JE
UNAIJUA BENKI YA KUZIMU INAITWAJE?
SHARE
HOLDER WAKE?
JINSI
ILIVYOKUWA INAWAPA WATU PESA DUNIANI?
SASA
YESU WA NAZARETI KAIBOMOA SATANIC WORLD BANK!
BWANA YESU ASIFIWE, ASIFIWE YESU WA NAZARETI. Kama nilivyowaelezea
tokea YESU aniite nikamtumikie lengo ni kuwakomboa watu wa mataifa yote
wamrudie yeye na kuwatoa katika mateso ya shetani na kuubomoa ufalme wake kama
ilivyo sasa na mpaka ule mwisho wake. Hapa ulimwenguni siyo jambo geni mnasikia
watu wamekuwa freemason iwe katika kila sekta ili wapewe pesa na shetani, ni
wengi mmesikia kuwa kuna watu wanapesa nyingi hata ukifikiria asili ya pesa
zake hautajua alipatia wapi na ndio matajiri wengi katika ulimwengu wote hao
walikuwa wanachukua pesa katika benki ya shetani ilivyokuwaga kuzimu ila sasa
benki hiyo imechomwa na YESU WA NAZARETI haipo tena na wala watu waliokuwa
wanategemea pesa za freemason mtaona wakiporomoka, filisika katika dunia yote,
myaonapo hayo ujue ujumbe aliyokuletea Nabii Hebron wa Tanzania umetimia,
hawatapata pesa tena sababu benki ya kuzimu nimeichoma moto pamoja na
wafanyakazi wake wote huko kuzimu.
Benki hiyo ya kuzimu ilikuwa inaitwa (JLM BANK) kirefu chake
ni majina matatu ya shareholders (Joka kuu, Lusifa, Maxwell Bank) benki hii
ilikuwa inatengeneza pesa aina ya dola tu na cha ajabu hata huku duniani
zikiwekwa katika machine ya kukagua pesa zinaonekana ni original kama hizi hizi
zinazotumika duniani. Pesa hizi ndio walizokuwa wakipewa watumishi waliojiingiza
katika mtandao wa freemason, wasanii, viongozi mbali mbali, wafanya biashara na
baadhi ya vyama vya siasa katika nchi mbali mbali (pesa chafu). Nitaelezea
katika kanisa ili watu wapone wasidanganyike sababu kupitia hizi pesa kanisa
kupitia watumishi wanaompenda shetani walijiingiza na kuliingiza kanisa kiasi cha
98% ikatekwa na shetani na YESU akabakia na 2% ya watu, 98% ikawa ni idadi ya
joka kuu. Ndugu msomaji pesa hizi zilikuwa zinaletwa kimwili kutoka kuzimu
kupitia malango ya nchi ambazo nimezitaja katika makala ya Nabii Hebron isemayo
Je unajua kuzimu ipo wapi katika ramani ya dunia? Na cha ajabu hata hizo
serikali za nchi hazihusiki na kupokea hizo pesa wala kujua. Ilikuwa ni jambo
la siri, na cha ajabu mtaona baadhi ya makanisa yanaibuka na utajiri ambao
unaleta maswali ghafla ghafla, waliokuwa wanapewa pesa ili waje waieneze injili
ya shetani kwa speed ili YESU akose watu, na utaona ukichunguza sababu wengi
mnayajua haya ila leo ni siku ya
kuhakikishiwa jibu lako ulilosubiri muda mrefu hadi leo YESU WA NAZARETI
anakufichulia. Na kupitia pesa hizo za shetani hapa ulimwenguni yamejengwa
makanisa mengi sana kupitia pesa za shetani na watu wakaona ni pesa kutoka kwa
MUNGU kumbe ni shetani. Nanukuu maneno ya YESU alivyonieleza hata kabla ya
kuiivunja hii benki, akaniambia Hebron mtumishi wangu wanadamu wanafikiri mimi
nipo katika hayo magorofa, vinanda, mimi sipo hapo kabisa na sitendi mimi, hayo
ni majengo ya shetani, mimi nilibakia nikishangaa ila sasa namuelewa, kumbe
pesa ni za shetani. Je nikuulize swali, je shetani akijenga nyumba yake YESU
ataweza kuja kukaa katika hekalu la shetani? Jibu, haji, hii ni sababu ya pesa
za freemason na unapoabudu katika kanisa la jinsi hilo na wewe muumini tayari
umetekwa na shetani, leo ufunguke utoke huko.
Kanisa lenye benki- benki hiyo asili ya mwanzilishi wa
huduma hiyo uelewe ukweli, huyo amepewa mtaji na shetani na kazi anayoifanya ni
kueneza ufalme wa shetani, na kupitia benki hizo kila anayeweka pesa hapo ananyang’anywa
nyota, uthamani wa pesa zake zinapelekwa kwa joka kuu na matokeo yake matatizo
na kufilisika hakukuachii na mwisho wa kifo chako unabakia kuzimu, sababu pale
tu unapopeleka pesa yako katika benki za kanisa nafsi yako inatekwa unakuwa
umeshakufa kiroho ila mwili unabakia gogo. Siri anakuwa anajua kiongozi mkuu wa
huduma hiyo hayo ni maagano ya kutoka kwa shetani afanye biashara. Wakati YESU
WA NAZARETI alisema usisumbukie chochote, fanya kazi yangu, sasa pima maneno
hayo.
Yatakayotokea na yameshaanza kuanzia sasa, mtaona muelekeo
unapotoa na kufilisika na mengineyo atafanya MUNGU peke yake sababu ya hasira
aliyotesewa watoto wake na baadhi ya wachawi na watumishi kuwateka watoto wa
MUNGU, ndivyo ilivyo na kutabadilika.
Pesa hizi za kuzimu zinatumika katika nchi mbali mbali
kuvuruga amani iliyoletwa na MUNGU, kazi kubwa ni VITA.
NOTE:
Hivi umeshajiulizaga huko wanakotoaga misaada ya kuwaletea
pesa makanisani na miradi je wao hawana shida na hizo pesa? Hivyo ndivyo
ilivyotumika kuliingiza kanisa kwenye freemason na kupitia watumishi ambao
wanatekwa na shetani. Na kuanzia kutumia jina la YESU kuzini roho za wana wa
MUNGU pasipo kujua na kupenda. Leo tubu BWANA YESU naomba unisamehe naja kwako,
uniandike jina langu katika kitabu cha uzima, niondolee maroho ya freemason niliyoyapata
katika majengo yaliyojengwa kwa pesa chafu za kuzimu, sirudi huko tena. Niongoze
YESU WA NAZARETI, YESU WA KWELI, Amen.
NABII HEBRON.