaridadi wa shetani siku zote aliokutumia mwisho.

BWANA YESU ASIFIWE

Lakini amenituma nikueleze habari njema, ubatizo ule wa kikombe umeletwa na hao waasisi wa dini ili kuwapiga watu alama za shetani, ndio maana  ukizaliwa tu unawahiwa mapema ili YESU asikupate utakapofika katika umri wako YESU alisema utakapokuwa na ufahamu wako mwenyewe, kama yeye ndio ubatizwe kama yeye sasa shetani anakuwahi ukizaliwa tu Kap! Anakupiga chapa yake unaishi maisha mabaya mpaka watu wanalalamika, wanalaani kwanini wamezaa watoto, shida ipo wapi, tayari wewe sio wa YESU, huna Baraka zile toka ukiwa mtoto mdogo kwa hiyo utashangaa watoto ni walevi, majambazi, ni majangili, haya yote ni kwa sababu ya ubatizo wa kikombe umepingwa pando la shetani, usijali kwa jina la Baba na  Mwana na la Roho Mtakatifu, alafu na kikombe. MUNGU anaangalia Neno lake, haliendani na Neno lake hayo unayoyafanya, hivi nikuulize kuna mtu waanayetakiwa kuheshimiwa kama MUNGU?hakuna ! sasa kwanini Neno lake aliloandika mnaweka dosari dosari , tiki, vema mstari hapa mnabadilisha badilisha ina maana MUNGU hana akili, enyi wanadamu nani aliyewaloga? Wazungu hamna kitu wameleta utapeli katika makanisa. Makanisa huku yakasimamisha mizizi kuendesha utapeli hata wao sasa hivi ulaya hawaendi makanisani kabisa wameshtuka, wengine wameona ni utapeli tu lakini wameshtuka lakini watakuja kupona Tanzania ninawasihi rejeeni kwa YESU okokeni,

BWANA  YESU ASIFIWE!

Ni wakati wa mapando ya shetani kuyakataa hautaambiwa ni pando la shetani , ahaaaa Maneno unayofundishwa wewe mda wote unatembea hapa na msalaba. Msalaba ndio YESU? YESU anatakiwa akae moyoni,

BWANA YESU ASIFIWE,
Lakini haya yote ni mafundisho ya uongo yakachanganywa na uchawi, na miujiza ya kipepo kama hii ya kufufua misukule YESU alipokuwa akifufua misukule alionyesha maiti hii hapa na akafufua,wewe unaambiwa yule njoo njoo njoo njoo  haya ni mazingaumbwe hao ni mashetani.

BWANA YESU ASIFIWE
Yako ndani yao ili kuvuna roho, unaweza ukaambiwa ni kanisa la uponyaji, la miujiza la ufufuo, au la kinabii au la kitume, hii imewadanganya watu. Chunguza matendo yao ndio utawajua,  kivipi wanayoyafundisha? Lakini ole wao hao ndio maadui wa YESU.

BWANA YESU ASIFIWE!
Wengine wamekuwa ni wachawi wananyang’anya mali za watoto wa MUNGU, MUNGU amewaumba ninyi wanadamu amewapa vitu vyenu mmefilisika mnabaki kumlaumu MUNGU mbona MUNGU ninakutolea sana mbona naishiwa? Ninakuambia hivi amechukua shetani wala usimlaumu MUNGU nenda mwambie akupe mali yako aaache kukuchezea kabisa

 BWANA YESU ASIFIWE

Haya makanisa yote yenye Mabenki ni ya shetani nawaeleza YESU alipokuwa hapa ulimwenguni alisema hivi usichukue fedha wala riba sasa kanisa linakuwa lina riba ayaaa hilo ni pando la shetani.
Ninawaeleza  matawajuaje? Chunguza matendo yao , Ni wakati wa kufunguka na kuelewa BWANA YESU ASIFIWE
Msitishwe na habari za miujiza ila sasa hivi ile miujiza  hawana nguvu, YESU anawashughulikia wanakijua kwenye ulimwengu waroho .

