JE UNAIJUA
AINA ZA STYLE ZA KUNYOA ZA SHETANI?
NA WANADAMU
WANAINYOA?
SOMA HAPA….
Aina za kunyoa nywele ya kuzimu, ambayo ndiye majini
yanayonyoaga cha ajabu niliona kuzimu na aina hizi za minyweo alizibuni jini
Abubakari ili kuhakikisha tu kwa kila njia shetani aweze kuwateka wanadamu pale
tu mtu anapofanya kitu cha kuzimu tayari na yeye anakuwa wa kuzimu sasa maji
siku zote yanafuata mkondo, hayaendi mahali pasipo na njia hivyo hivyo na
mwanadamu na yeye anapoiga kunyoa style za shetani basi anayafungulia majini
yamfuate alipo na yanamkontrol maisha yake na kukufanya wewe ni wa kuzimu na
hauendi mbinguni. Ameitumia njia hii pia ili pale MUNGU atakapo kukuchukua
wakati wa unyakuo isiwezekane haijalishi umeokoka na unaishi maisha matakatifu,
tayari unakuwa kichwa chako ni cha jini katika ulimwengu wa roho na kukuzuia
usifike mbinguni, na zaidi majini yanakuwekea tabia zao mfano ulevi, ugomvi, wizi,
ufisadi, kupenda miziki ya kidunia na umalaya. Na hata wewe chunguza utaona asilimia
kubwa ya watu wenye kunyoa style za ajabu tabia zao zinafanana.
AINA ZA
STYLE ZA MAJINI WANAZINYOA
1.
KIDUKU- ina maana upande wa kulia ni dunia
imekutawala na upande wa kati kati penye nywele ni shetani amekaa kati kati
yako wewe uliyenyoa na upande wa kushoto ulio hauna nywele na ni dunia
imekushika.
2.
KISAHANI- ina maana katika kichwa chako
uliyenyoa hivyo juu ya kichwa chak shetani amejenga mji wake, kule kuzimu mji
wa jka kuu unaitwa Freeman Village na ramani yake ni ya duara (kisahani style) hapo juu ya kichwa chako ni mji wake.
3.
PUNK ZOTE- aina zote za punk ni style za jini
anayeitwa makata yeye peke yake ndie anayenyoa style hii, hivyo unaponyoa na
wewe unafungulia urafiki majini makata wakufuate na kuharibu maisha yako na
kisha hata unapokata roho hawa makata huja kuichukua sababu na wewe katika
ulimwengu wa roho unaitwa makata japo hapa ulimwenguni unaitwa fulani.
4.
KUNYOA NYWELE ZOTE HALAFU UNAWEKA KIBWENZI- aina
hii unakuwa umenyoa aina ya mnyoo wa tumbili (velvet monkey) hivyo katika
ulimwengu wa roho na wewe unaitwa tumbili na tabia za tumbili zinakufuata
ikiwemo tabia zake kubwa ni uzinzi na uwizi na utapeli.
5.
KUANDIKA CHOCHOTE KATIKA KICHWA- unapoandika
chochote katika kichwa au umeweka alama yeyote ile ni dhambi, pili kila unachoandika
unakuwa umejiandika jina la jini lililopo kuzimu, iwe umeandika hata kama jina
lako iwe ni kwa mkasi au ni kwa kupiga rangi, hapo tayari unakuwa umejitenga na
MUNGU usiende mbinguni, huu ni mtego wa shetani japo unampenda MUNGU lakini
unapigwa upofu, sasa mshukuru YESU aliyenituma mimi Hebron niwaeleze ukweli wa
habari njema ili mpone. Na shetani alichokifanya hawa wanaoandika vichwani majina huwapa majini ya
kuwapa umaarufu, ila sasa hakuna tena huo umaarufu wa shetani kufanya kazi hapa
ulimwenguni. Nimekwisha bomoa na mtaona haya ninayowaeleza uyaonapo usishangae
ukumbuke ujumbe huu niliokuletea Nabii Hebron Kisamo, ingia www.prophethebron.blogspot.com
usome zaidi na vitabu vyangu.
