JE
UNAJUA KUWA MAWIGI (WEAVE) NI NYWELE ZA SEHEMU ZA SIRI ZA MAJINI YALIYOPO
KUZIMU?
ZAIDI
SOMA HAPA….
BWANA YESU ASIFIWE watu wote wa mataifa yote na ambao
mmeumbwa kwa mapenzi ya MUNGU na siyo shetani ila shetani hawapendi wanadamu
kabisa na anataka waangamie na kuja kuchomwa naye moto kwa kumfanya mwanadamu
amkosee MUNGU eiza kwa kujua mwanadamu mwenyewe au mwanadamu asijijue kuwa
amemkosea MUNGU. Katika makala hii nitaelezea machache ya yale ambaye niliyaona
kuzimu kwa macho yangu bila kuhadithiwa na mtu yeyote na zaidi ilikuwa ni
mpango wa MUNGU mimi Hebron niende nikaone kila kitu ambacho shetani na
serikali yake wanachokifanya na kwa ajili ya kuwateka wanadamu wamkosee MUNGU
na wasifanikiwe sawa sawa na mpango wa MUNGU, na pia sikuonyehswa haya nije nikae
kimya nilionyeshwa ili niwaeleze watu ili wapone na atakaye kaza shingo asije
akamlaumu MUNGU Ufunuo Wa Yohana 3:6 (yeye aliye na sikio na asikie neno hili
ambalo ayaambia makanisa, kanisa ni wewe mtu ambaye siku ya unyakuo YESU
atakunyakuwa kama ukiwa umeokoka, batizwa ubatizo wa maji mengi na kuishi
maisha matakatifu, ikiwa kinyume hautanyakuliwa.
Nilipofika kuzimu nilipelekwa sehemu za viwanda na viwanda
vingi ambayo nilikuta kuzimu huku duniani vipo na viwanda hivyo vimeletwa
ulimwenguni ili kuwadhoofisha wanadamu na kuwaharibu maisha yao, japo sasa
nitaelezea kuhusu mawigi (weave) asili ya hizi nywele ya wigi, hizi nywele
zinatoka kuzimu, kuna majini ambayo ni makubwa kuliko majini yote yanaitwa
(GOLO) na yana manywele mengi sana, upana au unene wake ni kama mita nne kwa
unene. Haya majini ndiyo yakisha nyolewa hizo nywele zao za siri ndizo
zinazoletwa huku duniani kasha watu wanazivaa kichwani. Niliogopa sana na
kushikwa na mshtuko na kuna salooni maarufu kuzimu ya kuwanyolea nywele za siri
hawa majini hiyo salooni inaitwa YML saloon kirefu chake ni Yezebel, Makata,
Lusifa. Katika hii salooni ndipo hawa majini wanaendaga kunyoa nywele zao kama
vile hapa ulimwenguni watu wanapoenda salooni kunyoa nywele zao, ila tofauti
hawatumii mashine ya kunyolea kama hizi ambazo watu hunyolea huku duniani wa
hutumia mapanga makali sana na shoka kali kunyolea nywele zao za siri sababu ni
nyingi kama kakichaka, na wakishazinyoa hizo nywele hukusanywa na hiyo salooni
ya (YML) kisha zinaletwa huku duniani zinauziwa watu na wanazivaa katika
vichwa, nilizidi kushtuka ila MUNGU akanitia nguvu sababu ni jambo la kutisha
niliporudisha picha duniani, mamilioni ya watu wanavaa kitu wasichokijua asili
yake ni nini? Na lango lake ni nini? Ndugu wasomaji ingekuwa labda ni wewe sijui
ungejisikiaje japo nitaeleza kwa ufupi. Sasa unapoona haya mawigi (weave)
kwanza uelewe siyo salama kwa mwanadamu, pili hizo ni nywele zilizotokea katika
viungo vya siri vya majini ya kike na kiume, hivyo unapovaa ujue katika kichwa
chako umevaa nywele za sehemu za siri za majini katika kichwa chako, na hata
kama unafanya biashara ya kuvaa mawigi uelewe unafanya biashara ya kuuza nywele
za siri za majini na hata kama unazo uelewe unazo nywele za majini katika miji
yako.
MADAHARA
YA KUVAA WIGI (WEAVE).
1.
Kwanza kabisa uelewe katika kichwa chako unakuwa
umevaa nywele za siri za majini na pia umevaa pepo.
2.
Madhara yake unakuwa umeuzuia utukufu wa MUNGU
ushuke katika kichwa chako sababu tayari upo utukufu wa shetani katika kichwa
chako yamkini unavaa pasipo kujua au kwa kujua.
3.
Akili yako na maono yako yanaibiwa na shetani na
kasha shetani anakuwekea yak wake pasipo wewe kujua.
4.
Mawigi yanakufanya usiweze kusimama katika
wokovu.
5.