BWANA YESU ASIFIWE!

Sio kama anashindwa kuwaangamiza anawaangalia tu,anawachekecha anawachekea, msifikiri YESU ni mpole, YESU ni mkali, hatari mngekuwa mmetumwa nay eye au mnajua  na yeye au mnamjua yeye msinge fanya upuuzi huo kama ni ubabe ni YESU, aliingia hekaluni walikuwepo mamia lakini aliwafukuza wote sasa wewe unafikiri YESU ni mpole ole wenu mnaoendelea na mambo hayo wacheni nawaeleza utafika wakati msioujua mtakumbuka maneno haya msifikiri ni sauti ya Hebron  ni sauti ya MUNGU inasema, rejea kwa YESU achana na mambo ya dini pokea wokovu, utakatifu, ubatizo wa maji mengi basi hicho ndio YESU alichokileta YESU hajaleta madhehebu hajaleta dini yaani yalikuwepo tu yeye ndiye mzabibu wa kweli akazaa tawi lake sasa YESU tawi lake ni wokovu, utakatifu na maji mengi basi. Lakini leo ni madhehebu yako hata milioni mia moja dunia nzima YESU, hakuleta madhehebu. Madhehebu ni Elimu ya wanadamu na  Yalikuwepo na kwa sababu yalikuwepo sio aliyaanzisha, MUNGU  na ndio maana alimtuma YESU. YESU mwenyewe alipokuja wanampinga, wanamkataa na alikuwa anawaambia enyi vipofu , enyi vipofu, enyi vipofu rejeeni,  rejeeni acheni na mimi leo hii nawaambia enyi vipofu, enyi vipofu acheni rejeeni kwa YESU, acheni kupokea mafundisho ya kipepo

BWANA YESU ASIFIWE

Mmefunga sana ni kazi bure navyowaambia jicho la MUNGU linawaangalia mtamjibuje  BWANA YESU, YESU, anarudi na anarudi na anashukia Tanzania anayedharau , dharau lakini utakumbuka maneno haya. Mimi sidaiwi roho yako BWANA YESU amesikia nimekueleza fanya uamuzi mwenyewe acha uchawi, acha ushirikina, acha ulevi. Wachawi wote hapa duniani tayari wao ni wa kuzimu tu, hata kama una hirizi wewe ujue huendi mbinguni jina lako liko kuzimu, una mipando ya shetani wewe tayari huendi mbinguni

BWANA YESU ASIFIWE

Cha kufanya haraka ni wewe uokoke leo hii hapa uachane na hayo na BWANA atakurehemu, lakini wako ambao wametengeneza  mambo ya uchawi hao wameshagombana na MUNGU hayo mimi hayanihusu wata pambana na yeye, maana hata mimi siwezi kufanya lolote ni yeye yuko ndani yangu, ni kama chombo tu nikueleze BWANA YESU ASIFIWE.
Toka mwaka 2010 aliponituma kwenye kazi yake nikaianza mwaka 2011 nilikutana na vita vingi sana lakini aliniambia hakuna hata limoja ambalo litafanikiwa juu yako nami nimeyaona na bado nayaona zaidi maadui wanaangamia nakuteketea mimi nasonga mbele watu wanazidi kumjua YESU,ndio kitu mimi ninachotaka na kulala usingizi wangu,

BWANA YESU ASIFIWE

Msiogope watoto wa MUNGU mlizoea kuambiwa uchawi mnalongwalogwa, usiogope wewe nitakapakuombea, ole wake anayekuloga namfyeka, haijalishi uko wapi , sijui wapi ninapoomba utafuatwa,

