JE UNAZIJUA
SIFA ZA NABII WA MWISHO?
BWANA YESU ASIFIWE, yeye ambaye ndie Nabii wa mwisho ambaye
alitumwa na MUNGU hapa ulimwenguni, kukomboa ulimwengu, nitaelezea kwa ufupi
kuhusu Nabii wa mwisho, katika vipengele viwili. Kwanza katika kifungu cha
kwanza katika biblia kuhusu Nabii wa mwisho. Alikuwa ni YESU WA NAZARETI peke
yake, na katika kipindi kile na katika kipindi hiki cha mwisho MUNGU ameteuwa
mtu ambaye ndio Nabii wake wa mwisho lakini katika sehemu hii watu wengi
wanapotoshwa na bado wanazidi kupotoshwa na watumishi ambao wanajiita wao ni
Nabii wa mwisho na kumbe ni waongo watupu. Wanamsingizia MUNGU kuwa wao ndio
Nabii wa mwisho, hii imetokea katika ulimwengu wote, ni wengi wanaojiita hivyo.
Sasa unatakiwa ujiulize je MUNGU alisema atakuwa na manabii
wengi wa mwisho? Jibu, siyo, huu ni uongo na sababu ni baada ya watuishi
kumsaliti YESU ikaingia roho nyingine ya kuasi hivyo kujiita yeye ni Nabii wa
MUNGU wa mwisho hivyo usishangae, ujue analo pepo, ila nitakufundisha ili upate
kupona na umuelewe kimwili yule ambaye ndiye Nabii wa mwisho wa MUNGU, ina
maana akiwa yeye ndio Nabii wa kweli wa MUNGU wa mwisho, kwanza MUNGU
hatamnyanyua Nabii yeyote yule mwingine sababu MUNGU yeye siyo kigeugeu.
SIFA ZA
NABII WA KWELI WA MWISHO ALIYETEULIWA NA MUNGU MWENYEWE…
a.
Nabii huyu hatakufa kimwili wala kiroho atafanya
kazi ya YESU aliyotumwa mpaka siku ile ya unyakuo amkabidho YESU watu na ripoti
ya kazi aliyoifanya.
b.
Hujua majibu ya viumbe vyote na nchi zote na
hakuna jambo lolote ambalo litamshinda yeye sababu ndani yake yeye ni MUNGU anaishi.
c.
Haabudiwi kama MUNGU au YESU.
d.
Habatizi watu kwa majina yake, wala haibadilishi
biblia akaongeza maneno yake.
e.
Siyo mzinzi, muuza madawa, mchawi, freemason,
siyo mfanya biashara ya aina yeyote.
f.
Anaongozwa na MUNGU peke yake wala siyo kutumia
akili zake.
g.
Unabii anaoutoa unatimia kila anaposema, hanyang’anyi
watu mali zao wala pesa zao, na hafanyi kazi ya MUNGU kwa kutafuta pesa kama
ilivyo leo hii,wamekuwa ni wezi wanalichafua jina la YESU na MWENYEZI MUNGU.
h.
Endapo Nabii atasema yeye ndio Nabii wa mwisho
halafu akafa kimwili sasa upate picha huyo ni muongo kabisa na kama angekuwa
yeye ni wa mwisho nikuulize swali je mbona hatujanyakuliwa? Na bado tupo hapa
ulimwenguni? Au je sasa tupo tayari katika kipindi cha dhiki kuu? Jibu, bado. Hapo
uelewe Nabii wa jinsi hiyo popote katika ulimwengu wote watoto wa MUNGU uelewe
huyo anajiita jina hilo na kumkufuru MUNGU na pia kwa picha hiyo hata branch yake
itakuwa inao msingi wa uongo na ni mahali pa kuulia roho za wana wa MUNGU.
i.
Siku zote Nabii wa mwisho hawezi kuimaliza kazi
aliyotumwa na MUNGU ni mpaka katika siku ya unyakuo, atakapokuja YESU
kulinyakua kanisa na yeye ndiye atakayekuwa wa kwanza kushikwa mikono na YESU
na kukumbatiwa kwa ajili ya pongezi ya kazi aliyoifanya wala siyo kinyume. Hivyo
inapotokea au itatokea hapa mataifa yote mfunguke ufahamu. Shetani amewapa
manabii wengi vyeo vya uongo ili kuwapotosha watu ili wawaamini wao ili watu
watekwe. Ila umshukuru MUNGU sababu umeelewa sasa ukweli na ujitenge nao na
uyachunguze matendo yao, hapa nimeelezea kidogo kwa upande wa kimwili ila kwa
upande wa kiroho wewe omba utaijua kweli aliye Nabii wa mwisho na wa kweli.
j.
Kila jambo linatokea liwe zuri au baya iwe ni
katika kanisa lake, nchi yake, ni lazima MUNGU amjulishe yeye kwanza na haiwezi
ikatokea pasipo yeye kujua, na inapotokea na kuleta madhara kwa watu wake sasa
uelewe kabisa huyo siyo, sababu biblia inasema MUNGU hatafanya jambo lolote bila
kumjulisha Nabii wake. Sasa iwaje asijue? Jibu unalo.
NOTE:
YESU anachukia sana watu wanaomchafulia MUNGU majina yake
ambayo hajawapa, hawajui, ila yeye atapambana nao, neno la MUNGU halirudi bure,
maneno haya siyo yangu mimi Hebron, ni maneno yaliyotoka katika serikali ya
mbinguni kwa ajili ya mataifa yote.
NABII HEBRON.