Pages

Wednesday, October 29, 2014

ALIYE ACT SINEMA YA YESU HUYO SIYO YESU!
BRIAN DEACON- YEYE SIYO YESU WENGI WAMEMWEKA BRIAN KATIKA MIOYO YAO KAMA YEYE NDIYE YESU.

Katika ulimwengu huu kwa kweli watu wengi wamepotea roho zao na mioyo yao kwa kutokujua na wengine wakijua kabisa, ila ipo neema ya YESU WA NAZARETI aliyenituma kwa mataifa yote alinionyesha kweli yake ya njia ambayo amenionyesha ili niwaongoze watu kwenda mbinguni kama vile alivyomuagiza Musa kule jangwani awaongoze wana wa Israeli waende katika nchi ya ahadi, na sasa ni kipindi cha mwisho, nchi ya ahadi sasa ni mbinguni, njia hii inaongozwa kiroho katika kweli yake tu na siyo kwa copy.

Wakristo wengi wamedanganyika kuwa Brian yeye ndiye YESU na katika fahamu zao iyo sura ya Brian hata wakiomba inawatokea wanasema wamemuona YESU na kumbe siyo kweli. Brian aliyetunga sinema pamoja na wenzake nia yao ni kufundisha na siyo wao wachukue sehemu ya YESU, natumaini hata wao wanamkiri YESU kama BWANA NA MWOKOZI WAO. Sasa cha ajabu hii ni katika makanisa baadhi hata wanathubutu kusema uongo eti hii ni picha ya YESU. Nawaeleza wacheni uongo mmewapoteza watu kwa uongo wakaacha kusoma neno na kumtafakari YESU katika roho badala yake mioyo ya wakristo ndani yao na katika fahamu zao wamemjaza binadamu aliye act katika sinema. Hivyo madhara yake watoto wa MUNGU kwa kupitia njia hii imani zao zinaibiwa na shetani na wala hawapati YESU wa kweli. Zaidi hivi kama kweli hawa ni watumishi walioitwa na YESU waifanye kazi yake je niwaulize swali, je mlimuona ndio anafanana na Brian? Au Brian ndiye kivuli cha YESU?

Hii inaonyesha wazi wazi kuwa hao siyo watumishi wanaomjua YESU wa kweli ndio sababu wanamsingizia Brian ndiye YESU na kuwafundisha watoto wa MUNGU wakaanza kumuabudu Brian wakati hata yeye hapendi aitwe YESU au afanywe ndiye YESU au achukue utukufu wa YESU. KAZI YA Brian na wenzake ni nzuri waliyoifanya ili kuwaelimisha watu, ila watumishi vipofu wanaiharibu kwa kumfanya Brian eti ndiye YESU. Hivi nikuulize swali ndugu msomaji, je Brian alizaliwa na Maria miaka 2000 iliyopita ? jibu, hapana. Je Brian alikufa na kufufuka na akapaa mbinguni? Jibu, yupo Uingereza ni mwanadamu tu kama wewe.

Huku Afrika watu wengi wanamuita Brian ndio YESU na wengine mpaka wanalalia picha ya Brian wakisema wamelala na YESU. Mmh… fungukeni mtubu, tayari ni dhambi kumuabudu binadamu na hata makanisa mengi yanadanganya watu eti yeye ndiye YESU. Hii ni sababu hawa pastors hawajaitwa na yeye YESU na ndio sababu hawamjui. Hii ni hatari sana, roho za watu zinapotezwa na shetani, ametumia mtego huu ili kuwateka watu waone Brian ndiye YESU na ukiona ndiye ujielewe umepotea sababu huu ndio ukweli. Kupitia picha ya video ni ya mafundisho tu wala yule siyo YESU WA NAZARETI, leo funguka ili YESU aingie katika moyo wako, utoe picha za video zilizo act katika ufahamu wako. Hakuna picha wala sura ya YESU katika ulimwengu wote, huo ndio ukweli na ukweli uwaweke huru. Zaidi endelea kusoma makala ya Nabii Hebron ili upone roho yako usidanganyike tena na viongozi vipofu, kama ulivyopotezwa.


NABII HEBRON.