BWANA YESU ASIFIWE

Na ninaona kila kitu rejeeni kwa YESU msitoe tena pesa makanisani za michango, hayo ni mapango ya biashara mahali alipo YESU yeye ambaye anakaa ndani ya Mchungaji au mtumishi YESU hasemi leta hela, leta leta hela, ahaaaaaa! Yeye ni Neno lake, ukitaka utatoa mwenyewe, mchango ! mchango ! Mchango! Mpaka Tanzania imeingia kwenye laana. Michangio !  michango ! michango makanisani !  Mmebaki kulaumu nchi na kulaumu viongozi sasa kama viongozi wa kanisa wenyewe vipofu watawaombeaje viongozi wa nchi? Unakuta ni hao hao viongozi vipofu , utakuta huyu yuko kwenye chama hiki, huyu yuko chama hiki, ni mwanachama kabisa na anakadi sahihi kabisa, mtumishi aliyeitwa ma MUNGU hutakiwi kuwa na chama chochote kile.Unatakiwa uwaombee vyama vyote.

BWANA YESU ASIFIWE!

Lakini unakuta mtumishi anakadi ya chama Fulani huyo ni pepo, tayari anaubaguzi ndani yake sio MUNGU huyo ni kipofu, muwafukuze muwatoe huko wanawaletea laana, mtumishi wa MUNGU haruhusiwi kugombea kabisa uchaguzi wa aina yeyote, haruhusiwi ndio maana wengine makanisani mnapiga debe mpigieni mtu Fulani, tayari wewe una chuki sasa heeeee nyie si vipofu utabisha.
Vichwa vyenu watoto wa MUNGU visiongozwe na wanadamu tena mwangalieni MUNGU, peke yake, mzidi kufuatilia vipindi vyangu kila wakati, kwenye television, kwenye radio kwenye you tube, website yangu,kila wakati na vipindi vyote katika redio na vitabu vyote nilivyoandika, endelea kusoma utapona roho yako.

Ninamwamini YESU mimi ni muuminina mshirika wa YESU  peke yake sina chama chochote cha kimwili hapa duniani zaidi ya BWANA YESU, peke yake, huwezi kuwa na mabwana wawili leo una biashara alafu unakuja kanisani ni kipofu.
Kazi yangu ni kuombea kila mtu. BWANAYESU ASIFIWE, anayesikia asikie na anayekataa akatae ile siku mtajuta na kulia na kusaga meno itakuwa ni siku ya kutisha.Na isiyoelezeka hata waliokufa nakwambia watasimama wotw kupita mbele kwenye mstari, kila mtu atalipwa sawasawa na matendo aliyoyafanya na wakati ule utakuwa sio ule wakati wa kuongea na YESU na kumshauri mimi sikujui sikujui, atakuambia sikujui, sikujui wewe ni mzinzi, ulivunja amri zangu kumi, sikujui wewe ni mchawi, sikujui wewe ulikataa ubatizo wangu, nenda kule, nenda kule. Neno la MUNGU halirudi bure ndio maana kuna jehanamu na kuna paradise sasa wewe shetani ndio amewekewa jehanamu pamoja na wafuasi watakaomfuata. Mimi nawaomba nawasihi rejeeni maana ninaona huruma kwa jinsi nilivyoona mateso, watu wanavyoteseka huko kwanzia sasa hivi, na wengi walipewa mapando ya kristo wa uongo wako na masanamu, walidanganyw watawaombea mwaka kwa mwaka, ninawaambia wote wako kule for you information dunia nzima, hakuna cha cheo gani au elimu gani kila kitu ni upeezi mbele za MUNGU.