AINA ZA
KUNYOA NDEVU (STYLE ZA KUZIMU)
1.
O style- unakuwa unajini linaitwa Abubakari
(Sharubaro).
2.
Kuchora chini ya kidevu staili yeyote- jini
Makata.
3.
Kupaka ndevu dawa iwe njano, nyekundu,
yeyote ile (Abubakar jini).
4.
Kuwa na nywele (ndevu) ndefu zinazogusa hata
sehemu ya chakula (unakuwa wewe ni beberu wa kuzimu).
5.
Kunyoa ndevu kama style za mbuzi- uelewe tayari
unalo jini ndani yako (je na wewe unanyoaje ndevu?)
NOTE:
Kila anayenyoa staili hizi ajielewe katika ulimwengu wa roho
yeye amekuwa ni shoga ameolewa na hayo majini na inawezekana haujui lakini
mshukuru YESU WA NAZARETI aliyeniokoa mimi Hebron kwa ajili ya kufanya kazi
yake, watu wamjue MUNGU na wasije wakachomwa moto, niwafunulie siri za shetani
ili asiweze kuwatega tena na niwafunulie siri za ufalme wa MUNGU ili mwende
mbinguni na giza liondoke, sababu giza linatanda katika idadi kubwa watu
hawajui na huko ndiko kutekwa na shetani na kanisa limemsaliti YESU kupitia watumishi
wao wanaofanya biashara sasa wameamua kuitenda dhambi na hawasemi ukweli 98% na
ndio sababu hata hii minyweo ya shetani ikaingia katika ulimwengu wote sababu
YESU hakumpata wa kumueleza na kumuonyesha haya ili watu wasifanye na hadi kutekwa,
na cha ajabu hata ukiangalia style za watumishi wanazinyoa utaona nao wengi wao
wamenyoa aina hizi hizi na kama wananyoa aina hii hii ina maana na watumishi wa
jinsi hiyo nao wameolewa na majini katika ulimwengu wa roho, na kama ameolewa
na majini je unatazamia uipate injili yenye YESU wa kweli? Au atakuwa anamuaga
maroho machafu katika kanisa, na kanisa kuwa ni watenda uchafu, ufisadi
(wametekwa na shetani).
Ukikuta mtumishi ametoboa masikio anavaa hereni halafu
anawahubiria injili ya YESU, elewa huyo ni shoga katika ulimwengu wa roho na
hata awe ni mwanaume yeyote yule ajielewe ameolewa na jini, sasa amua leo
uitupe hiyo herein ili mahusiano yako ya kuolewa na jini yaishe uokoke upya. Pia
nataka muelewe katika nchi nyingi watu wanasema mashoga wanaoonekana kuwapinga
hii ni sawa kabisa, lakini je hawa mashoga wa kiroho mbona watu hawawapigi
marufuku au kuwapinga, mfunguke hawa ni wale wale katika roho ndio sababu
imetimia katika mwili wanavaa vitu vya kike, na kama umevaa hauelewi madhara
yake, sasa funguka acha ushoga wa kimwili na kiroho, jehanamu inawasubiri,
mtubu na kuokoka, acha kuolewa na majini na kwa watumishi hao hawaoi wala
kuolewa ni sababu katika ulimwengu wa roho ni wake za majini au waume wa
majini.
Zaidi fuatilia makala ya Nabii Hebron usome alichonituma
YESU na masomo hakika utapona, sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu
zote, uniandike jina langu katika kitabu cha uzima wa milele, sitaki tena kuwa
shoga kimwili na kiroho na nyoa aina zote za nywele za ndevu za mapepo zote. Mimi
siyo mfuasi wa majini tena katika jina la YESU WA NAZARETI, unibadilishe YESU,
unilinde siku zote za maisha yangu. Nashukuru kwa kunifanya nisinyoe tena style
za kuzimu. Amen.
Ujumbe huu watumie na wengine kwa njia ya facebook, twitter,
google, email usambae kila mahali watu wapone, ubarikiwe. Karibu katika kanisa
la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, Arusha, Tanzania.
NABII HEBRON.