JE UNAYAJUA
MADAWA YA NYWELE AMBAZO ZIMETOKA KUZIMU NA ZINATUMIKA HAPA ULIMWENGUNI?
SOMA HAPA…
Kama nilivyokwisha elezea katika makala na vipindi mbali
mbali ya redio na television, nasema tena wazi wazi shetani ni mpumbavu na
hawapendi wanadamu wamtafute MUNGU na zaidi lengo lake ni kuyaharibu maisha ya
watu peke yake yamkini unajua au haujui. Katika nchi ya kuzimu vipo viwanda vya
mafuta ya nywele za wanadamu ambavyo hata mimi Hebron pasipokujuaga hapa ulimwenguni
niliyapaka lakini namshukuru ROHO MTAKATIFU sana pale nilipoitwa na YESU
nilipokea neema ya kubadilika na nilijikuta ghafla siyapendi mafuta ya nywele
nikawa napaka mafuta ya kawaida.
Nakumbuka siku moja hata mke wangu aliniambia daddy mbona
unajipaka body lotion mpaka kichwani kwani nywele si paka mafuta yake yapo na
hayajaisha nikashangaa najipaka tu wala siyapaki, kumbe ROHO MTAKATIFU aliye
ndani alikuwa ananiongoza, ila siku aliponipeleka YESU kuzimu na kunipa
maelekezo ya kufanya nikapitishwa katika viwanda vya vipodozi, madawa ya
nywele, nikaona yanavyotengenezwa na vitu vinavyowekwa huko na kasha viletwe
huku duniani ili kuwaangamiza wanadamu. Mafuta haya ambayo hata mimi
niliyatumiaga pasipo kujua nikakuta kule kuzimu yanachanganywa na mafuta ya
mwili ya watu waliokufa na vitu vya ajabu ajabu, ila nitaelezea kwa ufupi.
a.
Mafuta yote ya curl yanatoka kuzimu na
nimeyaona.
b.
Mafuta ya kuzifanya nywele ziwe nyeusi (mfano
nywele za watu ni nyeupe halafu anapaka dawa zinakuwa ni nyeusi) anapopaka
katika kichwa chake anayaweka mapepo na pia anauzuia utukufu wa MUNGU usishuke
katika kichwa chake, na pia maisha yake yatakuwa nyeusi au yana giza siku zote,
na akili zake na nyota imeibiwa na mapepo.
c.
Mafuta ya kubadilisha nywele rangi mfano
zinakuwa njano, blue, nyeupe, au brown na rangi nyinginezo zote zimetoka kuzimu
na madhara yake soma katika kifungu (b) yanafanana.
d.
Kwa jinsi nilivyoangalia na niliporudi ulimwenguni
niliona mafuta ya nywele 95% yote ni ya kuzimu ikiwemo na vipodozi, madawa yote
ya kujichubua.
e.
Mafuta ya kujifanyia scrub- mafuta ya aina
yeyote ya scrub yanatoka kuzimu, unapofanyiwa na mafuta hayo, kwanza yanaondoka
na uthamani wa ngozi yako na maisha yako, na kama unafanyiwa katika uso au
kichwani unanyang’anywa macho ya rohoni, akili zako, sura yako, kibali chako
ulichopewa na MUNGU na kuwekewa ya kipepo.
f.