BWANA YESU ASIFIWE

Ni wakati wa kumrejea YESU  nawasihi atapita Malaika Mikaeli na BWANA YESU, maana yeye ndiye Malaika mkuu, sijui niwaelezeje, ninawaomba muweze kuelewa ndani ya mioyo yenu na mioyo yenu ifunguke maana haifai hata , mengine kinywa changu kinafungwa, mdomo nisiseme maana siwezi nikuzungumza,  mdomo unafunga nisiseme hili hapana , bado wakati, bado wakato wake, linawekwa kaa la moto nyamaza lakini ninachowaomba mumrejee BWANA YESU muokoke acheni mambo ya dunia unapoipenda dunia wewe ni wa kuzimu na unapopenda ya mbinguni wewe ni wa Mbinguni hapa ni pa kupita tu, ingekuwa ni mahali pa kuishi miaka yote ungekaa  pote basi. Hapa duniani hakuna kitu kama ni magari mazuri yako mbinguni, kama ni majumba mazuri yako mbinguni, kama ni kila kitu kiko Mbinguni hizi ni takataka watoto wa MUNGU. 

Mali mlizonazo, vyeo mlivyonavyo ni takataka mbele za MUNGU. Vyeo viko huko, hivi ulishawahi kufikiri kama watu wanajiona hapa duniani wana waliumbwa na MUNGU wana maisha mazuri eee wanajisikiaaa sasa hebu rejesha akili yako tu je yeye  aliyewaumba wanadamu akawapa na uwezo wa kutengeneza  maisha yao mkayaona mazuri yeye atakuwa anaishije? Yeye atakuwa anaishije? Hayo yamefichwa ninawasihi na ndio maana hii miili ile siku ya mwisho kwa sababu tumetenda dhambi, utavalishwa miili mingine tazama ELIYA peke yake ndio alipaa pamoja na HENOKO na BWANA YESU, sababu miili yao ilikuwa mitakatifu hawakutenda dhambi hii miili itavurugwa yote upewe miili mingine lakini wewe uwe jina lako tayari lipo kwa BWANA YESU,

BWANA YESU ASIFIWE

Ninachowaeleza kitabu cha BWANA YESU hakina majina kabisa, hakina yaa ni machache sana utakuta katika Tanzania labda 4,000,000wanasema wameokoka nakuambia hivii wako 15,000  au 12, 000 nakuambia hivi hata wewe uliyeokoka jichunguze njia zako, jichunguze maisha yako. Nahitaji na wengine muokoke nitakapo kuongoza sala ya toba nikupe tiketi ya kweli maana mimi si kipofu maana kama uneongozwa sala ya toba na kipofu ni connection yake ni ya kipofu, BWANA YESU ASIFIWE, kama umeongozwa na mtumishi mchawi, mzinzi, anayenyang’anya mpaka waumini wake, alafu anakuja kuuambia haleluya. Haleluya BWANA anasema, mchawi ! 

Msidanganyike, ikishasikia habari ya partner usitoe, mimi nakuambia ohhhhh ! wewe nenda ukale hizo pesa upate afya ukitaka kumtolea MUNGU uamue na uangalie pia, ukishaoma mtumishi anamapando ya  shetani kimbia ninakuambia kuna watu wana miaka ishirini (20) sadaka yao haijawahi kwenda kwa MUNGU  hata moja, lakini kila jumapili yuko kanisani wanatoa unajua unapotoa sadaka unatakiwa uwe kichwa sio mkia kutokana na ahadi za MUNGU, ukisoma katika Malaki inasema utakuwa kichwa wala sio mkia . heeeeh ! hebu jiangalie, msikubali kuwa vitega uchumi vya watumishi ndivyo wakristo wamefanya na YESUameniambia watoto wake wamefanywa kama wafanyakazi wa watumishi, watafute wawaletee, basi wawanyang’anye na wanawawekea mapando yao, mapando yao, ehe !

Mtumishi: Unataka kuniona ehee leta elfu hamsini, leta laki, MUNGU amesema toa mara nne ni uongo, MUNGU anaangali Neno moyo wako tu MUNGU sio wa ubaguzi,

BWANA YESU ASIFIWE

Na wote ambao wanabatiza ubatizo wa kikombe hao ni viongozi vipofu  soma katika biblia haupo wanaabu sanamu ni vipofu sasa vipofu wamewakamata vipofu wamekuwa wengi sana nami ninawafungua huo upofu utoke mrudi kwenye neon la MUNGU “Biblia” ambacho ni kitabu kitakatifu alafu muone, vitabu viko vingi sana, kitabu cha kweli bwana ni biblia tu, katika ukristo, sijui cha nani na nani vyote ni vya uongo, hichi ndicho  kilichohakikishwa hivyo vingine vimetoka wapi? Msicheze na elimu ya MUNGU, msiongozwe maisha yenu kwa theologia.

