JE
UNAJUA KILA UNAPOVAA NGUO ZA MTUMBA
UNAJIKABIDHI KUZIMU?
JE
UNAJUA NGUO HIZO UNAIVAA MIZIMU YA WENYE HIZI NGUO?
NA JE
UNAJUA KUWA UNAPOVAA MTUMBA UNAFUNGULIA MALANGO YA MIZIMU KATIKA MAISHA YAKO?
BWANA YESU ASIFIWE, YESU WA NAZARETI, ambaye ndiye mtoto wa
pekee wa MUNGU na ndiye ambaye kupitia jina lake tunapona na unampiga shetani.
Katika blog hii nawaelezea kuhusu nguo za mitumba au mavazi ya mitumba, hasara
zake, sababu hata mimi sikuelewa hayo ni mpaka pale YESU aliponifundisha
mwenyewe sababu hata mimi Hebron nilikuwa nazo nyingi sana ila aliponijulisha
mara moja nilizichoma siku bakiza hata moja. YESU akanieleza Hebron ningemtuma
nani? Sasa uyajue haya na watu wapone, ila nimekujulisha wewe uliyenikubali ili
niuokoe ulimwengu kupitia mwili wako, akaniambia Hebron nilikueleza nitautumia
mwili wako kuukomboa ulimwengu huu lakini huu mwili wako ni mtakatifu sababu
mimi ninaishi ndani yako ila usiogope sababu ya haya ninayokueleza. Hizi nguo
za mtumba unapozivaa huwa unanajisika ndani yako, niliogopa sana, ni sababu ya
nguo hizo, zina mizimu na mapepo na ni mali zao.
MTUMBA
NI NINI?
Mtumba ni kitu chochote ambacho kimeshamilikiwa na mtu wa
kwanza likiwa kipya nay eye, na linapotumika na mtu mwingine yeye anakuwa
anatumia mabaki ya mtu mwingine.
MADHARA
YAA KUVAA MITUMBA.
Unapokuwa unavaa nguo ya mtumba au viatu au mkanda au nguo
yeyote ile, ile nguo inakuwa inayo mizimu ya hao watu ambao ndio waliokuwa
wamezivaa kwanza. Na unapovaa mtumba uelewe kuwa kama yule mwenye nguo alikuwa
na mikosi na wewe utaipata tu sababu umeivaa nguo yake ndio sababu inaitwa
mtumba, kama alikuwa anayo madhaifu ya aina yeyote ile na wewe utayarithi, iwe
ni magonjwa, tabia za ajabu, uzinzi, ulevi, hasira, uwizi, uongo, ni mchawi, ni
freemason, unapovaa na wewe hiyo mizimu inakufuata ulipo sababu ya hiyo nguo
yao ambayo wewe umeivaa.
Najua mitumba imetoka katika mataifa mbali mbali na nchi
nyingi raia wake wanavaa nguo za mitumba, ila hawaelewi madhara yake ni nini
kiroho. Mimi aniponifunulia haya YESU WA NAZARETI ni sababu ananipenda, na mimi
nawafunulia ulimwengu wote ni sababu YESU wa mataifa yote anawapenda na anataka
mpone ili awabariki na awaokoe na shetani asipate kitu cha kukushtaki na
shetani asipate chochote cha kukuibia.
Nataka uelewe jambo hili, je utakuwa unajua nguo za mitumba
unazovaa ni za mtu aliyekufaga au yupo hai? Jibu haujui. Na je unajua kuwa
katika kila nguo ya mtu kuna vitu vyake vinakaa hapo? Tazama vazi la Eliya
lilikuwa lina vitu vya Eliya na alivyolipokea Elisha nay eye akavipokea, hivi
ndivyo ilivyo nguo zote za mitumba inavyo vitu vya watu na unapovaa ile mizimu
ya kwao inakufuata na kuharibu maisha yako katika roho na kumfanya mtu kuwa na
tabia za ajabu ajabu ni sababu ya nguo za mtumba, na cha ajabu hata kanisa
linapigwa upofu halikuelewa madhara ya mitumba na kulifanya kanisa ndio
msambazaji maarufu wa mitumba ili kuwaletea watu maangamizi.