Shampoo zote siyo salama, asili yake ni kuzimu. Shampoo
ile nzito nzito iwe ya aina yeyote ila kule kuzimu ni makohozi ya majini yote
vinavyotemewa yanahifadhiwa kisha wanayaleta kwa wanadamu wajipake, na madhara
yake ni mikosi, kujipaka nuksi balaa. Na shampoo nyingine ni ile ambayo ni
shampoo nyepesi, hiyo shampoo nyepesi kule kuzimu ni mbegu za kiume na kike za
majini, unapoitumia huku ulimwenguni wewe binadamu unafanyika kuwa nyumba ya
kuzaa majini pasipokujua, na inasababisha vijana na mabinti unakuta yeye haoi
au kuolewa kumbe sababu moja wapo ni kuwa yeye ni chombo cha kuzalia majini
hivyo akija mwanadamu ili watafute mtoto unakuta uzazi yaani yai lina majini
vitoto, na kufanya mtu hazai kabisa katika maisha yake, na pia majini hukamata
akili za wanadamu pale wanapopata mlango kisha wanawawekea kupenda vitu vyao na
ukipata pesa utashangaa unaenda kuvinunua vitu vyao na kuvitumia na kwa njia
hiyo, biashara ya kuzimu inayofanywa na majini ikashamiri duniani na viwanda
kukua kumbe ni vya shetani vimeletwa ili kuharibu maisha ya wanadamu na ndiyo
sababu watu wengi ni vigumu kumpenda MUNGU au kumfuata MUNGU ni sababu ya product
za shetani wanazozitumia, watu wasingeijua siri hii naelewa hata shetani pamoja
na wale wafuasi wake ambao ni wanadamu ambao wanashirikiana na shetani
hawafurahi kabisa sababu waujua malengo yao yamefika mwisho na watu wa MUNGU
hawatawapata tena na katika mitego hiyo YESU kaifichua siri. Sasa uamuzi ni
wako wewe, pia sabuni asilimia kubwa ni makohozi ya majini, ila watu hawajui
wanadanganyika na harufu za manukato yanayowekwa, ndio sababu watu nuksi na
mikosi haziishi, faraka katika ndoa, magonjwa ya ngozi, sura kuharibika na
mengineyo mengi ni sababu ya sabuni za kuzimu.
- Mfano
shetani akabuni njia ya kuwakamata au kuiba uthamani wa mikono yao na pesa zao,
kila unapotumia hand wash kuoshea mikono hapo unaibiwa kila kitu, unabakia
kulalamika pesa hazikai na hazifanyi kazi.
- Kupiga deki
na shampoo- unakuwa unaipaka makufuru nyumba yako au makohozi, mfano unamfahamu
kono kono huyu ni kiumbe ambaye yeye hutumika na shetani kusambaza makufuru kwa
ile njia ya kumwaga ule ute ambao ukiuangalia hauna tofauti na makohozi, kon
kono akipita kwako uelewe ameacha makufuru, sasa cha ajabu watu wengine
wanakula kono kono waelewe walikula makufuru au wanakula makufuru.
NOTE:
BWANA YESU namba unisamehe dhambi zangu, uniandike jina
langu katika kitabu chako cha uzima simtaki kabisa shetani navikataa vipodozi
vyake na mafuta yake sipaki tena unirejeshee vitu vyangu ili niwe nina vyote
ulivyonipa na niishi katika utukufu siku zote za maisha yangu. Naomba ROHO
MTAKATIFU anionyeshe mafuta yote ya kuzimu na vipodozi vyote nisitumie tena na
nivichome, visikae tena katika nyumba yangu balaa ikanifuata sababu ni mlango. Nirejeshee
uzuri wangu na sura yangu nipendeze zaidi.
Ili kuyajua mafuta yanaytokea kuzimu- yanaharufu kali na
ukiona tu katika perfume ukasikia harufu ya ubani au harufu ya mchele mchele,
iwe ni katika sabuni au perfume na mafuta yenye picha ya mwanamke ya curl, haya
nimekufunulia uelewe yanatoka huko. ROHO MTAKATIFU akufunulieni zaidi awape
macho myajue sababu ni aina nyingi hata nikiandika 100 days bila kupumzika
sitayamaliza, ina maana maduka ya vipodozi 95% ni vitu vya kuzimu, hii ni
katika ulimwengu wote. Hapo ndipo penye mtego kubwa wa shetani. Ila mshukuru MUNGU
ambaye amekufunulia haya ili watu wapone. Sababu na MUNGU hapendi kabisa watoto
wake wapake mafuta ya nyama za watu au vitu vya majini mfan makohozi, mikojo,
jasho. Huduma za shetani sasa mwisho katika jina la YESU.
NABII HEBRON.