Pages

Friday, December 12, 2014

MAHUBIRI YA NABII HEBRON KUPITIA TELEVISION NA REDIO: ZITAMBUE IBADA ZINAZOMCHUKIZA MUNGU

·        IBADA ZA SANAMU
·        IBADA ZA WAFU

BABA yangu na MUNGU wangu asante kwa ajili ya muda huu na libariki jina lako na litukuza asante kwa ajili ya Wasikilizaji mahali popote wanakusiliza maana wanakusikiliza wewe wala hawanisikilizi mimi. Eeee MUNGU naomba ukamfungue. Natuma Malaika wako kwa nguvu na Mamlaka na  upanga ulionipa wafunguliwe fahamu zao na akili zao wapate kujua wewe ni BWANA na huu ujumbe wa siku ya leo ukaingie ndani ya fahamu zao na na akili zao na hitaji kuongea na Mwanadamu kamili sihitaji kuongea na mapepo, mapepo yote yatoke ndani maroho ya dini yatoke yote ndani ya kila mmoja katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI.

BABA yangu ninakurudishia sifa na Heshima na Utukufu, Asante kwa Malaika wako walioshuka mahali hapa. Sifa na Utukufu nakurudishia wewe. AMEN

Ndugu msikilizaji mahali popote ulipo Nchi yeyote, Bara lolote, Kijiji Chochote, Mkoa wowote.

Leo hii nina mambo baadhi ya kuyazungumza.

Jambo la kwanza nitazungumzia kuhusu Sanamu, Ibada za Wafu na mengineo ambayo nitaendelea leo kukuelekeza siyo mimi nakueleza ni YESU mwenyewe anayekuhitaji wewe, Wewe kazi yako ni kusikiliza na kubadilika tuu, mambo yameharibika Ulimwengu umetekwa na Shetani, kweli imeondoka, uongo tuu wa shetani, Na YESU anahuzunika sana, lakini sikiliza siku ya leo naulifanyie kazi, hakika hautakuwa kama ulivyokuwa.

Nitaanza kuhusu SANAMU: Ningependa nikueleze kidogo maana ya Sanamu ni nini?
SANAMU ni kitu chochote kisicho na uhai, ni kitu kilichotengenezwa na mwanadamu na hakina uhai wala hakipumui wala kuongea. Naomba usikilize tena!
SANAMU ni kitu chochote kilichotengenezwa na mwanadamu hakipumui wala hakiongei wala hakina uhai.

BWANA YESU ASIFIWE……………..
Tutasoma Neno la MUNGU KUMBUKUMBU LA TORATI 5: 8-9 Neno la MUNGU lina sema  Usijifanyie  Sanamu ya kuchonga mfano wa kitu chochote kilicho juu mbinguni au kilicho Duniani au kilicho majini chini ya Nchi usivisujudie wala kuvitumikia kwa kuwa mimi BWANA MUNGU wako, ni MUNGU mwenye wivu nawapatiliza wana uovu wa baba zao hata kizazi cha tatu na cha nne wanichukiao

BWANA YESU ASIFIWE………………
Ndugu msikilizaji napenda nikueleze kidogo asili ya sanamu imetoka kwa shetani ili kukuangamiza wewe usimwabudu MUNGU aliye hai, maana Sanamu yenyewe haipumui kwanza, mungu huyo unayemwabudu inamaana hana pumzi ni mfuu, kama nilivyokwisha kukueleza kwamba ni kitu chochote kilichoumbwa na MUNGU na mwanadamu ukakiabudu.

Ukisoma katika KUMBUKUMBU LA TORATI 5: 8 – 9 inaelezea vizuri sana huu ni mpango wa shetani. Na asili ya kuwafanya watu waabudu sanamu ilitokea kwa Lucifa yaani shetani tokea vizazi na vizazi na baadae shetani kuwateka wanadamu ndipo MUNGU akamtuma MUSA ulimwenguni kuja kuwaokoa Wana wa Israeli kwa Farao ili awatoe kifungoni na alipokuwa amewatoa kifungoni ni huyu huyu Musa alienda mlimani kuongea na MUNGU, MUSA akakawia kule, na ndipo MUNGU akamwambia rudi nenda ukaangalie watu wako wanashingo ngumu yaani hawaamini hawaelewi wametekwa na shetani, na hata MUNGU wa kweli hawamtaki.

BWANA YESU ASIFIWE…………
Watu wanaoabudu sanamu mnafananishwa na wale wana Waisraeli pale jangwani, wenye shingo ngumu hawataki kumsikiliza MUNGU aliyekweli, aliye waumba anafanana na sura yao.
Muache baadae MUSA ukiendelea kusoma, MUSA akakuta wametengeneza sanamu mfano wa ndama ndio wanamuabudu eti ndio mungu huyu.