Mwanzoni nilipoanza huduma nilikuwa na mtumishi mmoja rafiki yangu, lakini nilishangaa sana akaanza kunifundisha mambo ya kipofu unajua katika maombi bwana wakati unapoomba pale ukiona wamama wengi yaani lazima ukizema kuna mama anaumwa tumbo hapa lazima ztatokea ehheee nilishtuka sana, alafu ukisema kuumwa kichwa lazima ukisema utakuta mtu anaumwa kichwa tu ,  ehee ukisema BWANA ameniambia kuna mtu anaumwa kichwa ehe! Wanaona kweli kumbe ni fix, mhhh nilimsikiliza.

Siku nyingine akaniambia Hebon tafuta wamama sitini, kila mwezi wakupe laki moja, kwa mwezi una milioni sita, haujauchinja maisha yako, mimi nilizidi kushangaa tena kumbe ndivyo mnavyodanganywa, watoto wa MUNGU na mmedanganywa dunia nzima,

BWANA YESU ASIFIWE,

Jambo lingine nalopenda kuwaeleza  hi habari ya stika, hizi stika zinatoka nch za Afrika Magharibi, watu wanaweka kwenye magari halafu zina saini, unanunua pesa nyingi, nawaeleza kuwa zile stika ni hirizi, nawaeleza kuwa zina nguvu amayo unapokaa nayo wewe nyumbani kwako au kwenye gari kuna nguvu,  aliyoivuvia pale ya kipepo, kwa hiyo maisha yako na Baraka zako zinanda kwake zote anakucontrol na wengi sana wamekwenda ndio shida imewazidi ujiulize unakwenda kwenye msaada wa MUNGU eti shida ndio inazidi? 

Uelewe hivyo, kuna watu wanastika ambazo zina mikono hivi, unaambiwa kaa nazo sema MUNGU ananilinda, haya hizo ni hirizi, ukazitupe au uzichome au kitambaa unaambiwa chukua elfu kumi au elfu tano YESU hakai kwenye vitambaa choma tupa nimekuambia hizo ni hirizi yeye anakucontrol anakuunganisha na yeye kipepo ili akuchune, hawa sio wachungaji wa MUNGU ni wachungaji wa kipepo na ninayowaambia wengine watakufa mda sio mrefu, haya nimewaambia! 

BWANA YESU ASIFIWE!  Vifo vibaya sana sio mimi nimetamka hayo ni MUNGU, mtakayo yaona haya msishangae wala kuogopa, mjue ni MUNGU, ni MUNGU, wala msilie mimi nimewaeleza maana MUNGU anafanya kazi yake mwenyewe amewatuma wengi – walipopata pesa wakamkimbia wakaamua kuifuata dunia, wengine, wanasema wanakula maisha sasa kwa YESU ndio kuna maisha, hayo maisha wanaokula usifikiri ni chakula ahaa wameenda kwenye kunywa pombe na uzinzi na wanawake, na kukataa kukaa katika utakatifu, na kumfanya MUNGU aonekane maskini omba, omba, MUNGU sio maskini, MUNGU sio omba omba, BWANA YESU ASIFIWE,  na baadae hao wengine wakaamua kwenda kwa huyo muovu awape nguvubaada ya YESU kwaaacha, kwa hiyo wakaendelea, BWANA YESU ASIFIWE, maana wamekataa njia zake na kumchafua BWANA YESU, ninawasihi mumrejee BWANA YESU muokoke

Mbinguni hakuna kwenda kwa jina ni utakatifu peke yake, na wokovu na ubatizo wa maji mengi, ameniambia waeleze dunia nzima. Kama wewe unajua haujabatizwa na maji mengi, huendi mbinguni, huo ndio ukweli kama haujaokoka huendi na umeokoka, vitu vyote vitatu na uishi maisha matakatifu.

