PEPO BENEDICT NI PEPO GANI?
NDIYE PEPO ALIYEANZISHA UBATIZO WA KIKOMBE NA NYINGINEZO!
BWANA YESU ASIFIWE, katika somo hili nitaelezea kuhusu pepo
linaloitwa Benedict. Huyu ni pepo moja wapo mkubwa na yeye alikuwepo kuzimu ila
kwa sasa nimeshamuangamiza kabisa pamoja na kazi zake ambazo alikuwa anazifanya
kwa ajili ya kuwapotosha wanadamu wasimfuate YESU wa kweli bali wamfuate yesu
wa uongo. Pepo huyu ndiye aliyeanzisha ubatizo tofauti na ule wa YESU wa
Yordani na ule ubatizo wa Yohana, ubatizo ambao ulitoka kwa MUNGU ili watu
waoshwe dhambi zao zote. Sasa pepo Benedict katika kitengo chake cha kanisa la
shetani, na yesu wa uongo wakabuni mbinu za kuwateka wanadamu ili wasije
wakaoshwa dhambi zao na YESU wa kweli, wakabadilisha ubatizo tofauti na formula
za biblia ya MUNGU wa kweli. Na ndio sababu katika dunia hii utaona watu wanabatizwa
ubatizo tofauti na YESU uelewe hao hawajaoshwa dhambi zao mpaka sasa na pia
siyo mwili mmoja na YESU wa kweli, sababu kubwa ni njia ya ubatizo wa uongo
ambao haupo hata katika biblia ya kweli ila upo katika biblia ya shetani, mimi
nimeiona na najua kilichoandikwa ndani yake. Na ndio sababu nawaeleza ukweli
ili mpone jamani.
Pepo Benedict ndiye aliyebuni ubatizo wa kikombe, ubatizo wa
watoto wadogo, ubatizo wa kisima, ubatizo wa maji mengi ila mtumishi
anakubatiza kwa jina lake. Hii yote ni ili wewe utekwe na upigwe upofu uone upo
salama kumbe umeshatekwa. Batizo hizi zote asili yake ni kuzimu na siyo
mbinguni, sasa ujiulize je kuzimu inaokoa? Kuzimu kuna YESU wa kweli? Kuzimu inatoa
msamaha wa dhambi? Jibu unalo. Huyu pepo ndiye aliyebuni ubarikio wa watu
wazima. Niwaulize je mpo tayari kufuata yaliyomo katika biblia ya YESU wa kweli
au wa uongo? Ukifuata ya uongo tayari na wewe unakuwa ni mtoto wa yesu wa uongo.
Mimi Hebron alipokuwa ananifundisha YESU ili niifanye kazi yake na aliponieleza
Hebron sina watu ninao wachache sina, wengi ni wa shetani, niliogopa,
akanieleza mengi ambayo ni yangu binafsi na alivyosalitiwa na mahali
wanapochukua masomo ya chuo cha kuzimu ambacho jina la chuo hicho cha elimu ya
uongo, principal wake anaitwa AMAKUTA. Huyu na yeye nimemuangamiza, huyu ni jinni
mwalimu wa uongo. Sasa ubatizo wa uongo, kuabudu sanamu, vyote vilikuwa
vinatengenezwa na jinni Amakuta halafu wanaleta duniani na watu mnapokea injili
ya uongo, mnakufa roho zenu na hamuendi mbinguni. Sasa unafunguka ufahamu. Tafuta
katika biblia, ukiona ulibatizwa tofauti na YESU ujue umepokea ubatizo wa pepo
Benedict, na hiyo ndiyo dalili ya kuwa wewe siyo mkristo wa kweli. Ni sababu
ubatizo wako siyo wa neno la kweli kutoka katika biblia unayoijua bali ni
ubatizo uliopo katika biblia usiyoijua. Je hauoni umepotea, mshukuru YESU
ambaye amenifunulia haya ili upofu wa kiroho ukutoke na sasa uone nuru ya
kweli.
Uokoke sasa BWANA YESU naomba unisamehe dhambi zangu zote
uniokoe, uniandike jina langu katika kitabu chako cha uzima, uniondolee ubatizo
wa pepo Benedict, uniongoze nikabatizwe ubatizo wa kweli ambao ulibatizwa wewe
YESU WA NAZARETI. Amen.
NABII HEBRON.