SIRI ZA
KUZIMU
SIRI
ZA SHETANI (PART I)
BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE, YESU ambaye aliyenichagua na
kunituma kwenu nyie mataifa yote ambao mnategemea kwenda mbinguni siku moja ila
kati yenu mlio idadi kubwa mmefungwa msiende mbinguni kwa sababu mbali mbali,
ila amenituma, atakayesikia atapona, atakaye kaza shingo yake atayapata majibu
kwenda kwa farao. Wiki mbili zilizopita nilikuwa naongea na MUNGU ambaye vitu
vyote hivi ni yeye kaviumba, akaniambia Hebron mimi ndiye nilikuandaa kwa kazi
yangu na nilijua ukifika wakati wake utaifanya na nitakutuma kwa mataifa yote
ili kupitia wewe watu wanijue mimi MUNGU wa kweli sababu niliwatuma 98%
wanafanya kazi ya shetani na kuwatesa wanadamu ambao wananipenda ila wao
wananwapeleka katika njia ya jehanamu. Akaniambia mengi ila machache
nitayasema, haya mengine ni yangu.
Kazi hii unayoifanya ni mimi MUNGU ndiye ninayoifanya peke
yangu kupitia mwili wako sababu wewe ni mwanangu mpendwa wangu, na rafiki yangu
kama ilivyokuwa kwa Musa, Eliya, Ibrahim na mwanangu wa pekee na wengine
waliopita ndivyo na kwako ilivyo. Ghafla akaniambia hivi Hebron unajua ni lini
mwanangu atakuja kulinyakua kanisa? Nikashtuka, akaniambia andaa kanisa muda wa
mwanangu kurejea umefika ila ni siri yangu mimi MUNGU ndiye ninayeijua siku
hiyo, akaondoka, kurudi katika kiti chake cha enzi. Nawasihii mrejeeni YESU
muokoke na kubatizwa ubatizo wa maji mengi na kuishi maisha matakatifu ili
katika unyakuo unyakuliwe na wewe.
Hapa sasa ninaelezea baadhi ya siri za shetani zilizopo
kuzimu ambazo amezibuni ili kuhakikisha amekupa wewe na haya yote nilikwenda
kuzimu nilikuwa na Mikaeli malaika mkuu na kuvunja viwanda vya shetani vya nguo
vilivyopo kuzimu ambavyo wanatengeneza nguo zao na kuzileta ulimwenguni ili
unapozivaa unakuwa umetekwa na unamtukuza shetani, joka kuu na mama wa makahaba
(Yezebeli) na jini Abubakar . nitaelezea katika mambo mawili:-
a.
Mavazi ya Kuzimu.
b.
Magari ya kuzimu na mengineyo kidogo, yapo mengi
sana.
A. MAVAZI
YA KUZIMU (YAJUE)
Mavazi haya yamebuniwa kwa jinsia mbili; moja ya wanawake na
ya pili ni ya wanaume. Mavazi haya yapok wa lengo maalum ili kumwangamiza
mwanadamu. Nitaelezea vazi linaloitwa BIKINI (nguo za ndani za kike). Nguo hii
unapoivaa hapa ulimwenguni unakuwa umeolewa na majini katika ulimwengu wa roho,
unakuwa unamtukuza mama wa makahaba, majini mahaba yanakuwa ni rafiki yako,
unakuwa ni shoga katika ulimwengu wa roho. Unakuwa unaoana na jini la kike japo
ni mwanadamu, unapoivaa hiyo BIKINI mapepo yanatumia ndio mlango wa kukuibia Baraka
zako ulizoumbwa nazo na MUNGU, wanaiba uthamani wa ndoa na kukufunga binti
usiolewe au kukufunga hata kizazi, kukufarakanisha usimpende YESU WA NAZARETI
na usidumu katika wokovu wa kweli. Na pia nguo hii ndiyo chupi ya mama wa
makahaba anayoivaaga. Amelibuni yeye na unapovaa ujielewe umemvaa mama wa
makahaba, funguka usivae tena, choma kwa usalama wako ili uwe upande wa MUNGU. Nguo
hii wanawake wengi zaidi wanazivaa lakini hawajui wengi wao, ila wale
washirikina au freemason wanajua, ni lazima avae ili kumtukuza mama wa
makahaba. Zaidi okoka na uendelee kufuatilia makala ya Nabii Hebron pamoja na
YouTube na katika vitabu nilivyoandika.
