Pages

Thursday, December 18, 2014

JE UNAJUA OFISI YA JOKA KUU KUZIMU IPO HIVI?

Watu wote wa mataifa yote nawasalimu kwa jina la YESU KRISTO WA NAZARETI aliye hai na aliye ndiye BABA yangu na aliyenichagua nimtumikie na kuipeleka habari ya kweli kwa mataifa yote bila kwenda kinyume na yeye. Katika makala za Nabii Hebron nimeelezea katika makala nyingi kuhusu huyu mjinga joka kuu ambaye ndiye baba yake lusifa. Siku zote anawawazia wanadamu wamkosee MUNGU kama yeye alivyomkosea ili pale mwanadamu atakapoenda kinyume na yeye tu basi aangamie na yeye katika shimo la moto. Mimi Hebron nakueleza kwa ufupi tu upate kuelewa na ikusaidie. Mimi nimepata bahati ya kumuona kwa macho yangu huyu joka kuu aliyefukuzwa mbinguni, na hata kumtandika na kumfunga pingu na kuiharibu serikali yake, yote hayo siyo kwa uwezo wangu ni kwa uwezo alionipa YESU wa kuupindua ufalme wa shetani.

Nitaelezea jinsi ofisi yake ilivyo hii ni ofisi yake ambayo nilikuta imeandikwa katika kibao “THE BOSS OF THE KINGDOM OFFICE” na kibao kingine kimeandikwa “DON’T SPY OUR GROUP OF THREE LEADERS” (hawa viongozi ni joka kuu na lusifa na kiongozi wa tatu alikuwa ni mwanadamu anaitwa Maxwell, ila sasa ameokoka anaitwa Isaya, yupo katika kanisa langu). Katika jingo hili juu ya paa upo msalaba kama vile misalaba ya makanisani, ila nimeilipua ofisi hiyo nikiwa na malaika Mikaeli na wazee 24 na malaika waliopo mbinguni. Sasa cha ajabu huku duniani watu wakapigwa upofu na wengine wanajua kabisa kuweka msalaba katika kanisa hilo hekalu linaunganishwa na ofisi ya joka kuu pasipo watu kuelewa na wengine wanaelewa kabisa kuwa msalaba ni ishara ya mauti na siyo kitu kitakatifu au ni ishara ya mzigo au laana. Basi makanisa yanapoweka misalaba inakuwa ni ishara yao kule kuzimu kulijua kanisa lao. Na hata kama mtumishi anao nguvu zao au amepewa utumishi na joka kuu ni lazima utawaona wamevaa misalaba na unapovaa msalaba katika ulimwengu wa roho uelewe unasulubiwa na mapepo na pia tayari umebeba mauti katika shingo yako.

Watu wengi hawaelewi huu msalaba haujatoka mbinguni, bali imetoka kwa joka kuu na kila mahali panapotumika misalaba uelewe ni joka kuu yupo hapo, hata katika makaburi haifai kumzika mtu na msalaba. Yeye siyo mlaaniwa na zaidi huyo aliyekufa anapozikwa na msalaba ina maana katika ulimwengu wa roho amesulubiwa na mapepo na shetani anatumia mlango huo. Embu tazama Baba yetu Ibrahim hakuzikwa na msalaba, mitume wa YESU, YESU mwenyewe yeye ambaye alituonyesha njia hata alipozikwa hakuzikwa na msalaba. Sasa nataka muelewe msalaba ni mauti, au mahali pa mateso au pa kuuliwa roho yako na ndivyo makanisa yalivyo sasa yana misalaba kwa ishara ya kuulia roho za watu na watumishi waulize biblia haijaruhusu kanisa liwekewe msalaba.

Mimi Hebron mwaka 2013 YESU akaja nyumbani kwangu akanifundisha kuhusu msalaba niliogopa sana nikaujua ukweli, nikawafundisha watu, na hata mtu akifariki au muda wake umeisha wa kuishi katika dunia hii, kanisa langu nimeshawaeleza ni marufuku mtu akifariki azikwe na msalaba, watazikwa kama Ibrahim, au YESU na siyo kuzikwa na misalaba tena na milele. Unapokuta msalaba katika kanisa, inawezekana watu hawajui ila viongozi wanajua hasa wale wachawi na walioenda kupewa utumishi na shetani moja ya sharti ni lazima waweke msalaba katika jengo, katika mavazi. Na unapowekwa tu yale mapepo yanakuja kuwatawala watu wote, na kwa njia hiyo YESU anazuiliwa kuja katika jengo hilo sababu yeye alishasulubiwa na akafufuka, na katika ulimwengu wa roho yeye hata sulubiwa tena. Hiyo ndiyo njia aliyoifanya joka kuu kuyafanya makanisa huku ulimwenguni yawe majengo yake na anayo uhalali sababu moja wapo ni misalaba.


NABII HEBRON.