Ooooooh!! Leo yamerudi!
Ndugu msikilizaji na Mwana wa MUNGU tena unafanana na yeye unapumua kama yeye! Embu  funguka ufahamu wako akili zako umjue MUNGU wa kweli na usiwe kama wale wana wa Israeli pale jangwani , walivyo muuzi MUNGU, Soma neno la MUNGU linaeleza wazi wazi ya kwamba msiabudu sanamu na kuifanya mungu wako utaangamia.

Soma KUTOKA 32 :  35 MUNGU hakuwa mjinga kukuambia wewe, kukuumba wewe kwa  mfano wake, amekuumba ili umjue yeye peke yake, wala usiabudu hata kitu alichokuumba yeye, iwe kwenye nchi, majini hata angani, hata Malaika wake hata Watakatifu walioko mbinguni hao ni yeye amewaumba ni viumbe vyake vyote wanategemea msaada kutoka kwake, kwa taarifa kamili ameniambia YESU na mimi sibadilishi mnaofanya hivyo mmepotea, nilipokuwa ulimwenguni, YESU na MUNGU alivyoniambia niliwahaidi nitawatumia msaidizi ambayeni ROHO MTAKATIFU ndiyo yupo kwa ajili ya kukuombea wewe sasa nikuulize swali, ndugu msikilizaji? 

YESU alituachia msaidizi huyu. Msaidizi atakayekuongoza ili ufike mahali alipo YESU, yaani yeye, Je?  YESU alisema hawa Watakatifu wawe wasaidizi na ndio watakuombea na kukuongoza ufike mahali alipo yeye jibu ni hapana. Hapo tayari umeabudu Sanamu na unapotea funguka ufahamu wako, hata kwenye kitabu cha UFUNUO 22: 19 – 20  Ole wake atayeongeza maneno ya unabii wa kitabu hiki, Nikuulize Swali ndugu msikilizaji Je? Hawa Watakatifu wapi kwenye biblia wameandikwa au tumeambiwa hao watuombee??

Tafuta hakika asilimia mia moja (100%) hautaona kuanzia mwanzo mpaka mwisho, sasa na kufungua ufahamu huu ni mchomeko wa Shetani ili wewe upotee, uangamie na huu ni mchomeko  kamili ni sawa sawa na Wanawaisreli walivyokuwa jangwani, MUSA alivyoondoka kwenda kuomba shetani akawaingizia mchomeko wakatengeneza sanamu kumfanya mungu , Sasa nikuulize wewe , wewe umerudi kuabudu sanamu huyo sanamuinapumua, kama MUSA  mwana wa MUNGU Mtumishi wa MUNGU alizivunjavunja akaziboma kwani leo hii zimerudishwa tena, Kataa funguka muabudu MUNGU aliye kweli.

BWANA YESU ASIFIWE……….
Kitu tofauti na hicho na MUNGU aliyeumba Ulimwengu, huyu MUNGU wa IBRAHIM, MUNGU wa ISAKA  na MUNGU wa YAKOBO usiabudu utahukumiwa. Soma KUTOKA 32:33-35 Na BWANA atamfuta jina lake katika kitabu cha uzima mtu anayeabudu sanamu,

Narudia soma KUTOKA 32:33-35 Mtu yeyote anayeabudu Sanamu BWANA atamfuta jina lake katika kitabu cha uzima. Inamaana kama sasa hivi unamuabudu bado sanamu tayari jina lako halipo ila uamue tayari jina lako halipo ila uamue utoke huko ndiyo jina lako litafutwa. Sawa sawa na wana wa Israeli Musa alivyovunja ili sanamu ndiyo wakaondoka wakapona kinyume na hapo wangeangamia.

Musa akasema walio pamoja na mimi MUNGU wangu wanifuate wale walimfuata MUNGU aliye hai MUNGU wa MUSA wakapona na ile sanamu ikabomolewa, inamaana wangebaki kwa yule mungu sanamu wangekufa.
Oooooh!!! MUNGU tusaidie hivi ndivyo mwana wa MUNGU injili ilivyobadilishwa, imekuwa tofauti kabisa na YESU alivyoagiza ndiyo maana watu wanaangamia hamna majibu hata Mbinguni hawaendi.

BWANA YESU ASIFIWE………..

Oooooh!! MUNGU atusaidie yawezekana wewe unampenda MUNGU ila umerithi sasa yakatae ili upone maana ni machukizo kwake.

Ndugu msikilizaji soma katika kitabu cha KUMBUKUMBU LA TORATI 5: 8 – 9 MUNGU amekataa usichonge na kujifanyia sanamu na kitu chochote Duniani hata kilicho chini ya Bahari usikiabudu na hii ni moja ya amri aliyompa Musa kwa ajili ya Wanadamu wote na wewe sasa hii umeshavunja hii amri ukisoma katika kitabu cha YEREMIA 17: 5 , 7  Amelaaniwa amtegemeaye Mwanadamu Amebarikiwa amtegemeaye MUNGU, Inamaana umwabudu yeye tuu. 