Viatu vyote vyenye sura kama magamba ya nyoka au scales za
mamba, kitu chochote chenye scales, iwe ni pochi, mikanda, hata saa, kanga,
gauni au nguo ina magamba ya chatu kwa sura, mtu akivaa utaona ni nguo ila kava
chatu, na perfume zenye sura yeyote unayoona inatisha au macho unayaona hilo
silo jicho la kawaida ni jicho la mama wa makahaba, na matokeo unakuwa mzinzi
na hauachi uzinzi sababu hiyo, bikini ina maroho ya mama wa makahaba, na
unayeivaa katika ulimwengu wa roho unakuwa ni makahaba.
Na upande wa mwanaume amebuni nguo za ndani (chupi) ambazo
ni tofauti na chupi, yupo jini anayeitwa Abubakar, huyu ndiye anayebuni mtindo
ya sharobaro ili aweze kuwateka wanaume na yeye akabuni vazi la mnyama ambaye
yupo kuzimu, mnyama huyu ni nyani. Kuzimu wapo wanyama ambao wanabuniwa na joka
kuu, nitaelezea kwa uoande wa nyani. Nyani wa kuzimu anaitwa BOXER, huku
ulimwenguni nyani (baboon). Sasa nyani wa kuzimu huwa anavaa maroho ya uzinzi,
uhuni, ukorofi, ukatili, ushoga, tabia chafu chafu. Katika kiwanda cha kuzimu
wakatengeneza nguo za ndani tofauti na chupi (za kawaida), nguo hizo hapa
ulimwenguni zinaitwa Boxer wanaume wanazivaa sana, inawezekana pia labda
umeivaa muda au unazo nyingi. Sasa nguo hizo siyo salama, unapoivaa unakuwa
umevaa nyani wa kuzimu anayeitwa Boxer na ndio sababu hata hapa ulimwenguni
inaitwa Boxer, sasa uelewe asili ya boxer ni chupi (nguo ya ndani ya nyani wa
kuzimu) na unapoivaa unakuwa umemtukuza jini Abubakar, na yule nyama maroho
yake yanakufuata huku ulimwenguni. Madhara yake unapoivaa tu katika ulimwengu
wa roho unaolewa na majini, unaitwa shoga, hapa ulimwenguni unakuwa mzinzi wa
kupindukia kama alivyo nyani, ukimuona katika mbuga za wanyama pozi anafanya
uzinzi na ushoga hasa akiona watu wanamuangalia, kwa wanaowajua nyani fananisha
tabia zake na mtu anayevaa boxer. Hupenda wanawake wanayovaa hizo BIKINI na
mengineyo, ulevi, bangi, madawa ya kulevya, na miziki ya kidunia. Na anayevaa
siku zote roho mchafu lazima aishi ndani yake.
Vazi hili huwafanya vijana wanapotembea suruali huvalia kwenye
mapaja na nguo za ndani kuonekana na watu, hii ina maana anajionyesha sasa yeye
ni shoga katika ulimwengu wa roho na kimwili baada ya muda itatimia anakuwa
shoga kabisa, ushoga ni maroho ya zinaa ya shetani ili akupate wewe. Zinaleta faraka
katika ndoa, kuua nguvu za kiume ili usikutane na mwanadamu kimwili wabakie
mapepo waliokuoa wewe. Ili upone na uende mbinguni okoka, usivae mavazi haya
kama unataka kwenda mbinguni na mapepo yakukome na uweze kukaa na YESU vizuri. Hizi
ni siri ambazo watu hawajui, wanampenda YESU lakini utashangaa unaanguka katika
dhambi, ni sababu unavaa vazi la kuzimu ambalo ni chupi ya nyani wa kuzimu
anayeitwa BOXER, jitenge naye, fanya maamuzi.
Nyingine ni nguo za harusi za kuonyesha mabega wazi, mgongo,
unapovaa vazi hilo katika ndoa yako uelewe ndoa yako umempa mama wa makahaba,
hivyo mtavuna ukahaba siku zote. Utafunguliwa na utapona roho yako, sema BWANA
YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote nilizozitenda najivua mavazi yote ya
mama wa makahaba kiroho na kimwili, najivua mavazi ya nyani wa kuzimu (Boxer)
na sivai tena, nazichoma kwa jina la YESU WA NAZARETI. BWANA YESU uniandike
katika kitabu chako cha uzima wa milele, uniokoe, uniongoze siku zote nisitekwe
na shetani na mavazi yake na chochote. Amen.
Karibuni enyi mataifa yote mnaomtafuta YESU wa kweli na mnaohitaji
kwenda mbinguni.
NABII HEBRON.