YAJUE MAVAZI
YA KUZIMU NILIYOYAONA KUZIMU YAKIWAMO MAGAUNI YA HARUSI (BIBI HARUSI).
BWANA YESU ASIFIWE kama nilivyokwisha kueleza katika
mafundisho kanisani na kwenye mitandao, shetani aliwateka wengi hata waliookoka
katika maeneo mbali mbali ila YESU amenituma niwaeleze ukweli sababu anaona
mnavyoteseka na hampati majibu na akaniambia Hebron haya mateso yasingewapata
wanadamu ila yamewapata sababu niliowaita wamemgeukia shetani na ndio anakuwa
baba yao hivyo wanafanya kazi ya baba yao ambao ni lusifa hata wanangu
wanateseka na kuangamia ila nimefurahi sasa sababu upo wewe Hebron, nimekupata
wewe uliyenikubali kunitumikia na kuyatenda yale ambayo mimi na BABA yangu
mbinguni na ROHO MTAKATIFU ndio tunayoyataka, na pia Hebron nataka uelewe kabla
yaw ewe kuumbwa MUNGU alishakuandaa na akajua ikifika muda wake atakusimamisha
na anajua utaifanya kazi yake sababu anajua yeye aliyokuumba hivyo usiogope
lolote. MUNGU alikuficha siku zote kama vile alivofichwa Musa akatunzwa na
Farao hakuuwawa, hivyo ndivyo ilivyo kwako na utaifanya kazi yangu vizuri sana
na kuzimu haitakuweza milele. Sasa nimefurahi sababu kila akusikilizaye na
kubadilika na kutii unayowaeleza atapona sababu ndani yako MUNGU ameweka majibu
ya viumbe vyote na kila kitu. Maneno haya kila nikumbukapo nasikia machozi
yananitoka kwa ajili ya watumishi walivyomsaliti YESU hata na kugeuka freemason,
wachawi, waongo, wanyang’anyi ila usiogope ninajua kinachokuja na watu
mtamfurahia YESU WA NAZARETI.
Haya magauni ya harusi ya kuzimu- kila gauni la harusi lenye
kuburuza mkia- ina maana ule mkia unaoburuzwa ni mkia wa lusifa. Lusifa anao
mkia ila nilimkata mkia wake. Unapofunga ndoa na gauni la jinsi hiyo ndoa yako
unampa lusifa. Na unapovaa gauni la harusi unaonyesha mabega na manyonyo
unakuwa unavaa gauni la pepo kuzimu la kufungia harusi zao na wewe
unajiunganisha hivyo hivyo na mama wa makahaba. Ukiangalia leo hii watu ndio
wanasema ndio fashion. Hii siyo fashion mimi nasema yote ili nisije nikaulizwa
na YESU siku ile ya mwisho sikuwaeleza ukweli ili mpone na usijisumbue hata kama
jina lake YESU linatajwa haiunganishi hiyo ndoa sababu la hilo vazi mimi pia
nilikuwa sijui, ila sasa uelewe ili upone. Wanawake mkatae sasa msiwekewe tena
mikia ya shetani ukauburuza.
Kujipaka rangi ya kucha. Kila rangi inayo maana yake, rangi
zote ulimwengu maana za kucha asili yake ni kuzimu. Ukipaka hizo rangi
unaharibu maisha yako pasipo wewe kujua na hizo rangi zimechanganywa na rangi
za ngozi za watu waliokufa baada ya kuchunwa ngozi zao na mashetani wakala
nyama zao. Sasa unapozipaka unakaribisha majini katika maisha yako na uthamani
wa mikono unaibiwa, hata pesa hazikai wala kazi zako hazibarikiwi sababu MUNGU
hana mahali pa kupitishia baraka katika mikono yako sababu shetani ameshaweka
vitu vyake katika mikono yako.