Watakatifu wote hawa walikuja ulimwenguni ni mwanadamu hawa siyo MUNGU wakati YESU ananielezaujumbe huu pembeni yake nilmuona Ibrahim BABA yetu wa Mataifa ambao sisi ni kizazi chake ni mmoja wa wazee 24 na pembeni yake mama yake  YESU akihuzunika sana na kuumia moyo wake akichukia yeye kuuabudiwa, YESU akaniambia nafikiri unaona hata mama yangu analia, na kwanini YESU alinionyesha ilikuwa ni katika shule anayonifundisha ili nijue cha kueleza maana mimi haya yote ni yeye ananifundisha mimi Sifundishwi na mwanadamu, Yanatoka juu anakuletea wewe. Ni jambo la kuhuzunisha soma jinsi mpango wa MUNGU ulivyobadilishwa, hata amri zake kuzarauliwa tena wazi wazi aacheni moto unawasubiri wafanyao hivyo aacheni mtaangamia,hii ni janja ya shetani ndani ya kanisa ili msimuone YESU. 

YESU siyo mnafiki na mahali ambapo amri za MUNGU hazifuatwi haijalishi jina lake linatajwa hapo, ni kupoteza muda maombi hayo hayaendi mbinguni ni machukizo ameniambia YESU na mimi sipunguzi neno lolote nampenda na kumheshimu, wala siogopi  wala sipunguzi alivyofanya yeye na mimi ndivyo nafanya hivyo hivyo.

Nilivyoelezwa na MUNGU  sibadilishi, Funguka upone nikuulize swali je? kama umeshajua sanamu haina  uhai na unaabudu je?  Itakujibu? Na je Majibu utakayojibiwa yatakuwa ni ya ni MUNGU aliye hai au Mungu mfuu, jibu ni mungu mfuu, mungu mfuu ni shetani.

Ukiangalia Wana wa israeli pale jangwani baada ya Musa kuja kupasua ile sanamu wakashutuka wakaona kabisa ni mungu mfuu hii sanamu, MUSA akasema walio na mimi wanifuate wasio na mimi wakae pembeni, sasa na wewe umefanyika kwamba unayeabudu sanamu hauko na MUNGU wa Musa,uko na mungu mfuu, uko na mungu shetani wakakimbia na wewe kimbia ili upone.

BWANA YESU ASIFIWE………
Mpango wa MUNGU kitu chochote kisiabudiwe na kufanywa Mungu ukishiriki wewe ni mali ya mfuu na huendi mbinguni na chanzo cha kuabudu sanamu ndani na nje ya kanisa ni baada ya wale Mitume wa YESU kuondoka wengine wakakengeuka na kumkufuru ROHO MTAKATIFU.

Narudia chanzo cha kuabudu sanamu ni kumkufuru ROHO MTAKATIFU na hiyo dhambi haisameheki,  tafadhali wacha ujumbe huu ni kwa ulimwengu wote wanofanya hivyo ujue umepotea na hauna YESU na panapofanya Ibada kama hizi YESU ameniambia sipo, Hayupo hapo na kama YESU hayupo, shetani ndiyo yupo ndiyo amekaa hapo funguka, utaona Musa mwenyewe alivyovunja ile sanamu ile ya ndama na zaidi hata mama yake YESU na wazee 24 hawataki waabudiwe na wanachukia sana na zaidi wanafanya hivyo hamsikilizwi maana kama MUNGU ameshakataa hata pia katika kitabu cha Muongozo wa Safari ya Mbinguni yaani BIBLIA imekataa na haya ya kuabudu sanamu YESU amekataa sasa ni kwanini mnajilazimisha kuabudu kataa wewe soma katika kitabu cha UFUNUO 22: 18-20 aliyeyaleta haya hukumu inamuhusu na amemkufuru ROHO MTAKATIFU, Tafuta kitabu chote hautaona, Mrudie YESU na umuabudu yeye ndiye Mfalme wa Wafalme, Bwana wa Mabwana.

BWANA YESU ASIFIWE……

Jambo la pili nitanzungumzia juu ya Ibada za Wafuu.

IBADA ZA WAFUU : YESU hazitaki hayo ni mapokeo ya shetani ni ibada ambazo zinaushirikiano kati ya wewe na mizimu, mizimu ni roho za watu waliokufa walivyokuwa hapa ulimwenguni hawakuokoka au kuishi maisha Matakatifu, sasa wakifa hawa huenda kwa baba yao kuzimu maana kuzimu ni mahali ambapo shetani anakaa, Ndiyo maana wanaitwa mizimu, ukienda Mbinguni unaitwa Mtakatifu na wanaokufa katika Utakatifu wanaenda Paradiso. Wanapumzika wanasubiria ule mwisho, siku hizi watu husema peponi YESU ameniambia sio sawa peponi ni nyumbani kwa mapepo.

