Pages

Monday, October 27, 2014


KULA GOMBO!

PATA KUZIJUA AINA ZA GOMBO ZINAZOTUMIKA KATIKA MAKANISA YA LEO. 98% NI GOMBO LA SHETANI!

BWANA YESU WA NAZARETI ASIFIWE, katika makala ya leo nitaelezea katika somo linaloitwa GOMBO. Ukisoma katika kitabu cha Ezekiel 3:1-3 neno linasema hivi “1ole! Akaniambia mwanadamu, kula uonacho; kula gombo hili, kisha eneda ukaseme na wana wa Israeli. 2Basi nikafunua kinywa change naye akanilisha lile gombo. 3Akaniambia, Mwanadamu, lisha tumbo lako, ulijaze tumbo lako kwa hili gombo nikupalo. Ndipo nikalila, nalo kinywani mwangu lilikuwa tamu, kama utamu wa asali.”
Enyi mataifa yote MUNGU amenituma niwaeleze habari za ufalme wake sababu idadi kubwa imepotezwa kwa kupitia watu kulishwa gombo ambalo halijatoka kwa MUNGU yaani mbinguni. Nitaelezea maana ya neno gombo, gombo ni elimu ya MUNGU itokayo mbinguni, na elimu hii MUNGU humwekea mtumishi wake aliyemuita yeye peke yake kwa kusudi lake. Mbinguni ipo shule ya neno la MUNGU ambayo mtumishi anapoitwa na MUNGU lazima afundishwe na MUNGU ili aifanye kazi yake. Tazama mifano kama kina Musa, Eliya, Yohana hata YESU pia, ni lengo la MUNGU kulisha mtumishi gombo lake ili akawalishe kondoo hicho alicholishwa na MUNGU, na wanapoyapokea watafanyika kuwa wana wa MUNGU na mbinguni watafika.

Ila shetani na yeye alikuwa anacho chuo cha gombo la kuzimu au jina lingine chuo kikuu cha injili ya kristo wa uongo ambacho principal wake alikuwa anaitwa jinni AMAKUTA, (huyu ndiye jinni aliyebuni vitengo vya madhehebu mbali mbali ambayo yanaongozwa na kristo wa kuzimu na yapo hapa ulimwenguni ni mengi sana. Ila kwa sasa chuo hicho nilitumwa na YESU WA NAZARETI nilikwenda mpaka kuzimu nikakichoma chote ili sasa watu waliopo huku ulimwenguni wanaompenda YESU wa kweli wamrejee na wamkatae yesu wa uongo.

A.    GOMBO LA MBINGUNI LIKOJE?
Ni injili kama ilivyoandikwa katika biblia bila kuongezwa kitu, kufupishwa au kubadilishwa kuanzia kitabu cha Mwanzo  hadi cha Ufunuo. Na ndivyo inavyotakiwa kila mtu anayempenda YESU na anayetegemea siku moja atakwenda mbinguni aifuate ilivyo.

B.    GOMBO LA KUZIMU LIKOJE?
Ni injili ambayo haipo katika kitabu cha biblia ya kweli na unapoabudu katika madhabahu ambayo inatenda kinyume na gombo la mbinguni haijalishi pengine wanatumia biblia kweli halafu wanatenda mambo ambayo hayapo katika kitabu kitakatifu (biblia) hapo uelewe mnalishwa mana ya kuzimu au injili ya kuzimu na hautaenda mbinguni kabisa, na hata ukristo wako uelewe ni ukristo feki, wa uongo na kiongozi wako na pia mbinguni hawakujui bali unajulikana mahali pako ndipo huko na inawezekana na wewe unajijua au haujijui ila sasa ni wakati wako wa wewe kujua na kumrejea YESU na utoke katika kanisa ambalo utakuwa umepata picha ni la aina gani. Nitaelezea baadhi ya mifano ya kukujulisha kanisa linaongozwa na gombo la kuzimu na wewe ukafikiria unalishwa neno la MUNGU wa kweli ili uwe hai milele kumbe unalishwa maneno ya injili ya kristo wa uongo ili usiwe na uzima wa milele
a.      Ukikuta kanisa linabatiza ubatizo ambao haupo katika biblia, usipoteze tena muda ondoka hapo ni kitengo cha kukulisha gombo la kuzimu na litakuwa limejaa katika tumbo lako na unayo afya kiroho ya kuzimu. Inakuchochea ujiunganishe na kuzimu badala ya mbinguni na wakati wewe haujui linachoendelea.