Kucha za bandia- hizo ni kucha za majini walizozikata kuzimu kama vile na wewe unavyokataga zako,
unapozivaa kucha za bandia unakuwa unawapa majini uthamani wa kucha zako ambapo katika kucha
zako zipo Baraka wanaziiba zako unabakia na zao na unakuwa tayari umeingia
urafiki na majini pasipo kujua japo wengine wanajua na wanayapenda majini.
Nguo zote ambazo za wanawake zinakuwa na mipasuko zote hizo
asili yake unakuwa unajitengenezea mkia wa lusifa na lusifa kuitumia njia hiyo
kukupata.
Nguo ambazo ni short ni fupi zinazoonyesha mapaja na
hupendwa sana kuvaliwa na masecretary katika ofisi mbali mbali, sasa hilo vazi
kila unapolivaa ina maana unamkubali shetani kabisa ila sasa uelewe haifai.
Kuvaa pini katika ulimi, unapotoboa ulimi tayari unampa mama
wa makahaba ulimi wako na vitu vyako kisha unabakia na ulimi wake na anakamata
fahamu zako na kisha kwa kutumia ulimi huo uliovalisha pini anautumia kunyonya
viungo vya siri vya kiume na mwanaume atakayefanyiwa hivyo anakuwa viungo vyake
vimemezwa na Yezebeli katika ulimwengu wa roho kupitia mwili wa mwanadamu. Kazi
kubwa ni kumeza viungo vya kiume kwa njia ya kuvinyonya na pia hata ukinyonywa
ulimi au kiungo chochote na mtu aliyetoboa ulimi, uelewe anatumika kumeza vitu
vya watu na ndani yake yupo Yezebeli na ndiyo sababu ametoboa ulimi. Ili kumjua
mtu mwenye Yezebeli au Yezebeli anaishi ndani yake angalia ulimi ametoboa na
katika ulimwengu wa roho na yeye anakuwa ni mtoto wa Yezebeli na Yezebeli
anauhalali sababu anayo alama yake katika ulimi.
Alama nyingine ya Yezebeli ni inayokufanya kuunganika katika
kitovu cha mtu na Yezebeli utaona mtu anatoboa kitovu au anatoboa pembeni ya kitovu,
hii ina maana amejiunganisha kupitia kitovu,
huyo mwanadamu atakuwa anatabia za kipepo, hata kutembea uchi, mlevi, hafai
kuolewa au kuwa mke bora, sababu atakuwa ni kahaba.
Na wengine wanatoboa (wanawake) wanakitoboa KISIMI wanakivalisha
pini, yaani ukiona hivyo uelewe kile kiungo cha kike alicho nacho huyo binti
siyo cha bindadamu ni cha pepo, kama alivyo mama wa makahaba na yeye amejitoboa
na anavaa pin kubwa ya dhahabu ambayo ina urefu wa 30 cm na unene wa 2 cm. Mmh,
haya mambo yanatisha kiasi hata mimi nimeandika huku nilikataa nisione alivyo
ila YESU amenitia nguvu ili niwaeleze mjiepushe msifikiri ni vizuri hayo sasa
yaelewe, okoka uvitupe hivyo vitu.
Na alama nyingine ya mtu mwenye Yezebeli anavaa pini katika
macho, bangili miguuni hasa bangili moja katikamguu mmoja na kujichora katika
mapaja au kuchora moyo na alama ya mshale au kuandika majina ya watu katika
mapaja au tumboni, mgongoni au popote katika mwili. Tubu BWANA YESU naomba
unisamehe, nimekosa sana, nashukuru kwa kujua ukweli, uniandike katika kitabu
chako, simtaki Yezebeli tena, na pin zake nazitupa, arejeshhe viungo vyangu,
vyake sivitaki katika jina la YESU WA NAZARETI, uniongoze YESU WA NAZARETI siku
zote za maisha yangu. Nisipotee tena na nisitoke katika mkono wako, uniongoze
katika kanisa alilopo mtumishi wako wa kweli ili aniongoze salama. Amen.
NABII HEBRON.