Nikuulize swali wewe msikilizaji, kwa nini tunasema toka pepo? Shindwa pepo, umelaaniwa pepo, hata Kiswahili unashindwa kukielewa hii ni technique amekamata shetani  alivyokamata kanisa hata kinywa, anaenda peponi inamaana umemwambia mtu anaenda kwa mapepo, ni Paradiso tuu hicho ni Kiswahili kimebadilishwa, nafikiri mnaelewa mapepo, huu usemi sio sahihi ni kuulize je unapenda kwenda kwa mapepo au unapenda kwenda Paradiso, maana kinywa kinywa kinakiri unaenda wapi, Jibu hapana Watu wameshikwa ufahamu wa kujua wanatamka nini. Ibada za wafuu huo ni mpango wa shetani ili wewe usitengeneze maisha yako au ushirikiano wako wewe na MUNGU ukijua kwamba ukifa utaombewa na kwambia inakula kwako.
Soma kitabu cha MUHUBIRI 9: 4-9 Nitaanza MUHUBIRI 9 : 5 – 9 Kwasababu walio hai wanajua ya kwamba hawatakufa wafu hawajui neno lolote maana hawana ijara tena maana kumbukumbu lao limesahaulika.

BWANA YESU ASIFIWE……..
Ukishakufa tu yamekwisha sasa unaombewa nini, Acha kudanganywa na zaidi hata soma katika kitabu cha WAEBRANIA 9: 27 Neno la MUNGU linasema ukisha kata kauli baasi.
WAEBRANIA 9 : 27 Na kama vile watu wanawekewa kufa mara moja na baada ya kufa hukumu sasa nikuulize Ibada ni za nini hizi, wewe unaacha kutengeneza unasubiri utafanyiwa, funguka hizo ni Ibada za vipofu tuu, kama imeandikwa ukikata roho ni hukumu hizo Ibada za wafu ni za nini tena unapoteza muda usidanganyike hizo Ibada kila unaposhiriki wale wafu wanakunajisi na wewe, uwe kampani moja mkamwabudu shetani.

Funguka usishiriki  ni Ibada sawa nakuabudu sanamu , kufanya matambiko kushiriki uchafu, nikuulize swali je? YESU ndiye ametufundisha haya? Hapana; kama hapana imetoka wapi? Imetoka kwa yule muovu, YESU ameniambia hata kaburi lake lisiabudiwe limetengenezwa na mwanadamu tena limechongwa na yeye akaenda kuwekwa tu na yeye hayupo hapo yupo mbinguni ndipo makao yake kiakili kibinadamu tunajua YESU ameenda kutengeneza makao na amesema hivi hapa siyo kwenu, makao yenu yako mbinguni, sasa kwanini usimuabudu aliyoko Mbinguni, unaabudu vitu vilivyokuwa hapa.

Kaniambia hapa ulimwenguni kwenye Mabara yote Baadhi ya Watumishi wamejenga makaburi na kuyaita kaburi langu na kuliita ni Makaburi ya Watumishi walio maliza kazi ya hapa Duniani yaani ni wale Mitume wale wa kwanza, mwingine kaburi la Paulo, mwingine la Isaya , mwingine Daudi, mwingine Yoshua, na mengine mengi, kaniambia ooooh Namuona YESU mbele yangu anavyohuzunika jinsi ulivyopotea ulimwengu. Akaniambia hawa sasa hata waliokufa 99% Watumishi Wa sasa hivi 99% hawajaenda Mbinguni wapo kuzimu hawajapokelewa wanasubiria hukumu huu ni ukweli asilimia 100% siyo kufikiria kuwa utumishi ndio tiketi ya kwenda Mbinguni utakatifu na kufuata aliyoagiza MUNGU, kama hukufuata na ukaabudu vinginevyo mfano sanamu utaenda kwa mwasisi wa sanamu mwasisi wa sanamu ni shetani ambaye ameazisha kazi hiyo maana anaouhalali na wewe unamwabudu MUNGU aliye hai MUNGU aliye hai hana uhalali na wewe maana haujamwabudu yeye na umemkana na yeye anakukana waziwazi. 

Badilika mrudie YESU wa kweli usidanganyike maana Wana wa MUNGU ukiambiwa hapa ni nyumbani mwa mtakatifu yeyote hapa duniani makao yao yapo mbinguni nakwambia, na ukikuta kunakaburi ukaambiwa, na ukaambiwa hapa ni Goligota au lamba udongo,au sujudia au lala hapo juu, piga magoti msujudie mungu piga kichwa chini usikubali, YESU ameniambia huu ni usanii kwanza kiafya tuu, kulamba udongo utapata minyoo magonjwa na ni uchafu.