b.     Ubatizo wa maji ya kikombe, kubatiza katika kisima, katika tenki, kubatiza watoto wadogo, kubarikia watu wazima, kubatizwa kwa jina la mchungaji haijalishi anasema ameokoka, tena hao ndiyo kina Yuda wa leo waliomsaliti YESU yampasa muelewe.

c.      Kuponywa kwa kudaiwa utoe pesa, kufungisha ndoa za ushoga, kufungisha ndoa kwa agano la shida.

d.     Kanisa lenye watumishi ambao hawajaokoka, batizwa kwa maji mengi na hawajaitwa na YESU wanatafuta pesa (mishahara) hao asili yake wapo katika gombo la kuzimu, injili wanayoeneza usije ukafikiri wanaujenga ufalme wa MUNGU hapana. Hapa mtaona wanafanya kazi ya MUNGU bali katika ulimwengu wa roho wanaubomoa ufalme wa YESU WA NAZARETI na kuuimarisha ufalme wa kristo wa uongo. Kabla ya mimi Hebron kuyajua haya nilikuwa najua ni watumishi wa kweli nikawa nawaheshimu nikijua ni wapakwa mafuta wa MUNGU wa kweli, heee kumbe ni wapakwa mafuta wa shetani na wengine wanafanya kazi hiyo hawajijui, sasa elewa ukweli ndio huo uamue kumfuata YESU wa kweli au kristo wa uongo, mimi sitadaiwa damu yako kwa hao ambao wameshaujua ukweli na wanang’ang’ania. Hiyo ni kazi chafu mbele za MUNGU, ni kazi ya kuangamiza roho za wana wa MUNGU aliowaumba yeye, sasa sijui utamjibuje MUNGU ile siku ya hukumu.

e.      Kanisa linaloabudu sanamu, nyota, mwezi, jua, wanyama, miti au wanadamu hapo ni branch ya gombo la kuzimu, ukweli ni huu na nitasema kweli tu sitanyamaza, MUNGU amekasirika sana kwa jinsi watumishi wanavyofanyika kuwa geti la kuwazuia wengine wasiende mbinguni, wakati hata wao siyo watumishi wake.

f.       Mtumishi anayefanya mazingaumbwe, anayevuta bangi, pombe, sigara, waliopo katika chama cha freemason, wazinzi, wanyang’anyi, kuvaa misalaba, kofia na mengineyo soma katika makala ya Nabii Hebron utafunguliwa zaidi.


NOTE:
Ni hatari sana, ni sumu ya roho yako, ni tiketi ya kukupeleka jehanamu unaposhiriki neno lililochanganywa na uongo au kuongezwa na unashangaa miujiza wanayotenda na wanafanya hayo, uelewe ni miujiza ya kristo wa uongo na unapoipokea na wewe ndani yako linakuwepo pando la kristo wa uongo. Na zaidi ukiona maji yanamwagiwa watu yanaitwa maji ya Baraka, elewa ni kinyume, yale ni maji ya kuzimu, ni maji ya maiti ili kuwaangamiza watoto wa MUNGU wasiende mbinguni. Sasa tubu na uokoke muda huu ili usajiliwe na YESUWA NAZARETI na akutapishe gombo la shetani litoke katika tumbo lako ili neno la kweli liingie ambalo ndie MUNGU likuponye roho yako mauti na ikutoke; sema BWANA YESU nakushukuru kwa kujua ukweli kupitia Nabii wako Hebron, naomba unisamehe dhambi zangu, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima. Namkataa shetani na elimu yake, niongoze wewe na nisijichanganye, nifungue macho yangu, nionyeshe mahali pa kweli ulipo wewe ili nikutane na wewe. Amen.

Karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE.


NABII HEBRON.