Leo mkristo ni mlevi, mzinzi, mvuta bangi na mshirikina muabudu sanamu, wewe unaenda wapi wewe? Umnamjoke MUNGU wacha ujinga!  usidanganywe na upofu nimekufungua macho, Soma biblia usimrudie MUNGU kwa mazoea mazoea, MUNGU sio mchezousimwone MUNGU mdogo wako, utakabana naye, utabenana naye, wakati Malaika Gabriel anakuja kuchukua roho yeye anayejua inaenda wapi.

Matendo yako uliyoishi nayo hapa ndio huko huko okoka, Narudia kila mlevi haendi mbinguni, kila mchawi  haendi, kila mwenye hirizi haendi, wakati ni leo okoka, tubu na mubadilike na usidhirikiane hivyo vitu tena maana hivyo ni vitu vya kuzimu, usizini na watumishi wanaokuzinisha,  ondoka huo ni uchafu, pepo huyo mtumishi anazini inamaana haiwezekani YESU hayuko ndani yake YESU angekuwa ndani yake asingezini.

Mrejeeni BWANA YESU, Mambo yameharibika lakini ninakuletea habari njema nitakuongoza sala ya toba.

Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozifanya Kwa kujua au kutokujua namkataa shetani na kazi zake zote.

Ee BWANA YESU , ninakureja wewe nishike mkono, niondoe kwenye mapando, niondolee na roho yoyote inayonishikilia inayonifanya nisikufuate wewe, roho yako iingie ndani yangu niongoze wewe unishike,

Mimi ni mali yako hata huko huko nilipo mbali unilinde tembea na mimi, usiniache, Amen

BABA ninawaombea wagonjwa, ninawafungua kwa nguvu na mamlaka ya jina la YESU, nawaombea usalama wataifa, nawainua, nawainua wanajeshi, nawainua maaskari, nawawainua  mawaziri namwinua raisi, Kwa jina la YESU kwa damu ya YESU nawakomboa na kuwasafisha nawaombea neema ya MUNGU ikajae ndani yao kwa damu ya YESU.

Nazidi kuiinua  Tanzania juu naondoa  roho yoyote ya upofu katika nchi ya Tanzania na hizi nchi nyingine zote kwa damu ya YESU kristo wa Nazareti
Mioyo ya watu naifungua kweli yako MUNGU ikajae ndani yao kwa jina la YESU, ninaifunika kwa damu ya YESU Kristo wa Nazareti mlioshikiliwa na shetani namnyang’anya, mliokuwa kuzimu nawatoa nafsi zenu, nazirejesha kwa jina la YESU Kristo wa Nazareti muwe sasa ni wa YESU nawakabidhi kwake MUNGU awabariki, MUNGU awainue, msikubali tena kudanganywa na vipofu kuanzia sasa ninakuambia kwa nguzvu na mamlaka ya jina la YESU uwe hai uwe mzima, usonge mbele usikubali tena kwenda kanisani kumwabudu mtumishi kumpigia magoti na kumwomba yeye akujibu majibu huyo ni pepo, maombi unatakiwa ujibiwe huko mbinguni , 

BWANA YESU ASIFIWE,

Usikubali kubatizwa kwa jina la mtumishi, usikubali kutoa  huduma ya M- pesa, kanisani popote pale, ili upewe huduma  hilo sio kanisa ni wizi, pesa zenu makae nazo, mle mfurahie maisha yenu.
Nami naendelea kuwaombea huko huko mlipo, tutaonana siku yeyote MUNGU akipenda kama sio hapa duniani tutakutana Paradiso.AMEN

NABII HEBRON