Pili Maana yake kulamba udongo makaburini unapolamba huo udongo nafsi yako unajipatanisha na mauti iliyo juu ya ilo kaburi.

Tatu unaanza kuporomoka maisha yako ya kiroho na kimwili na mwisho wake na wewe ni wakuzimu

Nikuulize swali, Wapi YESU aliagiza hivyo yeye ndiye njia ya uzima na kweli soma katika kitabu cha YOHONA  14:6  Sasa ndiye mwasisi amesema tufanye hayo, Jibu hapana unakuwa umeabudu sanamu.

BWANA YESU ASIFIWE ……………………
Jambo lingine hili ni sugu kiasi ambacho inafanyika kwakumpinga YESU ndani ya Kanisa jambo hili ameniambia ni kuhusu sadaka ya mavuno,  ameniambia niwaeleze watoto wangu hiyo sadaka siitaki na sizipokei kwa maana, hata nilivyokuwa ulimwenguni, moja wapo ya mambo niliyoyakataa ni hiyo sadaka ya mavuno kwa jinsi ilivyoletwa kwenye nyumba ya Baba yangu pia ikafanya nyumba yangu siyo nyumba ya sala tena imekuwa Soko ukisoma katika kitabu  MARKO 11: 15-18 inaelezea vizuri  YESU aliingia  Hekaluni bakakuta nyumba ya Baba yake imekuwa  Soko, akanimbia mwanangu na kufunulia zaidi nilikuta hivi hivi, sasa mimi siyapendi, waeleze watoto wangu, wafunguke maana wananipenda.

Funguka ndugu msilikilizaji nakuelezea vizuri uelewe maana ya sadaka ya mavuno au mazao hii sadaka ya fungu la kumi kutokana na kile ulichokipata, ndicho ukitoe katika mazao yako. Sasa hii wewe uza kwanza mfano umepata magunia 10 ilo limoja liuze ile hela weka kwenye bahasha ndio ukapeleke kanisani ni gunia moja tu uza uweke kwa bahasha, akijua mtu tu tayari hapo ni sanamu .

Pili unapoleta hayo mazao kila mtu anajua umemtolea nini, Matokeo yake siyo siri tena haupati thawabu ya MUNGU unapata thawabu ya wanadamu. Jambo lingine unavyoleta hiyo unamfungulia shetani nafasi ya kurudisha yale aliyoyakataa YESU yasifanyike ndani ya nyumba ya sala mazao hayo utashangaa baada ya Ibada kanisa linakuwa soko au mnada , Elfu , Elfu ishirini, mia, laki sasa halijakuwa soko jibu limekuwa soko, sasa ndugu msikilizaji Embu soma kitabu cha MARKO 11 : 15- 18 inaeleza jinsi YESU alivyowakuta wakiuza ndani ya Kanisa alikasirika akatibua kila kitu maana hayo hayafai na sio mahali pake, siku hizi hayo mambo yamerudishwa, na aliyerudisha ni shetani. 

Nikuulize swali je mnada unaruhusiwa ndani ya kanisa au YESU anapenda biashara ifanyike ndani ya nyumba ya sala au je kazi yake kanisa ni kunadi vitu jibu ni hapana, usishiriki tena ndugu msikilizaji, unatakiwa utoe uuze uweke kwenye bahasha ufunge isionekane na mtu yeyote, Madhara yake sasa kwako wewe unayeshiriki unakuwa unashiriki kuchafua nyumba yake ya MUNGU unakuwa haubarikiwi, maana kila mtu anajua siri yako. Neno la MUNGU linasema kushoto wala kulia isijue, unavyobebana na magunia yako, watu wote siwanaona ni siri tena hiyo inakula kwako.

Jambo la tatu Baraka zako zinanadiwa watu wanapanda bei zaidi ya watatu nahao wanakuwa wameshiriki, mnagawana unabakia hauna unafilisika unabakia hauna Mkono wa MUNGU  haupo juu ya mazao yako, Nikuulize swali je MUNGU yeye hajui kwamba wewe umetolea ilo gaunia moja na anajua thamani yake lakini huyo huyo kwanini watu wengine waende kuuongezea thamani huyu MUNGU aliye kupa hayo magunia kumi anajua thamani yake na Baraka zake ziko katika gunia lako limoja katika fungu la kumi haya mengine yametoka wapi kuja kuharibu Baraka zako huo ni mchomeko wa shetani ili kuuondoa Baraka zako kuongezea na baraka za shetani  usikubali, Baraka zako za fungu la kumi kushirikiana na watu wengine kataaaa.