Ile mizimu ya yule ambaye umevaa nguo yake inakuwa inakuja
kukumiliki wewe katika maisha yako kiroho na kimwili na ndio sababu utakuta
watu wanampenda MUNGU lakini hawaokoki hii ni sababu mizimu wa mtumba
unakushikilia na kukutumikisha pasipo wewe kujua. Nguo hizi hazikomboleki.
Kama mwenye nguo hiyo amekufa na yupo kuzimu na wewe
unayavaa mtumba huo utavutwa kuzimu
usiende mbinguni, hii ni sababu unalo vazi lake yeye aliyekuwa mmiliki wa vazi
la kwanza.
Kama mwenye nguo wa kwanza yeye ni freemason na wewe unayo
vazi lake, kule kuzimu mizimu inakuona wewe ni mtu wao na itakufuatilia inahakikisha
tu na wewe unamfuata mwenye nguo hiyo.
Unapovaa mtumba uelewe mlango wa shetani kukupata upo wazi
kabisa na mapepo kukuvamia, hata kama unalalia mashuka, blanketi za mitumba
kila unapolala na wewe unachukuliwa nafsi yako unapelekwa kutumikishwa kama
msukule na siku zote maisha yako ni shida na mahangaiko tu.
Kila ukivaa mtumba uelewe umevaa mizimu, sasa watu wengi
hawapendi mizimu wanaipiga ila wameivaa, hapo umejisumbua, jibu ni kuacha kuvaa
mitumba upone, ili Baraka zako zikae katika hekalu la MUNGU ambalo ndio mwili.
Nguo za kurithishwa za watu wallliokufa hizo pia ni mtumba,
zinazo madahara makubwa sana. Unayavaa madhaifu ya aliykufa na hata
kujiunganisha na kifo alichokufa, kama amekufa cha HIV na wewe itakufuata au
ajali au ugonjwa fulani na wewe linakufuata, au kama marehemu alikuwa na matatizo
na wewe unayarithi. Jambo hili ni hatari kweli. Je ni salama kwa picha hii
uliyoipata? Mimi Nabii Hebron ninajua shetani hanipendi kabisa na ukweli hata
mimi simpendi. Zaidi ya 100% na kupitia blog hii na mafunuo ninayowaeleza watu
wote wa mataifa yote, sasa hivi shetani anatoa machozi hapa ninapoandika ujumbe
huu ninamuona analia machozi ila sina huruma kwa shetani, analia anasema Hebron
usitume somo hilo sababu sitawapata watu niwachezee maisha yao na kuishi katika
miili yao.
Nitaelezea kuhusu nguo za ndani za mtumba. Kila unapovaa
nguo ya mtumba ya ndani, kile kiungo chako cha siri linakuwa ni cha mizimu na
mizimu wanakuoa au kukufanya mume wao na kukuwekea tabia za uzinzi, utajitahidi
uache lakini unashindwa ni sababu ya hiyo nguo ya ndani ya mtumba, na ndoa
zinaharibikia, na pia mapepo hupitia katika njia hiyo kuharibu uzazi, au kumfanya
mwanamke atoke damu kupitiliza siku. Mizimu ndio inayofanya hayo, inakunywa
damu yako ni chakula chao ila wewe binadamu haujui.
NOTE:
Kuvaliana nguo pia ni hatari kiafya na kiroho. Kiafya kama
mtu anayomagonjwa ya mwili na wewe utayapata na kiroho mtu anapovaa nguo yako
anavaa na matatizo yako, balaa, mikosi, magonjwa ya kurithi, kama ni masikini
na wewe unauvaa, mlevi na wewe unauvaa, muongo na wewe unauvaa uongo. Kwa njia
hii wengi zaidi shetani amewateka, ashukuriwe YESU pamoja na serikali yake ya
mbinguni akiwamo Eliya, Musa, Ibrahim wa mbinguni wanaonifundisha na wote 24,
MUNGU awabariki sana.
