Pages

Saturday, December 20, 2014

HERI YA KRISMASI!
MERRY CHRISTMAS AND A HAPPY NEW YEAR 2015!

Nawasalimu watu wote wa mataifa yote kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye hai. Krismasi hii iwe kweli na Krismasi ambayo utamtukuza MUNGU kwa ajili ya kukumbuka ile siku ambayo YESU alizaliwa miaka 2000 iliyopita, kama inavyotakwa na MUNGU na siyo miungu au mapokeo ya dini au mapokeo ya mizimu. Kama nilivyokwisha elezea katika makala ya Nabii Hebron kuhusu father Christmas ni nani? Na Christmas tree ni nini, na Christmas card ni nini? Wewe usome utaelewa vizuri na endapo utashiriki na kuziweka hivi vitu nilivyovitaja basi wewe utakuwa unashiriki Krismasi yako na mashetani na mizimu, na serikali ya kuzimu, sababu na wao wanayo Krismasi yao na wanaye yesu wao wa uongo. Krismasi ya kuzimu inaanza tarehe 23.12 hadi 27.12 kila mwaka na unapokuwa na hivyo vitu basi na wewe unakuwa umeunganishwa katika krismasi ya kuzimu. Najua wengi hamjui ila mimi ninayajua ili niwaeleze watu wote ukweli, sababu haya yalifichika na hakuna binadamu aliyeyajua, zaidi soma katika blog www.prophethebron.blogspot.com, uyasome hayo niliyo yaelezea hakika utafunguka.

Mwaka huu ninataka shetani asiwashirikishe watoto wa MUNGU katika krismasi yake sababu na hao hawampendi ila hawaujui ukweli. Pia sikiliza katika YouTube ya Prophet Hebron kuhusu masomo ya krismasi utaelewa zaidi, na ukipiga picha katika ulimwengu wote utaona watu hawajui na ndiyo sababu wanayapamda katika nyumba zao, makanisa, badala ya kumpamba YESU kwa kumpa mioyo yao na kuokoka wengi wao wengi wanamtukuza shetani na masanamu pasipo kupenda. Mfano huyu father Christmas siyo YESU wala hastahili yeye kuitwa baba wa krismasi, wala yeye siyo baba yetu kama alivyo YESU, bali father Christmas ni mzimu wa Saint Nicholas. Inasikitisha sana wakristo wanapigwa upofu hata wakashindwa kuyajua haya na hii ni sababu watumishi wamemsaliti YESU siku nyingi na YESU akakosa wa kumjulisha ili awaeleze watoto wake wapone.

Nawasihi kama unampenda YESU na unampenda MUNGU usiweke father Christmas, Christmas tree, Christmas card, mambo haya yameanzia kuzimu yakaletwa kwa wanadamu na unapoyashiriki tu basi na wewe unaunganishwa na krismasi ya kuzimu. Nikuulize swali, je mbinguni wana father Christmas anayeitwa Santa Claus? Jibu, hakuna. Mbinguni ipo siku ya kuzaliwa BABA yetu YESU peke yake. Na pia nikuulize swali je mbinguni upo mti wa kuabudiwa? Jibu hakuna mti, ni MUNGU peke yake ndiye anayeabudiwa, huu mti wa krismasi ndio mungu taamuzi, mpaka hapo umenielewa. Shetani alivuruga Krismasi ya kweli akaileta ya uongo ambayo ni ya kina Santa Claus. Sasa wewe unasherekea Santa Claus au YESU? Hapo uelewe hayo yote ni machukizo mbele ya MUNGU na kwa shetani kwake ni furaha na anashangilia wanadamu wanapigwa upofu wasimjue YESU wa kweli na Krismasi yake inavyotakiwa iwe na ndiyo sababu watu wanakuw hawana baraka za kweli za Krismasi bali wana za shetani, nuksi, balaa, mikosi, mateso, magonjwa, faraka na mengineyo.  Sasa umeijua siri hii na usishiriki tena.

Na zaidi illuminati ndio wakati wa wao kuwaibia watu nyota zao na vitu vyao kwa wale ambao wanashiriki vitu hivyo, na pia napenda muelewe, joka anacho chama chake alichokianzisha. Chama hicho linaitwa illuminati. Sasa hata katika sign za illumiati google utaona ipo picha ya father Christmas, Santa Claus, hivyo na wewe katika ulimwengu wa roho unaunganishwa pasipokujua. Ila sasa umtukuze YESU kwa kujua ukweli na ikuweke huru. Niliwaeleza shetani ameiteka dunia 98%. Sasa hata kwa kupitia hii father Christmas, wewe chunguza utapata picha na siyo ajabu na wewe ni mmoja wao au ndugu lakini ulikuwa haujui.

Jambo lingine, nawasihi muokoke ili muwe wakristo na muishi maisha matakatifu, sababu ili uwe mkristo wa kweli ni lazima kumkiri YESU na uokoke, sasa watu wengi wanajiita wakristo lakini hawajaokoka. Sasa kama hawajaokoka waelewe ni wakristo jina tu siyo wakristo halisi, na YESU atakuja kuwachukua wakristo halisi hatawachukua wakristo jina. Mkristo jina yeye ni mkristo aliyeokoka katika giza na giza bado linamshikilia ambali ndilo shetani, bali aliyeokoka na kuishi maisha matakatifu yeye ndiye mkristo halisi. Ila sasa uokoke, sema:

BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote, niandike katika kitabu chako cha uzima niwe mkristo halisi. Natoka katika ukristo giza nije katika nuru ambaye ndiye wewe. Amen.

NOTE:
Nawatakia wokovu watu wote wa ulimwengu, mumrejee YESU WA NAZARETI, usishiriki krismasi kwa kupamba haya mapambo yao bali umpambe YESU katika moyo wako na usherekee vizuri. Usimame imara katika wokovu wako ambao ndiye nguzo ya ukristo. Zaidi mataifa yote karibuni katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Arusha, Tanzania.

MERRY CHRISTMAS AND A HAPPY NEW YEAR 2015.


NABII HERBON.