BWANA YESU ASIFIWE……………….
Ndugu Msikilizaji embu angalia Kanisa lilivyotekwa na Shetani, mpaka mambo ya shetani, yanapewa kipao mbele na ya YESU yanapuuzwa nakwambia 98% YESU hayupo ulimwenguni asilimia 2% tu. Amua uingie upande wa YESU wa kweli, Kanisa limekuwa ni biashara kweli haipo, Watumishi 45% ni washirikina kwa kiwango cha juu sana, sasa kweli utaponea wapi mwangalie YESU.

BWANA YESU ASIFIWE………………………
Jambo lingine nitanzungumzia kuhusu madhabau iliyokufa sababu katika kitabu cha TORATI 5: 8 utasoma mwenyewe muda hautoshi, Madhabahu iliyokufa ni Madhabau ambayo haifuati taratibu za MUNGU na maelekezo aliyoacha YESU chunguza madhabahu unayoabudu ukikuta haiko sawa na YESU mwasisi wa Kanisa alivyopanga ikiwa kinyume ujue hiyo ni madhabahu mfuu ukikuta inachangisha pesa hiyo ni mfuu, kwasababu MUNGU hataki ukikuta mnaandika majina kwenye sadaka hiyo ni mfuu MUNGU hataki.

BWANA YESU ASIFIWE……………………
Nitaelezea kidogo maana ya Sadaka halafu nitaendelea tena.
SADAKA ni Ibada yako kamili kati yako wewe na MUNGU aliyekuumba unamtolea MUNGU ili sadaka yako inene kama ya Abel na ili sadaka yako inene mbele ya MUNGU kwanza mtu asijue umetoa kiasi gani, ukisoma katika injili ya MATHAYO 6 : 2-4 Inaelezea usishauriwe na mtu hata Mtumishi asijue umetoa kiasi gani, Sadaka yako ya kweli ni fungu la kumi na shukrani, Sadaka za michango hizo hazi muhusu MUNGU sadaka za kuahidi  madeni Imani eti ukipata eti ulete na zote hata Ukombozi siyo     ya mpango wa MUNGU, Hiyo ni ujanja wa shetani  ameliteka kanisa na kubadili mpango wa MUNGU na wewe usifanikiwe na ushindwe kufanya hayo ambayo aliyaruhusu upate kushiriki dhambi.

BWANA YESU ASIFIWE……………………………………
Ukiambiwa toa mpaka ikuume usifanye hivyo haipokelewi toa kwa furaha YESU hanyang’anyi pesa kama ilivyo makanisani siku hizi huyo ni shetani na anayefanya hivyo ndani ya moyo wake Mtumishi huyo ana roho ya kuasi na tamaa juu ya pesa ukifuatwa kudaiwa pesa nyumbani kwako eti mchango kanisani labda pesa mfano wa kununua kitu mfano kinanda, gari, mabati msitoe.

YESU ameniambia mimi siyo omba omba na hana shida kama nimpango wake ataleta watu watafanya tena kwa furaha ukitoa ndugu msikilizaji haubarukiwi ni sawa sawa na kutupa jalalani wote mlikuwa mnafanya hivyo mmetupa jalalani, Unashangaa  Asubuhi saa 12 ni ngongoooo nataka hela ya kununua mabati tunataka hela ya mbao. Kama hilo kanisa ni YESU amelileta ataleta hela pale kanisani siyo kukufatafata huko mjue hayupo huko au unaambiwa kinanda mchango, unafutwa asubuhi na mzee wa kanisa. Eeeh leta leta , hata unayefanya hivyo hujui, Funguka usiende kukusanya ooooya una muudhi MUNGU, ameniambia YESU niwaambie ulimwengu wote YESU anarudi Utukufu wake ni wa mwisho ndio huu sasa umeaanza ni kweli tu mpaka aje na sasa hivi anaharibu uovu wote.

BWANA YESU ASIFIWE………………………….
Ukikuta madhabahu inachangisha au kukopa pesa benki hapo hayupo nasema sadaka zenu zinapotea YESU halipi Riba. Leo oooh mnalazimishwa kulipa riba, YESU kama yeye mwenyewe alishakataa huyo ni shetani ameingia ndani ya kanisa mnalipa riba, hapo shetani amekunja nne anawachuna, YESU hakopi wala kulipa Riba leo hii iweje kanisa likope benki siyo kanisa likope benki siyo kanisa lake ameniambia hata kama jina lake linatajwa hayupo ni machukizo, Soma katika kitabu cha MARKO 7 : 6 -7 Inaelezea vinzuri kabisa.

BWANA YESU ASIFIWE…………………….
Funguka ufahamu ndugu msikilizaji mahali popote, madhabahu iliyokufa inakopa Benki hiyo ni mfuu ukikuta madhabau inatoa huduma za kiroho mfano kukuombea unaambiwa utoe pesa hiyo ni mfuu madhabahu inafanya kazi ya Biashara ni mfuu, madhabahu hauwezi kutumikia Mabwana wa wawili, madhabahu ya YESU , YESU hakutumikia mabwana wa wawili, YESU na yeye mwanzoni alikuwa fundi Seremara aliacha kamtumikia MUNGU peke yake, Sasa leo hii mwasisi wa Kanisa amesema hawezi kuwatumikia mabwana wawili hizo biashara si mabwana wengine hayupo hiyo ni mfuu.