Unapovaa mtumba kama aliyevaa mara ya kwanza katika ukoo wao
hawafanikiwi na wewe inakufuata hivyo hivyo.
Unapovaa mtumba ROHO MTAKATIFU haishi ndani yako sababu
unakuwa umelifunika hekalu lako.
Unapovaa mtumba ile mizimu inakuja kukuibia vitu vyako mfano
Baraka zako ulizokuwaga nazo umepewa na MUNGU, na kukutesa.
Na unakuwa hata kama umeokooka shetani alikukosa au
amekutafuta katika ulimwengu wa roho hakuoni. Ila endapo ukiwa umevaa mtumba tu
tayari anakuona ulipo sababu ile nguo uliyovaa inakuwa na mizimu, na mizimu
inayo uhusiano mkubwa na shetani.
Viatu vya mtumba, viatu hivi unapoivaa kama nilivyoelezea
kuwa siku zote katika kitu cha kuvaliwa na mtu wa kwanza ni chake tu, hivyo hivyo
mizimu inabakia katika viatu hivyo unavyozivaa tu, hivyo mizimu inaiba utayari
wa maisha yako, utayari wa kuokoka, kwenda mbinguni, utayari wa mafanikio yako
katika maisha yako na ndio sababu hata kimwili fuatilia utaona watu wengi sana
wanaovaa mitumba wachunguze au kama ni wewe jichunguze. Matatizo hayaishi na
unafanikiwa kwa shida au hata haufanikiwi, hii ni sababu siku zote aliyekufa
ambaye ndiye mzimu hupendi ufanikiwe huku ulimwenguni ni hivyo atahakikisha tu na
wewe usifanikiwe. Inawezekana aliyekufa yeye hajaolewa au hakuoa na wewe
atahakikisha na wewe hufanikiwi katika eneo hilo au yeye hajasoma na wewe
hautasoma, au yeye hakuwa tajiri
atahakikisha na wewe unakuwa maskini tum au yeye alikuwa ni mchawi, freemason,
tapeli atahakikisha na wewe yanatokea kwako.
Jambo lingine mitumba kama nilivyoelezea madhara yake kiroho
katika mitumba ni mkusanyiko wa nguo za watu wengi idadi hakuna ajuaye. Sasa inamaana
pia inakuja na maroho ya mizimu ya mataifa mbali mbali na madhaifu mbali mbali
na unapoivaa na wewe unakuwa unayakaribisha katika mwili wako.
Unakuwa kama mtu asiye na msimamo kiroho na kimwili na
hatima yako labda neema ya MUNGU ikushukie vinginevyo siku unakata roho
wanakuchukua wanakupeleka kuzimu sababu wanao uhalali na wewe.
NOTE:
Ili maisha yako isiwe na balaa epuka mitumba, na usivae hata
kurithishwa nguo za watu waliokufa tayari hiyo inakuwa ni mtumba. Watu wengine
wanasema itakuwaje nitavaa nini. Yakupasa kumshukuru YESU ambaye amenifunulia
mimi Nabii Hebron wa kanisa la YESU NI BWANA NA MWOKOZI WA MATAIFA YOTE, ili
ugonjwa huu sugu uliyofichika sasa unafichuliwa ili watu wapone roho zenu.
Roho za mfilisi zimeambatana na biashara ya mtumba, omba
MUNGU akupe biashara ya nguo mpya. Sema BWANA YESU naomba unisamehe dhambi
zangu zote. Uniokoe, uniandike katika kitabu chako cha uzima wa milele. Na univue mavazi ya mitumba na mizimu iachie
maisha yangu ili unimiliki wewe. Nifungulie milango ya nguo mpya na mimi nivae
mpya. Amen.
NABII HEBRON.