JE
UNAJUA KUZIMU IPO KATIKA ARDHI YA NCHI ZIPI KATIKA RAMANI YA DUNIA?
BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI aliye ndiye mwana wa
pekee wa MUNGU ambaye ndiye aliyenituma kuukomboa ulimwengu na mamlaka yake ya
ajabu, leo mtapata jibu ambalo najua hamjui, katika haya mawili;
I.
Hakuna anayejua mbinguni ilipo.
II.
Hakuna anayejua kuzimu ipo wapi katika ulimwengu
huu tunaoishi.
Ila sasa nitaelezea tu kwa leo kuzimu ni wapi na ipo katika
ardhi na nchi Fulani. Watu wengi wanafikiri kuzimu ipo chini kila mahali,
hapana. Kuzimu ni kweli ipo chini na urefu wake ni kuanzia ardhi ya kwanza hadi
ya milioni mianane (800,000,000 km) urefu wa kutoka duniani hadi mwisho. Ila katika
hizi km serikali ya joka kuu hawakai mahali pamoja wanaishi mbali mbali, ila
wanaishi karibu karibu, ni joka kuu yeye yupo katika ardhi ya 300,000,000 km,
na lusifa yeye yupo katika ardhi ya 299,500,000, na roho mchafu ambaye aliitwa
Maxwell yeye aliishi 299,000,000, ukiagalia utaona hawa wapo karibu karibu ila
hao wengine wote wapo katika ardhi ya 100,000 laki moja.
Haya yote alinifundisha mwalimu wangu na mwokozi wangu YESU
WA NAZARETI ili niupindue ufalme wa shetani. Mimi kama Hebron
sikutegemeaga kwenda kuzimu au kuja kuwa
mtumishi wa MUNGU ambaye hata MUNGU alimjua siku zote mpiganaji lazima uwe na
maelekezo ya vita, na mimi nilipewa na kamanda mkuu ambaye ndiye YESU WA
NAZARETI pamoja na malaika wa vita (Mikaeli). Nakuja kuelezea kuzimu ilipo
sababu hata mimi nilifikiria kuzimu ipo chini ya miguu yangu au ya ardhi
yeyote, kumbe siyo. Ila niliyajua haya pale ambapo aliponituma YESU kwenda
kuzimu kuharibu ufalme wa shetani na joka kuu, hayo niliyoyafanya kuzimu
nitaelezea siku nyingine, ila endelea kusoma makala ya Nabii Hebron, utafunguka
zaidi. Shetani alishauteka ulimwengu 98% na mpaka sasa mataifa yote mfunguke,
injili 98% katika ulimwengu wote ilikuwa inaongozwa na roho mchafu, mpinga
kristo, au injili ya uongo, nah ii ilitokana na watumishi kumgeuka MUNGU badala
ya kujenga ufalme wa MUNGU sasa hivi wanaubomoa ufalme wa MUNGU, na kanisa
kukosa mwelekeo na YESU wa kweli, akabakia yesu wa uongo.
Katika ramani ya ulimwengu huu na kabla ya kwenda kuzimu
YESU alinionyesha ilipo na njia zao na wanapitia wapi na katika kimwili ni
wapi, japo watu hawajui. Kuzimu ipo kama ilivyo huku duniani, ipo bahari,
visiwa, mabara na miji na yapo makanisa ya shetani (joka kuu) ila nimeyabomoa
yote na kuyachoma moto sababu hawa manabii wa uongo ndipo walipokuwa wanapata
hizo nguvu za kuwadanganya wanadamu huku, na mtaona kila aliyetumia uchawi
ataporomoka myaonapo hayo muelewe ndio wale ambao Nabii Hebron anatuelezea. Katika
ardhi hii kuzimu ipo chini ya bara la Asia, ipo chini ya mji wa Lagos, ipo
Sudan, ipo katika mji wa London, na Russian Federation, Australia, Madagascar,
Somalia, America (katika jimbo moja), Syria, Libya na Egypt. Na vipo visiwa
ambavyo sijavitaja. Kwa wale freemason, wachawi, manabii wa uongo, wao haya
siyo mageni sababu ndizo njia za kwenda kwa mungu wao. Ila ipo habari njema,
malango haya nimeshayafunga yote, na sasa watu watamjua MUNGU wa kweli na
watamjua mungu wa uongo na injili ya kweli.
Nawaeleza YESU anarudi, maneno haya ninayowaeleza mataifa
yote siyo ya Hebron, ni kauli katika kinywa cha YESU WA NAZARETI, mrejeeni
yeye, okokeni na muishi maisha matakatifu. Miaka 1000 imeshaanza tayari sasa
wakati wowote ni unyakuo, atawanyakua wale waliookoka peke yake na kuishi
maisha matakatifu. Msidanganyike na mafundisho ya uongo eti unajiita mkristo
lakini hautaki kuokoka, nawaeleza habari njema, ili uwe mkristo ni lazima
uokoke, kinyume na kuokoka wewe ni mkristo jina tu sababu kiunganishi yaw ewe kuwa
mkristo ni uokoke. Watu wengine wanaona wameokoka ila mtumishi aliyemuongoza
sala ya toba kumbe anaongozwa na yesu wa uongo. Na kama ni hivyo na wewe pia
siyo mkristo, leo sema BWANA YESU WA NAZARETI naomba unisamehe dhambi zangu
zote, uniokoe na kuniandika jina langu katika kitabu chako cha uzima wa milele,
simtaki yesu wa uongo na yesu wa unyang’anyi, michango, sanamu, ubatizo wa
watoto wadogo, nakutaka wewe, karibu ndani yangu, uniongoze wewe kuanzia sasa.
Amen.
NOTE:
Utashangaa sana ukiona baadhi ya watumishi wengi cheki
passport zao hizo sehemu wameenda, hao wanaotumia nguvu za giza. Sasa wanapoenda
katika nchi hizo huwa wanaenda kwenye njia za kwenda kwa joka kuu kuzimu,
wanapewa mapepo na miujiza ya kiepo, wanakuja kuwanajisi wanadamu wasiende
mbinguni. 98% ya watumishi wa kanisa wanaoenda katika hizo nci huenda kuingia kuzimu
wala siyo kingine. Nimeyafunga hayo malango huo ndio mwisho wao, YESU WA
NAZARETI NI MFALME, NI JEMEDARI anawapenda ndio sababu amenifunulia hayo mpate
kuelewa ili muwe huru.
Zaidi karibu katika kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA
MATAIFA YOTE. Nawapenda mataifa yote karibuni nyie mumrejee YESU wa kweli na
akae ndani yenu na mumpokee awe BABA yenu na muwe salama.
Nabii hebron.