Kazi ya Kanisa siyo kufanya biashara ukiona hauoni majibu unakaa hapo miaka nenda rudi haukuwi kiroho wala kimwili wala kubadilika ujue mfuu hilo, Ukiona ni mateso magonjwa na umaskini, ufakara tu ndio umekujaa ujue kwamba ni mfuu ilo kanisa, huwezi kaa kwenye kanisa hai hayo matakataka yabaki ndani yako ukiona nguvu za giza zinakutesa na hazikutoki unaenda hapo kanisani na hayatoki miaka na miaka wewe unanyongwa na majini mapepo wachawi wanatembea nyumbani kwako madukani kila mahali watoto, mambo hayaendi naunaenda hapo kanisani ujue hapo unaposali ni mfuu.

BWANA YESU ASIFIWE……………….
Sasa napenda nikuulize kwa nini madhabahu zinakufa sababu unakuta mtumishi hana muda na YESU.
Moja ni mzinzi, ni mlevi, au anatumia nguvu za giza au anaifanya hiyo kazi kama ya mshahara, au amejiita mwenyewe na hata  wengine wameitwa lakini wamebadilika kwahiyo akibadilika tu madhabau inakufa au yupo kwa kusudi la pesa tu. Japo wengi ni washirikina mahali hapo hautaona jibu na zaidi unapokuwa kwenye madhabahu mfuu tayari na wewe hapa duniani unakuwa mfuu japo unatembea unakuwa box tu.

BWANA YESU ASIFIWE…………………

Hii ndiyo namna ndugu msikilizaji nazidi kukufungua ujue jinsi kanisa lilivyotekwa ni pesa tu, limerudia tu, sasa hivi wameacha kuyasema haya kweli na haya mengine yametoka kwa wanzilishi wa hizi dini wakaleta huku kwetu tukayapokea na mahali pameandikwa Wa kwanza atakuwa wa Mwisho na wa Mwisho atakuwa wa Kwanza, na hii injili ilianza kwa watu weupe wakaijua ukweli wanaukataa sasa YESU amerudi anaufungua ukweli yeye mwenyewe, Watumishi wamekataa kusema kweli japo YESU ameniambia wanakuchukia lakini usijali mimi nimekushika kwa mkono, Mimi niko ndani yako nina hitaji watoto wangu kwa gharama yeyote sasa nawafungua wanijue mimi njia zake si njia zetu, Akili yake sio akili yako, akasema BWANA YESU akaniambia watu wakisikia habari za YESU wanafurahi ninafurahi na mimi na wewe YESU anakufurahia lakini umepotoshwa.

Funguka na hayaniliyokueleza siku ya leo yakafanye kazi mimi sitoi hapa duniani ananichukuwa kaa andika ananifundisha na mimi na kueleza yashikilie sana haya ndugu msikilizaji utapona usiabudu sanamu tena unapoabudu sanamu mungu unaabudu mungu mfuu mwasisi wa sanamu ni shetani ukiabudu shetani unamchukiza MUNGU hata ukisema sala ya Baba yetu hausikiwi wala haziendi huko, zinaenda kwingine.

Funguka soma tu mwenyewe katika kitabu cha Neno la MUNGU ambalo ndio mwasisi aliyeagiza yafuatwe na MUNGU mwenyewe alivyowatuma Manabii wake akiwepo MUSA, YEREMIA,wote walitolewa juu wakiwa wanapewa ili kuyafanya, anasema watumishi wanamtaja kwa midomo yao tuu kwamba wanampenda lakini hawayatendi, ni waulize ndugu wasikilizaji hata wewe funguka je anayaabudu sanamu huyo anampenda MUNGU? Anamuheshimu MUNGU, huyo kama hamuheshimu kama angekuwa anamuheshimu MUNGU angefanya kama MUSA uvunjevunje haya masanamu.
Ndugu msikilizaji funguka wachana na hayo mambo mambo, ni machukizo na ni mabaya sana sana yanakunajisi wala  Mbinguni huendi wala usibusu sanamu imetupasa kumuomba MUNGU na kumuabudu katika roho.
Sasa mmerudi kimwili wewe unaabudu sanamu kwanza haujarudi kimwili utamuona MUNGU humuoni MUNGU.

