JE UNAJUA
JINSI OFISI YA MBINGUNI ILIVYO?
BWANA YESU ASIFIWE, watu wengi wamekuwa wakijiuliza sana
habari za mbinguni palivyo, mbinguni ipo ofisi kubwa sana ambayo katika ofisi
hiyo inahusika na MUNGU BABA, ROHO MTAKATIFU na YESU WA NAZARETI katika ofisi
hii. Aliponiita YESU ili nimtumikie nilifika katika ofisi hiyo na kunipa maagizo
kwa ajili ya injili yake na kuukomboa ulimwengu na kumwandalia kanisa ili aje
kulinyakua na mengine ni yangu peke yake.
Katika ofisi hiyo sijaona kitu kinaitwa msalaba wala mavazi
yenye misalaba, wala ubani, wala mikuki, wala kofia za kuvaa kuhubiria, wala
sijaona huduma ya askofu ndiye awe kiongozi wala hakuna kitabu cha injili
tofauti na biblia hii takatifu peke yake. Na ilinichukua muda mpaka siku
nilipokwenda kuibomoa serikali ya joka kuu nikaingia katika ofisi yake. Nilishangaa
kuona katika ofisi ya joka kuu upo msalaba juu ya paa ni misalaba za dhahabu na
ukubwa wake kwa urefu na upana ni kama 2 square kilomita. Akanieleza YESU pale
ndipo penye siri zote za kuwaangamiza wanadamu na kuwasulubisha, hivyo hata katika
ulimwengu unapoona mahali penye msalaba tayari uelewe Hebron hiyo madhehebu au jingo
linaongozwa na head office ya joka kuu, hiyo ndiyo namna alivyoifanya joka kuu
na kuwateka wanadamu, na niliwaita watumishi kila nilipokuwa nataka niwafunulie
habari hizi walinisaliti na wengine hata sasa angalia majina yao yapok wa joka
kuu tayari ni watumishi wake. Na majina niliyoyaona yalikuwepo majina ya
watumishi wote maarufu katika nchi mbali mbali zote katika dunia hii 99.8% wote
wapo kwa shetani na wengine wapo katika chama cha illuminati pastors, niliogopa
sana sababu haikuwa ni jambo jepesi kwangu, hata mimi nilionaga msalaba na kitu
kitakatifu na kinamfurahisha MUNGU, kumbe lilimfurahishaga shetani, nilitubu na
kuomba rehema, na hata mlikula katika mkate kanisani kumbe mlikula laana,
mauti, vifungo katika ulimwengu wa roho na kufungwa usiende mbinguni kupitia
ule mkate wenye msalaba. Hilo ndilo lengo la joka kuu, sasa ufunguke na uamue. Unataka
kushiriki katika kanisa lenye msalaba au kanisa lisilo na msalaba wala mavazi
ya msalaba. Sababu hayapo katika ofisi ya mbinguni bali yapo katika ofisi ya
joka kuu.
Zaidi fuatilia masomo yangu katika website www.prophethebron.org. Sema BWANA YESU
naomba unisamehe dhambi zangu zote, naomba unisamehe na unifungue katika
vifungo vya msalaba katika ulimwengu wa roho. Uniandike katika kitabu chako cha
uzima wa milele. Kuanzia sasa mimi ni wa YESU WA NAZARETI na siyo wa misalaba
tena katika ofisi ya joka kuu bali niwepo jina langu katika ofisi yake ya
mbinguni.
NABII HEBRON.