Mawigi haya yanaletwa ulimwenguni ili kuwazuia
wanawake wasiende mbinguni sababu shetani anajua kabisa katika mioyo ya
wanawake wengi wanampenda YESU kama vile kipindi ambacho YESU aliuwepo
ilionekana wanawake ndio waliokuwa wengi na hata sasa ukiangalia idadi kubwa ya
wanawake ndio wengi waliookoka kuliko wanaume. Sasa alichokifanya shetani
akabuni njia hii wanadamu wavae nywele za siri za majini kwa kuwapiga upofu
wasielewe (huku ndiko kutekwa na shetani). Ila YESU atakaporudi kulinyakua
kanisa wale waliookoka wakiwa wamevaa mawigi, wasiweze kunyakuliwa sababu
katika vichwa vyao vitakuwa vimefunikwa na nguvu za giza ambazo ndizo nywele za
majini yanayoitwa (GOLO). Ashukuriwe YESU aliyenipeleka na kunionyesha haya ili
niwaeleze watu mpate kupona na niliporudi katika mwili akasema na mimi Hebron
nimekufunulia haya uyaone na uyajue ili
uniandalie kanisa ambalo nitalinyakua katika unyakuo wangu, tazama
wanadamu wananipenda ila mwovu amewatengenezea njia ili wasifike mbinguni,
uwafundishe, uwaeleze ili wapone, na hata katika unyakuo niweze kuwanyakua.
6.
Ndani yako mizimu inaishi.
7.
Mapepo yanakuwa na uhalali wa kuishi ndani yako
na wachawi hukuloga kwa urahisi na kukuibia vitu vyako.
8.
Unakuwa unayo alama ya mama wa makahaba
(Yezebel) sababu unavaa vitu vyake.
NOTE: vitu vyte venye asili ya kuzimu ni vitu vya shetani
hivyo havikomboleki wala havitakasiki, wala havibarikiki kwa jina la YESU WA
NAZARETI sababu hauwezi ukazibariki kazi za shetani kwa jina la YESU, bali kazi
za shetani huharibiwa kwa jina la YESU WA NAZARETI.
9.
Humfanya mwanamke kuwa na tabia za uzinzi,
asiweze kutulia katika ndoa na huwaletea ndoto za uzinzi, na kuwaibia wanawake
baraka zao walizoumbwa nazo na mwenyezi MUNGU.
10.
Kila anayevaa nywele hizi katika ulimwengu wa
roho yeye ni mke wa jini pasipo kujijua na wengine hujijua, haijalishi umeokoka
au haujaokoka, ukweli ndio huo.
11.
Katika ulimwengu wa roho jina lako unaitwa
kahaba, na mfano rahisi tu angalia watu wenye tabia za ukahaba katika ulimwengu
wote leo hii kwa upande wa watu weusi. Hata katika street wale wanaofanya
uzinzi kujiuza mwili tazama katika kichwa utaona mawigi.
12.
Mwanawake anapokufa akazikwa na wigi tayari
anajifungia asinyakuliwe katika unyakuo sababu anacho cha kuzimu na MUNGU
anaangalia haki amenituma niseme ukweli ili watu wapone, sababu shetani
alishaona kuwa watu waliookoka hatawapata sasa akabuni njia hii ya mawigi, nikuulize
swali labda umeokoka unampenda YESU na unaishi maisha matakatifu lakini katika
kichwa chako umevaa mapepo je utukufu wa MUNGU utashuka katika maisha yako?
Jibu hakuna na je MUNGU atakubarikije wakati unavaa kofia ya shetani?
13.
Na majini haya ambayo yanayotoa nywele za siri
ambazo ndizo wigi, majini haya nguo za ndani wale wa kiume wanavaa boxer na
majini ya kike yanavaa BIKINI. Ukubwa wa size ya kiuno ni kama mita 4 kiuno.
14.
Ufahamu unashikiliwa na shetani na anayeongoza
maisha yako na hapo ndipo unapotea na kuacha njia za MUNGU pasipo kupenda hii
ni sababu moja wapo ni hizi zinazovaliwa zinatoka katika viungo vya siri ya
majini.
NOTE:
Yapo madhara mengi ila zaidi pata dvd na cd kutoka kwa
kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE na usome makala ya Nabii
Hebron Kisamo na katika YouTube sikiliza utayapata maelekezo zaidi na utapona
roho yako ukiamua na kwa njia hii shetani anaitumia kuliteka kanisa 98%.
Rudisha picha angalia makanisa utaona ni mawigi yamejaa, na watu wakifikiri
ndio kujiremba kumbe ni kujipa cheo cha mama wa makahaba pasipokujua au
kupenda. Nimewajulisha na mataifa yote sababu YESU aliyenituma ni wa mataifa
yote na siyo nchi moja au kabila moja leo amenituma nikuletee habari hii na
yeye anakuangalia wewe unayeupata ujumbe huu anasema na wewe. Amua na uchukie
kabisa na uzivue katika kichwa chako ili akurejeshee akili zako na afunge
milango ya kuzimu katika kichwa chako, na uokoke, sema BWANA YESU naomba
unisamehe dhambi zangu zote, nimeamua kutovaa tena nywele za majini, nazitoa na
nitazichoma, unikomboe YESU, unifunike sasa kwa uweza wako. Nilikuzuia muda
mrefu, ila karibu ndani yangu uniandike na katika kitabu chako cha uzima wa
milele, uniongozee wewe nisipotee tena kuvaa vitu vya kuzimu. Amen.
NABII HEBRON.