BWANA YESU ASIFIWE……………….
Hii ndiyo shetani pia ameliteka kanisa na kidonda sugu ni sadaka ukiambiwa sasa hivi hivi mwana wa MUNGU ndani ya nyumba ya MUNGU  wa laki laki simama, miatano mchango usitoe hata unakuwa umeshiriki kufanya biashaya ndani ya nyumba ya MUNGU , usitoe hata mafandraise ya michango ya majengo usishiriki ameniambia hivyo YESU, yeye sio omba omba, Watumishi wamuombe yeye, yeye ataleta Sadaka zote ulizokuwa umeahidi na kwambia usitoe na hizo naziri nazifute leo wala usirudi huko unaibiwa haziendi kwa YESU, nazungumza kwa ujasiri sana na mimi wala siogopi alivyotumwa Musa alivyotumwa Paulo, alivyotumwa Yeremia, Na YESU mwenyewe alivyotumwa na BABA yake Mbinguni na mimi MUNGU nimeongea naye ameniambia na wewe nenda kafanye kazi hii mimi siogopi.

Nakueleza ukweli nitapita hivi hivi siku zote nchi zote nitamaliza, wako wengine wanaomba niondoke Tanzania, Siondoki ng’oo ng’oo ukweli lazima ujulikane uchawi mwisho, Kuzimu nimeshafunga tangu mwezi wa 4.2012 watu wamrudie MUNGU Jehanamu ipo ila ya waovu, hawawezi kupona wote, Embu nikuulize asilimia 2% Ulimwengu mzima embu angalia nyie mnaoenda makanisani mnaomba mnaomba halafu hiyo asilimia 2% haupo, Jenga urafiki na YESU tu mwangalie YESU atakusaidia atakuongoza, badilika badilika na leo mnakwenda kufunguliwa sana tupa ma sanamu huko, wala usiambiwe MUNGU Fulani mpaka nisaidie.

Aaaah!, MUNGU hana mpaka wewe unamuwekea MUNGU mpaka unaakili kwanza wewe. Unamuomba Mtakatifu Fulani nisaidie mbinguni nisaidie,MUNGU alikwisha tuachia  ROHO MTAKATIFU ndiyo atuombee, jenga ushirika na ROHO MTAKATIFU basi.

BWANA YESU ASIFIWE………………………
Ndugu msikilizaji MUNGU akubariki sana. 
Nitaenda kukuongoza sala ya Toba kwa wale wanaopenda kuokoka na kuacha ma sanamu ni machukizo na usitoe tena mambo ya sadaka ya mavuno usiende kufanya biashara utapigwa.

SEMA BWANA YESU….
Naomba Rehema naomba unisamehe hata nilipo abudu sanamu na kurudia wewe, uandike jina langu kwenye kitabu chako cha uzima wa milele, Na mkataa Shetani na kazi zake zote na Ibada zake zote, usiniache nishike mkono niongoze mimi ni mali yako YESU, sio mali ya mwanadamu au ya dhehebu au ya jengo nilitoka kwako nishike mkono hapa duniani uliponileta nikazaliwa nimekutana na machafu haya nikanajisika ili nisirudi ulipo wewe. Ulikotoka Mbinguni ukaja Duniani BWANA YESU, Ukashinda ukarudi kwa BABA na mimi najikonect hivyo hivyo nishinde nirudi ulipo haya ma sanamu ma ibada mengine matambiko sitaki tena niongoze mahali ulipo wewe YESU. AMEN

Nakuombea wenye magonjwa na shida zingine.                                     
BABA katika jina la YESU kwa nguvu na mamlaka uliyonipa kufungua wana wako dunia nzima Bara lolote, mahali popote, mtu yeyote anayesikiliza rangi yeyote maana ni rangi zako, wewe sio MUNGU wa ubaguzi, maskini kwa matajiri wote BABA!! Ninatuma Malaika wakufungue na wale wanao ng’ang’ania uchawi yawatese hayo mauchawi mpaka wakurudie, katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI yule ambaye anajikonect na nguvu uliyonipa ili akatumie kwenda kuiba fedha na kuchangisha watu hakika na kwambia haitakuwa wala haifanikiwi

BWANA YESU ASIFIWE…..
Ninabomoa nateketeza, nyota zenu mrudishiwe mapepo ngome zote za shetani, malaika wa shetani lucifa kwenye anga la kwanza la pili, Baharini angani, kaskazini mashariki dunia nzima mfee wote, mikutano yote ya kipepo ninaharibu wala msiende katika jina la YESU KRISTO WA NAZARETI, msiende mahali popote alipo shetani kwa nguvu na mamlaka ya Jina la YESU Asante MUNGU wa IBRAHIM, Asante MUNGU wa ISAKA. Sifa na Utukufu na kurudishia wewe MUNGU akubariki MUNGU akuinue MUNGU akutengeneze, mrudie yeye akushike mkono. MUNGU wa IBRAHIM, MUNGU wa ISAKA.
 Akulinde akuongoze, jina la BWANA litembee na wewe, Malaika watembee na wewe, katika Jina la YESU. AMEN!


NABII HEBRON.